Kichekesho%20Kipya Usikose 📕Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE👧👗👠 Kinamwelezea🔎Mwanamke🔍 kinagaubaga✔
👉Bofya hapa KuchukuaKizuri

.

👉 Jinsi ya kufuga vizuri kuku wa kienyeji

UFUGAJI BORA WA KUKU WA KIENYEJI

Idadi ya wanyama wanaofugwa kwa chakula imezidi ile ya binadamu zaidi ya mara mbili kote ulimwenguni. Kuna maelfu ya wanyama kote duniani ilihali ni wachache tu wanaoweza kufugwa. Kati ya hawa wanyama, ni aina nne (Ng'ombe, kondoo, mbuzi na kuku) wanaochukua asilimia 95% ya wanyama wote wanaofugwa. Wanyama hawa hupatikana katika nchi za hari kwenye nyanda za chini. Lakini kati ya mifugo hawa, kuku ni maarufu katika nchi za hari na hata kote ulimwenguni.
Lengo la makala haya ni kutoa maelezo ili kusaidia wafugaji wa kiwango kidogo katika nchi
zinazostawi, katika kupunguza umaskini. Sehemu ya kwanza (I) itatoa maelezo kuhusu ufugaji na
hasa ufugaji wa kuku, Sehemu ya pili (II) itaangazia maswala yafuatayo katika kuinua hali ya uchumi
kwa kufuga kuku:
1. Kuendeleza ufugaji wa kuku za kienyeji kwa kutumia njia zisizohitaji gharama nyingi.
2. Kutafuta mbinu na njia muafaka za kuzalisha viwango vya kuku bora kwa njia ya kiasili.
3. Matumizi ya njia za kiasili au zile zisizo gharimu pesa nyingi kutibu na kuzuia magonjwa ya
kuku.

SEHEMU YA I: MAELEZO KUHUSU UFUGAJI WA KUKU KATIKA NCHI. ZINAZOENDELEA

NAFASI YA MIFUGO

Licha ya kukosa mashamba makubwa ya kuendeleza ufugaji wa ng'ombe, jamii nyingi katika nchi za
hari (tropics) hupata nafasi ya kufuga kuku kwa kiwango kidogo. Idadi ya wanyama wanaofugwa
huongezeka sambamba na ile ya watu. Idadi ya watu inapoongezeka ndipo ile ya mifugo huzidi.
Idadi kubwa ya watu huhitaji chakula kingi na matumizi huongezeka, hivyo basi watu hufanya bidii
kuzalisha chakula na mapato kutoka kwa shamba.
Ufugaji wa ng'ombe na wanyama wanaohitaji lishe kwa wingi huhitaji kiasi kikubwa cha shamba ili
kupanda mimea na lishe la mifugo. Ukilinganisha na ufugaji wa kuku, utahitaji mabaki ya vyakula
na sehemu ndogo ya shamba. Ufugaji wa kuku umeweza kunawiri hata pasipo fedha.
Katika nchi za hari ufugaji wa kienyeji hautahitaji kazi nyingi, kazi hii hufanywa na akina mama na
watoto. Kwa kawaida katika nchi hizi kazi nyingi za nyumbani hutekelezwa na mama. Vyakula vya
kuku vyaweza kutoka kwa: 1) Mabaki ya chakula, 2) Mabaki ya mimea, 3) Mabaki kutoka jikoni
na 4) Vyakula vya kujitafutia (kwa mfano kwekwe, mbegu, wadudu, nyongonyongo, n.k). Mfumo
wa kufuga kuku kwa njia ya kienyeji hutumia viungo vinavyopatikana kwa urahisi na kuimarisha hali
ya kiuchumi na chakula bora kwa jamii.
Ni muhimu sana kufuga mifugo hata ikiwa ni kwa kiwango kidogo kwa sababu ya 1) Chakula bora
na kuongeza mapato ya jamii kwa viwango vya kuridhisha; 2) Mifugo ni hakiba au banki, faida yake
huzaana tu kama riba ya benki; 3) Mifugo yaweza kuuzwa ili kugharamia karo ya wanafunzi,
malipo ya hospitali, gharama nyingine za nyumbani na hata shambani; 4) Kwa matumizi ya kijamii
(kwa mfano kulipia mahari, shughuli za kidini, n.k); 5) Mifugo husaidia katika kukabili wadudu,
kwekwe na kuimarisha rutuba kutokana na mbolea ya kinyesi. Ni bayana kwamba mifugo ni
muhimu sana kwa mkulima yeyote yule

Usikose 📕Kitabu cha Mbinu za Kilimo Bora Cha Mboga🌿🍅.

