Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
☰
AckyShine

Jinsi ya kuongeza mvuto kwa mpenzi wako

Featured Image

Kama umeshushwa thamani unakuwa kwenye hatari ya kuachwa. Hata kama mwenzako alikuwa ameshafikiria suala la kuingia kwenye ndoa na wewe lakini kwa sababu ameshakushusha thamani ndoa inaweza kuyeyuka. Ukiwa kwenye ndoa ni hatari zaidi maana mwenzako hukuchukulia wa kawaida mazoea huzidi na hapo ndipo uhitaji wa kuwa na mwingine wa pembeni unapoanzia. Haoni cha muhimu tena kwako, ndiyo maana wazo hilo huvamia ubongo wake kwa kasi sana.

Itafikia hatua, kama upo ndani ya ndoa, mwenzako atagoma kuongozana na wewe na kama ikitokea hivyo mkikutana na rafiki zake njiani hatakutambulisha. Hisia kwamba hamuendani humwingia.

UNAFANYAJE SASA?

Kubwa unalotakiwa kufahamu rafiki yangu mpendwa, suala la kupanda au kushuka thamani lipo mikononi mwako. Yapo mambo ambayo ukiyazingatia, mwenzako hawezi kukuchoka na kufikia hatua ya kukushusha thamani.

Tayari tumeshaona athari zake lakini hapa sasa nataka kukupa mbinu ambazo ukiwa nazo makini basi itakuwa rahisi kwako kubaki namba moja na mtu muhimu zaidi (ndiyo inavyotakiwa kuwa) kwa mpenzi wako maana ni haki yako.

ANZIA MWANZO

Ni rahisi zaidi kulinda thamani yako kuanzia mwanzo wa uhusiano wenu. Ikiwa tayari mmeshakomaa halafu tatizo hilo likajitokeza, hutumika nguvu nyingi zaidi kulirekebisha kuliko kujizatiti kuanzia mwanzo wa uhusiano. Ni mambo gani hayo? Twende hapo chini.

CHUNGA KAULI ZAKO

Naomba ieleweke wazi kuwa mada hii ni maalum zaidi kwa wanawake. Kitu muhimu cha kwanza kabisa kwa mwanamke ambaye anataka kuilinda thamani yake kwa mpenziwe ni kupima sana kauli zake.

Acha kuropoka hovyo, pima maneno yako na ikiwezekana kama unadhani kuna jambo huna uhakika nalo usizungumze kabisa. Katika eneo hili, uwe makini zaidi mnapokuwa na watu wengine. Kama mwanamke usiwe mchangiaji hoja sana.

Utulivu wako unaweza kuwa silaha kubwa ya kukufanya ubaki na thamani yako kama mwanamke anayejitambua.

USIRUHUSU MAPENZI

Msichana mwenye kujitambua na kufahamu thamani yake sawasawa hawezi kuruhusu mwili wake ujulikane na mwanaume harakaharaka. Onesha unajitambua na usikubali kirahisi kuuacha mwili wako uchezewe.

Mpe hoja; kwanza mapema, hajakuoa wala kukuchumbia, haraka ya nini? Wakati unawaza kuhusu kutoa penzi lako, lazima ufikirie kuhusu athari zinazoweza kukupata kwa kukurupukia mapenzi. Mwanaume ambaye bado hamjachunguzana na huna uhakika naye wa kutengeneza maisha, kichwani mwake hakuweki kwa asilimia kubwa.

Ukumbuke kwamba, ukipata matatizo yoyote – binafsi au yanayosababishwa na uhusiano wenu, anakuwa hana uwajibikaji wa asilimia kubwa kwa tatizo hilo. Utabaki wewe na matatizo yako!

Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

[products columns="2" ids="30827"]

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Jinsi ya Kuimarisha Ushirikiano na Uwiano katika Ndoa na mke wako

Jinsi ya Kuimarisha Ushirikiano na Uwiano katika Ndoa na mke wako

Kuimarisha ushirikiano na uwiano katika ndoa ni muhimu sana kwa ustawi na uimara wa uhusiano wako na... Read More
Jinsi Mwanamme Unavyoweza kubobea katika Mapenzi na Mahusiano

Jinsi Mwanamme Unavyoweza kubobea katika Mapenzi na Mahusiano

Read More
Vidokezo vya Kuwa na Mazungumzo ya Kina na Msichana

Vidokezo vya Kuwa na Mazungumzo ya Kina na Msichana

Kama kijana, kuna wakati unaweza kukutana na msichana na unataka kuzungumza naye kwa kina lakini ... Read More

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Usawa katika Mahusiano: Kujenga Umoja na Uwiano

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Usawa katika Mahusiano: Kujenga Umoja na Uwiano

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Usawa katika Mahusiano: Kujenga Umoja na Uwiano

Mahusiano ... Read More

Je, nini imani ya watu katika kuzungumza waziwazi juu ya ngono/kufanya mapenzi na kutokuwa na aibu?

Je, nini imani ya watu katika kuzungumza waziwazi juu ya ngono/kufanya mapenzi na kutokuwa na aibu?

Habari rafiki yangu! Leo tutaongea kuhusu umuhimu wa kuzungumza waziwazi juu ya ngono na kufanya ... Read More

Jinsi ya kusuluhisha Migogoro mke wako

Jinsi ya kusuluhisha Migogoro mke wako

1. Kuwa na Mawasiliano Mzuri: Anza kwa kuwa na mawasiliano mazuri na mke wako. Jenga mazingira ya wa... Read More
Jinsi ya Kuweka Mawasiliano Mzuri katika Familia: Njia na Vidokezo Vyema

Jinsi ya Kuweka Mawasiliano Mzuri katika Familia: Njia na Vidokezo Vyema

Mawasiliano mzuri katika familia ni muhimu sana kwa ustawi wa kila mmoja. Kwa uhusiano mzuri, wat... Read More

Jinsi ya Kuunda Mazingira ya Kujifunza katika Familia yako

Jinsi ya Kuunda Mazingira ya Kujifunza katika Familia yako

Jinsi ya Kuunda Mazingira ya Kujifunza katika Familia yako

Kujifunza ni muhimu sana katika... Read More

Jinsi ya Kuzungumza na mpenzi wako kuhusu mipango ya kustaafu na maisha baada ya kazi

Jinsi ya Kuzungumza na mpenzi wako kuhusu mipango ya kustaafu na maisha baada ya kazi

Kuzungumza na mpenzi wako kuhusu mipango ya kustaafu na maisha baada ya kazi ni muhimu katika kujeng... Read More
Jinsi ya Kukabiliana na Changamoto za Kifedha katika Familia

Jinsi ya Kukabiliana na Changamoto za Kifedha katika Familia

Karibu katika makala hii ambayo inalenga kuzungumzia jinsi ya kukabiliana na changamoto za kifedh... Read More

Kukabiliana na Kutofautiana kwa Tamaa katika Kufanya Mapenzi: Kuunda Ushirikiano wenye Kuridhisha

Kukabiliana na Kutofautiana kwa Tamaa katika Kufanya Mapenzi: Kuunda Ushirikiano wenye Kuridhisha

Kukabiliana na Kutofautiana kwa Tamaa katika Kufanya Mapenzi: Kuunda Ushirikiano wenye Kuridhisha... Read More

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kuendeleza na kudumisha stadi za uongozi

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kuendeleza na kudumisha stadi za uongozi

Karibu kwenye makala hii inayozungumzia "Jinsi ya Kusaidiana na Mpenzi Wako Katika Kuendelez... Read More