Jinsi ya kulima mazao ya mikunde na nafaka

By, Melkisedeck Shine.

Yafuatayo ni maelezo ya jinsi ya kulima mazao ya mikunde na nafaka

Mtama:

1. Aina:

Tegemeo.

• Sifa za jumla.
Inakomaa mapema siku 120 na ina urefu was m 1.5 hadi 1.8 na mbegu zake ni nyeupe.

Maeneo yanayofaa kulimwa:
• Eneo lenye mwinuko wa mita 0 hadi 1300 kutoka usawa wa bahari. Pia eneo liwe na mvua za kiwango cha mm 500 hadi mm 1200 kwa mwaka. Udongo wenye rutuba ya wastani ambao hautuamishi maji. Hukomaa baada ya siku 120 toka kupandwa. Aina hii huzaa kati ya tani 3 hadi tani 3 - 5 kwa hekta moja. Aina hii ya Mtama huvumilia ugonjwa wa mabaka (blight) aina hii ya mbegu iliidhinishwa kutumika toka mwaka 1983. Mbegu hii ilizalishwa katika Kituo cha Utafiti cha Ilonga kwa ushirikiano na Kituo cha Naliendele na Hombolo.

Pato

– Sifa za jumla:
• Aina hii inarefuka hadi kufikia mita mbili na kukomaa mapema (siku 120) inatoa mbegu nyeupe na ncha za ganda lake ni nyekundu. Aina hii inashauriwa kupandwa sehemu zenye mwinuko wa mita 0 hadi 1300 toka usawa wa bahari. Inahitaji kiasi cha mvua cha mm 500 hadi 1200. Inahitaji udongo wenye rutuba ya ustawi. Inachukua siku 120 kukomaa kuanzia ilipopandwa. Inaweza kuzalisha tani 3 hadi tani 3.5 kwa hekta moja. Inavumilia ugonjwa wa madoa ya majani, lakini kwa kiwango kidogo hushambuliwa na ugonjwa wa mabaka ya majani (leaf blight). Aina hii ilitolewa na kuruhusiwa mwaka 1995. Mbegu hii ilizalishwa na Kituo cha Utafiti Ilonga kwa ushirikiano na Kituo cha Naliendele na Hombolo.

Macia – Sifa za jumla:
Aina hii inashina lenye nguvu. Mmea hukua na kufikia sm 1.2 hadi sm 1.5 Inakomaa mapema siku 120 na ina mbegu nyeupe. Inashauriwa kupandwa maeneo yenye mwinuko wa mita 0 – 1300 toka usawa wa bahari. Kiasi cha mvua kinachotakiwa ni mm 500 – 1200. Inahitaji udongo wenye rutuba ya wastani. Inakomaa kwa siku 120 tangu kupandwa. Kiasi cha mavuno ni tani 3.5 – 4 kwa hekta moja. Inavumilia ugonjwa wa mabaka ya majani. Aina hii ilizalishwa mwaka 1999. Kituo cha Utafiti kilichozalisha ni Ilonga kwa kushirikiana na Naliendele na Hombolo.

Hakika – Sifa za Jumla:
• Aina hii hukomaa mapema kwa siku 105. Hakika hukua hadi urefu was m 1.5 – 1.6 mbegu zake ni nyeupe na inavumilia gugu la kifuha pamoja na kuvumilia ukame. Inashauriwa kulimwa katika maeneo yenye mwinuko wa mita 0 – 1500 kutoka usawa wa bahari. Inahitaji mvua ya mm 200 – 500 kwa mwaka pamoja na udogo wenye rutuba ya wastani ambao hautuamishi maji, mavuno hufikia tani 2.5 – 3 kwa hekta moja. Inavumilia ugonjwa wa mabaka ya majani. Ilizalishwa mwaka 2002 katika Kituo cha Ilonga kwa ushirikiano na Hombolo na Ukinguru.

Wahi

– Sifa za jumla:
• Inakomaa mapema kwa siku 100. Mme hurefuka hadi sm 1.4 – 1.5 ina mbegu nyeupe na inavulia gugu aina ya kuduha, pamoja na kuvumilia ukame. Aina hii inapendekezwa katika maeneo yenye mwimuko wa mita 0 – 1500 toka usawa wa bahari. Inahitaji kiasi cha mvua cha mm 200 – 500 kwa mwaka. Udongo wenye rutuba ya wastani usiotuamisha maji. Mavuno hufikia hadi tani 2.5 – 3 kwa hekta moja. Huvumilia ugonjwa wa mabaka ya majani ilizalishwa mwaka 2002 na kituo cha utafiti cha Ilonga kwa ushirikiano na Hombolo na Ukiriguru.

TEKINOLOJIA ZA KIAGRONOMIOA ZINAZOSHAURIWA:

• Kutayarisha shamba:
Shamba litayarishwe kabla ya mvua kuanza. Tayarisha shamba liwa laini kwa kuondoa majani, mawe na mabonge ya udongo kwa vile mbegu ni ndogo sana muda wa kupanda ni Januari. Panda kwa kutoboa mashimo. Panda katika nafasi ya sm 75 x sm 30 kwa kuweka mbegu mbili kila shimo. Hekta moja hupandwa kilo 4 – 7 za mbegu. Ukifuata kiwango hiki utapata miche 83,333 – 90,000 kwa hekta.

