Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
☰
AckyShine

Ishara 10 za mwanamke aliyekuzimia na anayekupanda

Featured Image

Ishara hizi zinaweza zikakusaidia kumgundua msichana anayekupenda, wasichana wanatofautiana ila wengi wao wana-share ishara tofauti. Mwanamke anayekupenda hatakosa kati ya hizi


 

Siyo kwamba ishara hizi zote anaweza kuwanazo msichana mmoja, ila kila mmoja kwa ishara zake.


Ishara hizo ni kama ifuatavyo


1. Mnapokutana na kuongea


Msichana anayekupenda anakuwa na tabasamu unapoongea naye kama amekuzoea, ila kama hajakuzoea anapokuona gafla tabasamu hutoweka maana anakuwa na aibu. Hawezi akakuangalia machoni atakuwa anakuangalia kwa kuibia. Sikiliza sauti yake, kama anaona aibu sauti yake itakuwa ya upole/laini anaweza akaanza kushika shika nywele zake au kuweka sawa mavazi yake.


 

2. Ajali za kijitakia


Anaweza akatafuta sababu yoyote ilimradi tu akushike. Anaweza akaona kitu kidogo tu au mdudu halafu anakurukia, au anakukumbatia.


3. Anaibia kukuchunguza


Unapokuwa umetulia zako unakuta anakuangalia kwa kuibia, ukigeuka anajifanya yuko bize na mambo yake kumbe anakuchunguza taratibu.


4. Anapenda mgusane


Mwanamke anayevutiwa na wewe mnapotembea naye mahali anapenda kushika mkono wako, au unapokutana naye anaweza kukukumbatia.


 

5. Anatafuta ukaribu


Mwanamke aliyevutiwa na wewe anapenda kuwa karibu na wewe muda wote. Mfano akiwa na marafiki zake halafu mkakutana gafla atakufuata halafu waangalie marafiki zake utakuta kama wanateta, ukiona hali hiyo kuna siri yao yeye na marafiki zake kuhusu wewe. Anapokuwa na marafiki zake akikuona anaweza akajitenga, hata kama mmeenda out pamoja na marafiki
zake utakuta yupo karibu na wewe.


6. Anapenda umjali


Anapokuwa na tatizo au anajisikia vibaya lazima akuambie, mfano mmeenda mahali kukawa na baridi hata kama si baridi sana atasema anahisi baridi ili mradi umsaidie koti lako, hata kama kuna watu hawezi kuona aibu kuvaa badala yake atajisikia vizuri anapovaa koti lako.


7. Hawezi kuzuia tabasamu


Unapomwonyeshea tabasamu lazima na yeye akuonyeshee, hata kama kuna kitu kimemwudhi atakuonyeshea tabasamu ili mradi aonyeshe umemkuta katika hali ya furaha.


 

8. Ishara za mwili


Anapopita mbele yako anaweza akafanya madoido mengi ambayo yatakuvutia ila kama anajiamini. Kama hajiamini anapokuona gafla anakosa amani, utamwona anashtuka gafla.


9. Anafurahishwa na vituko vyako


Mwanamke anayekupenda daima ni mwenye furaha mkiwa pamoja. Huwezi ukamboa, hata kama ukifanya kituko ambayo haichekeshi utakuta anafurahia.


10. Anakujali


Anakuwa anakujali, mfano akiona umeumia labda umejigonga, yupo radhi akuhudumie. unapokuwa naye anaweza kuuliza "unahitaji chochote? unaweza ukasema "nina kiu ngoja ninunue maji" utamsikia "nina maji, kunywa haya yangu kwanza".basi ujue kwamba anakujali.






Yafahamu Mambo Mbalimbali kuhusiana na Wanawake kwa Ku-Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE




Kitabu hiki kina topiki Zifuatazo;
1. Mambo anayohitaji mwanamke kutoka kwa Mwanaume
2. Mambo yanayowavutia wanawake kutoka kwa wanaume
3. Mambo wanayoyapenda wanawake wakati wa kufanya mapenzi
4. Dalili za mwanamke kicheche
5. Maswali ya kujiuliza kama mwanamke anakupenda kwa dhati au anakudanganya
6. Tabia za mwanamke anayekupenda lakini hawezi kusema
7. Ishara za mwanamke aliyevutiwa na wewe
8. Dalili za mwanamke anayeelekea kukukubali
9. Mambo ambayo mwanamke hawezi kukwambia
10. Njia za kudumisha na kuamsha mapenzi na mwanamke





Kitabu hiki ni Soft copy [pdf] kwa hiyo unaweza kusoma moja kwa moja kirahisi kabisa hata kwenye simu yako. Utatumiwa Kopi ya kitabu hiki kwenye email yako na utaweza kukihifadhi na kusoma wakati wowote utakaotaka.





