Kichekesho%20Kipya Usikose 📕Kitabu cha 😂Vichekesho Vikuu Vikali 👍300+✔ kwa Tsh 2,500/= tuu!. Kina kurasa 270 zenye picha na vichekesho 300+.
👉 <<Bofya hapa Kuoda>> Kizuri

.

👉 Je, watu wanaoishi na hali ya ualbino wanaweza kuzaa watoto bila matatizo?

Ulemavu wa watu wanaoishi na ualbino hauingiliani na uwezo
wa kuweza kuzaa. Tuelewe kwamba ulemavu huu uko tu kwenye
ngozi na siyo kwenye via / mfumo wa uzazi. Kwa maana hiyo
basi; Albino anaweza kuzaa watoto wenye afya nzuri. Pia
wanaweza kuzaa watoto wenye ngozi ya kawaida (blackii) kama
mzazi mwenzie hatakuwa amebeba vinasaba vya ualbino.

Je, watu wanaoishi na hali ya ualbino
wanaweza kuzaa watoto wangapi?

Kwa vile Albino hana tofauti na watu wengine inopokuja
kwenye suala la idadi ya watoto wa kuzaa jambo la msingi ni
yeye mwanamke au mwanaume Albino kuzaa idadi aliyojipangia
mwenyewe. Akitia maanani uwezo alio nao wa kuwatunza na
kuwapa mahitaji muhimu.

🙉🙉🙉Usisahau kushare posti hii kuhusu; Je, watu wanaoishi na hali ya ualbino wanaweza kuzaa watoto bila matatizo?.💯✔ Share facebook, twitter n.k bila kusahau WhatsApp!👍

📚Msomaji wangu mpendwa, leo nimekuandalia 📖 📕Kitabu cha 😂Vichekesho Vikuu Vikali 👍300+✔ ambacho nakupa kwa bei ya sawa na bure ya Tsh 2,500/= tuu!🙉🙉🙉 Kina kurasa 270 zenye picha na vichekesho 300+📄📄📄. 👉<<Bofya hapa Kuoda>>👈 ili nikutumie kwenye📧 email yako Leo Leo☑ Usikubali Kukosa.👍💪

🐼 Endelea kusoma kuhusu;-🙉

miss-you-puppy-smiley-emoticon.gif

.

MBINU-YA-KILIMO-BORA-CHA-MBOGA.jpg

Kina kurasa 100 na utaalamu wa mazao zaidi ya 10

Jipatie 📕Kitabu cha 👋Mbinu za Kilimo Bora✔ Cha Mboga🌿🍅 kwa Tsh 2,500/= tuu.
jua%20zaidi%2C%20dont%20delete

.

vichekesho.jpg

Kina kurasa 270 zenye picha na vichekesho 300+

Jipatie 📕Kitabu cha 😂Vichekesho Vikuu Vikali 👍300+✔ kwa Tsh 2,500/= tuu.
jua%20zaidi%2C%20dont%20delete

.

📰 Posti nyingine👇

📌 Utoto raha..!

Leo nimepulizia Air Fresh yenye Harufu ya Pilau nyumbani kwangu sasa watoto wa Jirani wamehamia Mlangoni kwangu ndio wanacheza hapo. Kila nikitoka wananisalimia. Mama yao ndio kanimaliza kabisa nimetoka akaniambia
"Kumbe wewe ni Mpishi mzuri, Hongera"

👋soma zaidi kuhusu👉Utoto raha..!

📌 Ifahamu Saratani ya Tezi Dume, chanzo, Dalili, Uchunguzi na Tiba

Saratani ya tezi dume inashika nafasi ya tatu kwa kusababisha vifo vinavyotokana na kansa kwa wanaume duniani. Pia ni chanzo kikuu cha vifo vinavyosababishwa na saratani kwa wanaume wenye umri wa miaka 70 na kuendelea. Hata hivyo, satarani ya tezi dume kwa sasa inawapata sana wanaume kuanzia miaka 25. Lakini kabla ya kuendelea mbele hebu kwanza tujue tezi dume ni zipi.
Kama tulivyosema neno saratani ni jina la gonjwa ambalo hutokea wakati chembe chembe za uhai au seli katika sehemu fulani ya mwili zinapoanza kukua bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili na kutengeneza vijiuvimbe vidogo vidogo. Kwa kawaida seli huwa zinajigawa, kupevuka na baadaye kufa kwa kufuata taratibu za mfumo wa mwili. Lakini seli za saratani hazifuati mfumo huo. Badala ya kufa, zenyewe huishi muda mrefu kuliko chembe chembe za kawaida na wakati huo huo huendelea kutengeneza seli nyingine na kuwa uvimbe wa saratani au tumour.
Tezi dume linapatikana katika mwili wa mamalia dume tu na pale seli katika kiungo hicho zinapoanza kukua bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili hapo ndipo mtu hupata saratani ya tezi dume. Ugonjwa huu pia hujulikana kama saratani ya kibofu cha mkojo. Saratani ya tezi dume huwapata wanaume tu na hasa wenye umri wa takribani miaka 50 na kuendelea. Kutokana na tafiti mbali mbali, saratani hii imethibitika kushika nafasi ya pili, ukiachia mbali saratani ya mapafu kwa kusababisha vifo vya wanaume wenye umri wa takribani miaka 50 na kuendelea.
Tafiti za Chama cha Saratani cha Marekani (ACS) na cha Afrika Kusini (CANSA) zimebaini kuwa, mwanaume mmoja kati ya sita hupata saratani ya tezi dume katika uhai wake. Kutokana na takwimu za mwaka 2010 za dunia nzima, malaria iliua watu laki tano, kifua kikuu watu milioni 2.1, Ukimwi watu milioni 1.8 na saratani watu milioni 9.9. Kwa mujibu wa takwimu hizo, idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na ugonjwa wa saratani ni kubwa ikilinganishwa na ya magonjwa mengine. Dk Emmanuel Kandusi ambaye ni miongoni mwa waathirika wa saratani hiyo, na mwanzilishi wa kampeni ya kuangamiza saratani ya tezi dume nchini Tanzania ya '50 Plus Campaign' anasema kuwa, ugonjwa huu ukitambuliwa mapema huweza kutibika kwa urahisi. Ameongeza kuwa, kutokana na ugonjwa huo kuwa hatari nchini, ifikapo mwaka 2020 unatarajiwa kuua watu milioni 20.

👋soma zaidi kuhusu👉Ifahamu Saratani ya Tezi Dume, chanzo, Dalili, Uchunguzi na Tiba

📌 Simulizi ya mapenzi

SIMULIZI, hii iwasute na kupatwa na hofu ya mungu nyote mlio ktk mahusiano/ndoa yenu.

👋soma zaidi kuhusu👉Simulizi ya mapenzi

📌 Simu ilivyozua utata

Mama alichukuwa simu akampa mwanawe. Mama..Mpigie babako mwambie chakula tayari. (Mtoto akachukuwa na kupiga) Mtoto…Mama simu ya baba imepokelewa na mwanamke. (Mama kwa hasira) Akirud atanitambua leo. (Baada ya muda kidogo baba akarud,kufika mlangon tu kapokewa na sufuria ya kichwa. Hajakaa vzur mwiko wa pua) Mama..Mwanangu ulipopiga simu ya babako mwanamke wake alisemaje?? Mtoto..Alisema mteja unaempigia hapatikan kwa sasa…..