• Palizi na kupunguzia mimea:
Palizi ya kwanza na kupunguzia mimea ifanyike wiki / majuma 2 – 4 tangu kupanda . Unaweza kuchanganya na mazao mangine jamii ya mikunde hasa mbaazi.

Kiasi cha mbolea kinachoshauriwa:
Aina zote za mbolea zinashauriwa. Mbolea za viwandani na zile za kawaida kama samadi, mbolea za viwandani tumia kilo 60 N kwa hekta na kilo 40 N kwa hekta. Zile za uvundo tani 10 – 15 za samadi kwa hekta. Mbolea ya Naitrojeni hutumika / huwekwa mara mbili nusu ya kwanza wakati wa kupanda na nusu ya pili huwekwa baada ya palizi ya kwanza – mbolea ya fosiforasi (P205) huwekwa wakati wa kupana. Samadi huwekwa kabla ya kupanda. Namna ya kuweka mbolea hizi ni fosiforasi huwekwa kwenye shimo la mbegu na ile ya Naitrojeni hunyunyiziwa juu ya ardhi.

KUZUIA WADUDU WA SHAMBANI NA WALE WA GHALANI:

• Kipepeo wa Mtama (Sorghum shoot – fly)
Hawa hushambuliwa sehemu yam mea inayoota na kusebabisha mmea kufa. Alama za ugonjwa hujitokeza wiki 1 – 4 baada ya kupanda. Mdudu huyu hutokea katika maeneo yote yanayostawi Mtama. Namna ya kumzuia mdudu huyu ni kupanda mapema na kupalilia vizuri. Pia kutumia madawa ya Thiodan ya unga 4%.

• Vitoboa shina (Stolla borer):
Hawa hushambulia jani linaloota na kusababisha vishimo virefu vidogo. Mdudu huyu hupatikana maeneo yote yanayolimwa Mtama. Mdudu huyu anaweza kuzuiwa kwa kupanda mapema na kupalilia vizuri. Tumia dawa ya Thiodan ya unga 4%.

• Viwavi wa ghalani (Storage weevils):
Viwavi hushambulia kwa kutoboa mbegu na kula sehemu yote yenye wanga. Wadudu hawa wanaweza kupanguza mazao hadi asilimia 90% kama hatua za kudhibiti hazitachukuliwa. Wadudu hawa hupatikana sehemu zote zinazolimwa Mtama. Ili kuzuia wadudu hawa nafaka ikaushwe vizuri kufikia kaisi cha umaji maji 11% kabla ya kuhifadhi. Pia tumia dawa ya Actelic Super katika kiwango cha gram 100 za dawa kwa kila kilo 100 za nafaka.
• Kuzuia Magonjwa:
Ukungu wa nafaka (Grain Mould):
Ugonjwa huu unasababishwa na fangasi, mvua za muda mrefu na joto la kiwango cha juu wakati wa kuchanua maua na kuweka mbegu ambapo husababisha ukungu. Huenea katika maeneo yenye unyevu na joto. Namna ya kuudhibiti ugonjwa huu ni kupanda mapema na kutumia dawa ya Fernasun – D katika mbegu.

• Sinuts:
Ugonjwa huu husababisha Mtama ushindwe kutoa mazao kwa vile ugonjwa husababisha suke la mtama lishindwe kuzalisha nafaka. Ugonjwa huu uko katika ardhi.

Aina nyingine ya Sinut husababishwa na fangasi na huzaliwa kwenye mbegu. Husababisha madhara wakati mche wa mtama mchanga. Hata hivyo ugonjwa huu huonekana sana katika Kanda ya kati mwa Tanzania. Ugonjwa huu huzuiwa kwa kutumia mbegu ambazo lazima ugonjwa zilizochaguliwa toka mme isiyo na ugonjwa. Fukia au choma mot mimea iliyoshambuliwa na ugonjwa huu. Pia tumia madawa ya fangasi ya Topsin na Fenasan – D.
• Ergot:
Dalili za mwanzo za ugonjwa huu ni umaji maji mweupe wenye kunata unaotokana kwenye mimea iliyshambuliwa. Hii husababisha suke la Mtama kuwa cheusi. Ugonjwa huu hutokea zaidi katika uwanda wa chini hasa pwani. Namna ya kuzuia ni kupanda kwa kubadilisha mzunguko wa mazao na kuchoma mabaki yam tama baada ya kuvuna.

