Tafuta

Unatafutwa na marafiki zako wa zamani Bado wanakupenda sana ndio maana wanakutafuta

👉SOMA ZAIDI HAPA...

👉 IBILISI NA DHAMBI👇✔

IBILISI NA DHAMBI

Somo: Waebrania 2: 9 - 18

Ni kweli Biblia inamwongelea Ibilisi. Ibilisi ni nini au ni nani? Neno la Kiyunani ni ‘diabolos’. Hebu tuone kama Biblia inaweza kutupa jibu yenyewe.

Katika 1 Yohana 3:8 tunapewa sababu ya Mungu kumtuma Yesu; ni, “Ili azivunje kazi za Ibilisi.” Alidhihirishwa kusudi anayofanya Ibilisi yasiwe yakishinda. Katika Waebrania 2:14 tunaambiwa pia kuwa, Yesu alikuja amharibu Ibilisi na kazi zake.

Waebrania 2:14 Maana
“Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo,
ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu ya mauti yaani Ibilisi”. Waumini wana damu na mwili (ni binadamu); na Yesu alikuwa kama wao.
Yesu alikufa ili aweze kumwangamiza yeye aliye chanzo cha kifo ambaye ni Ibilisi (yaani dhambi).

Huu msitari unachosema ni kwamba, Yesu alizaliwa kama anavyozaliwa mtu; na hili ni ili aweze kumwangamiza Ibilisi, kwa kufa msalabani.

Tujiulize: kama Ibilisi angekuwa kiumbe kisicho cha kawaida kwa namna yoyote, Yesu angewezaje kwa kufa kwake kukiangamiza? Na kama kimeangamizwa hakiko basi!

Tunajua ya kuwa dhambi ndiyo iletayo mauti; mshahara wa dhambi ni mauti. Kwa hiyo, Ibilisi ambaye Yesu alimwangamiza katika Waebrania 2:14 alikuwa hasa ni nguvu ya dhambi, iliyokuwa ndani yake. Nguvu hiyo iko ndani yetu sisi wote. Kumbuka: Yesu aliirithi hulka hii kupitia kwa mama yake, Mariamu. Katika Waebrania 9:26 tunaambiwa kuwa:
“Katika utimilifu wa nyakati, (Yesu) amefunuliwa, azitangue dhambi kwa dhabihu ya nafsi yake”.

YESU ALIMSHINDA = YESU ALIISHINDA NGUVU YA
(‘ALIMWANGAMIZA’) IBILISI DHAMBI NDANI YAKE

Yesu aliishi maisha makamilifu; hakuitii dhambi. Tunaambiwa: “Alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi” (Waebr. 4:15). Sisi tunajaribiwa, tunaanguka. Yesu alijaribiwa lakini kamwe hakushindwa; hakuanguka. Aliweza kuishinda dhambi kwa namna hii, kwa kuwa alikuwa Mwana wa Mungu.

Alipambana na dhambi maisha yake yote, na hatimaye msalabani aliibomoa kabisa dhambi kwa kuishinda ile hulka iliyomfanya ajaribiwe. Kwa sababu hiyo, Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, na kumpa ‘mwili wa utukufu’, usiojaribika kwa dhambi na usiokufa.

Kwa hiyo Ibilisi ni nini?
Ibilisi na dhambi ni kitu kile-kile. Yote ambayo Biblia inasema juu ya Ibilisi, inasema pia juu ya dhambi:
-Ibilisi ana uadui na Mungu …ndivyo ilivyo dhambi
-Ibilisi anamjaribu mtu …ndivyo ilivyo dhambi
-Ibilisi ni mdanganyifu…ndivyo ilivyo dhambi
-Ibilisi ana nguvu ya mauti…na dhambi inayo
-Ibilisi aliangamizwa kwa kifo cha Kristo…ndivyo ilivyokuwa dhambi.

Kwa kulinganisha hivi tunaona kwamba, Ibilisi na dhambi ni kitu kimoja. Kwa hiyo dhambi inatoka wapi? Biblia ina jibu kwa swali hili, pia. Dhambi inatoka katika mioyo yetu wenyewe. Yesu aliwahi kusema:
“Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu. Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi” (Marko 7:21-23).

Mambo haya mabaya hayapo tu katika mioyo ya watu wabaya. Hata watu wanaoonekana bora kabisa, wana uovu mioyoni mwao. Mtume Paulo akiwa ni mtu mwema kama alivyokuwa, aliona vigumu kufanya yaliyo sahihi, na rahisi kufanya yasiyo sawa. Anasema katika Warumi 7:18 kuwa, ndani ya mwili wake, ‘halikai neno jema’.

Yakobo anatupa ujumbe huo-huo. Ni kutoka ‘ndani’ yetu, na sio kutoka nje tunapopata majaribu ya dhambi. Anasema:
“Kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa. Halafu, ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti” (Yak. 1:14, 15).