Kina kurasa 100 na utaalamu wa mazao zaidi ya 10

<<Bofya hapa kuchukua>>

UMUHIMU WA UFUGAJI WA NJIA YA KIENYEJI

Ufugaji wa kuku katika nchi zinazostawi waweza kugawanywa mara mbili:
1) Ufugaji wa kitamaduni au kienyeji pasipo kuwepo gharama, na
2) Ufugaji wa kisasa unaohitaji fedha nyingi. Ufugaji wa viwango vikubwa kwa kuzingatia mfumo wa kisasa ni maarufu katika kuzalisha kuku wa nyama na wale wa mayai. Mfumo huu hujumuisha asilimia ndogo sana ya aina ya ufugaji.
Itafahamika kwamba mfumo wa kisasa haujaadhiri ule wa kienyeji. Idadi kubwa ya watu katika nchi
za hari hutegemea mfumo wa kienyeji kwa nyama na mayai.
Mfumo wa kisasa huhitaji pesa nyingi za kununua vyakula vya kuku. Aidha mfumo wa kisasa huhitaji kazi nyingi ili kutekeleza. Mfumo wa kisasa
umefaulu katika nchi zilizostawi kutokana na hali nzuri ya kiuchumi katika kuzalisha (kuku wa hali
ya juu, kuangua vifaranga kwa stima, vyakula vilivyo na madini mengi, vifaa na zana za mashine,
utaalamu wa hali ya juu n.k). Haitafaa sana kuanzisha mfumo kama huu katika vijiji vya mataifa
yanayostawi.
"Mageuzi" katika ufugaji (kuambatanisha mfumo wa kisasa pamoja na ule wa kienyeji) yamefanyiwa
majaribio katika mataifa yanayostawi tangu miaka ya 1950. Matokeo ya kuku wapatao 200 hadi 300
kwa shamba moja hayajawai kufaulu. Hasara imepatikana na waweza kuona nyumba zilizokuwa na
kuku bila chochote, pesa nyingi zimepotea na kuku hawapo.
Mfumo wa kienyeji ni bora (Katika hali ya kiuchumi) iwapo idadi ya kuku haitazidi kuku 50. Ni
rahisi kuweza kuwatunza kuku, kwani hakuna gharama nyingi. Iwapo vyakula au zana za kisasa
zitanunuliwa, basi haitakuwa kwa viwango vikubwa. Mazao ya nyama na mayai yataleta faida.
Sehemu nyingi katika mataifa yanayostawi hakuna stima, katika nchi za hari, ufugaji kwa kiwango
kidogo umeweza kufaulu na kuimarisha uchumi.

Usikose 📕Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE👧👗👠.

Kinamwelezea🔎Mwanamke🔍 kinagaubaga✔

<<Bofya hapa kuchukua>>

FAIDA ZA UFUGAJI WA KUKU KWA NJIA YA KIENYEJI

Faida za uzalishaji kuku ili kuimarisha uchumi kwa njia hii zimepuuzwa na viongozi na wafadhili.
Kuku huleta faida kwa jamii kama tulivyoona katika sehemu ya I. Zaidi ya hayo, ufugaji wa kuku waweza kuimarishwa pasipo gharama nyingi ukilinganisha na mifugo wengine.
· Hutupatia fedha kwa kuuza nyama na mayai
· Mayai ni chakula kilicho na madini muhimu na kisicho ghali katika soko lolote. (madini kama methionine na cystine), madini haya ni muhimu sana kwa afya ya watu hasa watoto wachanga. Pia hutupatia protini.
· Kinyesi cha kuku ni mbolea safi
· Kiwanda asilia cha kutotoa vifaranga
· Gharama za kuanzisha na kuendeleza ni nyepesi
· Kitoweo chepesi na rahisi kwa wageni, kitoweo hakihitaji hifadhi hutumika mlo mmoja au miwili na kumalizika
· Jogoo hutumika kama saa inapowika
· Manyoya ya kuku hutumika kutengenezwa mapambo mbalimbali, mito na magodoro
· Kuku wanahisimu wadudu waharibifu
Kuku ndiye mnyama wa kipekee anayeweza kuishi mahali popote hapa ulimwenguni bila kuadhiriwa
na viwango vya hali ya hewa. Ufugaji wa kuku ndio shughuli inayofanyika kwa wingi duniani kuliko ufugaji wa aina yeyote. Kuku hunawiri vyema katika nchi za hari kutokana na uwiano uliopatikana wakati wa mwanzo binadamu alipofuga Asian jungle fowl aina ya kuku-mwitu. Mayai pia yaweza kuhifadhiwa kwa urahisi na huchukua nafasi ndogo kuliko aina ya bidhaa zozote za mifugo. Mayai yaweza kuwekwa mahali kwa muda mrefu bila kuhitaji barafu. Hautahitaji kuhifadhi kuku kwa njia yoyote, kwani nyama yake hupatikana pale unapohitaji kwa kuchinja.

Upungufu wa kuku wa kigeni ukilinganisha na wale wa kienyeji ni kama ufuatao:

• Kuku wa kigeni hawawezi kukalia na kuangua mayai, hivyo basi wahitajika kununua vifaranga (gharama);
• Vifaranga wa kigeni huhitaji utunzaji maalum na vyakula maalum (gharama);
• Kuku waliozalishwa kwa njia ya kisasa huhitaji chakula kingi ili kutaga mayai (gharama);
• Kuku wa kisasa huhitaji zaidi kuchanjwa dhidi ya magonjwa (gharama)ukilinganisha na wa kienyeji (japo nao huhitaji chanjo);
• Kuku wa kutaga mayai huhitaji mwangaza wa stima (saa 14 kwa siku) ili kutaga mayai (gharama)
Kwa kuongezea, rangi ya nyama na mayai ya kuku wa kienyeji huvutia kuliko ile ya kuku wa kisasa.
Hivyo basi jaribu kuendeleza na kuhimiza ufugaji wa kuku za kienyeji.

Iwapo mkulima ana jogoo mmoja na kuku kumi na mbili, basi kila mwezi waweza kupata kuku
akikalia mayai 10-12 kwa mwezi (mayai yote kwa wakati mwingi hayataanguliwa) kuna hakikisho la
kupata vifaranga vinne kila mwezi. Kuku mzima atachukua miezi minne kuchunga vifaranga
walioanguliwa. Kwa hivyo, kati ya kuku wote kumi na mbili kila mara kutakuwa na kuku wanne
wakitunza vifaranga, huku wale wengine wanane wakitaga mayai.
Kuku waliofugwa kwa njia ya kitamaduni hupata vyakula vyao kwa kutafuta mbegu, wadudu
nyongonyongo, n.k; Lakini kuku hawa hukosa vyakula vya kutosha vilivyo na nguvu ili waweze
kutaga mayai. Vyakula vya kutoa nguvu daima huwa ni haba.