• Uozo wa Mkaa (Charcoal Rot)
Ugonjwa huu husababisha mmea udumae na husababisha ujazo wa mbegu kupungua kwa vile eneo la chini la mmea hudhoofika na kuwa laini. Ugonjwa huu hutokea katika maeneo yote yanayolimwa mtama, yenye mwinuko wa mita 0 – 1500 toka usawa wa bahari na 400 – 500. Ugonjwa huu unazuiwa kwa kubadilisha mazao na kuchoma masalia ya mimea baada ya kuvuna. Ukame, kiwango kikubwa cha Naitrojeni, na kiasi kikubwa cha mimea kwa eneo ni mazingira mazuri ya kusababisha ugonjwa huu.

Mimea Jamii ya Mikunde (KUNDE):

Aina za Kunde:

• Tumaini – Sifa za jumla:
Hukomaa kwa muda wa siku 75 – 90. Aina hii ya kunde husambaa ina maua yenye rangi za zambarau na mbegu zake ni mviringo. Maeneo yanayoshauriwa kupanda ni yenye mwinuko wa mita 0 – 1500 toka usawa wa bahari. Inahitaji udongo mwepesi wenye rutuba na usiotuamisha maji. Kunde hizi hutoa mazao hadi tani tatu kwa hekta moja. Huvumilia virusi vya mozaiki vinavyotokana na wadudu mafuta wa kunde na bakiteria. Aina hii ya kunde ilizalishwa mwaka 1992 na Kituoa cha Utafiti cha Ilonga kwa ushirikiano na Naliendele.

Fahari – Sifa za jumla:
Aina hii hukomaa kwa siku kati ya 75 – 9-0. Mmea husambaa na maua yana rangi ya zambarau. Mbegu zake ni za mviringo. Hustawi maeneo yenye mwinuko wa mita 0 – 1500 kutoka usawa wa bahari. Hutoa hadi tani 3 kwa hekta moja. Huvumilia magonjwa ya CABMV na mabaka. Fahari ilitolewa mwaka 1982 na Kituo cha Utafiti Ilonga kwa kushirikiana na Naliendele.

Vuli – 1 Sifa za Jumla:
Inakomaa kwa siku 55 – 65. Hukua ka kunyooka na kusambaa kidogo. Mbegu zake ni nyekundu na za mviringo. Inastawi vizuri maeneo yenye mwinuko wa mita 0 – 1500 toka usawa wa bahari. Ikipataiwa matunzo mazuri huto hadi tani 2 kwa hekta moja. Vuli – 1 inavumilia CABMV, BP na BB Vuli – 1 ilizalishwa mwaka 1987 kutoka kituo cha utafiti Ilonga.

Vuli – 2 Sifa za Jumla:
Inakomaa baada ya siku 65 – 70 baada ya kupandwa inaota ikiwa imenyooka na kusambaa kidogo. Mbegu zake zina weupe uliofifia na ni mviringo. Aina hii husitawi vizuri maeneo yenye mwinuko wa mita 0 – 1500 kutoka usawa wa bahari. Katika matunzo mazuri aina hii huzalisha hadi tani 3.5 kwa hekta moja. Vuli – 2 huvumilia CABMV, BP na BB Vuli – 1 ilizalishwa mwaka 1987 kutoka kituo cha utafiti Ilonga.

TEKINOLOJIA ZA KI-AGRONOMIA ZINAZOPENDEKEZWA:

• Aina zinazoota kwa kusimama na kukoamaa mapema:
Shamba lilimwe na kusawazishwa vizuri kwa vile mbegu ni ndogo. Aina hii hupandwa katika mvua fupi. Ikibidi zipandwe wakati wa mvua kubwa zipandwe mwezi mmoja kabla ya mvua kwisha, ili zikomae kukiwa hakuna mvua. Panda kwa kutoboa vishomo kwa fimbo. Panda katika nafasi za sm 50 x sm 20, kwa kuweka miche / mbegu 2 kila shimo kiasi cha mbegu kwa hekta ni kilo 20. Jumla ya mimea kwa hekta moja ni 200,000. Hikikisha shamba lako halina magugu kwa wiki sita na baada ya hapo palilia inapobidi. Unaweza kuchanganya na mazao mengine ya kunde kwa mbaazi.
AINA ZINAZOSAMBAA NA KUCHELEWA KUKOMAA:
Lina na kusambaza udongo shambani hadi uwe laini kwa vile mbegu ni ndogo. Aina hii ya kunde hupandwa wakati wa mvua nyingi, na ipandwe miezi miwili kabla ya mvua kumalizika. Panda kwa kutoboa mashimo kwa fimbo / kijiti. Panda kwa nafasi ya sm 75 x sm 20, mbegu moja kwa shimo. Kiasi cha mbegu kwa hekta ni kilo 8. Kiasi cha mimea kwa hekta moja ni 66,666. Shamba lipaliliwe lisiwe na magugu kwa wiki sita. Baada ya hapo palizi ifanyike kama kawaida.