👋soma zaidi kuhusu👉Simu ilivyozua utata

📌 Jinsi ya kutengeneza Keki Ya Mbegu Za Mchicha

Unga ngano vikombc 3
Unga mbegu za mchicha kikombe 1
Baking powder vijiko vidogo
Maziwa kikombe 1
Sukari kikombe 1
Blue band kikombe ½
Mayai 10-12

👋soma zaidi kuhusu👉Jinsi ya kutengeneza Keki Ya Mbegu Za Mchicha

📌 MASWALI YA MWL

1.
Ticha:"Punda ni mnyama
anaefugwa
nyumbani,lakini akiwa mwituni
anaitwa
pundamilia….Je sungura anayeishi
mwituni
anaitwaje?"
ZUZU:"Sunguramilia."
2.
Ticha:"Rais wa kwanza wa kenya
aliitwa
KENYATTA…Je rais wa kwanza wa
Tanzania
aliitwaje?"
ZUZU:"TANZANIATTA."
3.
Ticha:"Kuku yuko katika jamii ya
NDEGE…Je
samaki yuko katika jamii ya nini?"
ZUZU:"MELI."
4.
Ticha:"Coach wa Arsenal anaitwa
ARSENE,wa
Man-city anaitwa MANCINI….Je wa
Liverpool
anaitwaje?
ZUZU:"LIVER."
5
Ticha:"Ukiwa na mbuzi 10,wezi
waje waibe
5,utabaki na nini?"
ZUZU:"Hasira nyingi sana!"

👋soma zaidi kuhusu👉MASWALI YA MWL

📌 WACHEPUKAJI WENGI WANATABIA HIZI

1.Hachezi mbali na simu yake kila wakati.
2.Inbox na sending items hufutwa kila wakati.
3.Ukimuomba simu yake ghafla lazima akwambie hebu kwanza…….
4. Kamwe haiiti always vaibration.
5. Namba nyingi ha save.
6. Kuna simu hapokei hata iweje….anapenda sms zaidi
7.Majina mengi kwenye simu yameseviwa kwa majina ya kufikirika.
8.Muda mwingi ni mtu wakujihami.
9.Anapenda password na anabadili mara kwa mara.
10.Akiazima simu yako, akitumia tu anafuta deal no haraka.
11.Always yuko na simu…..hadi bafuni ikibidi.
12. Anajazba ukimuuliza chochote kuhusu simu….anajishtukia.
13. Akiwa anachati anakuangalia mara kwa mara kiwiziwizi
14. Hana jeuri ya kukuweka profile picture na akikuweka humalizi masaa anakudampu huko Hapa kuna ukweli asilimia millioni moja kabisa Share na washikaji zako😜😜i

👋soma zaidi kuhusu👉WACHEPUKAJI WENGI WANATABIA HIZI

📌 Unashangaa kwa nini hufanikiwi?

Sikia haihitaji ukalishwe chini ndo uelewe, Ukweli ni kwamba unajishughulisha Sana na mambo yasiyo Kuhusu katika mafanikio.wazungu husema mind your own business sasa Sijui huu msemo unauchukuliaje?? Imagine unamjua Ali kiba hadi bafuni kwake, tour zote za mwaka huu unazijua hadi nyingine unataka kumpangia, nikuulize wewe ni mwanamziki??

👋soma zaidi kuhusu👉Unashangaa kwa nini hufanikiwi?

📌 Ningekufa kwa ajili ya mwanamke

Leo nimepita kisimani nikamkuta dada mmmoja akifua. ,Nikamuuliza eti dada unavijua visa vya wanawake??
Akajibu kaka niache, nikakomaa anijibu…
Badala ya kujbu akaanza kupiga mayowe, na kelele za kuomba msaada.. hadi wananchi wenye mapanga, mawe na mishale wakaanza kuja, dada huyo alivyoona wanakuja akajmwagia maji mwili mzima. Nikajua leo ndio mwisho wangu nikajuta sana kutaka kujua kila kitu…
Wananchi walivyofika, wakamuulza, kuna nini? Akawajibu, nilidumbukia kwenye kisima na huyu kaka ndie amensaidia!!
Wakanipongeza sana sana kisha wakaondoka…
Yule dada akaniambia, hivyo ndivyo visa vya mwanamke anaweza kukuua au kukulinda! So muheshmu mwanamke hata kinafiki, usijfanye jeuri!!!

👋soma zaidi kuhusu👉Ningekufa kwa ajili ya mwanamke

📌 Jinsi ya kulima bamia inavyotakiwa

Bamia ni zao linalolimwa sana nchi za joto. Zipo aina nyingi za bamia, aina zile za kiasili nazo hutofautiana kulingana na eneo moja na lingine. Bamia huliwa kama matunda au hupikwa kama mboga pamoja na nyama, samaki au mboga nyingine.

👋soma zaidi kuhusu👉Jinsi ya kulima bamia inavyotakiwa

📌 Huyu jamaa amekomeshwa, majambazi ni shida!

CHEKA KIDOGO
Majambaz waliliteka gar moja lililokua limeshehen abiria
Baada ya abiria kusachiwa na majambaz hao na kukutwa hawana pesa, majambaz wakasema kila m2 atapigwa viboko (bakora) kutokana na namba ya shati alilovaa
Aliyekua hana namba atasalimika
Kaz ikaanza, jamaa alievaa jez ya ROONEY wa Man U akapigwa fimbo 10, mwengine alievaa nguo ya 50cent akapigwa 50, n.k, sasa kwa pemben kulikua na jamaa analia sn yaani kila akijiangalia, kumbe alikua amevaa fulana limeandikwa LOWASA 2015 duuuh! Unajua kilichotokea ngoja niweke cm chaji kwanza.

👋soma zaidi kuhusu👉Huyu jamaa amekomeshwa, majambazi ni shida!

📌 Jamaa alikuwa anagombana na mkewe

Jamaa alikuwa anagombana na mkewe,hatimae
akamwambia kwa ukali
"Unajua nimechoka sasa, haya kusanya nguo
zako na…….. Kabla hajamalizia sentensi simu
ya mkewe ikaita, kumbe alikuwa ni baba yake.
Basi mzee akaanza kuongea na binti yake huku
jamaa anasikia
"Aisee mwanangu nimebahatika kuuza ile
nyumba yangu sasa nimeona niwatumie milioni
20 mjaribu kuanzisha mradi na mwenzio.
Haya mwambie yeye nitampigia kesho kama
ana mradi mwingine nimpe hela kidogo".Baada
ya simu kukatwa mke akamgeukia jamaa
akamuuliza,"eeenhee!!! ulikuwa unasema
umenichoka nikusanye nguo zangu halafu
iweje? Jamaa kwa upole akajibu "Nilikuwa
nasema ukusanye nguo zako na unipe nifue".

👋soma zaidi kuhusu👉Jamaa alikuwa anagombana na mkewe
miss-you-puppy-smiley-emoticon.gif

📓 Posti za sasa👇

A Je, ni madhara gani atapata mama mjamzito endapo atajamiiana na mwenzi wake?