Waweza kuwalisha kuku kwa nafaka ili wapate chakula cha nguvu (mfano kilo moja ya nafaka
iliyopondwa kila siku kwa kuku 10), nafaka hii yapaswa kuwa kavu. Vifaranga wapewe kiasi kidogo
cha nafaka au mchele wiki za kwanza. Kuku wanaolishwa nafaka baada ya kujitafutia chakula nje
huongeza idadi ya mayai (kutoka asilimia 20-25% hadi 40-50%). Kuna umuhimu wa kuhifadhi
nafaka kama lishe badala ya kuuza kwani utapata mayai mengi ambayo baadaye utaweza kuuza.
Hautahitaji kununua vyakula vya protini kwani kuku hujitafutia lishe la protini.
Ikiwa hauna nafaka, waweza kutumia vyakula vya mzizi au ndizi. Vyakula vya aina hii hata hivyo,
huwatatiza kuku wanapovitonogoa, kiwango cha mayai sio kikubwa kama cha wale wanaolishwa
nafaka.
Kwa kuwalisha kuku kwa nafaka utapata hakikisho la mayai manne kwa siku kutoka kwa wale kuku
wanane. Iwapo hakuna nafaka, kati ya kuku wanane wanaotaga utapata mayai mawili tu kwa siku.
Ni bora kutumia nafaka hii kama lishe kuliko kuuza na hatimaye kununua vyakula vya dukani.
Kuku kumi na mbili na jogoo mmoja wanaolishwa kwa kilo moja ya nafaka kila siku waweza
kuelezwa hivi:
• Waweza kuuza kuku wanne kila mwezi na kujaza pengo hilo na wale vifaranga (vifaranga
wanne huanguliwa kila mwezi) na
• Dazani kumi za mayai kila mwezi (mayai manne kila siku).
Kwa mwaka mmoja waweza kukadiri ile faida utakayopata na vile hali ya kiuchumi yaweza
kuinuliwa katika mataifa yanayostawi.

Hata hivyo faida hii haitaafikiwa iwapo magonjwa
hayatazuiwa au kukabiliwa kama ifuatavyo.

Usikose 📕Kitabu cha Mbinu za Kilimo Bora Cha Mboga🌿🍅.

Kina kurasa 100 na utaalamu wa mazao zaidi ya 10

<<Bofya hapa kuchukua>>

TEKELEZA UTARATIBU WA KUZUIA MAGONJWA

Magonjwa ndio husababisha hasara katika mfumo wa ufugaji wa kuku. Kuku waliochanjwa dhidi ya
magonjwa hudumisha afya bora. Jaribu kila mara kuzuia magonjwa, kwani kuzuia ni bora kuliko
kuponya. Kinga yaweza kutolewa mara kwa mara (kila baada ya miezi mitatu) dhidi ya magonjwa
yafuatayo:

Ugonjwa wa Newcastle

Ugonjwa huu ndio huadhiri kuku na kusababisha hasara katika nchi za hari. Virusi vya ugonjwa huu
huenea kwa kasi na rahisi kiasi cha kusababisha vifo kwa asilimia 100%. Dalili za kwanza ni shida
ya kupumua na kung'amua hewa, sauti kama ya kikohozi na kutokwa mate. Kinyesi chaweza kuwa
na rangi ya kijani kibichi. Hadi sasa hakuna dawa.
Waweza kuzuia ugonjwa huu kwa kutoa chanjo. Dawa za chanjo hupatikana kote ulimwenguni hata
katika nchi za hari kwenye vipimo vya vitone mia moja. Madawa haya yaweza kuhifadhiwa kwa
muda. Waweza kuweka kwa wiki moja mbali na jua au joto kali (Chanjo hii ni ya kipekee, kwani
aina nyingine ya chanjo huwekwa kwa friji). Waweza kutoa chanjo kwa kutia vitone kwenye
mdomo. Kuku wote (wakubwa kwa wadogo) wapaswa kupewa chanjo baada ya kila miezi mitatu.

Minyoo

Minyoo kama chango (roundworms) na tegu (tapeworms) huadhiri kuku wa kienyeji. Kuku hukosa hamu ya chakula, mayai hupungua na magonjwa mengine hushambulia. Ni bora basi kutoa minyoo.
Mchanganyiko wa madawa ya aina tatu ndio hutumiwa kuangamiza minyoo, madawa haya ni
piperazine, phenothiazine na butynorate. Madawa haya hupatikana kama vidonge (tumia kidonge 1
kwa kuku mzima na 1/2 kwa vifaranga). Iwapo hautapata dawa hii, waweza kutumia Panacur au
dawa nyingine ya kuangamiza minyoo. Wapatie kuku dawa ya minyoo kila baada ya miezi mitatu.

Wadudu

Wadudu kama chawa au utitiri husumbua kuku katika ufugaji wa kienyeji. Chawa au utitiri
husababisha harara ya ngozi, kuku walio adhiriwa hupata shida na kukosa usingizi. Hali hii
hupunguza kiwango cha mayai na uzito wa kuku.
Tumia asilimia 5% ya unga wa malathion kwa kupulizia kuku (puliza kwa chupa uliyo toboa
mashimo) pulizia kila kuku ili kuzuia chawa na utitiri (kilo moja ya unga huu yaweza kutibu kuku
150). Pulizia dawa hii baada ya kila miezi mitatu, waweza kupuliza kwa wakati mmoja wa kutoa
chanjo na dawa zilizotajwa hapo juu. Puliza unga huu pia kwenye viota vya kuangulia mayai.
Waweza kutayarisha 5% ya malathion kwa kuchanganya 25% ya unga wa malathion (kiwango cha
kilimo) na sehemu nne za jivu kutoka jikoni.

Magonjwa ya mapafu

Magonjwa ya mapafu huadhiri njia inayopitisha hewa na kuambatanisha mate na sauti kama ya
kikohozi. Ugonjwa huu huenea polepole. Uambukizanaji pia hutokea kwa polepole na vifo sio kwa
wingi. Hata hivyo, kutaga mayai na uzito hupungua. Shida hii yaweza kusambaa hata kutoka mahali vifaranga huanguliwa hadi pale walipouzwa.
Tylosin19 ndio dawa inayoweza kutibu magonjwa ya mapafu. Kiasi cha 35mg ya tylosin hutosha
kuku mmoja (kiwango hiki hufaa kuku na hata vifaranga) dawa hii husimamisha madhara kutokana
na magonjwa ya mapafu. Tibu kuku kila baada ya miezi mitatu, waweza kutekeleza kwa wakati
mmoja wa kutoa kinga na kuangamiza minyoo. Tylosin hupatikana kwa pakiti ndogo ya 4gm.
Waweza kutayarisha dawa hii kwa kutumia maji na 35gm ya tylosin (gramu nne kwa vikombe viwili
vya maji), kiasi hiki chaweza kutolewa kwa vitone kwa kila kuku.

