Je, mtu anaweza kuzuia kupata mimba baada yakujamiiana bila kinga (kufanya ngono zembe) kwa mfano amebakwa

Mpendwa Msomaji, baada ya kukuandalia makala inayopendwa kuhusu; Unamkabidhi Moyo kibaka wa mapenzi unategemea nini!!, sasa nimekuandalia makala hii kuhusu;

Je, mtu anaweza kuzuia kupata mimba baada yakujamiiana bila kinga (kufanya ngono zembe) kwa mfano amebakwa.

Endelea kefurahia makala nzuri kila siku unapotembelea tovuti hii.

USIKOSE HIIπŸ‘‰ Jinsi ya kupika Biskuti za kokoa

Je, mtu anaweza kuzuia kupata mimba baada yakujamiiana bila kinga (kufanya ngono zembe) kwa mfano amebakwa

By, Melkisedeck Shine.

Kama umebakwa au kulazimishwa kujamiiana unaweza kupata
huduma katika hospitali, kituo cha afya , zahanati au kutoka
kwa mhudumu wa afya ambaye atakupatia vidonge vya dharura
vya kuzuia mimba. Hivi ni vidonge ambavyo vinatumika ili
kupunguza uwezekano wa kupata mimba kama ulijamiiana bila
kinga, au umesahau kutumia njia yako ya uzazi wa mpango au
ulilazimishwa kujamiiana.

Ili ufanye kazi, njia hii ya dharura ya kuzuia mimba inatakiwa
itumiwe ndani ya saa 120 (ndani ya siku tano) baada ya tukio.
Inakuwa vizuri zaidi kama njia hii ya dharura itatumika punde
bila kusubiri kwani kwa kufanya hivyo, ufanisi wake unakuwa
wa kuaminika zaidi.

Hii njia ya dharura inazuia tu mimba kutungwa, haiwezi kusababisha
kutoka kwa mimba pindi mimba ikishatunga. Utakapotafuta
msaada wa kupata huduma ya vidonge vya dharura
vya kuzuia mimba hasa kwa wale waliobakwa au kulazimishwa ,
mwombe mhudumu akusaidie kupata huduma ya kuzuia maambukizo
ya UKIMWI. (Post exposure prophylasis). Unaweza
kupata taarifa zaidi kwa mtoa huduma wa uzazi wa mpango
kwenye kliniki za serikali, kliniki za UMATI, kliniki za Marie
Stopes au sehemu yoyote wanapotoa njia za kisasa za uzazi
wa mpango.

Unaweza kusoma makala mpya nzuri kila unapotembelea website hii wakati wowote. Baada ya kusoma makala hii kuhusu; Je, mtu anaweza kuzuia kupata mimba baada yakujamiiana bila kinga (kufanya ngono zembe) kwa mfano amebakwa, sasa endelea kusoma makala hizi nyingine nzuri nilizokuandalia;

FURSA..! Kuna nafasi za kazi 100.

Au soma zaidi hapa

.

ndugu.gif
Ndugu.gif