Kama kati ya mwanamke na mwanaume hakuna mwenye magonjwa ya zinaa, hakuna madhara yoyote kwa mwanamke mwenye mimba kujamii ana na mwenzi wake. Mfuko wa mimba hufunga kabisa na kifuko kinamzunguka mtoto vizuri, na hivyo hakuna uwezekano wowote wa mbegu za kiume kupenya na kumfikia mtoto.
Inashauriwa lakini wakati wa kujamii ana na mwanamke mjamzito tumbo lisigandamizwe sana. Wanawake wengine hawana hamu kubwa ya kujamii ana hasa mwishoni mwa ujauzito, na mwanaume anashauriwa kuheshimu hisia hizi za mwanamke.
Kama mwanaume atakuwa ameambukizwa magonjwa ya zinaa wakati wa kujamii ana, hii i ii inaweza kuwa hatari sana kwa mwanamke na pia kwa mtoto tumboni. Wakijamii ana mume na mke wakati wa ujauzito, lazima wawe na uhakika kwamba hamna mwenye magonjwa ya zinaa au watumie kondomu kwa ajili ya kinga. Iwapo watakuwa na wasiwasi wowote, wamwone daktari kwa uchunguzi.

👋soma zaidi kuhusu👉Je, ni madhara gani atapata mama mjamzito endapo atajamiiana na mwenzi wake?

A Je, kwa nini inatokea kuzaa mtoto mlemavu?

Kuna aina mbalimbali za ulemavu na kuna sababu mbalimbali za kuzaa mtoto mlemavu. Ulemavu wa mtoto unaweza kuwa wa kurithi au ukatokea katika hatua tofauti wakati mimba inakuwa, kama vile , wakati wa utungaji mimba, wakati wa ujauzito na wakati wa kuzaa. Baadhi ya ulemavu ni kwa sababau ya hitilafu ya kinasaba (jenetiki) ambayo tayari i i inajulikana kwenye familia, au inayojitokeza ghafla. Hii ni aina ya ulemavu ambao hauwezi kuzuilika.
Ili mimba i iweze kutungwa, kuna mlolongo wa mambo mengi ambayo yanatakiwa yatokee wakati mwafaka. Ule mwenendo wa kujiunga yai lililopevuka likutane na mbegu ya kiume siyo kitu rahisi na i inawezekana yakatokea makosa. Makosa kama hayo siyo rahisi kuyazuia na mara nyingi kutokea kwake ni kwa bahati mbaya.
Sababu mojawapo ni mwanamke kuumwa wakati wa ujauzito. Kama mwanamke mjamzito anaumwa kwa mfano, malaria na anakunywa madawa makali, ugonjwa wenyewe au matumizi ya dawa yanaweza kuleta madhara kwa mimba i inayokua tumboni. Malaria ni ugonjwa mmojawapo unaosababisha mimba kutoka na ulemavu kwa watoto wanaozaliwa. Wanawake wanashauriwa kuwa wangalifu sana wasiugue malaria wakati wa ujauzito. Sababu nyingine ni matumizi ya madawa ya kulevya, pamoja na sigara au pombe wakati wa ujauzito. Vitu hivi sio vizuri kwa mwili wa binadamu, hasa kwa mimba.
Wakati mwingine, ulemavu wa mtoto unatokea wakati wa kuzaliwa. Kwa hiyo ni muhimu sana mwanamke ahakikishe anahudumiwa na mhudumu mwenye ujuzi wa kutosha ambaye anayajua madhara na namna ya kukabiliana nayo.

👋soma zaidi kuhusu👉Je, kwa nini inatokea kuzaa mtoto mlemavu?

A ATHARI ZA ULEVI KATIKA JAMII

Watu wanokunywa kupitia kiasi huathiri jamii kwa njia
mbalimbali. Madhara mengine hutokea kwa kuwa wanafanya
vitu ambavyo wasingevifanya iwapo wasingekuwa wamelewa.

👋soma zaidi kuhusu👉ATHARI ZA ULEVI KATIKA JAMII

A Je, kwa nini watu waanzao kutumia dawa za kulevya hupenda kuendelea kuzitumia?

Hii ndio hasa sababu kwa nini dawa za kulevya ni hatari! Mara unapozizoea unakuwa na ugumu wa kuendesha maisha yako bila dawa za kulevya. Kwa dawa nyingi za kulevya ubongo huzoea kuwepo kwake kwenye damu na dawa zaidi na zaidi huhitajika i ili kuendeleza hali hiyo. Hii i ii ina maana kadri muda unavyoenda ndivyo unavyoongeza kiasi cha dawa za kulevya unachokihitaji.
Pale utakapojaribu kupunguza kiasi cha matumizi ya dawa za kulevya au kuacha kabisa unaweza kupata hali ya kimaumbile au kiakili i i itokeayo kutokana na kuacha kitu ulichozoea. Hali hii inaweza i isiwe ya kufurahisha, yenye kuumiza na pengine hatari kwa maisha yako. Mara mtu anapozizoea dawa za kulevya haiwi tu tabia bali ugonjwa. Watu wengi wanaotegemea dawa za kulevya hawazitumii kwa kujifurahisha bali kuzuia maumivu yasababishwayo na kuacha kitu ulichozoea. Njia nzuri ya kuzuia hali hii ni rahisi: kuwa jasiri na sema HAPANA. Usijaribu dawa za kulevya.

👋soma zaidi kuhusu👉Je, kwa nini watu waanzao kutumia dawa za kulevya hupenda kuendelea kuzitumia?

A Jinsi ya kulima bamia inavyotakiwa

Bamia ni zao linalolimwa sana nchi za joto. Zipo aina nyingi za bamia, aina zile za kiasili nazo hutofautiana kulingana na eneo moja na lingine. Bamia huliwa kama matunda au hupikwa kama mboga pamoja na nyama, samaki au mboga nyingine.

👋soma zaidi kuhusu👉Jinsi ya kulima bamia inavyotakiwa

A Mimi ni msichana Albino ninaogopa kuwa na rafiki mwanaume kwa kuhofia kuwa anataka tu kujamiiana na mimi na halafu aniache.

Wakati mwingine kuwa na muonekano tofauti na watu wengine
huvuta udadisi. Na hasa tukikumbuka kwamba uvumi uliopo
unasema kuwa Albino wako tofauti katika kujamiiana jambo
ambalo linaimarisha udadisi huu. Kwa maana hiyo basi, chukua
muda wa kutafakari. Kama vile tunavyofanya katika urafiki
mwingine ni lazima uchukue muda, ujaribu kujenga mazingira
ya kusikilizana na kuelewana. Mnaweza kufanya shughuli nyingi
pamoja na baada ya muda utaweza kugundua kama urafiki wenu
ni wa kweli kwa maana anakupenda wewe kama ulivyo na siyo
kwa kitu kingine. Baada ya hapo ndipo unaweza kuingia katika
uhusiano wa karibu bila kuogopa kuachwa.

👋soma zaidi kuhusu👉Mimi ni msichana Albino ninaogopa kuwa na rafiki mwanaume kwa kuhofia kuwa anataka tu kujamiiana na mimi na halafu aniache.