Usikose 📕Kitabu cha Mbinu za Kilimo Bora Cha Mboga🌿🍅.

Kina kurasa 100 na utaalamu wa mazao zaidi ya 10

<<Bofya hapa kuchukua>>

KWA UFUPI KUHUSU KUKU WA KIENYEJI (SUMMARY)

Kabila za Kuku

Si rahisi kupata kabila halisi (pure breed) au kizazi halisi (pure line) za kuku wa kienyeji kutokana na mwingiliano wa vizazi kati ya aina mbalimbali za kuku hao. Lakini hata hivyo baadhi ya kuku wa kienyeji wanaweza kutambuliwa kutokana na maumbile yao kwa mfano

1. Kuchi

Warefuna wenye kusimama mgongo ukiwa wima
Wana manyoya machache mwilini na vilemba vyao ni vidogo
Majogoo huwa na wastani wa kilo 2.5 na mitetea kilo 1.8
Mayai gram 45

2. Ching'wekwe (Umbo dogo)

Hupatikana zaidi Morogoro na umasaini
Majogoo kilo 1.6
Mitetea kilo 1.2
Yai gram 37
kuku hawa wanafaa sana kwa biashara ya mayai kwa kuwa hutaga mayai mengi sana.

3. Umbo la Kati

Majogoo kilo 1.9
Mitetea kilo 1.1
Mayai gramu 43
Hukua upesi na hupata kinga upesi baada ya kuwachanja dhidi ya ugonjwa wa Mdondo (New Castle)

4. Singamagazi

Hupatikana zaidi Tabora
Majogoo wana rangi ya moto na mitetea rangi ya nyuki
Majogoo kilo 2.9
Mitetea kilo 2
Mayai gramu 56

5. Mbeya

Wanapatikana Ileje Mbeya na asili yao ni Malawi
Mjogoo kilo 3
Mitetea kilo 2
Mayai gramu 49
Uwezo wao wa kuatamia mayai na kuangua ni mdogo sana ukilinganisha na kuku wengine

6. Pemba

Maumbo ya wastani na miili myembamba
majogoo kilo 1.5
mitetea kilo 1
mayai gramu 42

7. Unguja

Hawatofautiani sana na wa Pemba
Vilemba vyake ni mchanganyiko- vidogo an vikubwa
Majogoo kilo 1.6
Mitetea kilo 1.2
Mayai gramu 42

Usikose 📕Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE👧👗👠.

Kinamwelezea🔎Mwanamke🔍 kinagaubaga✔

<<Bofya hapa kuchukua>>

SIFA ZA KUKU WA KIENYEJI

  • Wastahimilivu wa Magonjwa
  • Wana uwezo wa kujitafutia chakula
  • Huatamia, kutotoa na kulea vifaranga
  • Wanastahimili mazingira magumu(ukame, baridi n.k)
  • Nyama yake ina ladha nzuri

KATIKA KUWAENDELEZA KUKU WA KIENYEJI NI VYEMA

Wajengewe nyumba bora
Wapewe kinga dhidi ya ugonjwa wa Mdondo (New Castle), Ndui (Fowl Pox) pamoja na kinga ya minyoo.
Malezi bora ya vifaranga
Kuwapatia chakula cha ziada pamoja na maji ya kunywa ya kutosha.

NYUMBA BORA

Eneo inapojengwa nyumba au banda la kuku liwe
Linafikika kwa urahisi
Limeinuka juu pasituame maji
Pasiwe na pepo zinazovuma
Vifaa kama miti, nyasi, makuti, fito, udongo mabanzi ya miti, cement, mabati n.k
Sifa za Nyumba Bora ya Kuku
Paa imara lisilovuja
Kuta zisiwe na nyufa
Sakafu isiwe na nyufa
Madirisha ya kutosha kupitisha hewa
Iwe na mlango wa kuingia kufanya usafi
Iwe na ukubwa (nafasi) unaolingana na idadi ya kuku. Wastani wa kuku 10-15 kwa mita moja mraba
Mambo muhimu ndani ya nyumba
Chaga za kulalia kuku
Sakafu iwekwe maranda (wood shavings), makapi ya mpunga, n.k
Viota vya kutagia mayai sentimita 35x35x35 na idadi ya viota iwe nusu ya idadi ya kuku waliofikia hatua ya kutaga na viwekwe sehemu iliyojificha (faragha)

Usikose 📕Kitabu cha Mbinu za Kilimo Bora Cha Mboga🌿🍅.

Kina kurasa 100 na utaalamu wa mazao zaidi ya 10

<<Bofya hapa kuchukua>>

UATAMIAJI WA MAYAI

Kuna njia 2
Njia ya kubuni (incubators)
Asili
Kumuandaa kuku anayeatamia
Weka maranda au majani makavu ndani ya kiota
Anapokaribia kuatamia toa mayai ndani ya kiota pamoja na maranda, hakikisha mikono haina manukato
Nyunyiza dawa ya kuua wadudu (viroboto, utitiri n.k) ndani ya kiota, pia mnyunyizie dawa kuku anayetarajia kulalia mayai
Rudisha mayai kwenye kiota ili kuku aanze kuatamia
Kwa kawaida kuku hulalia mayai yake kwa muda wa siku 21 ndipo huanguliwa

ULEAJI WA VIFARANGA

Kuna njia mbili
Njia ya kubuni
Njia ya asili
Njia ya ASILI
Kuku mwenyewe hutembea na vifaranga akivisaidia kutafuta chakula. Ni vizuri kumtenga kuku mwenye vifaranga katika chumba chake pekee ili vifaranga wasishambuliwe na kuku wengine hali kadhalika kuwalinda na wanyama na ndege wanaoshambulia vifaranga.