KUDHIBITI WADUDU WAHARIBIFU WA MAZAO JAMII YA MIKUNDE

MUHTASARI:

Wadudu waharibifu wa zao la Kunde wako katika makundi mawili:-

(i) Kundi la kwanza ni la wadudu wanaoshambulia mimea ikiwa shambani. Ina maana mmea hushambuliwa baada ya kuona hali inapokomaa na kutoa mbegu. Kundi la wadudu hawa lina tabia ya kufyonza (Sap = supu) yam mea kwenye majani, matawi, mashina, maua hata mbegu hasa zikiwa changa kama vitunda. Njia hii ndiyo pekee kwa wadudu wa kundi hili kujipatia mlo ili waishi na kuzaliana. Katika kundi la pili kuna wadudu wenye tabia ya kukata mashina na kuangusha mimea michanga na wengine hutafuna majani na maua. Zaidi ya uharibifu katika kula mimea, wadudu wengi ni hifadhi ya viini vya magonjwa ya virusi.

(ii) Kundi la pili nila wadudu waharibifu baada ya mavuno kulekwa ghalani. Athari ya wadudu hawa inapelekea wakulima kupoteza chakula ghalani pia kupunguza chakula ghalani pia kupunguza ubora wa mazao yanapopelekwa sokoni mfano Mahindi yanapofunguliwa soko lake ni duni. Jamii za wadudu na athari zao zinaelezwa katika aya zifuatazo:-

1. KUNDE:
(ii) Toliage heetle (Ootherca mutabilis)
Wadudu hawa hushambulia mimea ya kunde baada ya mbegu kuota (Seedling stage). Wakiwa kwenye hatua ya mdudu kamili (adult stage) hushambulia majani kwa kula sehehmu kati ya vihimili vya jamii (area between leaf veins).
Mashambulizi ya wadudu wengi (haye number hutokea mmea kupoteza majani yote na hatamaye mmea kufa.
Kuzuia jamii ya wadudu hawa:
Dawa za chemikali aina ya enolosulfan, Karate n.k. huongamiza mashambulizi kwa mpulizo mmoja.

(i) Aphiols (Aphis gaccivora)
Hawa ni kati ya wadudu wenye kusababisha hasara kubwa katika zao la kunde. Wanapendelea kula mvunga wa majani (under leaf), sehemu za vishina na hata vitumba (pools) vya mbegu. Athari za mashambulizi: Mmea hudumaa, majani husinyaa na kukunjamana pia hupukutika kabla hayajazeeka hatimaye mmea hufa.

Kuzuia Aphiols: Dawa za chemikali aina ya phosphomiolon na dimethroate kwa cc 40 katika lita 10 za maji.

(iii) Flower thrips (Megalurothrips sjostedti)
Hatua ya mdudu kamili hushambulia maua. Mimea ikishambuliwa sana haizai matunda kwasababu maua yameharibika. Mashambulizi yakiwa makubwa zao lote huangamia.

Kuzuia: Kwa kutumia chemikali aina ya Cypermethrin – kiwango cha cc 40 katika lita 10 za maji.

(iv) Poolborer (Maruca testulalis)
Wadudu hawa hula mvungu wa majani, ganda la shina na vitumba vya mbegu katika hatua ya kukomaa. Athari: Mmea hudumaa, umbo la majani huharibika (olistorted leaves) na hupukutika kabla ya kuzeeka. Mimea mingi hasa michanga hufa.

Uzuiaji: Kwa kutumia chemikali aina ya phosphomidon na dimethoate kwa kiwango cha cc 40 katika lita 10 za maji.
(v) Podsucking bugs (Anoplemenia, Riptortus, dentires, Acanthomia SPP)
Wadudu hawa hushambulia mikunde katika hatua ya kuweka vitumba (pools). Hasara, inayosababishwa, na wadudu hawa hufikia 90%. Madhara makubwa huletwa na hatua ya wadudu kamili (adult stage/ kwa kufyonza “Sap = Supu” ya vitumba teketeke ambavyo husinyaa na kukauka bila kukomaa wala kuwa na mbegu.

Kuzuia: Kwa kutumia chemikali za Endosulfan au dimethoate kwa kiwango cha cc 40 katika lita 10 za maji.

(vi) Cowpea storage weevils (Callosobrunchus macuhates callosobrun ams chinensis).

Mashambulizi ya wadudu hawa wawili huanzia shambani wakati kunde zimekaribia kukomaa. Wadudu hutaga mayai kwenye vitumba vilivyokomaa. Mayai yakiangauliwa, funza hupenya kupitia kwenye matobo yanayosababishwa na wadudu wengine. Funza wakiangaluwa hushambulia mbegu na uharibifu hufikia 70% ya mbegu safi.

Kuzuia: Tumia chemikali aina ya Acteric Super Dust 100 mg za unga wa dawa katika 10 Kg za mbegu safi (Seed grain).

NAMNA YA KUZUIA MAGONJWA YA ZAO LA KUNDE:

Magonjwa hatari yanasababishwa na vimelea vya virusi na vya bacteria aina tabia na uzuiaji wa magonjwa haya ni kama ifuatavyo:-

(i) Cowper aphiol-born mosaic virus:
Ugonjwa huu husababishwa na virusi na hupelekea mkulima kupata hasara ya 13 – 87% ya zao. Dalili za ugonjwa huu ni michrizi ya rangi ya kijani iliyochanganyika na njano au ya ugoro (mosaic & mottling) kwenye majani.
Kuzuia: Kwa kutumia aina za kunde zenye kustamili ugonjwa huu kama Tumaini, Fahari na Vuli.

