Jinsi ya kulima maembe kitaalamu

By, Melkisedeck Shine.

familia-mapenzi-na-mahusiano.png

Jinsi ya kulima maembe kitaalamu

KILIMO BORA CHA MAEMBE

Maembe hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Tabora, Pwani, Mtwara, Tanga, Mwanza, Morogoro na Mbeya. Uzalishaji wake ni wastani wa tani 159,472 kwa mwaka. Maembe ni zao muhimu la biashara na chakula.

MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA UZALISHAJI

Ili kupata mazao bora ni muhimu kuzingatia kanuni bora za kilimo cha maembe hasa kanuni zifuatazo:

  1. Kuchagua aina bora ya kupanda kulingana na mahitaji ya soko.
  2. Panda umbali wa mita 10 kwa kumi kama utatumia miembe ya kuunga, hii ni kwa sababu haiwi mikubwa sana kwa sababu haiishi miaka mingi, kwa ile ambayo si ya kuunga panda umbali wa mita 15 kwa 15 kwa kila mti mmoja wa muembe

DHIBITI MAGONJWA, WADUDU, NA MAGUGU

โ€ข Fanya ukaguzi wa shamba mara kwa mara ili uweze kudhibiti wadudu na magonjwa ya matunda kabla madhara hayajawa makubwa

UGONJWA WA KUTU KWENYE MAJANI

โ€ข Ni muhimu kudhibiti wadudu, magonjwa na magugu ili kupata mazao bora ambayo yatapata soko zuri na kuweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu.
โ€ข Hakikisha shamba ni safi wakati wote ili kupata matunda bora na kurahisisha uvunaji.

MAANDALIZI KABLA YA KUVUNA

Kusafisha shamba pamoja na barabara za shamba

โ€ข Safisha shamba ili kurahisisha uvunaji na usafirishaji shambani.
Kukagua shamba kuona maembe kama yamekomaa Maembe hukomaa katika kipindi cha miezi 4 hadi-6 tangu kutoa maua kutegemea hali ya hewa na aina.

DALILI ZA MAEMBE YALIYOKOMAA

โ€ข Maembe hungโ€™ara
โ€ข Kwa aina nyingine rangi ya kijani hufifia na kuanza kubadilika kuwa ya manjano.

ANDAA VIFAA VYA KUBEBEA, SEHEMU YA KUFUNGASHIA NA USAFIRI.

VIFAA VYA KUBEBEA

โ€ข Ngazi
โ€ข Vikapu
โ€ข Mifuko
โ€ข Ndoo
โ€ข Vichumio

VIFAA VYA KUFUNGASHIA

โ€ข Makasha ya mbao/plastiki na ya makaratasi magumu na matenga

VYOMBO VYA KUSAFIRISHIA

โ€ข Matoroli
โ€ข Magari
โ€ข Baiskeli
โ€ข Matela ya matrekta

KUVUNA

Njia bora ya kuvuna maembe ni Kuchuma kwa mkono
โ€ข Kwa miembe mifupi chuma maembe pamoja na kikonyo chake
โ€ข Kwa miembe mirefu chuma kwa kutumia kichumio maalumu

KICHUMIO MAALUM

โ€ข Acha kikonyo chenye urefu wa sentimita tatu hadi nne ili kuzuia madoa ya utomvu. Utomvu huchafua matunda na hushusha ubora. Pia embe lililovunwa bila kikonyo chake huingiliwa na vimelea vya ugonjwa kwa urahisi.
โ€ข Vuna wakati wa asubuhi au jioni ili kuepuka jua kali linaloweza kubabua matunda.
โ€ข Wakati wa kuvuna hakikisha maembe hayadondoshwi chini, ili kuepuka kuchubuka kwa matunda ama kupondeka hasa yale yaliyoiva barabara. Aidha beba matunda kwa vikapu au mifuko na kusanya kwenye kivuli.