Ingawa kifungu hiki kutoka katika Yakobo kinaongelea majaribu, hakitaji Ibilisi hapa. Kila mtu anajaribiwa na mawazo yake mwenyewe mabaya, yakimvuta na kumdanganya.

IBILISI NI MSUKUMO WA DHAMBI ULIO NDANI YA HULKA YA MWANADAMU

Ibilisi aliyemjaribu Yesu
Tulikwisha kuona katika Somo la 17 kuwa, yule mjaribu wa Yesu asingeweza kuwa Ibilisi anayeishi. Dunia ni mali ya Mungu na vyote viijazavyo (Zaburi 24:1). Yeye ndiye anayeidhibiti, na hakuna kiumbe kisichoonekana ambacho kingeweza kumpa Yesu, “Enzi hii yote na fahari yake”.

Zaidi ya hayo, tunajua Yesu asingelifuata ‘dudu’ la namna hiyo akijua kuwa ni ovu, kwenda nalo Yerusalemu au popote kwingine!

Kama tulivyoona, ‘Ibilisi’ katika majaribu hayo yalikuwa ni mawazo mabaya yaliyokuwa yakimjea Yesu; tamaa iliyokuwa ikimvuta kutaka kukwepa machungu na mateso ya msalabani.

Ni kwa nini ‘Ibilisi’?
Ni kwa nini Biblia mara nyingi inalitumia neno ‘Ibilisi’ badala tu ya kusema ‘dhambi’. Na kwa nini inamwongelea Ibilisi kama vile inasemea mtu mwenye mamlaka makubwa? Kwa hakika, ni ili tuweze kutambua jinsi dhambi ilivyo na nguvu na inavyodanganya.

Tunahitaji kulielewa hili vizuri kabla hatujaweza kutambua hasa jinsi wote tunavyohitaji kuokolewa na dhambi. Tunapokuwa tumetambua haja hii, tunaweza kuanza kuelewa lile Bwana Yesu alilofanya kwa ajili yetu katika ushindi wake juu ya dhambi.

Muumba mmoja mwenye uweza wote.
Mungu ni Mkuu juu ya vitu vyote. Angeweza kweli kupingwa na kiumbe kiovu kiwe ibilisi au shetani? Tunajua isingewezekana.

Lakini wazo la uwepo wa mamlaka iliyo kubwa ya uovu inayopingana na Mungu, limekuwa likishikiliwa na mataifa tangu enzi za kale. Waajemi wa zamani waliamini juu ya uwepo wa mamlaka mbili kuu, moja ikiwa ni Mungu na ya pili ikiwa ni ya shetani. Ya kwanza ilihesabiwa kuendeana na uwepo wa nuru na wema, na ya pili, giza na uovu. Kwa kuisahihisha imani hiyo potofu, Mungu alituma ujumbe kupitia kwa nabii Isaya, akisema:

“Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine; zaidi yangu mimi hapana Mungu. Nitakufunga mshipi ijapokuwa hukunijua; ili wapate kujua toka maawio ya jua, na toka magharibi, ya kuwa hapana mwingine zaidi ya mimi; mimi ni BWANA, wala hapana mwingine. Mimi naiumba nuru, na kulihuluku giza; mimi nafanya suluhu, na kuhuluku ubaya; Mimi ni BWANA, niyatendaye hayo yote” (Isaya 45:5-7).

(Neno ‘ubaya’ hapa tusilichanganye na ‘dhambi’. Lina maana ya matatizo, kama ambavyo Mungu anavyowaletea wadhambi wasioyatii mapenzi yake).

Kuna mamlaka iliyo kuu na ni moja tu juu ya mbingu yote, inayoyapanga mambo yote. Mamlaka hii ni ya Muumba mmoja tu, aliye Mkuu sana, anayeyashikilia mambo yote kwa Neno la uweza wake. Nguvu ya dhambi iliyoko katika moyo na maisha ya mwanadamu, ndio upinzani pekee anaoupata Mungu.

Dhambi ni tatizo kubwa
“Toka mbinguni BWANA aliwachungulia wanadamu, aone kama yuko mtu mwenye akili, amtafutaye Mungu. Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja, hakuna atendaye mema, la! Hata mmoja” (Zaburi 14:2,3).

Hivi ndivyo mwandika–Zaburi anavyoweka. Katika Warumi 3:23 Paulo anatuambia kitu hicho-hicho, anaposema:
“Wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu”. Maneno hayo hayavutii kusoma. Hakuna kati yetu anayependa kuambiwa, ‘umekosa!’

Kila tunapokuwa tumekosea, tunajaribu kuweka visingizio, au kumlaumu mtu mwingine. Hatupendi kukubaliana na ukweli kuwa tuna hulka ya uovu. Lakini, bila kufanya hivyo hatuwezi kuanza kuelewa lile Mungu alilotufanyia katika kumtuma Yesu Kristo, na hatuwezi kuuitikia upendo wake.