(ii) Bacterial blight (Xanthomonus vignicola)
Ugonjwa huu hushambulia sana miche na kiasi cha 60% ya miche yote hufa.
Dalili: Majani yaliyoathirika huwa na vidonda vyenye rangi kati ya njano ya chungwa. Katika mashambulizi makubwa vidonda vidogo huungana (merge – coleasce) na eneo kubwa la majani huharibika. Ugonjwa hushamiri katika kipindi cha mvua nyingi (Kifuku) na umwagiliaji kwa juu (Overhead irrigation).

Kuzuia: Tumia mbegu zinazovumilia ugonjwa kama Tumaini, Fahari na Vuli.
(iii) Bacterial bligh (Xanthomonas Spp)
Ugonjwa hushambulia aina ya kunde pori na zinazolimwa.

Dalili: Vidonda vidogo huonekana uvunguni mwa majani. Katika mimea dhaifu (more susceptible) vidonda huungana na kuwa na umbo la duara lenye ukubwa wa: kipenyo cha 1-3 cm. Mwanzoni vidonda huonekana kufutuka mvunguni mwa jani kadiri vinapokomaa huwa na rangi ya kahawia upande wa juu na majani. Baada ya muda vidonda hukauka na hubakisha migonyeo sehemu zilizoathirika. Majani mengi yaliyathirika hubadilika kuwa njano na baadaye huanguka / hupukutika.

Ueneaji: Ugonjwa huenea kwa kasi wakati wa kifuku (mvua nyingi) na umwagiliaji unapokuwa wa juu. (overhead irrigation). Kimelea cha bacteria huyu hudumu kwenye punje (mbegu). Kwa hiyo mbegu za namna hii huota zikiwa na viini vya ugonjwa.

Kuzuia: Kutumia mbegu zenye kustahimili ugonjwa huu kama Tumaini, Fahari na Vuli.

KILIMO CHA MBAAZI:

Kilimo cha Mbaazi kinahusisha jamii 3 maarufu kwa wakulima. Pia kilimo cha mbaazi kimegawanyika katika sehemu 2: Uzalishaji wa mbaazi zinazokomaa haraka (shurterm varieties), uzalishaji wa mbaazi zinazokomaa katika muda wa kati (Medium duration varieties) na muda mrefu (long duration varieties).

JAMII YA MBAAZI:

(i) Komba:
Aina hii iko kwenye kundi la mbaazi zinazokomaa katika kipindi kifupi ikifikia kilele cha kukua (kurefuka) matawi yake hutengeneza umbo mfano wa chaka. Aina hii huchanua maua ya rangi nyekundu na mbegu zake ni mviringo. Aina hii hustawi vizuri katika nyanda za 0 -1900 mita usawa wa bahari. Zenye udongo mwepesi, wenye rutuba ya kutosha hii kukomaa katika siku 120 bada ya kupandwa, mavuno hufikia 4 tons kwa hekta katika awamu. Mbaazi hizi huvumilia ugonjwa wa fussaruim wilt.

Aina hii iliruhusiwa kusambazwa mwaka 1999 na ARI – ILONGA ikiwa ni Makao Makuu ya Tafiti za mbaazi wakishirikiana na Naliendele.

(ii) Tumia aina hii ni ya kundi la mbaazi zinazokomaa katika muda wa kati (medium duration variety)

Huwa na matawi yaliyoelekea juu bakala ya sura ya kichaka (indeferminate), vishada vya maua vinapinda mfano wa pembe za ndovu na mbegu ni nyeupe za duara. Aina hii hustawi vizuri katika nyanda za 0 – 1900 mita toka usawa wa bahari. Udongo uwe wa rutuba ya kutosha na usituamishe maji. Hukomaa siku 140 – 180 baada ya kupandwa (kwa kutegemea muda wa kupanda na hali ya joto. Hutoa mavuno ya 3.5 tani kwa hekta katika awamu (muttiple harvest – not single). Aina hii ni dhaifu kwa kushambuliwa na ugonjwa wa Fussarium. Aina hii iliruhusiwa kusambazwa mwaka 2003 na ARI ILONGA ikiwa ………………… Naliendele

(iii) MALI:
Aina hii iko katika kundi la mbaazi zenye kukomaa katika muda mrefu (long duration variety). Ina matawi yanayoelekea juu. Maua yanasura ya kupinda kama pembe za ndovu na mbegu zake ni nyeupe za umbo la mviringo. Hustawi kwenye vyanda za 500 – 1900 mita toka usawa wa bahari. Udongo uwe wenye rutuba ya kutosha na usituamishe maji. Aina hii hukomaa siku 180 – 270 baada ya kupanda na hutoa mavuno ya 4 tani kwa hekta katika mtindo wa kuvuna kwa awamu (multiple harvert). Aina hii ni dhaifu kwa ugonjwa wa Leaf blight. Iliruhusiwa kusambawa mwaka 2002 na ARI ILONGA ikiwa ……………… Naliendele.