Njia ya KUBUNI

Vifaranga huwekwa kwa pamoja kwenye chumba maalum na kupatiwa joto maalum, chakula pamoja na maji. Tumia taa ya kandili (chemli), umeme au jiko la mkaa na hiyo taa iweke kwenye mzingo(mduara) walipo vifaranga. Pia kuna kifaa kinaitwa Kinondoni Brooder ni kizuri kwa kutunzia vifaranga. Kwa kutumia kifaa hiki kuku wanaweza kunyang'anywa vifaranga vyao mara tu baada ya kutotoa na kuviweka kwenye hii brooder na hao kuku wakaachwa bila vifaranga vyao, baada ya majuma matatu au manne, kuku hao huanza tena utagaji na kuendelea na uatamiaji hadi kutotoa tena. Kwa mtindo huu kuku anaweza kutotoa mara 5-6 badala ya kama ilivyo sasa mara 2-3 kwa mwaka. Vifaranga vikae ndani ya brooder majuma 3-4 na baadaye fungua milango ya brooder kuruhusu vifaranga vitoke na kuzungukazunguka chumbani bila kuvitoa nje kw kipindi cha mwezi mmoja au zaidi kutegemeana na mazingira.

KULISHA KUKU WA KIENYEJI

Kuku mkubwa huhitaji gramu 120 za chakula kwa siku, ni vizuri kuku wanaofugwa huria (free range) kupatiwa chakula cha ziada gramu 30 kila siku nyakati za jioni.
Kuku walishwe
Mizizi-mihogo, viazi vitamu, mbatata, magimbi, n.k
Nafaka-mahindi, Mpunga, Mtama, Ulezi na Pumba za nafaka zote
Mboga-Mikundekunde, nyanya, milonge, majani ya mapapai
Matunda-Mapapai, maembe, n.k
Mbegu za Mafuta-Karanga, ufuta, mashudu ya pamba, alizeti, n.k
Unga wa dagaa
Maji

KUCHANGANYA CHAKULA CHA KUKU

Pumba………….kilo20
Mashudu ya Pamba n.k…kilo 3
Dagaa iliyosagwa………kilo 1
Unga wa majani uliokaushwa kivulini na kusagwa……..kilo 2
Unga wa Mifupa ……….kilo 0.25
Chokaa ya mifugo ……..kilo 0.25
Chumvi……………………gramu 30
Vichanganyio/Premix…gramu 25

KUPANDISHA KUKU

Uwiano wa mitetea na jogoo ni mitetea 10-12 kwa jogoo mmoja
Sifa za mtetea ni mkubwa kiumbo, mtagaji mayai mengi, muatamiaji mzuri na mlezi wa vifaranga
Sifa za jogoo ni awe mkubwa kiumbo, miguru imara na yenye nguvu, mrefu, upanga/kilemba kikubwa, awe na uwezo wa kuitia chakula mitetea na awe na tabia ya kupenda vifaranga
Jogoo huanza kupanda akiwa na umri wa miezi 7-10 na kuendelea hadi miaka mitatu na asipande watoto wake
Mitetea huanza kutaga wakiwa na miezi 6-8

Usikose 📕Kitabu cha Mbinu za Kilimo Bora Cha Mboga🌿🍅.

Kina kurasa 100 na utaalamu wa mazao zaidi ya 10

<<Bofya hapa kuchukua>>

MAGONJWA YA KUKU

1. Mdondo/New castle

Virus vinavyosababisha ugonjwa huu huenezwa kwa hewa

Dalili

Kuhalisha choo cha kijani na njano

Kukohoa na kupumua kwa shida
Kupinda shingo kwa nyuma
Kuficha kichwa katikati ya miguu
Kukosa hamu ya kula na kunywa
Idadi kubwa ya vifo hadi 90%

Kinga

Chanjo (New Castle vaccine) kwa mpango wa siku 3, wiki 3, miezi 3
Epuka kuingiza kuku wageni
Choma au fukie mizoga ya kuku waliokufa kwa ugonjwa
Zingatia usafi wa mazingira

NDUIYA KUKU/ FOWL POX

Virus huambukizwa kupitia jeraha au mbu

Dalili

Vidonda vyenye utando wa kahawia/purple kwenye sehemu zinazoonekana
Kukosa hamu ya kula
Vifo vingi

Kinga

Chanja vifaranga wanapofikia mwezi 1-2 kwa kutumia chanjo ya Fowl pox vaccine
Epuka kuingiza kuku wageni
Zingatia usafi wa mazingira

HOMA YA MATUMBO/FOWL TYPHOID

Kuharisha kinyesi cha kijani na nyeupe
Kuku hukosa hamu ya kula
Kuku hukonda
Vifo hutokea kidogo kidogo kwa muda mrefu
Kinyeshi hushikamana na manyoya

Tiba

Dawa aina ya antibiotic, sulfa na vitamini
Kinga

Usafi

Fukia mizoga
Usiingize kuku wageni
Chinja kuku wote mara ugonjwa huu ukiingia na safisha banda, pia pumzika kufuga kwa miezi 6

MAFUA YA KUKU/INFECTIOUS CORYZA

Hutokana na bakitelia na hushambulia hasa kuku wakubwa

Dalili

Kuvimba uso
Kamasizilizochanganyikana na usaha unaonuka
Macho huvimba na kutoa machozi na pengine upofu
Hukosa hamu ya kula
Mbawa huchafuka na kutoa harufu mbaya

Tiba

Dawa za Antibiotic, sulfa na vitamini

KUHALISHA DAMU/COCCIDIOSIS

Husababishwa na vijidudu vya Protozoa

Dalili

Kuharisha damu
Manyoya husimama
Hulala na kukosa hamu ya kula

MINYOO

Dalili

Kunya minyoo
Hukosa hamu ya kula
Hukonda au kudumaa
Wakati mwingine hukohoa
Tiba
Dawa ya minyoo/Pipeazine citrate kila baada ya miezi mitatu