Si wengi wanaotulia na kufikiri jinsi Mungu alivyoyakusudia wayaishi maisha yao, na wachache wanaojaribu kufanya hivyo haraka wanajikuta katika mgogoro mkubwa. Yeremia akiusemea moyo wa mwanadamu ulivyo, anasema ni: “Mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha” (Yer. 17:9).

Kila mtu ambaye kikweli anajaribu kuishi maisha mazuri mbele ya Mungu, atasikitishwa na hili. Paulo anaelezea vizuri tatizo linalokuja katika waraka wake kwa Warumi, anaposema:
“Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati. Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo” (War. 7:18,19).

Hatuwezi kujizuia. Sasa tunapaswa tufanye nini?
Kama tumetambua dhambi ilivyo ndani yetu, ni lazima tujitahidi kuiepuka. Hiyo ndio maana ya kutubu; kugeukia upande na kwenda mbele.

Hili ni jambo ambalo hatuwezi kulifanya bila ya msaada wa Mungu na mafundisho ya Neno lake. Kupitia katika mauti ya Yesu, tunaweza kumkaribia Mungu na kupata msamaha wa dhambi, na kuwa na tumaini la uzima.

Toba inaanza tunapotambua jinsi tulivyo wadhambi na jinsi watu wote walivyo waovu. Toba inakuja tunapoitambua dhambi yetu na ubaya ulio ndani yetu (hili ni la muhimu sana).

Tunapotubu kwa utambuzi, tunakuwa wafuasi wa Bwana Yesu tukimfuata na kuiendea njia yake. Yesu aliishi maisha yaliyo makamilifu. Kuwa ‘wafuasi wake’ maana yake ni kujitahidi kwa uwezo wetu wote kuiepuka dhambi; kujaribu kuishi alivyoishi. Paulo anasema:
“Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi” (Warumi 6: 1, 2).

Hatuwezi kuendelea na namna yetu ya maisha tuliyoizoea. Mbele zaidi katika Sura hiyo ya Warumi 6, mtume Paulo anasema:
“Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake; wala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi; bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hai baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki” (ms. 12-13).

Itatubidi tuendelee kupambana na dhambi siku zote
Kitu kimoja ni cha uhakika: hatutaweza kuvishinda vita hivi katika maisha haya. Hatutakaa tufikie wakati ambao tutaweza kusema, “Mapambano dhidi ya dhambi yamekwisha, na tumeshinda”.

Kama isingekuwa ni kwa msamaha wa Mungu ulio katika Kristo, uliopo kwa ajili yetu katika maisha yetu ya kila siku, tungeona mapambano yetu kuwa kitu kisichowezekana. Lakini, siku moja vita hii itakwisha!

Bwana Yesu atakaporudi duniani kuusimamisha Ufalme wa Mungu, wale watakaokuwa wamekuwa wafuasi wake waaminifu watabadilishwa; watafanywa wawe kama malaika. Watapewa uzima wa milele, kama ulivyojifunza katika Somo la 19, 25 na 27.

Lakini haitakuwa hivyo tu. Hulka yao itabadilishwa kiroho, dhambi haitakuwa tena na nguvu ndani yao. Hawatakuwa tena wakitamani kufanya mambo yasiyo sawa au kufikiri mambo mabaya. Vita itakuwa imekwisha na dhambi itakuwa imeshindwa milele katika kufikiri kwa mfuasi. Tunasoma juu ya hili katika 1 Wakorintho 15:51-57.

Muhtasari
1. ‘Ibilisi’ ni neno la Kibiblia linalosimama badala ya nguvu ya dhambi katika hulka ya mwanadamu.
2. Yesu aliishinda nguvu hiyo ndani yake; ndio maana inasemwa kuwa alimshinda shetani au ibilisi.
3. Dhambi ni uovu, na haikubaliki kwa Mungu. Watu wote wanafanya dhambi au wamefanya dhambi (kasoro Yesu tu).
4. Ni lazima tutubu. Hili linamaanisha kusikitishwa kiukweli na dhambi zetu, na kukubali kwamba tumekosa.
5. Ni lazima tutubu na kuamini kuwa Mungu atatusamehe, hata kama tumekosea baada ya kuwa wafuasi.

Vifungu vya kusoma: Yakobo 1:12-27, Warumi 6, Warumi 7:14-25

Mistari ya kushika: Yakobo 1:14, 15
“Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa. Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti”.

🙉🙉🙉Usisahau kushare posti hii kuhusu (IBILISI NA DHAMBI).👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome💯✔

Marafiki zako wa zamani utawakuta hapa sasa Bado wanakupenda sana na wanakungoja kwa hamu kubwa

👉SOMA ZAIDI HAPA...

Marafiki-wa-enzi.GIF

.