KUCHAMBUA MAEMBE

Kuchambua ni kutenga matunda yaliyooza, kupasuka, yenye dalili za magonjwa au kubonyea, ili kupata matunda yenye ubora kwa ajili ya matumizi, kusindika au kuuza.
โ€ข Matunda yaliyooza na yenye wadudu ni vyema yafukiwe ili kuzuia kuenea kwa wadudu waharibifu na vimelea vya magonjwa.
โ€ข Matunda yaliyopasuka, kubonyea , kuchubuka kidogo wakati wa kuvuna au kuiva sana yatumike haraka kwa chakula.
โ€ข Matunda mazuri ambayo hayajapata madhara yoyote yatunzwe kwa ajili ya kusindikwa, kutumika au kuuzwa.

KUSAFISHA MAEMBE

โ€ข Baada ya kuchambua, safisha matunda kwa maji safi ili kuondoa uchafu na mabaki ya madawa.
โ€ข Maembe yanayokusudiwa kuuzwa nje ya nchi hunyunyiziwa nta ili kuzuia kunyauka na kudumisha ubora.
โ€ข Baada ya kusafisha tumbukiza maembe kwenye maji yenye nyuzi joto zipatazo 52 za Sentigredi kwa muda wa dakika tano. Maji haya pia yanaweza kuchanganywa na madawa ya klorini asilimia 1 ili kuzuia magonjwa ya ukungu.

KUPANGA MADARAJA

Madaraja hupangwa kwa lengo la kurahisisha ufungashaji, usafirishaji na uuzaji. Madaraja hupangwa kulingana na ubora, ukubwa , aina rangi na uivaji.

KUFUNGASHA MAEMBE

Ufungashaji hufanyika katika sehemu safi na yenye kivuli. Ufungashaji wa kujaza kupita kiasi husababisha upotevu wa maembe. Aidha ubora hushuka kutokana na kuminyana na kubonyea kwa matunda wakati wa kusafirisha

TENGA LA KUFUNGASHIA MAEMBE
Inashauriwa kufungasha kwenye makasha ya mbao/ plastiki , makaratasi magumu au tenga kwa sababu zifuatazo:

โ€ข Matunda yanaweza kupangwa na kusafirishwa bila kuchubuka, kubonyea au kupasuka.
โ€ข Huweza kupakiwa na kupakuliwa kwenye chombo cha usafiri kwa urahisi.

Wakati wa ufungashaji ni muhimu kuzingatia yafuatayo:

โ€ข Kasha moja lisizidi uzito wa kilo 20 ili kurahisisha ubebaji.
โ€ข Makasha yawe imara na yenye matundu ya kutosha ili kuruhusu mzunguko wa hewa.
โ€ข Ni muhimu kutanguliza vitu vilivyo safi ndani ya vifungashio ili kuzuia michubuko na mipasuko ya matunda wakati wa kusafirisha.
โ€ข Maembe yapangwe kwa kubananisha na kwa kuhakikisha kuwa vikonyo havitoboi matunda na kusababisha majeraha wakati wa kusafirisha. Kubananisha matunda husaidia kuzuia mgongano unaoweza kusababisha matunda kusambaratika na hivyo kubonyea au kupasuka wakati wa kusafirisha.

KUSAFIRISHA

Ili kuepuka upotevu na uharibifu wakati wa kusafirisha, ni muhimu maembe yapangwe kwenye vyombo vya kufungashia na kusafirisha kwa uangalifu, ndani ya matela, mikokoteni na magari. Epuka kutupa matunda wakati wa kupakia na kupakua. Wakati wa kupanga mazao katika vyombo vya usafiri yasirundikwe ovyo na yasijazwe kupita kiasi ili yasimwagike. Vilevile yafunikwe ili yasipigwe na jua. Jua huongeza kasi ya kuoza. Matunda yakipigwa na jua kwa muda wa saa mbili mfululizo husababisha kuoza kwa asilimia 100.