WADUDU

Viroboto, chawa, utitiri

Dalili

Kujikuna na kujikung'uta
Manyoya kuwa hafifu
Rangi ya upanga kuwa hafifu
Ngozi kuwa nene, ngumu na yenye magamba yanayodondoka kama unga
Kuzuia
Ziba mipasuko sakafuni na kwenye kuta za banda
Fagia banda mara mbili kwa wiki
Nyunyiza majivu au chokaa mara moja kwa wiki mara baada ya kufagia
Choma masalia ya mayai yaliyoanguliwa
Nyunyiza dawa kwenye viota
Weka maranda, majani makavu, makapi ya mpunga ya kutosha sakafuni ndani ya banda la kuku
Fuata kanuni za chanjo
Tenga kuku wagonjwa wakae mbali na kuku wazima

UPUNGUFU WA VIINI LISHE KWENYE CHAKULA KWA KUKU

Dalili

Kuku hupungua damu, uzito na kudumaa
Mifupa huwa laini na kutokuwa imara
Hutaga mayai yenye gamba laini na madogo
Huwa na manyoya dhaifu

🙉🙉🙉Usisahau kushare posti hii kuhusu; Jinsi ya kufuga vizuri kuku wa kienyeji.💯✔ Share facebook, twitter n.k bila kusahau WhatsApp, share wengine nao wafaidike!👍

Usikubali kupitwa na 📕Kitabu cha Vichekesho Vikuu Vikali 300+✔. Kina kurasa 270 zenye picha📷 na vichekesh😂 zaidi ya 300💨. 👉Bofya hapa Kuchukua👈

🐼 Endelea kusoma kuhusu;-🙉

.

Kichekesho%20Kipya Usikose 📕Kitabu cha Vichekesho Vikuu Vikali 300+✔ Kina kurasa 270 zenye picha📷 na vichekesh😂 zaidi ya 300💨👉Bofya hapa KuchukuaKizuri

.

Kichekesho%20Kipya Usikose 📕Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE👧👗👠 Kinamwelezea🔎Mwanamke🔍 kinagaubaga✔👉Bofya hapa KuchukuaKizuri

.

Kichekesho%20Kipya Usikose 📕Kitabu cha Mbinu za Kilimo Bora Cha Mboga🌿🍅 Kina kurasa 100 na utaalamu wa mazao zaidi ya 10👉Bofya hapa KuchukuaKizuri

.

📰 Posti nyingine👇

📌 Hii sasa kali kweli kweli! Kisingizio barafu

Wazazi wengine wanaandika *MBWA​MKALI* kwenye geti lao kama binti wao ana miaka 18……inaendelea....

👋soma zaidi kuhusu👉Hii sasa kali kweli kweli! Kisingizio barafu

📌 Jinsi ya kupika Biryani ya mbogamboga

Biriani ni miongoni mwa vyakula ambavyo ni nadra sana kupikwa katika familia nyingi tofauti na vyakula vingine. Inawezekana ni kutokana na watu wengi kutoelewa namna ya kuoika chakula hiki kutokana na kuhitaji viungo vingi ambavyo huwapa usumbufu wapishi.
Kuna aina mbalimbali za upishi wa biriani ambapo mara nyingi hutofautiana kutokana na viungo vinavyotumika katika upishi.
Biriani la mbogamboga ni miongoni mwa aina hizo za upishi. Chakula hiki kinaweza kuliwa na kila mtu hususan wale wasiotumia nyama wala samaki…..inaendelea....

👋soma zaidi kuhusu👉Jinsi ya kupika Biryani ya mbogamboga

📌 Jinsi ya kupika mboga ya majani ya mashona nguo

Mashonanguo mkono 1
Tui la nazi kikombe 1
Karanga zilizosagwa kikombe ½
Mafuta vijiko vikubwa 4
Kitunguu 1
Nyanya ndogo 2
Chumvi kiasi….inaendelea....

👋soma zaidi kuhusu👉Jinsi ya kupika mboga ya majani ya mashona nguo

📌 Angalia anachojibu huyu babu. Wazee wengine bwana

*Babu*: Mjukuu wangu ngoja nikusimulie hadithi ya mimi babu yako kwenye vita ya kagera
*Mjukuu*:Niambie babu
*Babu*:Kwenye vita ya kagera tulienda sehemu tukakamatwa wote askari na maadui wakatuambia chagueni kuuliwa au kubakwa.
*Mjukuu*:Sasa babu wewe ulichagua nn?
*Babu*:Niliuliwa!!!….inaendelea....

👋soma zaidi kuhusu👉Angalia anachojibu huyu babu. Wazee wengine bwana

📌 Mkwe kazua mpya, Hii dunia ina mambo sana

Mama mkwe alimuuliza mkwewe "binti" samahani mbona mtoto hajafanana na mwanangu kabisa?….inaendelea....