A METHALI MIA SITA NA KUMI ZA KISWAHILI (610)

METHALI MIA SITA NA KUMI (610)
1. Aanguaye huanguliwa.
2. Asiye sikia la mkuu, huvunjika guu.
3. Abebwaye hujikaza.
4. Adhabu ya kaburi aijuae maiti.
5. Adui aangukapo, mnyanyue.
6. Adui mpende.
7. Adui wa mtu ni mtu.
8. Afadhali ya Musa kuliko ya Firauna.
9. Ahadi ni deni.
10. Ajidhaniaye amesimama, aangalie asianguke.
11. Akiba haiozi.
12. Akili ni mali.
13. Akili ni nywele kila mtu ana zake.
14. Akili nyingi huondowa maarifa.
15. Akutukanae hakuchagulii tusi.
16. Akipenda chongo huita kengeza.
17. Akufaae kwa dhiki, ndiye rafiki.
18. Akufanyiaye ubaya, mlipe wema.
19. Akupaye kisogo si mwenzio.
20. Akutendaye mtende, mche asiyekutenda.
21. Alisifuye jua, limeuangaza.
22. Aliye juu msubiri chini.
23. Aliye kando, haangukiwi na mti.
24. Aliye kupa wewe kiti (kibao) ndiye aliye nipa mimi kumbi.
25. Aliye kutwika, ndiye atakaye kutua.
26. Akufukuzae hakwambii toka.
27. Aliyekupa mkeka ndiye aliyenipa kumbesa.
28. Amani haipatikani mpaka kwa ncha ya upanga.
29. Ana hasira za mkizi.
30. Anayekuja pasi na hodi, huondoka bila ya kuaga.
31. Angurumapo simba, mcheza ni nani?
32. Aninyimaye mbazi kanipunguzia mashuzi.
33. Apewaye ndiye aongezwaye.
34. Anaejipiga mwenyewe, halii.
35. Asifuye mvuwa imemnyea.
36. Asiye kubali kushindwa si mshindani.
37. Asiye kujua, hakuthamini.
38. Asiye kuwapo na lake halipo.
39. Asiye lelewa na mamae hulelewa na ulimwengu.
40. Asiye na mengi, ana machache.
41. Asiye uliza, hanalo ajifunzalo.
42. Asiyejua maana, haambiwi maana.
43. Atangaye na jua hujuwa.
44. Atangazaye mirimo, si mwana wa ruwari (Liwali).
45. Atekaye maji mtoni hatukani mamba.
46. Avumaye baharini papa kumbe wengi wapo.
47. Baada ya dhiki faraja.
48. Bahari hailindwi.
49. Bamba na waume ni bamba, hakuna bamba la mume.
50. Bandu bandu huisha gogo.
51. Baniani mbaya, kiatu chake dawa.
52. Bendera hufuata upepo.
53. Biashara asubuhi.
54. Bilisi wa mtu ni mtu.
55. Bora kinga kuliko tiba.
56. Bora lawama kuliko fedheha.
57. Bora mchawi kuliko fitina.
58. Biashara asubuhi.
59. Bora nusu shari kuliko shari kamili.
60. Bwawa limeingia ruba.
61. Cha mtu mavi.
62. Chaka la samba, halilali nguruwe.
63. Chamlevi huliwa na mgema.
64. Chanda chema huvikwa pete.
65. Chelewa chelewa, utakuta mtoto si wako.
66. Choko mchokoe pweza, binaadamu hutomuweza.
67. Chombo cha kuzama hakina usukani.
68. Chovya - chovya yamaliza buyu la asali.
69. Chui hakumbatiwi.
70. Chururu si ndo ndo ndo.
71. Dalili ya mvua mawingu.
72. Damu nzito kuliko maji.
73. Daraja livuke ulifikapo.
74. Dawa ya moto ni moto.
75. Daraja ukilibomoa, ujue kuogelea.
76. Dau la mnyonge haliendi joshi, likienda joshi ni matakwa ya Mungu.
77. Dawa ya moto ni moto.
78. Donda ndugu halina dawa.
79. Dua ya kuku haimpati mwewe.
80. Fadhila huna, hata hisani hukumbuki?
81. Fadhila ya nyuki ni moto.
82. Fadhila ya punda ni mateke (mashuz)
83. Fahari ya macho haifilisi duka.
84. Farasi hamuwawezi, tembo mtawalishani?
85. Fata nyuki ule asali.
86. Fimbo ya mbali haiui nyoka.
87. Fumbo mfumbe mjinga, mwerevu huligangua.
88. Funika kombe mwanakharamu apite.
89. Ganda la mua la jana, chungu kaona kivuno.
90. Gome la udi, si la mnuka uvundo.
91. Haba na haba, hujaza kibaba.
92. Haki ya mtu hailiki.
93. Hakuna masika yaso mbu.
94. Hakuna msiba usio na mwenziwe.
95. Hakuna siri ya watu wawili.
96. Hakuna ziada mbovu.
97. Hala hala mti na macho.
98. Hamadi ni ilio kibindoni, na silaha ni iliyo mkononi.
99. Hapana marefu yasio na mwisho.
100. Haraka haraka haina baraka.
101. haraka haraka haina baraka.
102. Haramu yako halali kwa mwenzio.
103. Hasidi hasada.
104. Hasidi mbaya.
105. Hasira, hasara.
106. Hatua ndefu hufupisha mwendo.
107. Hauchi hauchi, unakucha.
108. Hayawi hayawi, mara huwa.
109. Heri kufa macho kuliko kufa moyo.
110. Heri kujikwa kidole kuliko ulimi.
111. Heri nitakula na nini?, kuliko nitakula nini?
112. Heri ya marama kuliko kuzama.
113. Hiari ya shinda utumwa.
114. Hogo halihogoki mpaka kwa hogo jenziwe.
115. Hucheka kovu asiye kuwa na jeraha.
116. Ila ya kikwapa, kunuka pasipo kidonda.
117. Yaliyoopita si ndwele, ganga yajayo.
118. Iliyo jaa ndiyo ipunguzwayo.
119. Imara ya jembe kaingojee shambani.
120. Jambo usilolijua, usiku wa giza.
121. Jina jema hungara gizani.
122. Jini likujualo halikuli likakwisha.
123. Jino la pembe si dawa ya pengo.
124. Jitihada haiondoi kudura.
125. Jitihadi haiondoi kudura.
126. Jogoo la shamba haliwiki mjini.
127. Jungu kuu, halikosi ukoko.
128. Jununu fununu.
129. Kafiri akufaaye, si muislamu asiye kufaa
130. Kafiri akufaye si Isilamu asiyekufa.
131. Kama hujui kufa,tazama kaburi.
132. Kama wewe wasema cha nini, mwezio asema nitakipata lini.
133. Kamba hukatika pabovu.
134. Kanga hazai ugenini.
135. Kawaida ni kama sheria.
136. Kawia ufike.
137. Kazi mbaya siyo mchezo mwema.
138. Kelele za chura hazimzuwii ng'ombe kunywa maji.
139. Kelele za mlango haziniwasi usingizi (Kelele za mlango hazimuudhi mwenye nyumba)
140. Kenda karibu na kumi.
141. Kesho kesho, kesho kiama.
142. Kiburi si maungwana.
143. Kibuzi na kibuzi hununua jahazi.
144. Kichango kuchangizana.
145. Kidole kimoja hakivunji chawa.
146. Kikulacho ki nguoni mwako.
147. Kikushindacho kukila usikitie ila.
148. Kila chombo kwa wimblile.
149. Kila mbwa hubwekea mlangoni kwao.
150. Kila mlango na ufunguwo wake.
151. Kila mtoto na koja lake.
152. Kila mtu huzikwa na kaburi lake.
153. Kila mtu na bahati yake.
154. Kila mwamba ngoma ,ngozi huivuta kwake.
155. Kila mtu hulilia mamae.
156. Kila ndege huruka kwa ubawa wake.
157. Kila shetani na mbuyu wake.
