Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
AckyShine

Jifunze kitu kupitia kisa hiki cha mume na mke

Featured Image

Mwanaume mmoja alimuoa mwanamke mrembo. Alikuwa akimpenda sana. Siku moja mwanamke alipatwa na maradhi ya ngozi. Kidogokidogo alianza kupoteza urembo wake.
.
.
.


Mume alipata safari na wakati akirudi alipata ajali iliyomfanya apoteze uwezo wake wa kuona. Hata hivyo, maisha yao ya ndoa yaliendelea kama kawaida. Lakini kadiri siku zilivyosonga mbele ndivyo mke alivyoendelea kupoteza urembo wake. Kwa kuwa mume alikuwa kipofu hakulijua hilo na hivyo hakuna kilichobadilika kwenye upendo wao. Aliendelea kumpenda, na mke alimpenda sana mumewe.
.
.
.


Siku moja mke alifariki dunia. Ilikuwa huzuni kubwa sana kwa mume.
Baada ya kumaliza taratibu zote za maziko, mazishi na kutandua msiba, alipanga kuhama kwenye mji huo na kwenda kuishi kwenye mji mwingine.
.
.
.


Mtu mmoja aliposikia habari hiyo alimwendea na kumuuliza: “Sasa utawezaje kutembea peke yako? Maana siku zote hizi mkeo alikuwa akikusaidia kukuonesha njia.”


Akajibu: “Mimi si kipofu. Nilifanya ionekane hivyo kwa sababu angejua kwamba ninauona mwili wake ulivyobadilika kuwa mbaya angepata maumivu makubwa zaidi kuliko ugonjwa wake wenyewe. Alikuwa mke mwema sana. Nilitaka aendelee kuwa na furaha.”
.
.
.


FUNZO:


Wakati fulani ni vizuri ukajifanya kipofu na kuyapuuza mapungufu ya mwenzako ili kumfanya awe mwenye furaha.


Meno huung’ata ulimi mara nyingi, lakini vinaendelea kuishi pamoja kinywani. Huo ndio moyo wa KUSAMEHEANA. Macho hayaonani, lakini yanatazama na kuona vitu kwa pamoja, hupepesa na kulia pamoja. Huo unaitwa UMOJA.


1. Ukiwa peke yako unaweza kuongea, lakini ukiwa pamoja na mwenzako mnaweza KUZUNGUMZA.


2. Ukiwa peke yako unaweza KUFURAHI, lakini ukiwa na mwenzako unaweza KUFURAHIA.


3. Ukiwa peke yako unaweza KUTABASAMU, lakini ukiwa na mwenzako mnaweza KUCHEKA.


Huo ndio UZURI wa mahusiano yetu kama binadamu. Tunategemeana.


Kiwembe kina ukali lakini hakiwezi kukata mti; shoka lina nguvu na imara lakini haliwezi kukata nywele.


*Kila mtu ni muhimu kulingana na kusudio na lengo la uwepo wake. Usimdharau mtu yeyote kwa hali yoyote, kwa sababu huwezi kuwa yeye.


Mwenyezi Mungu atujaalie nguvu na moyo wa kusamehe, kustahmiliana na kuishi kwa umoja.
.
Tafakari
Mm na ww tunaweza kufanya haya!!!






Yafahamu Mambo Mbalimbali kuhusiana na Wanawake kwa Ku-Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE




Kitabu hiki kina topiki Zifuatazo;
1. Mambo anayohitaji mwanamke kutoka kwa Mwanaume
2. Mambo yanayowavutia wanawake kutoka kwa wanaume
3. Mambo wanayoyapenda wanawake wakati wa kufanya mapenzi
4. Dalili za mwanamke kicheche
5. Maswali ya kujiuliza kama mwanamke anakupenda kwa dhati au anakudanganya
6. Tabia za mwanamke anayekupenda lakini hawezi kusema
7. Ishara za mwanamke aliyevutiwa na wewe
8. Dalili za mwanamke anayeelekea kukukubali
9. Mambo ambayo mwanamke hawezi kukwambia
10. Njia za kudumisha na kuamsha mapenzi na mwanamke





Kitabu hiki ni Soft copy [pdf] kwa hiyo unaweza kusoma moja kwa moja kirahisi kabisa hata kwenye simu yako. Utatumiwa Kopi ya kitabu hiki kwenye email yako na utaweza kukihifadhi na kusoma wakati wowote utakaotaka.