👋soma zaidi kuhusu👉Mkwe kazua mpya, Hii dunia ina mambo sana

📌 Sababu za Magonjwa ya Figo na jinsi ya kujikinga

*SABABU ZA MAGOJWA YA FIGO. JIHADHARI NA ONYEKA!.*
Raia wa Ghana wanazidi kufa kwa matokeo ya ugonjwa wa Figo.
*JINSI YA KUONDOKANA NA JANGA HATARI LA UGONJWA WA FIGO:*
*1.Usichelewe kwenda HAJA.* Kutunza mkojo kweye kibofu chako kwa muda mrefu ni wazo baya. Kibofu kikijaa kinaweza kusababisha uharibifu. Mkojo ambao unakaa kwenye kibofu huzidisha bakteria haraka.
Mara mkojo unaporudi nyuma ya njia na Figo, sumu dutu husababisha maambukizi ya figo, pia njia ya mkojo na "nephritis", pamoja na "uremia". Wakati wito asili (unahisi mkojo) fanya hivyo haraka iwezekanavyo.
*2. Kula Chumvi kupita kiasi.* Inatupasa kula Chumvi isiyozidi 5.8 gramu kwa siku.
*3. Kula nyama kupita kiasi.*
Protini ikizidi sana katika mlo wako inadhuru figo zako. Mmeng'enyo wa Protini unazalisha amonia- sumu dutu ambayo ina uharibifu mkubwa kwa figo zako. Nyama nyingi inaleta uharibifu zaidi wa figo.
4. *Unywaji mwingi wa "Caffeins".*
Caffein hutokana na vinywaji vya Soda na vinywaji vingine laini kama Kahawa, Redblue n.k. Hupandisha shinikizo la damu na figo zako kuanza mateso. Unapaswa kupunguza kiwango cha Coke, Pepsi, Red Bull, nk ambavyo hunywa kila siku.
*5. Kutokunywa maji.*
Figo zetu lazima zichakatwe vizuri kutekeleza majukumu yake vizuri. Endapo hatunywi ya kutosha, sumu dutu inaweza kuanza kukusanyika katika damu, kama hakuna kimiminika cha kutosha kutoa kwa njia ya figo. *** Kunywa zaidi ya bilauri 10 za maji kila siku.
Kuna njia rahisi ya kuangalia kama unakunywa maji ya kutosha: Angalia rangi ya mkojo wako; Wepesi wa rangi, ndiyo vzuri.
*6. Kuchelewa matibabu.*
Tibu matatizo yako yote ya kiafya kwa uhakika na uwe unachunguza afya yako mara kwa mara. Wapendwa na wapenzi wangu, hebu tujisaidie wenyewe… Shirikisha wengine, kama unajali. ----
*Pia epuka vidonge hivi, ni hatari sana:*
D- baridi*
Vicks Action- 500*
Actified*
Coldarin*
Cosome*
Nice*
Nimulid*
Cetrizet- D
Hivi vidonge vina Phenyl propanol- amide PPA ambayo husababisha stroke na ni marufuku Marekani.
MWISHO… Tafadhali, kabla ya kufuta, msaidie rafiki yako kwa kumpitishia hii..!
*Inaweza kumsaidia mtu!*
Wasambazie wengi kwa kadiri uwezavyo.
Shirikisha ujumbe huu kwa mpendwa wako.
*Maonyo muhimu ya Afya*
1. Jibu (pokea) simu wito na sikio la kushoto.
2. Usinywe dawa zako kwa maji baridi….
3. Usile milo mizito baada ya saa 11 jioni.
4. Kunywa maji vuguvugu mengi asubuhi na kiasi usiku. Usinywe maji baridi kamwe.
5. Muda bora wa kulala ni kutoka saa 4 usiku hadi saa 10 Alfajiri.
6. Usilale mapema baada ya kumeza dawa au baada ya mlo. Usiku, Kula chakula laini.
7. Usipokee simu yako ikiwa haina chaji. Wakati huo mionzi huwa ina nguvu mara 1000 .
Je, unaweza kuwasambazia watu unao wajali?
Mimi nimeshafanya kwako….!!…..inaendelea....

👋soma zaidi kuhusu👉Sababu za Magonjwa ya Figo na jinsi ya kujikinga

📌 Tenda Wema Uende Zako

Nimekuta panya ana struggle kuingia chini ya mlango wa jirani yangu… Nikagonga mlango Jirani kafungua panya akapenya mi nkaenda zangu….. Tenda Wema Uende Zako!!! Sipendi Ujinga mimi kwanini panya wa watu apate shida….inaendelea....

👋soma zaidi kuhusu👉Tenda Wema Uende Zako

📌 Mbele ya hela binti usharobaro achia mbali

Boy:- hallow
Dem:- hellow
Boy:- ivi jina lako nani vile
Dem:- am miss precious A. K. A dope girl
Boy:-Okay, nmekutumia 50,000 nimeona Jina tofauti ngoja nipige customer care
Dem:-no no baby usipige Ah ah Hapana baby mi naitwa Andongolile Mwakasakafyuka 😂😂😂😂😂….inaendelea....

👋soma zaidi kuhusu👉Mbele ya hela binti usharobaro achia mbali

📌 Mke Mtarajiwa

Mke wangu mtarajiwa, najua uko sehemu
salamanukivuta muda na jamaa mwingine kabla
hatujaoana. Lakini kabla sijakuweka ndani Ninayo
machache ya kukueleza…
.
1. My future wife, Jiandae kuwa mother material
wala sio mom material.. usipaniki!!! ..
ntakuelewesha nachomaanisha, Mke wangu
mpendwa mmeo, ntakuwa father wala sio daddy
kwa watoto wetu, usishangae nitawalea watoto
wetu katika malezi ya tamaduni za kiafrika zaidi,
hivyo kwa hilo ntakuwa conservative. Ningependa
kukuona
ukiwa mother wala sio mom ukawalea watoto
kwa tamaduni za kigeni.
.
2. My future wife, ntakuoa kutokana na uzuri wa
asili uliojaaliwa na Mungu, hivyo bhas usitarajie
kupata wasaa wa kujipachika kope na kucha za
bandia wala mawigi (nywele za marehemu).
.
3. My future wife, huko uliko ni vyema ukaanza
kujifunza kuendesha biashara na kusimamia,
mmeo siamini katika kuajiriwa Bali kujiajiri.
.
4. My future wife Siku tutakayokula kiapo
kanisani, tutafanywa kuwa mwili mmoja, hivyo
bhasi nisingependa tuje kutenganishwa na
password kwenye simu zetu (no passwords).
.
5. My future wife, madhehebu yote hukiri kuwa
MUNGU ni mmoja tu, hivyo bhasi nisingependa
kukushuhudia ukihama madhehebu mbalimbali
kutafuta ukombozi kwa MUNGU yuleyule.
.
MY FUTURE WIFE, msalimie sana huyo
mnayevuta nae muda kwa kwenda $amaki
$amaki, Nyama Choma na Fiesta, mie
ntakupeleka kanisani na kukuweka ndan….inaendelea....

