.

Kichekesho%20Kipya Unaweza kuonana na watu mliopotezana hapa Bado wapo na wanakutafuta sana
πŸ‘‰SOMA ZAIDI HAPA...Kizuri

πŸ‘‰ Hatua za jinsi ya kuanzisha mradi wa nyukiπŸ‘‡βœ”

IMG_20170703_131010.jpg

Imehaririwa na; Melkisedeck Leon Shine. Tarehe 30 Jan 2016 03:53. [Legal & Authority]


Hatua za jinsi ya kuanzisha mradi wa nyuki

Hatua zinazostahili kufuatwa unapoanzisha mradi wa ufugaji wa nyuki

Hatua ya kwanza katika mikakati ya mradi wa ufugaji wa nyuki ni kupata ufahamu wa uhusiano baina ya nyuki na mwanadamu katika eneo lako.Zungumza na wale wanaojihusisha na nyuki.Andamana nao wakifanya kazi na nyuki.
Ikiwa hauna ujuzi wa kufanya kazi na nyuki,kuna uwezekano wa kujifunza mengi kutoka kwa wafugaji wa nyuki katika eneo lako.Kwa kufahamu jinsi wanavyofanya kazi,unaweza kutoa maoni ya kuboresha kwa kustahilika,na itakuwa rahisi kutumia teknolojia ya ufugaji wa nyuki inayofaa katika eneo lako.
Pia ,unafaa kupitia visa kadhaa vya kung’atwa kabla ya kujitolea kufuga nyuki.Kung’atwa na nyuki ni sehemu muhimu katika ufugaji wa nyuki.Mfugaji wa nyuki anapaswa kukabiliana nayo.
Pindi tu unapoelewa uhusiano baina ya nyuki wa kienyeji na mwanadamu,mawazo ya kuanzisha utaratibiu ulioboreshwa unaweza kuundwa.Yafuatwayo ni maswali yanayofaa kutiliwa maanani:
1.Ni nani wa kufanya kazi naye?

2.Vifaa gani vinafaa kutumiwa?

3.Ni wapi pa kuuza bidhaa za mzinga?

Ikiwa ndio unaanza na nyuki itakuwa bora ikiwa unafanya kazi na mtu mmoja ama wawili katika eneo lako.Kwa kuchagua wakulima wanaoheshimika na uhusiano mzuri na jamii ,juhudi zako zitaongezeka maradufu.Ukifuga nyuki mwenyewe na kutumia utaratibu tofauti na ule unaotumiwa katika sehemu yako
ni hatua katika mwelekeo unaofaa.Habari zitasambaa na punde ama baadaye utakuwa ukizungumza na marafiki ama majirani zako kuhusu ufugaji wa nyuki.
Mara kwa mara anza ufugaji wa nyuki na angalau mizinga miwili.Hii itakupatia fursa kulinganisha maendeleo baina ya mizinga,na la muhimu zaidi,inaruhusu mradi kuendelea ikiwa koloni moja itaangamia.Pia,udhibiti wa mizinga yote badala ya mzinga mmoja binafsi unaweza kusisitizwa.
Mabadiiliko huchukua muda.Ni lazima kuanza na wazo.Utoaji wa kufanikiwa wa wazo ni matarajio yanayoweza kutimilika ili kuanzisha utaratibu bora kwa uhusiano baina ya nyuki na binadamu katika maeneo mengine.
Katika kupanga mradi,weka malengo yanayoweza kutimilika.Mradi mdogo,unaofaulu,una maana kuliko mkubwa uliojaribiwa na haukufaulu.
Vifaa vitakavyotumiwa kwenye mradi hutugemea hali iliyoko.Unafaa kutathmini uwepo wa vifaa vinavyohitajika vile vile pia msaada wa kiufundi uliopo katika kuchagua aina ya ama aina za vifaa vya mzinga vinavyofaa.
Tambua watu katika sehemu yako wanaoweza kutengeneza vifaa vya ufugaji wa nyuki ujenzi wake unaweza kuwa mafanikio kivyake.Inawza kuhitaji uvimilivu unaporatibu kupata vifaa pamoja.
Milango ya uuzaji iliyopo kwa bidhaa za mzinga katika maeneo mengi.Tafuta watu ambao tayari wanatumia asali ama nta ya nyuki.Mara kwa maara wana hamu ya usambazaji thabiti wa bidhaa za hali ya juu.Ikiwa hawatumii asali,waoka mikate na watengenezaji wa peremende wana uwezekano wa kutoa soko.Watafute pia wale ambao wanaweza kutoa soko kwa nta ya nyuki.

πŸ™‰πŸ™‰πŸ™‰Usisahau kushare posti hii kuhusu (Hatua za jinsi ya kuanzisha mradi wa nyuki).πŸ‘ Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasomeπŸ’―βœ”

Nini maoni yako kuhusu, Hatua za jinsi ya kuanzisha mradi wa nyuki? Niandikie hapa
Add a New Comment
or Sign in as Wikidot user
(will not be published)
- +

IMG_20180109_192548.jpg

Ujumbe wangu kwako kwa sasa

"Tofauti ya maskini, tajiri na mwenye uchu/tamaa ni kwamba; Mtu maskini anafanyakazi ili apate chochote, tajiri anafanya kazi apate vitu vingi lakini mwenye uchu/tamaa anafanya kazi apate vitu vyote kitu ambacho hakiwezekani kwa hali ya kawaida."

kj.gif

.

.

b.gif

Mimi ni Melkisedeck Shine Mmiliki, Mwandishi /Mhariri. Karibu tena kila siku.

MAWASILIANO | KUHUSU MWANDISHI

Blog nyingine maarufu ndani ya AckySHINE.com

| Vichekesho | Videos | Picha | Ujasiriamali | Mahusiano | Kilimo & Mifugo | Katoliki | Afya & Mapishi | Hadithi | Misemo | SMS