TEKNOLOJIA ZA UZALISHAJI BORA WA MBAAZI:

Uandaaji shamba: Kwa aina inayokomaa katika muda mfupi.
(i) Shamba litifuliwe hadi udongo kuwa laini (fine seedbed muda wa kupanda wakati wa mvua nyingi za kifuku (masika). Pia upandaji unaweza kufanyika kwenye maeneo ya uhakika wa mvua za vuli (short rains areas).

Namna ya kupanda:
Mbegu itafunikwa na udongo katika vipimo vya 75 x 20 cm kwa kuacha miche miwili kila shimo au 50 x 20 cm kwa mche mmoja kila shimo. Mahitaji ya mbegu ya kupanda kwa hekta ni 20 Kg katika shamba lenye miche 2 kila shina na 30 kg kwenye shamba la mche mmoja kwa shimo. Kadirio la jumla ya mimea kwa hekta (plant olensity) ni 133,333 – 200,000.
Matunzo ya zao:
Palizi itafanyike bila kuacha magugu kwa muda wa majuma sita. Baada ya muda huu palizi ifanywe kadri ya magugu yatakayo ota.

Tahadhari: Aina hii haitakiwi kupandwa kimseto (mixed or intercropping).

Uandaaji shamba kwa aina zinazokomaa katika muda wa kati na mrefu.
Shamba lilimwe mpaka udongo ulainike (fine seedbed).
Muda wa kupanda: Mwanzoni mwa masika (kati ya Disemba na Februari). Aina hizi pia sinastawi kwenye maeneo ya uhakika wa mvua za vuli (areas with teliable short rains)
Namna ya kupanda: Upandaji afunike mbegu kwa udongo. Upandaji ni kwa mistari ikiwa ni 100 x 60 cm inapoachwa mimea 2 kila shimo kwa aina inayokomaa katika muda wa kati (medium duration variety). Njia nyingine kwa aina hii ni ya 90 x 60 cm inapoachwa mimea 2 kila shimo katika mseto na Mahindi au Mtama.

Upandaji kwa aina inayokomaa kwa muda mrefu bila mseto 180 – 50 cm kwa kuachwa mmea mmoja kila shimo. Inapopandwa katika mseto na Mahindi, nafasi kati ya mistari ni 90 x 60 cm kwa kuacha mimea 2 kila shimo. Mahitaji ya mbegu ya kupanda ni 5 Kg kwa hekta kwa aina ya kati bila mseto na 6 Kg kwa hekta katika mseto. Aina ya muda mrefu ni 2 Kg kwa hekta isipokuwa kwenye mseto na 7 Kg kwenye mseto na zao lingine.

Kadirio la mimea kwa hekta ni 33,333 bila mseto na 37,000 kwenye mseto. Kwa aina ya mali ni mimea 11,111 kwa hekta bila mseto na 37,000 kwa hekta kwenye mseto na mazao mengine.

Matunzo ya Zao:
Zao lipaliliwe bila kuacha magugu kwa majuma 6 na baada ya hapo palizi ifanywe mara kwa mara ili shamba liwe safi.

Muhimu: Baada ya majuma 6 tangu kupanda, mkulima apande mahindi katika nafasi iliyobaki wazi.

UZUIAJI WADUDU WAHARIBIFU SHAMBANI NA MAGHALANI:

Wadudu waharibifu kwa zao la mbaazi ni wale wenye mtindo wa kufyonza, kupekecha na kubungua.

(i) Sucking bugs (Chavigralla Spp)
Madhara: Jamii hii hushambulia vitumba (pools) na hatima ya mbegu changa hudhurika. Vitumba athirika husinyaa na kudondoka (shriell and abootion). Wadudu hawa ni maarufu katika maeneo yote yaliyonayo mbaazi.

Kuzuia: Kwa kupuliza chemikali aina ya PARETO – VIWANDA (Synthetic pysethroid) Mfano – ambus, decis, endosnlfom, (thiodan) dimethoorte na karate.

(ii) Poolfly: (Mehamogromony za chakosoma)
Madhara: Punje huharibika. Jamii ya wadudu hawa ni katika maeneo mengi yaliyonayo mbaazi

Kuzuia: Kwa kupulizia chemikali aina ya Karate.

Pod borer (Helicoverpe amigena:
Madhara: Mbegu changa kwenye vitumba huliwa na kubakia matundu makubwa maduara. Wadudu hawa hupatikana na sehemu nyingi zizalishazo zao hili.

Kuzuia / Kudhibiti: Kwa kupuliza chemikali aina ya ………, Karate.

KUZUIA MAGONJWA:

Ugonjwa uitwao Fusaariam wilt (Fussarium aolum) ndio wenye kishindo kikubwa cha uharibifu. Husababishwa na aina ya Fangasi (fungus). Kwa jina la Fussarium.

