Je, ni sahihi kufanya mapenzi wakati mkeo akiwa na MIMBA?

By, Melkisedeck Shine.

afya-mapishi-na-lishe.png

Je, ni sahihi kufanya mapenzi wakati mkeo akiwa na MIMBA?

Ni kawaida kwa mwanaadamu aliye mzima kupenda kuwa na mtoto, na kwa namna ya upekee katika kuumbwa kwa mwanaadamu, hakuna njia nyingine yoyote ile ambako mtoto anaweza kupatikana bila ya maingiliano ya kimwili baina ya watu wa jinsia mbili tofauti (ukiachilia mbali instances chache ambapo mambo ya test tube na artificial insemination hutumika).

Kifupi ni kwamba, kama mwanamke atataka kubeba ujauzito ni lazima akubali kuingiliwa, Vivyo hivyo kama mwanaume anataka kumbebesha mwenza wake ujauzito ni lazima ahakikishe kuwa amemwiligilia mke
Hata hivyo, licha ya ukweli wa kuwa ili ujauzito upatikane ni lazima kuwe na kufanya mapenzi, kumekuwa na mkanganyiko sana juu ya tendo hili la kufanya mapenzi au kutiana kama wengine wanavyosema, pindi inapotokea mwanamke ameshashika ujauzito.
Je, ni sahihi kufanya mapenzi wakati mwanamke wako ni mjamzito?
Je, ni hadi muda gani kabla ya kujifungua, ambapo mwanamke mjamzito anaweza kuwa anaingiliwa kimwili na mwenza wake?
Kwa maswali haya na mengine kadhaa, hebu twende pamoja mdogo mdogo kama ifuatavyo:-

(1). Je, ni sahihi kufanya mapenzi ikiwa mwanamke wako ni mjamzito?

Ndio, hakuna tatizo lolote kwa mwanamke kuendelea kufurahia mapenzi na mumewe au mpenzi wake wakati anapokuwa mjamzito.
Wataalamu wanaeleza kuwa, ikiwa ujauzito ulioubeba haukupi shida yoyote ile na unajisikia uko poa, basi hakuna hatari yoyote ile ikiwa utataka kufanya.
Tatizo pekee ambalo huwa linawakumba wengi wa wanawake wakiwa wajawazito ni kuwa, huwa wanapoteza hamu ya tendo lenyewe wanapokuwa katika hali hii, au kushindwa kumudu kutokana na kujisikia uchovu muda mwingi.
Ingawa pia wapo wanawake ambao wakiwa katika hali hii ndio kwanza, wanakuwa wanajisikia kukereketwa huko kwenye ki**i kupita maelezo, na wanatamani muda wote wafanye mapenzi.
Wapo baadhi ya wanawake ambao wanakuwa wako normal kimwili, lakini kisaikolojia wanakuwa na ile hofu ya kuwa kufanya kunaweza kuwaharibia mimba zao, fikra ambazo huwatoa kabisa katika mstari wa kufurahia tendo hili.
Kwa hiyo, ikiwa mwili wako uko poa, na madaktari wamekwambia kiumbe kinakua bila shaka, na unaweza kwenda kazini, huna haja ya kujibania utamu wa mumeo au kumbania mumeo.

(2). Je, kufanya wakati wa ujauzito kunaweza kusababisha ujauzito kuharibika?

Hili pia ni miongoni mwa maswali na hali ambazo zimekuwa zikiwachanganya watu wengi, waume kwa wanawake.
Ila ukweli ni kwamba, kufanya hakuhusiani na kuharibika kwa mimba au kujifungua kabla ya wakati muafaka.
Kwa kawaida, kuharibika kwa mimba hutokana na sababu zingine tofauti kabisa, ikiwa ni pamoja na kizazi cha mwanamke kuwa na matatizo hasa katika kuhimili ukuaji wa kiumbe tumboni na sababu zingine za kimazingira.
Wala sio kwa sababu ya kitu ambacho unakifanya au hukifanyi.

(3). Je, kufanya wakati wa ujauzito kunaharibu au kumdhuru mtoto?

