Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
☰
AckyShine

Wosia mzuri wa baba kwa mwanae

Featured Image

Mwanangu, mimi baba yako nimeishi miaka mingi kuliko wewe ndio maana unaniita baba. Ni kweli sijasoma kama wewe ulivyosoma Ila mambo niliyokutana nayo tangu nimezaliwa ni elimu tosha ambayo wewe huna. Sasa nataka nikupe Elimu hiyo ili ukijumlisha na elimu yako ya darasani ujue namna nzuri ya kuishi katika dunia hii iliyojaa mishangazo mingi.


Maisha ni jumla ya mambo yote unayoyatenda kila siku. Namaanisha kila unalolifanya Leo linaathiri maisha yako ya kesho kwa hali chanya au hali hasi. Na kama ni hali hasi ni kwa ukubwa gani halikadharika kama ni hali chanya ni kwa kiwango gani. Mwanangu kila jambo unalolifanya Leo huamua ni mlango gani Unaweza ingia Kesho lakini pia mlango upi huwezi ingia Kesho. Ndio maana ni muhimu kuijua Kesho yako ukiwa Leo.


Mwanangu ili ufanikiwe ni lazima ujue kuishi na watu vizuri. Na mimi sikushauri kabisa kwamba uwe na marafiki wengi. Kuwa na marafiki wengi ni moja ya eneo unaweza jitengenezea mtego mbaya wa kukuangamiza kesho yako. Mwenye hekima mmoja aliwahi kusema ajifanyiaye rafiki wengi ni kwa uangamivu wake mwenyewe. Mwanangu kwa kusema hivyo simaanishi uwe na maadui,hapana. Ila marafiki zako watakusaidia mlango unaotaka kuingia Kesho uingie kwa urahisi au kwa ugumu au usiingie kabisa na wakati mwingine Unaweza kuingia na wakahusika kukutoa kwa aibu kubwa. Ndio maana ni muhimu Kuwa na marafiki ila Kuwa nao wachache chagua kwa makini mno. Sio lazima kila akufaaye kwa dhiki ndiye awe rafiki. Kuna watu wanakufaa kwa dhiki Leo ila Kesho wakutumikishe Kuwa makini sana.


Mwanangu, kuwa makini sana na mahusiano yako ya kimapenzi maana yanagusa hisia zako na mtu unayehusiana naye moja kwa moja. Hivyo basi kuwa makini maana mahusiano hayo yanaweza kukufanya Kesho ukamkosesha raha utakayekuwa naye kama sio huyo uliyenaye leo ndie ukajaaliwa Kuwa naye Kesho. Mwanangu, Unaweza kuniona mshamba sababu ulimwengu wenu unaonekana kama haujali sana haya mambo ila tafadhari zingatia utakapofika Kesho utaelewa sana hiki ninachokuambia.


Mwanangu, jichunge sana na mambo unayoyafanya Leo na uwe muungwana na kupenda haki. Tamaa isikupeleke ukafanya mambo mabaya ambayo yatakulazimisha kutunza siri moyoni mwako hata kama utafika ile Kesho yako. Jiepushe kabisa na mambo mabaya ya siri ya nafsi. Hakuna utumwa mbaya kama utumwa ndani ya nafsi yako mwenyewe maana kila ukikumbuka nafsi itakusuta na kukukosesha raha ya kweli. Hivyo kubali na kuridhika na ulivyo kama huwezi kujiongeza kwa njia halali na za haki. Ni heri uwe masikini mwenye uhuru ndani kuliko uwe tajiri na maarufu mwenye siri mbaya ndani ya Moyo wako. Mwanangu tafadhari uwe makini sana.


Mwanangu, siwezi sahau kukwambia kuhusu Mungu. Maisha ya uchaji wa Mungu yatakuepusha na mengi. Hapa naomba unielewe kwamba usijifanye unamcha Mungu bali mche Mungu. Sio kwasababu unashida ya kufanikiwa ndio umche Mungu, hapana! Bali umche Mungu sababu ni Mungu na yeye ndiye anaijua Kesho yako vizuri kuliko wewe mwenyewe. Ukimshirikisha mambo yako na ukawa mwaminifu kwake hakika hatakuacha kamwe.


Mwanangu, usiku umeenda nenda kalale sasa ila usije ukapenda na kutamani waovu kwa uovu wao na wakakushawishi ujiunge nao. Tafadhari usikubali.


#Kizazi Ganzi#


JIFUNZE KUJIFUNZA


Mwl Makwaya
Kuwa Ni Kufanya.