Himaya za vimelea vya fungasi hawa ni kwenye udongo na mbegu (soil and seedborn oilseeds). Vimelea huishi mpaka miaka 3 kwenye mabaki au tabaka za mimea zilizooza kwenye udongo. Ugonjwa hubainika mmea unapokifia hatua ya kuchanua na kutoa vitumba (flowing and pooling stages). Pia ugonjwa unaweza kutokea mapema zaidi mimea ikiwa na umri wa miezi 1 – 2.
Dalili: Mabaka kwenye mimea iliyoharibiwa na ugonjwa huu wakati ikiwa katika hatua ya kutoa maua na vitumba. Dalili nyingine hutokea ndani ya gamba la shina na kwenye matawi makubwa. Sehemu hizi zikichanua na kuwa wazi, huonesha rangi za kahawia, au rangi ya ugoro na weusi kwenye vifereji vya mfumo wa usafirishaji kwa mmea (xylem tissues).

Ugonjwa huu ni maafuru katika maeneo mengi yanayolima mbaazi.
Kuzuia: Kwa kutumia aina zinazovumilia mashambulizi ya ugonjwa kama Mali. Kuacha kupanda aina zenye udhaifu wa kushambuliwa na ugonjwa huu (avoid planting susceptible varieties to the disease).

TEKNOLOJIA KWA MATUMIZI YA MBAAZI:

(i) KUsindika mbaazi na kupata ……… (kihembe). Mbegu zilizokauka hurowekwa usiku kucha halafu kukaushwa juani kwa siku 2. Baada ya kukaushwa mbegu hutolewa maganda (dehulling). Mbegu zilizotolewa maganda kwa utaratibu huu huitwa Daal au “Kihembe” in Swahili).
(ii) Utayarishaji Bangco (Mbaazi maua):
Mbegu hurowekwa usiku kucha halafu huchemshwa mpaka zikaiva. Baada ya kuchemshwa maji humwagwa na mbaazi zilioiva huungwa kwa kutumia vitunguu swaumu, vitunguu maji, nyanya na mafuta. Chembechembe za nazi iliyokunwa huchanganywa na mbaazi zilizoungwa halafu hukorogwa. Baada ya hatua hii mlo ni tayari.

JAMII YA FIWI = Green gram (Vigna unguiculata).
Aina:
(i) Nuru:
Aina hii hukomaa mapema na mbegu zake zina rangi ya kijani inayong’aa hustawi vizuri kwenye nyanda za 0 – 1500 mita juu ya usawa wa bahari.
Muda wa kukomaa ni siku 60 – 65 baada ya siku ya kwanza ya kupanda na mavuno ni tani 1.5 – 1.8 kwa hekta. Aidha hii huvumilia magonjwa ya Scab (Elsinoe phaseoli). Iliruhusiwa kusambazwa mwaka 1977 na ARI – ILONGA Kilosa.

(ii) Imara:
Aina hii inasifika kuwa kukomaa haraka. Mbegu haziungwi na zina umbo pana. Hustawi vizuri kwenye nyanda za 0 – 1500 juu ya usawa wa bahari. Mbegu hukomaa siku 60 – 65 baada ya siku ya kwanza ya kupanda na mavuno ni tani 1.5 – 1.8 kwa hekta. Aina hii huvumilia Scab (Elsinoe phascoli). Iliruhusiwa kusambazwa mwaka 1982 na ARI – ILONGA Kilosa.

TEKNOLOJIA MAHUSUSI KWA UZALISHAJI BORA WA FIWI:

Shamba litifuliwe (lilimwe) mpaka udongo uwe laini. Muda muafaka wa kupanda ni miezi 2 kabla ya kukatika mvua za masika. Upandaji pia hufanyika wakati wa uhakika wa mvua za vuli. Mbegu huzamishwa kiasi kwenye udogo kwa nafasi ya 50 x 20 cm na mimea 2 kila shimo. Mahitaji ya mbegu ya aina ya Nuru kwa hekta ni 10 Kg na aina ya Imara ni 11 Kg. Kadirio la jumla ya mimea kwa hekta ni 200,000.

Utunzaji: Zao lipaliliwe mfurulizo kwa majuma 6 tangu tarehe ya kupanda. Baada ya hapo palizi ifanywe kadiri magugu yanapoot

JAMII YA SOYA: Soybean (Glycine max):

Aina – Uyole Soya 1:
Aina hii huzaa mbegu kubwa zenye rangi ya siaji. Husitawi vizuri kwenye nyanda za 100 – 1800 mita juu ya usawa wa bahari kwenye udongo wenye rutuba ya kutosha usiotuamisha maji. Aina hii hukomaa baada ya siku 127 tangu tarehe ya kupanda, na hutoa mavuno ya 2.5 – 3.0 kwa hekta. Soya hii ni dhaifu kwa ugonjwa wa Bacterial blight. Iliruhusiwa kusambazwa mwaka 2002 na ARI – UYOLE, MBEYA.