Kiumbe kilicho tumboni wakati wa ujauzito huwa kinakingwa na ute maalum unaojulikana kitaalamu kwa jina la "amniotic fluid" ndani ya mji wa uzazi, pamoja na kuta za mji wenyewe wa uzazi.
Hakuna namna ambavyo muhogo unaweza kupita na kufika mahali mtoto anapokuwa anakua huko ndani, au zile mbegu kuwa zitapita moja kwa moja na kwenda kumdhuru mtoto.
Kumekuwa na ule msemo wa kuwa kufanya wakati wa ujauzito ni kulea mimba, watu wakiamini kuwa mbegu huwa zinakwenda moja kwa moja kwenye kiumbe.
Dhana hii ni potofu. Kama kilivyo chakula cha kawaida mtu anapokula, ndivyo ambavyo mbegu nazo huwa hivyo.
Kila kitu kwanza lazima kiingie katika mfumo wa kawaida wa usafirishaji wa virutubisho vilivyo sahihi kuelekea kwenye kiumbe husika.
Hii ikimaanisha kuwa mbegu nazo huingia katika mfumo huo huo, huchujwa na kile kinachoonekana kuwa ni kirutubisho kitasafirishwa kwenda kulea kiumbe, ilhali yale makapi lazima yatatoka.
Tofauti pekee hapa ni kuwa, "mbegu za kiume zina protini nyingi", hii ikimaanisha kuwa sehemu kubwa ya kile kinachomwagwa kwenye uke wa mjamzito, kina nafasi ya kutumika kwa ajili ya kuongeza rutuba kwa kiumbe kinachokuaa ndani ya tumbo.
Na nyingine zinaweza kutoka tu zenyewe bila matatizo yo yote.

(4). Ni mikao ipi (staili) ambayo ni mizuri zaidi kuitumia kufanya wakati wa ujauzito?

Hakuna mkao maalum. Ujauzito sio ulemavu kwamba mnalazimika kujipanga upya namna ya kuridhishana, wala sio ugonjwa pia.
Ikiwa mwanamke unajihisi uko fresh kuendelea kutumia staili ya mwanzo ambayo mlikuwa mnaitumia na unafikishwa na mwenzio, huku huyo mwenzio naye akiwa yuko ok kuitumia staili hiyo na anaimudu hata unapokuwa na tumbo lako, hakuna shida
Jichumishe mboga, jifanye mbuzi ulogoma kwenda, jifanye namna yoyote ile unayoona uko poa, na mambo yatakuwa vizuri.

(5). Vipi kuhusu kitu ule mtandao wetu na or*l s*x? (chumvi)

Or*l s*x ni salama kabisa wakati wa ujauzito. Hata hivyo, ni muhimu kuepuka hewa kuingia ndani ya uke wako wakati ukiwa katika hali hii.
Wapo wale watu watundu ambao hugeuza uke kama pulizo na kujitia umahiri wa kutaka kulijaza hewa wakati wa kupeana raha.
Katika mazingira ya kawaida, ikiwa mnafurahia hili, hakuna tatizo, ila wakati wa ujauzito, hii ni hatari kwani inaweza kuleta madhara katika mishipa fulani ndani ya uke, ambayo iko na uhusiano na mishipa ya kuelekea kwenye mji wa uzazi.
Kuhusu ule mtandao wa vijana (Tigo), ambao kwa kawaida hauruhusiwi kutumika, hakuna wakati unaokuwa mbaya zaidi kuutumia kama wakati huu wa ujauzito.
Katika wakati huu, uke wa mwanamke mara nyingi unakuwa sensitive zaidi ya wakati akiwa hana ujauzito, na kuendekeza kuf**ana, kunaongeza hatari ya bakteria kuhamia kwenye uke na kusababisha magonjwa ambayo yatadhuru kiumbe kilichobebwa ndani.

(6). Kuna umuhimu wa kutumia kondomu?