KUHIFADHI

โ€ข Maembe huweza kuhifadhiwa kwenye chumba chenye hali ya hewa yenye joto la nyuzi 8 hadi 10 za Sentigredi na unyevu wa asilimia 85 hadi 90. Katika hali hiyo, maembe yanaweza kuhifadhiwa bila kuharibika kwa mwezi mmoja.
โ€ข Kagua mara kwa mara ili kugundua uharibifu unaoweza kutokea


Endelea kusoma makala hizi zifuatazo;

a.gif Jinsi ya Kulima pilipili hoho

KILIMO BORA CHA PILIPILI HOHO
Jina la kitalaamu la PILI PILI HOHO ni Capsicum annum. Asili ya zao hili ni bara la Amerika ya Kusini. Hapa nchini zao hili hulimwa katika mikoa ya Iringa, Tanga (Lushoto), Mbeya, Ruvuma, Tabora na Arusha. Kilimo hiki kinaendeshwa na wakulima wadogo katika maeneo yenye ukubwa wa kati ya hekta 0.2-0.4 pia kuna maeneo ya wakulima wakubwa wenye hekta kati ya 2-20. Wakulima hao hujishughulisha na kilimo cha zao hilo kwa njia ya mkataba na kampuni hiyo… soma zaidi

a.gif Kilimo cha nyanya

Nyanya ni aina ya mboga inayo zalishwa kwa wingi sana duniani. Kwa Tanzania, nyanya ni zao la kwanza katika mazao ya mboga linalo limwa na kuliwa kwa wingi ukilinganisha na mboga zingine. Nyanya hutumika karibu Katika kila mlo. Kulingana na umuhimu wa zao hili kama chakula na pia kama zao linalomwingizia kipato Mkulima, kuna haja ya kutoa mafunzo kuhusu mbinu bora za uzalishaji wake. Pia kuna umuhimu wa kufundisha wakulima kutoka sehemu zingine wasiolima zao hili ili nao waweze kuzalisha nyanya na hivyo kuongeza idadi ya aina za mboga katika maeneo yao… soma zaidi

a.gif Kutengeneza jiko la udongo

Kutengeneza Jiko la Udongo Mfinyanzi
โ€œRocket Stoveโ€.. soma zaidi

[Picha Nzuri] ๐Ÿ‘‰Ungekua ni wewe hapa ungefanyaje?

[Msemo wa Leo] ๐Ÿ‘‰Umbali na upendo

[Jarida la Bure] ๐Ÿ‘‰Jarida la kilimo bora cha HOHO

[Hadithi Nzuri] ๐Ÿ‘‰Jinsi mke alivyotoboa siri ya Mmme wake

[SMS kwa Umpendaye] ๐Ÿ‘‰Ujumbe mzuri wa usiku mwema kwa umpendaye

a.gif JINSI YA KUPANDA MPUNGA KWA MBINU ZA KILIMO HAI

Chagua aina ambazo zinafaa kutumika katika mazingira husika.
Mpunga hujipevusha wenyewe. Hii inaruhusu kuchagua mbegu kutoka shambani kwako mwenyewe.
Usipure mbegu ambazo zinatumika wakati wa kusia
Mavuno ya kiangazi ni chanzo kizuri cha mbegu bora.
Tenga kilo 30 hadi 40 za mbegu kwa ajili ya kupanda hekta 1… soma zaidi

a.gif Wewe ni mshindi: Mambo yakuzingatia ili uweze kushinda chochote katika maisha

Mshindi ni mtu aliyeshinda, Hivyo wewe ni mshindi kwa kuwa umeshinda, kuwa hai leo ni ushindi, kuwa na Mungu mpaka sasa huo ni Ushindi, kuweza kujifunza semina na kufuatilia mafundisho kama haya wewe ni mshindi.
Ebu jiulize ni watu wangapi ulikuwa unawafahamu leo hawapo duniani? Wewe umeshinda Mungu kakuweka duniani ili uendelee kushinda… soma zaidi

a.gif Jinsi ya kutengeneza Labania Za Maziwa

Maziwa ya unga - 2 vikombe.. soma zaidi

a.gif Simulizi ya mapenzi

SIMULIZI, hii iwasute na kupatwa na hofu ya mungu nyote mlio ktk mahusiano/ndoa yenu… soma zaidi

a.gif Ukubwa wa uume si kigezo cha kumridhisha mpenzi wako

Utajuaje kuwa ni kubwa au ndogo? Obviously ni kwa kujipima….lakini wanaume wengi wanapenda au hata kujisifia kuwa wao ni wakubwa, wakidhani ni moja ya sifa au hitaji la muhimu la wanawake… soma zaidi

uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png

.

uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png
mtu.gif
picha-kali.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.