[products columns="2" ids="30827"]


AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Jinsi ya Kujitolea kwa Upendo katika Familia: Kuwasaidia Wengine kwa Furaha

Jinsi ya Kujitolea kwa Upendo katika Familia: Kuwasaidia Wengine kwa Furaha

Leo tutaangalia jinsi ya kujitolea kwa upendo katika familia na kuwasaidia wengine kwa furaha. Fa... Read More

Jinsi ya Kuelewa na kukidhi mahitaji ya kihisia ya mpenzi wako

Jinsi ya Kuelewa na kukidhi mahitaji ya kihisia ya mpenzi wako

Kuelewa na kukidhi mahitaji ya kihisia ya mpenzi wako ni muhimu katika kujenga uhusiano wa afya na w... Read More
Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha urafiki na watu wa dini yenu

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha urafiki na watu wa dini yenu

Urafiki na watu wa dini yenu ni muhimu sana katika uhusiano wako na mpenzi wako. Ni muhimu kujeng... Read More

Jinsi ya kusaidiana na mke wako kufikia ndoto za kibinafsi na za kazi

Jinsi ya kusaidiana na mke wako kufikia ndoto za kibinafsi na za kazi

Kusaidiana na mke wako kufikia ndoto zake za kibinafsi na za kazi ni sehemu muhimu ya kuimarisha uhu... Read More
Jinsi ya Kuelewa na kukabiliana na changamoto za kukua pamoja na mpenzi wako

Jinsi ya Kuelewa na kukabiliana na changamoto za kukua pamoja na mpenzi wako

Mahusiano ni safarini ndefu yenye changamoto ndogo ndogo. Kwa wale wanaotaka kukuza mahusiano yao... Read More

Jinsi ya Kuimarisha Maisha ya Kiroho katika Ndoa na mke wako

Jinsi ya Kuimarisha Maisha ya Kiroho katika Ndoa na mke wako

Kuimarisha maisha ya kiroho katika ndoa na mke wako ni muhimu katika kukuza uhusiano wenu na kuweka ... Read More
Jinsi ya Kukuza Ushirikiano wa Kifamilia katika Nyakati za Shida

Jinsi ya Kukuza Ushirikiano wa Kifamilia katika Nyakati za Shida

Kukuza ushirikiano wa kifamilia ni jambo muhimu sana, hasa katika nyakati za shida. Katika ulimwe... Read More

Njia za Kuimarisha Ushirikiano wa Kijamii katika Mahusiano: Kuweka Muda kwa Ajili ya Marafiki

Njia za Kuimarisha Ushirikiano wa Kijamii katika Mahusiano: Kuweka Muda kwa Ajili ya Marafiki

Hivi karibuni, jamii yetu imekuwa ikiishi katika haraka na kusahau umuhimu wa kuwa na muda wa kut... Read More

Je, watu wanapendelea kutumia kinga wakati wa kufanya ngono/kufanya mapenzi?

Je, watu wanapendelea kutumia kinga wakati wa kufanya ngono/kufanya mapenzi?

  1. Kutumia Kinga Hupunguza Hatari za Maambukizi ya Ngono Kutumia kinga ni hatua muhimu kat... Read More

Jinsi ya Kusimamia Teknolojia katika Familia: Njia ya Kuunganisha badala ya Kutenganisha

Jinsi ya Kusimamia Teknolojia katika Familia: Njia ya Kuunganisha badala ya Kutenganisha

  1. Fikiria kuhusu jinsi teknolojia inavyoathiri familia yako – Mara nyingi, teknolojia i... Read More

Je, kuna umuhimu wa kujadili masuala ya afya ya uzazi katika uhusiano?

Je, kuna umuhimu wa kujadili masuala ya afya ya uzazi katika uhusiano?

Je, kuna umuhimu wa kujadili masuala ya afya ya uzazi katika uhusiano? Jibu ni ndio, kwa kweli! M... Read More

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Mshikamano katika Familia: Kuunda Nafasi ya Kusaidiana

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Mshikamano katika Familia: Kuunda Nafasi ya Kusaidiana

  1. Familia ni kitovu cha mahusiano ya kijamii. Hivyo basi, ni muhimu kuhakikisha kuwa kuna... Read More