Yafahamu Mambo Mbalimbali kuhusiana na Wanawake kwa Ku-Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE




Kitabu hiki kina topiki Zifuatazo;
1. Mambo anayohitaji mwanamke kutoka kwa Mwanaume
2. Mambo yanayowavutia wanawake kutoka kwa wanaume
3. Mambo wanayoyapenda wanawake wakati wa kufanya mapenzi
4. Dalili za mwanamke kicheche
5. Maswali ya kujiuliza kama mwanamke anakupenda kwa dhati au anakudanganya
6. Tabia za mwanamke anayekupenda lakini hawezi kusema
7. Ishara za mwanamke aliyevutiwa na wewe
8. Dalili za mwanamke anayeelekea kukukubali
9. Mambo ambayo mwanamke hawezi kukwambia
10. Njia za kudumisha na kuamsha mapenzi na mwanamke





Kitabu hiki ni Soft copy [pdf] kwa hiyo unaweza kusoma moja kwa moja kirahisi kabisa hata kwenye simu yako. Utatumiwa Kopi ya kitabu hiki kwenye email yako na utaweza kukihifadhi na kusoma wakati wowote utakaotaka.





[products columns="2" ids="30827"]


AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Jinsi ya Kujenga Maisha yenye Furaha na Ufanisi katika Familia yako

Jinsi ya Kujenga Maisha yenye Furaha na Ufanisi katika Familia yako

Karibu kwenye makala hii kuhusu jinsi ya kujenga maisha yenye furaha na ufanisi katika familia ya... Read More

Jinsi ya Kupenda na Kuwaunga Mkono Watoto wa Kambo: Kuleta Umoja katika Familia

Jinsi ya Kupenda na Kuwaunga Mkono Watoto wa Kambo: Kuleta Umoja katika Familia

Kupenda na kuwaunga mkono watoto wa kambo ni muhimu sana kwa ustawi wa familia. Watoto wa kambo w... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya historia na utamaduni wa jamii yenu

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya historia na utamaduni wa jamii yenu

Siku zote ni muhimu kuwa na mawasiliano mazuri na mpenzi wako, na moja ya mambo muhimu ni kuwasil... Read More

Kuweka Kipaumbele cha Kusamehe na Kusonga Mbele ili Kuwa na Amani na Furaha katika Familia

Kuweka Kipaumbele cha Kusamehe na Kusonga Mbele ili Kuwa na Amani na Furaha katika Familia

Kuweka kipaumbele cha kusamehe na kusonga mbele ni muhimu sana katika familia ili kuwa na amani n... Read More

Namna ya Kujenga Mahusiano ya Kujifunza na Kujua Mke Wako

Namna ya Kujenga Mahusiano ya Kujifunza na Kujua Mke Wako

Kujenga mahusiano ya kujifunza na kujua mke wako ni muhimu katika kukuza uhusiano wa karibu na kudum... Read More
Kuweka Kipaumbele cha Furaha na Ustawi wa Familia yako

Kuweka Kipaumbele cha Furaha na Ustawi wa Familia yako

Mafanikio ya maisha yako yanategemea sana furaha na ustawi wa familia yako. Familia yenye afya na... Read More

Njia za Kukuza Ushawishi wa Mwanamke katika Kufanya Mapenzi: Kuamsha Uwezo wa Kujiamini

Njia za Kukuza Ushawishi wa Mwanamke katika Kufanya Mapenzi: Kuamsha Uwezo wa Kujiamini

Kama mwanamke, unapambana na changamoto nyingi katika maisha yako ambazo zinaweza kukuzuia kufany... Read More

Jinsi ya Kuunganisha Kizazi: Kuweka Mipango na Kujenga Ushirikiano katika Familia

Jinsi ya Kuunganisha Kizazi: Kuweka Mipango na Kujenga Ushirikiano katika Familia

Kuunganisha kizazi ni muhimu sana katika familia. Ni jambo linalofanya familia iwe na nguvu na ku... Read More

Kujifunza na Kukuza Maarifa pamoja na Familia: Ulimwengu wa Elimu Uliojaa Upendo

Kujifunza na Kukuza Maarifa pamoja na Familia: Ulimwengu wa Elimu Uliojaa Upendo

Habari za leo! Ni furaha kwangu kuwakaribisha kwenye ulimwengu wa elimu ambao unajaa upendo. Leo,... Read More

Jinsi ya Kuelewa na kukabiliana na mabadiliko ya kijamii na kitamaduni na mpenzi wako

Jinsi ya Kuelewa na kukabiliana na mabadiliko ya kijamii na kitamaduni na mpenzi wako

Mabadiliko ya kijamii na kitamaduni huwa ni sehemu ya maisha yetu, na kwa wakati mwingine yanawez... Read More

Jinsi ya Kuwa na Shukrani kwa Familia: Kuwa na Moyo wa Kuthamini

Jinsi ya Kuwa na Shukrani kwa Familia: Kuwa na Moyo wa Kuthamini

Kuwa na shukrani kwa familia ni kitu muhimu kwa maisha yetu ya kila siku. Familia ni kitovu cha m... Read More

Jinsi ya Kuunda Mazingira ya Kuwasaidia Watoto Kufanikiwa Shuleni na Maisha

Jinsi ya Kuunda Mazingira ya Kuwasaidia Watoto Kufanikiwa Shuleni na Maisha

Karibu kwenye makala hii ambayo itakupa mwongozo wa jinsi ya kuunda mazingira ya kuwasaidia watot... Read More