158. Kilimia kikizama kwa jua, huzuka kwa mvua, na kikizama kwa mvua, huzuka kwa jua.
159. Kilio huanza mfiwa ndipo wa mbali wakaingia.
160. Kimya kingi kina mshindo mkubwa.
161. Kinga na kinga ndipo moto uwakapo.
162. Kingiacho mjini si haramu.
163. Kinyozi hajinyoi.
164. Kinywa ni jumba la maneno.
165. Kipendacho moyo dawa.
166. Kipofu hasahau mkongojo wake.
167. Kipya kinyemi ingawa kidonda.
168. Kisebusebu na kiroho papo.
169. Kisokula mlimwengu, sera nale.
170. Kisokula mlimwengu,sera nale.
171. Kisu kimenifika mfupani.
172. Kitanda usicho kilalia hukijui kunguni wake.
173. Kitumbua kimeingia mchanga.
174. Kivuli cha fimbo hakimfichi mtu jua.
175. Kiwi cha yule ni chema cha; hata ulimwengu uwishe.
176. Kizuri chajiuza kibaya chajitembeza.
177. Konzi ya maji, haifumbatiki.
178. Konzo ya maji haifumbatiki.
179. Kosa moja haliachi mke.
180. Kozi mwandada, kulala na njaa kupenda.
181. Kuagiza kufyekeza.
182. Kuambizana kuko kusikilizana hapana.
183. Kucha M'ngu si kilemba cheupe.
184. Kuchamba kwingi, kuondoka na mavi.
185. Kufa kufaana.
186. Kufa kwa jamaa, harusi.
187. Kufa kwa mdomo,mate hutawanyika.
188. Kufanaya kosa sio kosa, kosa ni kurudia kosa.
189. Kuishi kwingi, kuona mengi.
190. Kujikwa si kuanguka,bali ni kwenda mbele.
191. Kujikwaa si kuanguka, bali ni kwenda mbele.
192. Kukopa harusi kulipa matanga.
193. Kukopa harusi, kulipa matanga.
194. Kuku havunji yai lake.
195. Kuku mgeni hakosi kamba mguuni.
196. Kula kutamu ,kulima mavune.
197. Kulea mimba si kazi kazi kulea mwana.
198. Kukopa harusi, kulipa matanga.
199. Kumuashia taa kipofu ni kuharibu mafuta.
200. Kunako matanga kume kufa mtu.
201. Kunguru mwoga hukimbiza mbawa zake.
202. Kupanda mchongoma, kushuka ndio ngoma.
203. Kupata si werevu, na kukosa si ujinga.
204. Kupoteya njia ndiyo kujua njia.
205. Kurambaramba ndio kula, kunenepa kwake Mola.
206. Kusikia si kuona.
207. Kutangulia si kufika.
208. Kutoa ni moyo usambe ni utajiri.
209. Kutu kuu ni la mgeni.
210. Kuugua sio kufa.
211. Kuvuja kwa pakacha nafuu ya mchukuzi.
212. Kuzima koleo si mwisho wa uhunzi.
213. Kwa mwoga huenda kicheko na kwa shujaa huenda kilio.
214. Kweli ilio chungu, si uongo ulio mtamu.
215. Kwenda mbio siyo kufika.
216. Kwenye miti hakuna wajenzi.
217. La kuvunda halina rubani.
218. La kuvunda halina ubani.
219. Lake mtu halimtapishi bali humchefua.
220. Leo kwako, kesho kwa mwenzio.
221. Leo ni leo asemayo kesho ni mwongo.
222. Liandikwalo ndiyo liwalo.
223. Lila na fila hazitangamani.
224. Lipitalo, hupishwa .
225. Lisemwalo lipo,ikiwa halipo laja.
226. Lisilo na mkoma, hujikoma lilo.
227. Lisilokuwapo moyoni, halipo machoni.
228. Maafuu hapatilizwi.
229. Macho hayana pazia.
230. Mafahali wawili hawakai zizi moja.
231. Maiti haulizwi sanda.
232. Maji hayapandi mlima.
233. Maji hufuata mkondo.
234. Maji ukiyavuliya nguo huna budi kuyaoga.
235. Maji usiyoyafika hujui wingi wake.
236. Maji ya kifuu, bahari ya chungu.
237. Maji yakijaa hupwa.
238. Maji yakimwagika hayazoleki.
239. Maji yamenifika shingoni.
240. Majuto ni mjukuu.
241. Mali ya bahili huliwa na wadudu.
242. Mama ni mama, hata kama ni rikwama.
243. Mama nipe radhi kuishi na watu kazi.
244. Mambo kunga.
245. Manahodha wengi chombo huenda mrama.
246. Maneno makali hayavunji mfupa.
247. Maneno mazuri humtowa nyoka pangoni.
248. Maneno si mkuki.
249. Mapenzi ni kikohozi, hayawezi kufichika.
250. Masikini akipata matako hulia mbwata.
251. Masikini haokoti,akiokota huambiwa kaiba.
252. Masikini na mwanawe tajiri na mali yake.
253. Maskini hana kinyongo.
254. Mavi usioyala, wayawingiani kuku?
255. Mavi ya kale hayanuki.
256. Mbinu hufuata mwendo.
257. Mbio za sakafuni huishia ukingoni.
258. Mbiu ya mgambo ikilia kuna jambo.
259. Mchagua jembe si mkulima.
260. Mchagua nazi hupata koroma.
261. Mchagua nazi si mfuaji.
262. Mchakacho ujao,halulengwi na jiwe.
263. Mchama ago hanyeli,huenda akauya papo.
264. Mchamba kwingi mara ujitia dole.
265. Mcheka kilema hafi bila kumpata.
266. Mchele mmoja mapishi mengi.
267. Mchelea mwana kulia hulia yeye..
268. Mcheza hawi kiwete, ngoma yataka matao.
269. Mcheza kwao hutuzwa.
270. Mcheza na tope humrukia.
271. Mchezea mavi, hayaachi kumnuka.
272. Mchezea zuri, baya humfika.
273. Mchimba kisima hungia mwenyewe.
274. Mchonga mwiko hukimbiza mkono wake.
275. Mchuma janga hula na wakwao.
276. Mchumia juani,hulia kivulini.
277. Mdharau biu, hubiuka yeye.
278. Mdharau mwiba humchoma.
279. Meno ya mbwa hayaumani.
280. Mfa maji haachi kutapatapa.
281. Mfa maji hukamata maji.
282. Mficha uchi hazai.
283. Mfinyazi hulia gaeni.
284. Mfuata nyuki hakosi asali.
285. Mfukuzwa kwao hana pakwenda.
286. Mgaagaa na upwa hali ugari kande.
287. Mganga hajigangi.
288. Mgema akisifiwa tembo hulitia maji.
289. Mgeni ni kuku mweupe.
290. Mgeni njoo mwenyeji apone.
291. Mgomba haushindwi na mkunguwe.
292. Mgonjwa haulizwi uji.
293. Miye nyumba ya udongo, sihimili vishindo.
294. Mjinga akierevuka mwerevu yupo mashakani.
295. Mjinga mpe kilemba utamuona mwendowe.
296. Mjumbe hauawi.
297. Mkaidi hafaidi mpaka siku ya idi.
298. Mkamatwa na ngozi ndiye mwizi.
299. Mkamia maji hayanywi.
300. Mkamia maji hayanywi.
301. Mkataa la mkuu huvunjika guu.
302. Mkataa wengi ni mchawi.
303. Mkataa ya Musa hupata ya Firauna.
304. Mke ni nguo, mgomba kupalilia.
305. Mkono moja hauchinji ng'ombe.
306. Mkono moja haulei mwana.
307. Mkono mtupu haulambwi.
308. Mkono usioweza kuukata,ubusu.
309. Mkosa kitoweo humangiria.
310. Mkuki kwa nguruwe, kwa mwanadamu uchungu.
311. Mkulima ni mmoja walaji ni wengi.
312. Mla cha mwenziwe na chake huliwa.