Kama nilivyodokeza hapo awali, wakati wa ujauzito uchi wa mwanamke unakuwa sensitive zaidi kwa magonjwa.
Unaweza tu kuguswa na mwenzako ambaye hakuwa amenawa mikono uzuri na ikakusababishia tatizo fulani, hivyo basi, inashauriwa kutumia kondomu ikiwa:
mwenza wako aliwahi au ana maradhi ya maambukizi
uko kwenye mahusiano na zaidi ya mtu mmoja
umeamua kungonoka na king'asti kipya wakati wa ujauzito

(7). Je, kukojoa au ku-squi*t mara kwa mara kunaweza haribu mimba?

Hapana. Licha ya ukweli kuwa wakati wa ujauzito uke huzalisha kemikali ambazo ni mahususi kwa ajili ya kumkinga mjamzito na uvamizi wa bakteria wowote wanaoweza kuwa tishio kwa ujauzito wake, na kwamba kemikali hizi wakati mwingine huweza kuhitilafiana na lile bao analopiga mwanamke na hivyo kumletea hali fulani ya kukwaza, kwa ujumla wake hakuna baya linaloweza kusababishwa na kukojoa au kufika kileleni .
Na wala kufanyana hakuwezi kuathiri kwa namna yoyote ile muda wako wa kujifungua (kuuchelewesha au kuuwahisha)

(8). Je, ni wakati gani mwanamke mjamzito anatakiwa kuacha kufanya mapenzi?

Ijapokuwa wapo wanawake wengi ambao wanaweza kabisa kuendelea kufurahia kufanywa hadi siku wanakwenda kujifungua , kuna baadhi ya nyakati mshauri wako wa afya anaweza kukushauri kuacha ngono kutokana na moja au yote kati ya yafuatayo:
umekuwa na tatizo la kujifungua kabla ya muda muafaka kabla ya ujauzito ulio nao
umetokewa na tatizo la kutokwa na damu kwenye uke
umekuwa ukitokwa na ute fulani ambao wataalamu wanauita kwa jina la "amniotic fluid"
umekuwa na tatizo la kwenye mlango wa uzazi, ambalo kitaalamu linajulikana kama cervical incompetence
kondo la nyuma limesambaa na kuziba kabisa mlango wa uzazi na kuanza kujitokeza kwa nje (placenta previa)

(9). Je, kuna tatizo lolote ikiwa huhitaji kufanya?

Hapana, na hii ni hali ya kawaida sana kwa baadhi ya wanawake wanapokuwa wajawazito, ama kutokana na hofu inayokuwa vichwani mwao kuwa atapata madhara kwa kufanya hivyo, au kutokana tu na aina ya homoni zinazozalishwa mwilini wakati huo.
Kuna mengi mnaweza kufanya bila kuhusisha maingiliano ya kimwili na ambayo yanaweza kumfanya mwanamke kuridhika anapokuwa katika hali hiyo.

(10). Ni baada ya muda gani toka kujifungua mwanamke anaweza kuendelea kufanya mapenzi?

Iwe kwa njia ya upasuaji au kwa njia ya kawaida, inaeleweka wazi kuwa baada ya kujifungua, mwanamke anakuwa na hali fulani ya mwili kuchoka, hali ambayo ni ya kawaida.
Ingawa wapo ambao wanaweza kujihisi wanamudu kushiriki tendo la ndoa kabla, lakini wataalamu wanashauri kuwa wakati mzuri wa kurejea kufanyana na mwenzio baada ya kujifungua, inakuwa ni baada ya kupita wiki sita.


[KichekeshoV.gif] ๐Ÿ‘‰SMS Mafua ndiyo hii

[Kitendawili…!] ๐Ÿ‘‰Nilikwenda nikichoma nikarudi nikichoma

[Fumbo Fumbo] ๐Ÿ‘‰Je, moshi ulielekea upande gani?

