Je, Uvutaji wa sigara unafurahisha na kuchangamsha?

Mpendwa Msomaji, baada ya kukuandalia makala inayopendwa kuhusu; Virusi vya kompyuta (computer virus), sasa nimekuandalia makala hii kuhusu;

Je, Uvutaji wa sigara unafurahisha na kuchangamsha?.

Endelea kefurahia makala nzuri kila siku unapotembelea tovuti hii.

Je, Uvutaji wa sigara unafurahisha na kuchangamsha?

By, Melkisedeck Shine.

Ndiyo, lakini ni mwanzo tu na kwa muda mfupi; hii ni kwa
sababu mwanzoni nikotini iliyomo katika sigara inasababisha
damu kumiminika kwa wingi kupita kwenye ubongo wako. Hivyo,
husababisha msisimko na kukufanya ujisikie raha. Nikotini
pia inasababisha misuli mwilini kujichua na hivyo kukufanya
ujisikie mchangamfu.

Baada ya muda utajisikia kinyume na ulivyojisikia mwanzoni.
Kama utavuta zaidi na zaidi damu na oksijeni kidogo vitatiririka
mwilini na kwenye ubongo. Hii itakufanya ujisikie mchovu na
mwenye huzuni.

Kwa bahati mbaya baadhi ya matangazo ya biashara au
marafiki watakushawishi kwamba, uvutaji wa sigara ni safi, poa
na hukufanya kujisikia mkubwa. Lakini hawaongelei madhara
mabaya kiafya yatokanayo na uvutaji wa sigara na ugumu wa
kuacha uvutaji huo pale utakapoizoea.

Nikotini mara nyingi
huitwa kianzisho. Hii inamaanisha kwamba wakati mwingine
vijana wanaanza kuvuta sigara na kisha kuhamia kwenye
utumiaji wa dawa za kulevya. Hata hivyo uvutaji ni gharama.

Unaweza kusoma makala mpya nzuri kila unapotembelea website hii wakati wowote. Baada ya kusoma makala hii kuhusu; Je, Uvutaji wa sigara unafurahisha na kuchangamsha?, sasa endelea kusoma makala hizi nyingine nzuri nilizokuandalia;

FURSA..! Kuna nafasi za kazi 100.

Au soma zaidi hapa

.

KADI-SHUKRANI-MZAZI.JPG
KADI-SALAMU-MCHANA-JION.JPG