313. Mla cha uchungu na tamu hakosi.
314. Mla kuku wa mwenziwe miguu humwelekea.
315. Mla mbuzi hulipa ngombe.
316. Mla mla leo mla jana kala nini?
317. Mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe.
318. Mlala na maiti haachi kulia lia.
319. Mlenga jiwe kundini hajui limpataye.
320. Mlimbua nchi ni mwananchi.
321. Mnyamaa kadumbu.
322. Mnywa maji kwa mkono mmoja,Kiu yake i pale pale.
323. Moja shika, si kumi nenda urudi.
324. Moto hauzai moto.
325. Mpanda farasi wawili hupasuka msamba.
326. Mpanda ngazi hushuka.
327. Mpanda ovyo hula ovyo.
328. Mpemba akipata gogo hanyii chini.
329. Mpemba hakimbii mvua ndogo.
330. Mpende akupendae asiyekupenda achana naye.
331. Mpiga ngumi ukuta huumiza mkonowe.
332. Mpofuka ukongweni,hapotewi na njia.
333. Msafiri kafiri.
334. Msafiri masikini ajapokuwa sultani.
335. Msasi haogopi mwiba.
336. Msema kweli hukimbiwa na rafiki zake.
337. Msema pweke hakosi.
338. Mshika kisu, hashiki makalini.
339. Mshale kwenda msituni haukupotea.
340. Mshoni hachagui nguo.
341. Msi bahati, habahatishi.
342. Msi mbele, hana nyuma.
343. Msishukuru mja, hamshukuru Molawe.
344. Msitukane wagema na ulevi ungalipo.
345. Msitukane wakunga na uzazi ungalipo.
346. Mstahimilivu hula mbivu.
347. Mtaka cha mvunguni sharti ainame.
348. Mtaka lake hasindwi.
349. Mtaka nyingi nasaba hupata mwingi msiba.
350. Mtaka unda haneni.
351. Mtaka uzuri hudhurika.
352. Mtaka yote hukosa yote.
353. Mtegemea nundu haachi kunona.
354. mtegemea nundu, haachi konona.
355. Mtego bila ya chambo, haunasi.
356. Mtembezi hula miguu yake.
357. Mteuzi heshi tamaa.
358. Mti hauwendi ila kwa nyenzo.
359. Mtondoo haufi maji.
360. Mtoto akililia wembe mpe.
361. Mtoto umleyavyo ndivyo akuavyo.
362. Mtoto wa nyoka ni nyoka.
363. Mtu hakatai mwito,hukata aitwalo.
364. Mtu hujikuna ajipatapo.
365. Mtu huulizwa amevaani ,haulizwi amekulani.
366. Mtumai cha ndugu hufa masikini.
367. Mtumi wa kunga haambiwi maana.
368. Mtumikie kafiri upate mradi wako.
369. Mtupa jongoo hutupa na mti wake.
370. Muhitaji khanithi walau kana rijaali.
371. Muiba yai leo kesho hua mwizi wa ng'ombe.
372. Mume wa mama ni baba.
373. Mungu hamfichi mnafiki.
374. Mungu si asumani.
375. Muonja asali haonji mara moja.
376. Muuza sanda, mauti kwake harusi.
377. Mvua nguo, huchutama.
378. Mvumbika changa hula mbovu.
379. Mvumbika pevu hula mbivu na mvumbika changa hula mbovu.
380. Mvungu mkeka.
381. Mvunja nchi ni mwananchi.
382. Mvuvi ajuwa pweza alipo.
383. Mwacha asili ni mtumwa.
384. Mwamba na wako hukutuma umwambiye.
385. Mwamini Mungu si mtovu.
386. Mwana maji wa kwale kufa maji mazowea.
387. Mwana mkuwa nawe ni mwenzio kama wewe.
388. Mwana simba ni simba.The child of lion is a lion.
389. Mwana wa kuku hafunzwi kuchakura.
390. Mwana wa mtu ni kizushi, akizuka, zuka naye.
391. Mwanga mpe mtoto kulea.
392. Mwangaza mbili moja humponyoka.
393. Mwanzo kokochi mwisho nazi.
394. Mwanzo wa chanzo ni chane mbili.
395. Mwanzo wa ngoma ni lele.
396. Mwapiza la nje hupata la ndani.
397. Mwekaji kisasi haambiwi mwerevu.
398. Mwenda bure si mkaa bure,huenda akaokota.
399. Mwenda mbio hujikwa kidole.
400. Mwenda omo na tezi marejeo ni ngamani.
401. Mwenda pole hajikwai.
402. Mwenda wazimu hapewi panga.
403. Mwenda wazimu hapoi, bali hupata nafuu.
404. Mwenye haja hwenda chooni.
405. Mwenye kelele hana neno.
406. Mwenye kovu usidhani kapowa.
407. Mwenye kubebwa hujikaza.
408. Mwenye kuchinja hachelei kuchuna.
409. Mwenye kuumwa na nyoka akiona jani hushtuka.
410. Mwenye macho haambiwi tazama.
411. Mwenye mdomo hapotei.
412. Mwenye nguvu mpishe.
413. Mwenye njaa hana miko.
414. Mwenye pupa hadiriki kula tamu.
415. Mwenye shibe hamjui mwenye njaa.
416. Mwenye shoka hakosi kuni.
417. Mwenye tumbo ni tumbole, angafunga mkaja.
418. Mwenzako akinyolewa wewe tia maji.
419. Mwibaji na watwana, mlifi ni mwungwana.
420. Mwili wa mwenzio ni kando ya mwilio.
421. Mwizi hushikwa na mwizi mwenziwe.
422. Mwomba chumvi huombea chunguche.
423. Mwosha hadhuru maiti.
424. Mwosha huoshwa.
425. Mwosha husitiri maiti.
426. Mzaha,mzaha, mara hutumbuka usaha.
427. Mzazi haachi ujusi.
428. Mzigo usiouweza unaubebea nini?
429. Mzigo Wa mwenzio ni kanda Ia usufi.
430. Mzika pembe ndiye mzua pembe.
431. Mzowea kutwaa, kutoa ni vita.
432. Mzowea vya kunyonga, vya kuchinja haviwezi.
433. Mzungu Wa kula hafundishwi mwana.
434. Nahodha wengi, chombo huenda mrama.
435. Nani kama mama?
436. Natuone ndipo twambe, kusikia Si kuona.
437. Nazi haishindani na jiwe.
438. Nazi mbovu harabu ya nzima.
439. Ndege mjanja hunaswa na tundu bovu.
440. Ndege mwigo hana mazowea.
441. Ndevu sio shani, hata beberu anazo.
442. Ndugu chungu, jirani mkungu.
443. Ndugu mwui afadhali kuwa naye.
444. Ndugu wakigombana, chukua jembe ukalime, wakipatana chukua kikapu ukavune.
445. Ngoja! ngoja? huumiza matumbo.
446. Ngoma ivumayo haidumu.
447. Ngoma ivumayo haikawii kupasuka.
448. Ngoma ya kitoto, haikeshi.
449. Ng'ombe avunjikapo guu hurejea zizini.
450. Ng'ombe haelemewi na nunduye.
451. Ngombe wa Maskini hazai.
452. Ngozi ivute ili maji. ( Udongo upate uli maji )
453. Nguo ya kuazima, Haistiri matako.
454. Nia njema ni tabibu, nia mbaya huharibu.
455. Nifae na mvua nikufae na jua.
456. Nimekula asali udogoni, utamu ungali gegoni.
457. Nimekupaka wanja, wewe wanipaka pilipili.
458. Nimerejesha kikombe na kisahani chake.
459. Njia ya muongo fupi.
460. Njia ya mwongo ni fupi.
461. Njia ya siku zote haina alama.
462. Nta Si asali; nalikuwa nazo Si uchunga.
463. Nyani haoni kundule, huliona la mwenziwe.
464. Nyani haoni kundule.
465. Nyimbo mbaya haibembelezewi mtoto.