Endelea kusoma makala hizi zifuatazo;

a.gif KUJUA JINSIA YA MTOTO WAKATI WA UJAUZITO

Ujauzito ni kipindi kinachoweza kuwa cha furaha hasa kwa wazazi watarajiwa. Katika kipindi hiki shauku kubwa huwa ni kujua mtoto atayezaliwa ni wa kike au kiume?.. soma zaidi

a.gif JINSI YA KUPATA MTOTO WA KIUME AU KIKE

Watu wengi hutamani kupata mtoto wa jinsia wanayoipenda. Nini nifanye ili nipate mtoto wa kike au kiume? Je kuna dawa au vyakula vya kusaidia kupata mtoto ninayemtaka? Siku gani nikikutana na mwenzangu naweza pata mtoto wa kiume au kike? Na maswali mengine mengi huonesha shauku kubwa ya kupata mtoto wa jinsia uipendayo… soma zaidi

a.gif KUFANYA MAPENZI BAADA YA KUJIFUNGUA

Unaweza ukawa unajiuliza ni wakati gani salama kuanza kufanya mapenzi baada ya kujifungua na kama kuna madhara kwa mtoto wako anayenyonya. Kuna dhana nyingi ambazo huzunguka suala hili ikiwemo kumbemenda na kutopata ujauzito mara baada ya kujifungua… soma zaidi

a.gif Uhusiano wa ubakaji na uvaaji wa nguo fupi

Ubakaji kamwe siyo kosa linalomhusu yeye aliyebakwa; ni kosa
linalomuhusu yeye aliyebaka. Unachovaa hakimpi mtu yoyote
haki ya kukubaka wewe. Wengi wanaobakwa huwa mara nyingi
hawakuvaa nguo fupi wakati wanabakwa. Ni maamuzi yako nini
uvae, ingawaje kama nguo unazovaa zinasababisha wengine
kupata mheko kutokana na mavazi yako, ni muhimu ufahamu
kuwa unaweza ukasababisha matatizo juu yako mwenyewe.
Uvaaji wa nguo ambazo jamii
inayokuzunguka hawaziruhusu
inaweza ikasababisha watu
wakakufedhehesha au kukutishia
ubakaji kila mara. Ubakaji ni
mbaya kwa sababu unasababisha
kuvunja haki za bindamu na
kumwacha mwathiriwa na
maumivu kimwili na kisaikolojia.
Katika hali yoyote mtu hana haki
ya kumbaka mwingine… soma zaidi

a.gif Kampeni ya usafi na Utunzaji wa mazingira

Kampeni hii ilianzishwa na Melkisedeck Leon Shine mwaka 2018.
Lengo la kampeni Hii ni kuhamasisha watu kusafisha na kutunza mazingira yao kwa manufaa yao ya sasa na kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Kampeni hii inaamini kuwa mazingira yakisafishwa na kutunzwa vizuri yanaweza kuwa msaada kijamii, kiuchumi na kiafya kwa kizazi hiki na kizazi kijacho… soma zaidi

a.gif Tabia 10 zinazoweza kuharibu figo

1.Kubana mkojo kwa muda mrefu
2.Kutokunywa maji ya kutosha kila siku
3.Kutumia chumvi nyingi kuliko kawaida
4.Kula nyama mara kwa mara au mara nyingi
5.Kutokula chakula cha kutosha.. soma zaidi

a.gif Dawa gani za kulevya ni hatari zaidi?

Kwa ujumla dawa zote za kulevya zinaweza kuwa ni za hatari. Kati ya dawa zilizohalalishwa kisheria nikotini, ambayo i ipo kwenye sigara, ndiyo hasa ya hatari. Inawezekana kuwa umeshakuwa tegemezi kwa sigara. Hii i ii ina maana ubongo wako utaizoea nikotini na utahitaji nikotini zaidi na zaidi i i ili kuendelea kuwa na hali nzuri. Nikotini pia ni hatari zaidi kwa sababu vijana mara nyingi huanza kutumia sigara kabla ya kuanza kutumia dawa kali zaidi… soma zaidi

a.gif Jinsi ya kupika Biskuti Za Kopa Za Kunyunyuziwa Sukari Za Rangi

Unga vikombe 2 ยผ.. soma zaidi

elimu-sayansi-na-tekinolojia.png

.

afya-mapishi-na-lishe.png
KADI-TUKUTANE-MZAZI.JPG
vichekesho-bomba-vya-siku.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.