Tafuta

.

Here a data collection expert For both qualitative and quantitative data.

πŸ‘‰SOMA ZAIDI HAPA...

πŸ‘‰ Athari za muda mrefu za pombeπŸ‘‡βœ”

Athari za muda mrefu za pombe hutapakaa baina ya uwezekano wa faida za kiafya kwa watumiaji wa viwango vya chini vya pombe hadi madhara makubwa katika hali ya matumizi mabaya ya pombe kwa muda mrefu. Viwango vya juu vya matumizi ya pombe huhusiana na ongezeko la hatari ya kuendeleza ulevi, ugonjwa wa moyo, kutofyonza vyakula, ugonjwa sugu wa kongosho , ugonjwa wa ini kutokana na pombe, na kansa. Uharibifu kwa mfumo mkuu wa neva na mfumo wa neva za pembeni unaweza kusababishwa matumizi kila mara ya pombe. Matumizi ya pombe kupita kiasi kwa muda mrefu yanaweza kuharibu takribani kila kiungo na mfumo katika mwili. Ubongo unaokua wa kijana aliyebaleghe huwa hasa katika hatari kubwa ya kudhurika na sumu ya pombe.

Kihistoria, madaktari wametetea pombe kwa faida zake za kiafya na hivi karibuni kwa ajili ya uwezo wake wa kulinda watumiaji dhidi ya ugonjwa wa moyo. Kuna ushahidi wa faida kwa mishipa ya moyo inayotokana na kutumia kinywaji 1- 2 kwa siku, hata hivyo, faida za kiafya kutokana na unywaji pombe kwa wastani ni swala lenye utata. Shauku zimetolewa kuwa sawa na ilivyo katika sekta ya dawa, wadau wa sekta ya pombe piawamehusika katika kutilia chumvi faida za kiafya za pombe. Pombe inapaswa kuonekana kama dawa ya burudani yenye uwezo mkubwa wa kusababisha athari mbaya kwa afya na hipependekezwi kwa-ulinzi wa moyo badala ya mbinu nyinginezo za salama na zilizothibitika za jadi kama vile lishe bora mazoezi na tiba za dawa.

Baadhi ya wataalamu wanadai kuwa faida za matumizi ya pombe ya wastani zinaweza kupitwa na ongezeko la hatari ikiwa ni pamoja na majeraha, vurugu, uharibifu wa mimba, aina fulani za saratani, ugonjwa wa kongosho na presha. Kwa vile faida bainifu za kiafya za matumizi ya pombe ya wastani ni ndogo kwa watu walio katika hatari ndogo ya kupata maradhi ya moyo, wataalamu wengine wanatahadharisha itumike kwatahadhari kwa sababu ya uwezekano kwamba kupendekeza matumizi wastani ya pombe kunaweza kusababisha la hatari ya matumizi mabaya ya pombe, hasa miongoni mwa vijana. Manufaa haya ya matumizi wastani ya pombe yanapitwa na hatari za matumizi ya pombe wastani.

Soma zaidi hapa

πŸ™‰πŸ™‰πŸ™‰Usisahau kushare posti hii kuhusu (Athari za muda mrefu za pombe).πŸ‘ Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasomeπŸ’―βœ”

wadogo.gif

.