466. Nyimbo ya kufunzwa haikeshi ngoma.
467. Nyongeza huenda kwenye chungu.
468. Nyota njema huonekana asubuhi.
469. Nyumba usiyolala ndani huijui ila yake.
470. Nyumba ya udongo haihimili vishindo.
471. Nzi kufa juu ya kidonda Si haramu. (Jihadi ya nzi, kufa kidondani)
472. Ondoa dari uwezeke paa.
473. Pabaya pako Si pema pa mwenzako.
474. Padogo pako Si pakubwa pa mwenzako.
475. Painamapo ndipo painukapo.
476. Paka akiondoka, panya hutawala.
477. Paka hakubali kulala chali.
478. Paka hashibi kwa wali, matilabaye ni panya.
479. Paka wa nyumba haingwa.
480. Panapo wengi hapaharibiki neno.
481. Papo kwa papo kamba hukata jiwe.
482. Pele hupewa msi kucha.
483. Pema usijapo pema; ukipema Si pema tena.
484. Penye kuku wengi usimwage mtama.
485. Penye mafundi, hapakosi wanafunzi.
486. Penye mbaya wako, hapakosi mwema wako/na mwema wako hakosi.
487. Penye miti hakuna wajenzi.
488. Penye nia pana njia.
489. Penye urembo ndipo penye urimbo.
490. Penye wazee haliharibiki neno.
491. Penye wengi pana mengi.
492. Penye wengi pana Mungu.
493. Pilipili usoila, wewe inakuwashia nini?
494. Pole pole ndio mwendo.
495. Pwagu hupata pwaguzi.
496. Radhi ni bora kuliko mali .
497. Radhi za wazee, ni fimbo.
498. Sahani iliyofunikwa, kilichomo kimesitirika.
499. Sahau ni dawa ya Waja.
500. Samaki mmoja akioza, huoza wote.
501. Samaki mpinde angali mbichi.
502. Shida haina hodi.
503. Shida huzaa maarifa.
504. Shika! Shika! na mwenyewe uwe nyuma.
505. Shimo Ia ulimi mkono haufutiki.
506. Shoka lisilo mpini halichanji kuni.
507. Si kila king'aacho ni dhahabu.
508. Si kila mwenye makucha huwa simba.
509. Si Mungu mtupu na mkono wa mtu.
510. Sikio halilali na njaa.
511. Sikio halipwani kichwa. (Sikio halipiti kichwa).
512. Sikio Ia kufa halisikii dawa.
513. Siri ya mtungi aijuaye ni kata.
514. Sitaacha kula mkate kwa kuogopa kiungulia.
515. Siku njema huonekana asubuhi.
516. Siku utakayokwenda uchi, ndiyo siku utakayokutana na mkweo.
517. Siku ya kufa nyani, miti yote huteleza.
518. Siku za mwizi, arubaini.
519. Simba mwenda kimya (pole) ndiye mla nyama.
520. Simbiko haisimbuki ila kwa msukosuko.
521. Sio shehe bali ni shehena.
522. Siri ya maiti aijuaye muosha.
523. Sitafuga ndwele na waganga tele.
524. Sitapiki nyongo harudi haramba.
525. Subira ni ufunguo Wa faraja.
526. Sumu mpe paka, mbuzi utamdhulumu.
527. Sumu ya neno ni neno.
528. Tabia ni ngozi ya mwili.
529. Tamaa mbele, mauti nyuma.
530. Taratibu ndio mwendo.
531. Tawi kavu kuanguka si ajabu.
532. Teke Ia kuku halimuumizi mwanawe
533. Tonga si tuwi
534. Tunda jema halikawii mtini.
535. Ucheshi wa mtoto ni anga Ia nyumba.
536. Ujuzi hauzeeki.
537. Uchungu wa mwana, aujue mzazi.
538. Udongo uwahi ungali maji (Udongo upate uli maji)
539. Udugu wa nazi hukutania chunguni (Udugu wa nazi hukutana pakachani)
540. Uji hajauonja, tayari ushamuunguza
541. Ukenda kwa wenye chongo, fumba lako jicho.
542. Ukimpa shubiri huchukua pima.
543. Ukimuiga tembo kunya, utapasuka mkundu.
544. Ukimwamsha alolala utalala weye.
545. Ukinyofoa mnofu, ukumbuke kuguguna mfupa.
546. Ukiona kwako kunaungua kwa mwenzako kunateketea.
547. Ukiona moshi, chini kuna moto.
548. Ukiona neno, usiposema neno, hutapatikana na neno.
549. Ukiona vinaelea, vimeundwa.
550. Ukiona zinduna, na ambari iko nyuma.
551. Ukistahi mke ndugu, huzai nae.
552. Ukitaja nyoka, shika fimbo mkononi.
553. Ukitaka kula nguruwe, chagua aliye nona.
554. Ukitaka salama ya dunia, zuia ulimi wako.
555. Ukiujua wa mbele, nina ujua wa nyuma.
556. Ukupigao ndio ukufunzao.
557. Ukuukuu wa kamba Si upya wa ukambaa.
558. Ulimi hauna mfupa.
559. Ulimi unauma kuliko meno.
560. Ulipendalo hupati, hupata ujaaliwalo.
561. Ulivyoligema, utalinywa.
562. Umeadimika kama la jogoo.
563. Umegeuka mung'unye waharibika ukubwani.
564. Umejigeuza pweza, unajipalia makaa?
565. Umekuwa bata akili kwa watoto?
566. Umekuwa nguva, huhimili kishindo?
567. Umeruka mkojo unakanyaga mavi.
568. Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.
569. Unajenga kwa mwenzio na kwako kunaporomoka!!
570. Unakuja juu kama moto wa kifuu.
571. Unamlaumu mwewe, kipanga yuwesha kuku.
572. Ungalijua alacho nyuki, usingalionja asali.
573. Ushikwapo shikamana (Ukibebwa usijiachie).
574. Usiache kunanua kwa kutega.
575. Usiache mbachao kwa msala upitao.
576. Usiache tawi kabla ya kushika tawi.
577. Usiandikie mate na wino ungalipo
578. Usicheze na simba, ukamtia mkono kinywani.
579. Usijifanye kuku mweupe.
580. Usikaange mbuyu ukawaachia wenye meno
581. Usile na kipofu ukamgusa rnkono.
582. Usimgombe mkwezi, nazi imeliwa na mwezi.
583. Usiniache njia panda.
584. Usinikumbushe kilio matangani.
585. Usinipake mafuta kwa nyuma ya chupa.
586. Usinivishe kilemba cha ukoka.
587. Usione simba kapigwa na mvua.
588. Usipoziba ufa utajenga ukuta.
589. Usisafirie nyota ya mwenzio.
590. Usisahau ubaharia kwa sababu ya unahodha.
591. Usishindane na Kari; Kari ni mja wa Mungu.
592. Usitukane wagema na ulevi ungalipo.
593. Usitukane wakunga na uzazi 'ungalipo.
594. Utakosa mtoto na maji ya moto.
595. Usiyavuke maji usiyoweza kuyaoga.
596. Utaula na chua kwa uvivu wa kuchagua.
597. Vita havina macho.
598. Vita si lele mama.
599. Vita vya panzi, neema ya kunguru
600. Waarabu wa pemba, hujuana kwa vilemba
601. Wache waseme.
602. Wafadhilaka wapundaka.
603. Wagombanao ndio wapatanao.
604. Watu wanahisabu nazi, wewe unahisabu makoroma.
605. Wapiganapo tembo wawili ziumiazo ni nyasi.
606. Watetea ndizi, mgomba si wao.
607. Wazuri haweshi.
608. Wema hauozi..
609. wengi wape.
610. Zinguo la mtukufu, ni ufito.

