Tafuta

Kutana na mabesti zako wa shule hapa Wewe pia ni besti wao mzuri sana

πŸ‘‰SOMA ZAIDI HAPA...

πŸ‘‰ Jinsi ya kujumuisha miti shambaniπŸ‘‡βœ”

Upandaji wa miti unalenga kupunguza madhara yanayotokana na uharibifu wa misitu, pamoja na kutumia ardhi kupita kiasi.

Uoto wa asili kama hautaingiliwa na shughuli za kibinadamu, ni mwanzo mzuri wa uwiano wa maji. Miti na vichaka ni kiashirio kizuri cha maji katika ukanda wowote. Katika ukanda wa tropiki wenye mvua nyingi, misitu yenye mvua nyingi na virutubisho vinavyotokana na mimea na wanyama vina nguvu zaidi. Kwenye ukanda wenye mvua kidogo, miti hupukutisha majani wakati wa kiangazi, hivyo kufanya uzalishaji wa mimea kuwa hafifu. Sehemu yenye mvua hafifu miti hunyauka, wakati ukanda wa savanna na miti hutawala zaidi.

Miti ni sehemu muhimu ya uwiano wa maji

Inahifadhi maji kwenye ukanda wa mizizi, kukinga udongo usikauke, kujenga tabaka la udongo, na kusaidia kuhifadhi maji. Matandazo yanayotokana na majani ya miti hukusanya matone ya mvua na kuhifadhi kwa muda, kuzuia mmomonyoko wa udongo, pia kuchuja maji yanayoingia ardhini taratibu. Miti hurudisha maji kwenye mzunguko kwa njia ya mvuke, na kuchangia katika kuunda mawingu ya mvua.

Endapo miti ikiondolewa, maji yote yataondoka na kupotelea ardhini kisha kuondoka kabisa kwenye mzunguko, huku yakichukua virutubisho na tabaka jembamba la udongo. Utafiti wa misitu na mbinu ya kujumuisha miti na vichaka kwenye mashamba ya kilimo, imekuwa mbinu muhimu ya kuzuia uharibifu wa udongo.

Weka nafasi nzuri ya miti kwenye shamba lako.

Miti kwenye shamba la mazao husaidia kurekebisha hali ya hewa, kuzuia maji kutiririka kwa kasi, kuhifadhi udongo na maji, kutoa malighafi zinazo oza kwa ajili ya udongo, na kuweka kivuli kwa ajili ya mimea. Pia ni chanzo cha chakula, malisho, nishati, na nguzo. Kutegemeana na aina ya miti na mazao yaliyopandwa, kwa kawaida hupandwa kwa nafasi ya mita 8 mpaka 10 au zaidi, ili kupunguza ushindani. Mizizi mirefu, na miti inayoongeza nitrojeni kwenye ardhi inapendekezwa zaidi.

Mbali na Lusina leucocephala, ambazo hazistawi vizuri katika ukanda wenye ukame, Sesbania sesban, Crotalaria grahamiana, Tephrosia vogelii, na Gliricidia sepium inapendekezwa, lakini miti ya matunda au yenye kokwa inafaida zaidi.

Mfano mzuri ni:
β€’ Miti ya matunda katika bustani ya nyumbani.
β€’ Miti ya kivuli katika shamba la kahawa, ina faida zaidi. Inazuia madhara yanayoweza kusababisha kutokuchanua kwa mimea katika majira ya mwaka. Hii inaweza kuongeza maisha ya mibuni mara mbili zaidi! Kwenye sehemu za miinuko, inasaidia kudhibiti mmomonyoko wa ardhi pia.
β€’ Grevillea robusta ni miti mizuri sana ya kivuli shambani mwako.

Tawanya miti kwenye shamba lako

Kwenye njia hii ya asili, miti huhifadhiwa kwa ajili ya mifugo kujitafutia malisho, kivuli, na mara nyingine kwa ajili ya matumizi mengine. Miti jamii ya mikunde ambayo ina kiasi kikubwa cha protini hufanya mifugo kufidia virutubisho wanavyokosa wakati wa kiangazi, na kusaidia kuongeza uzalishaji wa maziwa.

Uchochoro wa mazao

Kulima kwa uchochoro au mseto wa miti hufanyika pamoja na zao la msimu. Mbinu hii inafaa zaidi kwenye udongo wenye unyevu mwingi, lakini ukiwa na tatizo la rutuba. Miti ya Sesbania sesban inapopandwa kwenye shamba la nafaka husaidia kuongeza uzalishaji wa mahindi. Miti ni lazima itunzwe vizuri na kukatiwa mara kwa mara. Matawi yanayokatwa hutumika kulisha mifugo, kama matandazo kwenye shamba la mahindi kuboresha rutuba kwenye udongo, kufifisha magugu, na kwa ajili ya kuni, au nguzo. Kwa bahati mbaya, kuna ushindani mkubwa baina ya aina ya miti ya mbao na mazao kwenye eneo kame.

Uzio

Mstari wa miti au vichaka vinavyopandwa kando kando ya mipaka ya shamba. Hata hivyo huu ni utamaduni wa zamani sana, aina mbalimbali za mimea zinaweza kutumika. Endapo itapandwa kwa kusongamana, inaweza kusaidia kuzuia wanyama kuingia kwenye mazao. Fito au matawi yaliyokufa inaweza kusimikwa katikati yake, au waya unaweza kutumika kuweka uzio. Inatoa kuni kwa matumizi ya nyumbani, malisho, na kivuli kwa ajili ya mazao na wanyama, kuzuia upepo, matawi yaliyokatwa yanaweza kutumika kutengeneza uzio pia.

Akiba ya malisho

Majani ya miti husaidia wakati kuna uhaba wa malisho hasa wakati wa kiangazi. Ulishaji wa virutubisho mbadala vinavyotokana na Calliandra, Leucaena diversifolia, Gliricidia sepium, na vinginevyo huongeza uzalishaji na ubora wa maziwa kwa wanyama wa maziwa, na pia hupunguza gharama ya chakula kwa ajili ya ng’ombe wa maziwa. Lisha kiasi cha asilimia 30 ya majani kutoka kwenye miti ya malisho.

πŸ™‰πŸ™‰πŸ™‰Usisahau kushare posti hii kuhusu (Jinsi ya kujumuisha miti shambani).πŸ‘ Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasomeπŸ’―βœ”

Tafuta ndugu zako wa damu hapa Unawapata hapa moja kwa moja

πŸ‘‰SOMA ZAIDI HAPA...

Slide2-utotoni.GIF

.