TEKNOLOJIA MAHUSUSI KWA UZALISHAJI BORA WA SOYA:

Shamba lilimwe hadi udongo kulainika. Muda wa kupanda ni mwezi wa Januari mwanzoni mwa mvua za masika kwa nyanda za juu Kusini. Zao hili huhifadhi unyevu wakutosha kwenye udogo kipindi chote cha ukuaji.

Upandaji: Mbegu huzamishwa kiasi kwenye udongo. Nafasi ni 50 x 10 cm kwa kuacha mmea mmoja kila shimo 50 x 10 cm kwa kuacha mimea 2 kila shimo. Upandaji wa mbegu kwa hekta ni 25 – 30 Kg na kadirio la jumla ya mimea ni 200,000 kwa hekta. Palizi ifanyike mfululizo kwa majuma 6 tangu tarehe ya kupanda. Baada ya hapo palizi iwe ya kawaida.UJUMBE-WA-POLE-MPENZI-7798766.JPG

Endelea kusoma makala hizi zifuatazo;

a.gif Jinsi ya kulima muhogo

Utangulizi
Zao la muhogo ni muhimu sana kwa Tanzania zaidi kwa wakulima wadogo wenye kipato cha chini. Wakulima wengi huchanganya zao la muhogo na mazao mengine kama vile kunde, mbaazi, njugumawe, n.k. Umuhimu wa zao hili ni kutupatia cahakula na wakati mwingine kwa biashara. Kwa kanda ya kusini muhogo ni chakula kikuu ambacho kinachuku asilimia 75 ya chakula kwa maeneo yote yamikoa ya Lindi na Mtwara… soma zaidi

a.gif Jinsi ya Kulima karanga

Karanga ni mojawapo ya mazao yanayotoa mafuta. Katika Tanzania zao hili hustawi zaid katika mikoa ya Kusini Mashariki, Dodoma na Morogoro. Pamoja na kutoa mafuta vile vile zao hutumika kwa njia nyingine mbali mbali, nazo ni pamoja na:.. soma zaidi

a.gif Kulima Korosho

Ubebeshaji miche ya mikorosho ni moja ya mbinu muhimu katika uendelezaji wa zao la korosho kwa sababu ni teknolojia pekee inayohakikisha usahihi wa viwango vya uzalishaji wa aina ya mkorosho uliopandwa… soma zaidi

[Kitendawili Kwako] 👉Kipara cha mzee kinatoka moshi

KADI-POLE-MZAZI.JPG

a.gif Matumizi ya maji kutibu shinikizo la chini la damu

Matumizi ya maji ya kunywa ni moja ya dawa rahisi kabisa ya shinikizo la chini la damu… soma zaidi

a.gif Mabadiliko gani yanatokea kwenye miili ya wavulana Wakati wa makuzi au wakati wa kubalehe?

  • Utaongezeka urefu na uzito, mikono na mabega yatakuwa na nguvu zaidi, uume na korodani zitaongezeka ukubwa;
  • Ngozi yako i takuwa na mafuta zaidi na unaweza kuota chunusi usoni;
  • Kuota nywele sehemu za siri, makwapani na hatimaye usoni na kwenye kifua
  • Kubadilika sauti na kuwa nzito; na
  • Uume kusimama / kudinda mara kwa mara na utaanza kuota ndoto nyevu.. soma zaidi

a.gif Mapishi ya Viazi vya nyama

Viazi (potato) 1 kilo
Nyama ya ng'ombe 1/2 kilo
Nyanya ya kopo iliyosagwa 1/2 tin
Vitunguu maji 2
Tangawizi/ swaum 1 kijiko cha chai
Hoho 1
Curry powder 1 kijiko cha chai
Pilipili ya unga 1/2 kijiko cha chai
Limao 1/2
Chumvi
Coriander
Mafuta ya kupikia.. soma zaidi

a.gif Kunywa pombe Wakati wajawazito (Uhusiano wa pombe na mimba)

Kuna mengi ya habari utata na kwenda kinyume na kwenda karibu kuhusu kama au si wanawake wajawazito wanaweza mara kwa mara hutumia kiasi kidogo cha pombe. Baadhi ya madaktari kuwajulisha wagonjwa wao na si kunywa pombe yoyote wakati wa ujauzito bila kujali jinsi mbali pamoja wao ni. Madaktari wengine kuwaambia wagonjwa wao kwamba ni salama kula kiasi kidogo sana cha pombe wakati wa ujauzito. Ni rahisi kuwa kuchanganyikiwa na habari hii. Ni kweli kuna kiasi salama ya matumizi ya pombe wakati wa ujauzito?.. soma zaidi

a.gif Jinsi ya kupika Biriani ya Nyama Ng'ombe Na Mtindi

Mchele wa biriani - 5 gilasi.. soma zaidi

[Msemo wa Leo] 👉Umakini

[Jarida la Bure] 👉Biblia ya Kiswahili- Agano la Kale

FURSA..! Kuna nafasi za kazi 100.

Au soma zaidi hapa

.

Slide2-utotoni.GIF
SALAMU-JIONI98HBS.JPG

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.