👋soma zaidi kuhusu👉METHALI MIA SITA NA KUMI ZA KISWAHILI (610)

A mafuta kwenye kondomu

Mafuta yanayowekwa kwenye pakiti ya kondomu ni mafuta maalum na yana kazi ya kuhifadhi kondomu mpaka siku yake ya kutumiwa. Bila mafuta haya kondomu isingekuwa imara, ingekauka na isingekuwa nyumbufu vya kutosha. Vilevile mafuta hayo yanalainisha mpira ili kurahisisha uvaaji na matumizi yake. Kwa watu wengi, mafuta haya hayawaletei matatizo yoyote. Watu wachache sana ambao ngozi yao ni nyepesi kuathirika wanapata matatizo ya kuwasha baada ya kutumia kondomu.

👋soma zaidi kuhusu👉mafuta kwenye kondomu

A Hii sasa kali!!!

Mwalimu kauliza swali darasani
wanafunzi wataje
kazi za wazazi wao:
TINA: mimi baba yangu
mfanyabiashara mama
yangu mwalimu.
MWALIMU: Safi, haya juma
JUMA: Baba yangu dereva mama
yangu hafanyi
kazi.
MWALIMU: Vizuri, haya Zogo.
ZOGO: Mimi mama yangu malaya
anajiuza baba
simjui.
MWALIMU: Pumbavu wewe, nenda
ofisini kwa
mwalimu mkuu ukamueleze upuuzi
wote
uliosema hapa. Zogo anaenda ofisini
anarudi
huku anatabasamu na anakula
biskuti.
MWALIMU: Mwalimu mkuu kakupa
adhabu gani?
ZOGO: Kaniambia nimpe namba ya
mama…

👋soma zaidi kuhusu👉Hii sasa kali!!!

A TIBA ZA ASILI ZA CHUNUSI

Magadi soda ni mazuri sana kwa kusafishia uso na haswa ukiwa na chunusi. Changanya kiasi kidogo cha magadi soda na maji ya kutosha kuunda kidonge kidogo na kisha weka au kandika kidonge icho sehemu ilio athirika na chunusi. Kwa muda wa dakika 15-20 au mpaka ikauke, na kisha suuza kwa maji yasiwe ya moto. Unaweza kurudia rudia mara kadhaa kwa siku mpaka utakapo ona athari ya chunusi imepotea.

👋soma zaidi kuhusu👉TIBA ZA ASILI ZA CHUNUSI

A Njia za Kuzuia Mimba

Njia za uzazi wa mpango zinatofautiana sana na zinaweza kugawanywa katika makundi mengi:

👋soma zaidi kuhusu👉Njia za Kuzuia Mimba

A Kwa nini watu wengine wanabaki maskini??

KWA NINI WATU WENGINE WANABAKI MASKINI?
Sababu zifuatazo zinaweza kuwa na ukweli
mtupu;
1. Kushindwa kuamua haraka fursa
zinapojitokeza kwao
2. Fursa kali Zikitokea wanaziona kama ni uongo
na utapeli wa mjini
3. Kung'ang'ania kuajiriwa hata kama ajira hiyo
hailipi
4. Kudhania unajua sana hivyo huoni jipya la
kujifunza
5. Kukosa ujasiri wa kuanza. Unapanga mwezi
huu au mwaka huu ntafanya hili au lile. Lakini
mwaka unaisha hujaanza!!!
6. Kutokuwa na ndoto ya kiasi cha pesa
unazotaka kwa siku, kwa wiki mwezi au mwaka.
Unataka shs ngapi kwa siku? Wiki? Mwezi?
Mwaka? Kwa nini unataka kiasi hicho? Matumizi
yako ya lazima ni yapi? Ya starehe zako ni yapi?
7. Kununua vitu vya bei kubwa sana na visivyo
na tija yoyote katika kuongeza kipato chako.
8. Kuwaza kwamba maendeleo yanapatikana
uzeeni na siyo ujanani? Eti kumiliki mamilioni ya
pesa mpaka uwe mzee kama Reginald Mengi
vile.
9. Kufikiri eti huwezi kufanikiwa kuwa na fedha
kuubwa mpaka uwe freemason au fisadi. Ujinga.
10. Kuwa na wategemezi kibao nyumbani kwako
wakati kipato chenyewe kinatosha kula watu 2 tu
kwa mwezi. Hatari!!
11. Kusubiri siku utakayopata pesa nyingi sana
eti ndipo utafanya biashara hii au ile! Utasubiri
sana.
12. Kutokuweka akiba yoyote kwa malengo ya
maendeleo ya watoto na wajukuu zao.
13. Kufikiria kuwa kuna siku utapata msaada
kutoka kwa wafadhili, serikali au wazungu au
washikaji zako. Utangoja sana.
14. Kubadilisha mshahara wako au kipato chako
kuwa mali ya ukoo mzima. Kila mtu kwenye ukoo
wenu anakuomba pesa na wewe unampatia.
Usimpe mtu samaki mfundishe kuvua samaki
naye hatakuomba tena samaki. Usimpatie
maziwa ndugu yako mfundishe kufuga ng'ombe
wa maziwa.
Mpendwa wewe umeguswa na sababu ipi ktk
hizo?
Nakutakia Februari Njema

👋soma zaidi kuhusu👉Kwa nini watu wengine wanabaki maskini??
happy-elmo-smiley-emoticon.gif

Majarida na vitabu kutoka Ackyshine eBook Shop

MBINU-YA-KILIMO-BORA-CHA-MBOGA.jpg

Kina kurasa 100 na utaalamu wa mazao zaidi ya 10

Jipatie 📕Kitabu cha 👋Mbinu za Kilimo Bora✔ Cha Mboga🌿🍅 kwa Tsh 2,500/= tuu.
jua%20zaidi%2C%20dont%20delete

vichekesho.jpg

Kina kurasa 270 zenye picha na vichekesho 300+

Jipatie 📕Kitabu cha 😂Vichekesho Vikuu Vikali 👍300+✔ kwa Tsh 2,500/= tuu.
jua%20zaidi%2C%20dont%20delete

.

awesome-smiley-emoticon.gif
happy-spring-smiley-emoticon.gif