[products columns="2" ids="30827"]


AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Njia za Kuunganisha na Kuwa na Furaha katika Familia Yako

Njia za Kuunganisha na Kuwa na Furaha katika Familia Yako

Kuwa na furaha katika familia ni jambo muhimu sana kwa afya ya kiroho na kimwili. Kama mtaalamu w... Read More

Kuboresha Ushirikiano wa Kimwili katika Kufanya Mapenzi: Mazoezi ya Kuongeza Intimiteti

Kuboresha Ushirikiano wa Kimwili katika Kufanya Mapenzi: Mazoezi ya Kuongeza Intimiteti

  1. Kuboresha Ushirikiano wa Kimwili katika Kufanya Mapenzi: Mazoezi ya Kuongeza IntimitetiRead More
Utunzaji wa Afya ya Uzazi katika Kufanya Mapenzi: Kujifunza na Kuzungumza

Utunzaji wa Afya ya Uzazi katika Kufanya Mapenzi: Kujifunza na Kuzungumza

  1. Utunzaji wa afya ya uzazi ni kitu muhimu sana wakati wa kufanya mapenzi. Ni muhimu kuzu... Read More

Vidokezo vya Kuwa na Uhusiano Mzuri na Msichana

Vidokezo vya Kuwa na Uhusiano Mzuri na Msichana

Mara nyingi, wanaume wamekuwa wakipata wakati mgumu kuwa na uhusiano mzuri na msichana. Inawezeka... Read More

Kukabiliana na Mazoea ya Kutokuwa na Ushirikiano na Kutoelewana katika Familia Yako

Kukabiliana na Mazoea ya Kutokuwa na Ushirikiano na Kutoelewana katika Familia Yako

  1. Kukabiliana na Mazoea ya Kutokuwa na Ushirikiano na Kutoelewana katika Familia Yako
  2. Read More
Kuweka Mazingira ya Kufurahisha na Amani katika Familia Yako

Kuweka Mazingira ya Kufurahisha na Amani katika Familia Yako

Kuishi katika familia yenye amani na furaha ni jambo la muhimu sana kwa afya na ustawi wa kila mm... Read More

Jinsi ya Kujenga Uhusiano wenye Afya na Watu Wengine katika ndoa na mke wako

Jinsi ya Kujenga Uhusiano wenye Afya na Watu Wengine katika ndoa na mke wako

Kujenga uhusiano wenye afya na watu wengine katika ndoa ni muhimu kwa ustawi wa ndoa yenu. Hapa kuna... Read More
Kujenga Mazingira ya Ushirikiano na Kuthamini katika Familia

Kujenga Mazingira ya Ushirikiano na Kuthamini katika Familia

Kujenga Mazingira ya Ushirikiano na Kuthamini katika Familia

Familia ni kitovu cha maisha ... Read More

Je, kuna umuhimu wa kufanya mazoezi ya kuboresha nguvu na stamina wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna umuhimu wa kufanya mazoezi ya kuboresha nguvu na stamina wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna umuhimu wa kufanya mazoezi ya kuboresha nguvu na stamina wakati wa ngono/kufanya mapenzi... Read More

Jinsi ya Kujenga Uaminifu na Kuimarisha Ushirikiano katika Familia Yako

Jinsi ya Kujenga Uaminifu na Kuimarisha Ushirikiano katika Familia Yako

Kujenga Uaminifu na Kuimarisha Ushirikiano katika Familia Yako ni muhimu sana kwa ustawi wa famil... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu matarajio ya baadaye na ndoto za kibinafsi

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu matarajio ya baadaye na ndoto za kibinafsi

Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu matarajio ya baadaye na ndoto za kibinafsi ni muhimu katika kujeng... Read More
Kukabiliana na Mazoea ya Kutokuwa na Usawa katika Familia: Kuweka Haki na Uadilifu

Kukabiliana na Mazoea ya Kutokuwa na Usawa katika Familia: Kuweka Haki na Uadilifu

Kukabiliana na Mazoea ya Kutokuwa na Usawa katika Familia: Kuweka Haki na Uadilifu

Familia... Read More