👋soma zaidi kuhusu👉Mke Mtarajiwa

.

📓 Posti za sasa👇

A Jinsi ya kutumia alizeti kama chanzo cha chakula cha mifugo

Alizeti haitoi mailisho pekee, pia inatoa mafuta bora kwa afya ya binadamu na pia malighafi inayotumiwa na nyuki kutengeneza asali…..inaendelea....

👋soma zaidi kuhusu👉Jinsi ya kutumia alizeti kama chanzo cha chakula cha mifugo

A Vituko vinavyoandikwa kwenye daladala

.Huwa naenjoy sana kusoma yaliyoandikwa nyuma ya daladala hasa ninapokuwa kwenye foleni. Misemo maarufu
ya kwenye daladala…..inaendelea....

👋soma zaidi kuhusu👉Vituko vinavyoandikwa kwenye daladala

A Dogo mmoja baada ya kurudi shule akawa anaongea na baba yake

Ka ww

DOGO: baba mi siendi tena shule inaonekana walimu hawana uhakika na majibu yao.
BABA: Kwanini unasema hivyo?
DOGO: juzi walisema 3+4= 7, jana wakasema 1+6=7, halafu leo wanasema 5+2=7 sasa huoni kama wanatuchanganya.

ungekua wewe ungemjibu nini….inaendelea....

👋soma zaidi kuhusu👉Dogo mmoja baada ya kurudi shule akawa anaongea na baba yake

A Je, ukinywa pombe unaongeza damu?

Si kweli.

Pombe haiongezi damu, vitamini wala nguvu. Ukweli ni kwamba unywaji pombe kupita kiasi huvuruga ufyonzaji wa vitamini na madini kutoka kwenye chakula kuingia mwilini.

Vitamini ni muhimu kwa kuimarisha kinga ya mwili ambayo inasaidia kujikinga na magonjwa, pamoja na maradhi kama UKIMWI. Kwa hivyo, unatakiwa uhakikishe unakula matunda na mboga za majani kwa sababu vinakuongezea vitamini…..inaendelea....

👋soma zaidi kuhusu👉Je, ukinywa pombe unaongeza damu?

A SHAIRI: Kama mnataka mali, mtaipata shambani.

1. Karudi baba mmoja,
toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja,
na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja,
ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli iwafae maishani…..inaendelea....

👋soma zaidi kuhusu👉SHAIRI: Kama mnataka mali, mtaipata shambani.

A Siri za mafanikio na Jinsi ya kufanikiwa

Tafuta fulsa kila kona.
Tumia kipaji chako.
Kuwa na nidhamu katika fedha - matumizi mazuri ya pesa, nidhamu kwa watu wanaokuzunguka, usijikweze, usibague jamii, heshimu wote waliokaribu yako nk…..inaendelea....

👋soma zaidi kuhusu👉Siri za mafanikio na Jinsi ya kufanikiwa

A Ninaweza kupata mimba wakati nipo kwenye hedhi?

Ili mwanamke aweze kushika mimba, i inabidi yai lililopevuka likutane na mbegu za kiume. Yai pevu linapokosa mbegu hufa na kwa vile utando kwenye tumbo la uzazi ulishajiandaa kupokea yai lililorutubishwa hubomoka. Kwa pamoja, yai na utando hutoka kama damu kupitia ukeni na i le damu huitwa hedhi.
Hedhi ni dalili, kwamba yai halikurutubishwa na hivyo limeshakufa na kutoka. Kwa kawaida, wakati huo halitakuwepo yai jingine lililopevuka kuweza kurutubishwa na kwa hiyo uwezekano wa kupata mimba hautakuwepo. Lakini, mara chache kuna hitilafu katika mzunguko wa hedhi na yai jingine linakuwepo tayari kwa kurutubishwa, hata ukiwa kwenye hedhi. Kwa hiyo uwezekano wa kupata mimba wakati wa hedhi upo, hata kama ni mdogo…..inaendelea....

👋soma zaidi kuhusu👉Ninaweza kupata mimba wakati nipo kwenye hedhi?

A Huyu mama kweli tishio, mpaka askari wameogopa

Askari wameitwa kwenye nyumba ambayo kuna ugomvi. Wakafika halafu ikabidi waripoti kwa simu yale waliyokuta
Askari: mkuu tumekuja hapa tumekuta mama mwenye nyumba amempiga mumewe chuma cha kichwa na kumuumiza sana….inaendelea....

👋soma zaidi kuhusu👉Huyu mama kweli tishio, mpaka askari wameogopa

A Kali za leo

1. Ati wee ni m-black mpaka ukiingia kwa dinga(gari), dirisha zinakuwa tinted!….inaendelea....

👋soma zaidi kuhusu👉Kali za leo

.

Majarida na vitabu kutoka Ackyshine eBook Shop

Kichekesho%20Kipya Usikose 📕Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE👧👗👠 Kinamwelezea🔎Mwanamke🔍 kinagaubaga✔
👉Bofya hapa KuchukuaKizuri

.

Kichekesho%20Kipya Usikose Jarida la Kilimo Bora cha Bamia Linafafanua Kilimo cha bamia
👉Bofya hapa KuchukuaKizuri

.

Kichekesho%20Kipya Usikose Jarida la Kilimo Bora cha Kabichi Linafundisha kulima kabichi
👉Bofya hapa KuchukuaKizuri

.

Kichekesho%20Kipya Usikose Jarida la Kilimo Bora cha Matikiti Linafundisha ulimaji wa matikiti
👉Bofya hapa KuchukuaKizuri

.

Kichekesho%20Kipya Usikose 📕Kitabu cha Mbinu za Kilimo Bora Cha Mboga🌿🍅 Kina kurasa 100 na utaalamu wa mazao zaidi ya 10
👉Bofya hapa KuchukuaKizuri

.