Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
☰
AckyShine

Matatizo yanayotokana na ujauzito katika umri mdogo

Featured Image

Wataalamu wanashauri kwamba msichana anastahili kuanza kubeba mimba kuanzia umri wa miaka 18 hadi 20. Kabla ya umri huu, mwili wa msichana bado haujakomaa vizuri. Viungo vya uzazi bado ni vidogo na ngozi ni laini. Vilevile mfupa wa nyonga bado mwembamba kiasi cha kumwezesha mtoto kupitia wakati wa kuzaliwa.
Wasichana chini ya miaka 18 wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata matatizo, hasa wakati wa kujifungua. Matatizo hayo ni pamoja na mapigo ya moyo kuwa juu, kuumwa uchungu kwa muda mrefu, kukwama kwa mtoto, kujifungua kwa njia ya operesheni, kujifungua kabla ya wakati na watoto kuzaliwa na uzito mdogo. Mwili huwa na mahitaji makubwa wakati wa ujauzito na kujifungua na mwili wa wasichana wenye umri chini ya miaka 18 huwa haujakomaa vya kutosha kwa kazi ya kubeba mimba.
Mbali ya shida za kiafya, kuna matatizo mengine yatokanayo na kupata mimba mapema. Mara nyingi msichana na mwenzie wanakuwa bado wanasoma shule, msichana hufukuzwa shule na hata hutengwa katika jamii . Vijana mara nyingi hawana mapato ya kumlea na kumtunza mtoto, na mahali pa kuishi huwa hawana. Vilevile mvulana mara nyingi hayuko tayari kuchukua jukumu la kuwa baba. Kwa sababu hizi zote, ni vizuri zaidi mimba zitungwe baada ya msichana kufikia umri wa miaka 18.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Je, nini imani ya watu katika kuelewa na kuheshimu mipaka ya kimwili katika uhusiano wa ngono wakati wa kufanya mapenzi?

Je, nini imani ya watu katika kuelewa na kuheshimu mipaka ya kimwili katika uhusiano wa ngono wakati wa kufanya mapenzi?

Leo tutazungumzia kuhusu imani za watu katika kuelewa na kuheshimu mipaka ya kimwili katika uhusi... Read More

Nini matatizo ya watoto Albino shuleni?

Nini matatizo ya watoto Albino shuleni?

Ingawaje, akili zao hazina hitilafu watoto Albino mara nyingi
hawafanyi vizuri shuleni, na h... Read More

Jinsi ya Kuonyesha Ukarimu kwa Msichana Wako

Jinsi ya Kuonyesha Ukarimu kwa Msichana Wako

Habari za leo! Leo nataka kuzungumza juu ya jinsi ya kuonyesha ukarimu kwa msichana wako. Kama mw... Read More

Mabadiliko gani yanatokea kwenye miili ya wavulana Wakati wa makuzi au wakati wa kubalehe?

Mabadiliko gani yanatokea kwenye miili ya wavulana Wakati wa makuzi au wakati wa kubalehe?

Wakati wa makuzi au kipindi cha kubalehe, wavulana hupitia mabadiliko mbali... Read More

Je, kuna umuhimu wa kujadili matarajio ya ngono/kufanya mapenzi ya baadaye katika uhusiano?

Je, kuna umuhimu wa kujadili matarajio ya ngono/kufanya mapenzi ya baadaye katika uhusiano?

Kama wapenzi wapya au wapenzi wa muda mrefu, ni muhimu sana kujadili matarajio ya ngono/kufanya m... Read More

Sheria kuhusu utoaji mimba

Sheria kuhusu utoaji mimba

Sheria kuhusu utoaji
mimba zinatofautiana
kati ya nchi na nchi. Hapa
Tanzania utoa... Read More

Je, kuna njia salama ya kutoa mimba?

Je, kuna njia salama ya kutoa mimba?

Hatari inategemea na mazingira ambapo mimba inatolewa. Kama ni hospitalini na i inatolewa na mtaa... Read More

Nikishatambua kwamba nina mimba, nifanye nini?

Nikishatambua kwamba nina mimba, nifanye nini?

Ukishatambua kwamba una mimba kuna mambo mbalimbali tofauti ya kufanya. Kwanza kabisa mweleze mwe... Read More

Kwa nini mwanaume akiona mapaja ya mwanamke uume wake husimama?

Kwa nini mwanaume akiona mapaja ya mwanamke uume wake husimama?

Mapaja na nyonga ni sehemu ya mwili i i iliyo karibu na viungo vya uzazi vya mwanamke. Kwa sababu... Read More

Nifanyeje kuepuka vishawishi vya kujamiiana kutoka kwa watu wengine, hasa wakubwa?

Nifanyeje kuepuka vishawishi vya kujamiiana kutoka kwa watu wengine, hasa wakubwa?

Vijana wengi wanajikuta wanatumbukia katika matatizo mazito kama kupata mimba mapema, utoaji wa m... Read More

Kwa nini ngozi ya Albino inafanana ya watu weupe?

Kwa nini ngozi ya Albino inafanana ya watu weupe?

Ngozi ya Albino ina ukosefu wa rangi. Inaonekana kama ya watu
weupe ambao wana kiasi cha pig... Read More

Je, ni kweli kuwa ulemavu unaweza kugundulika mara tu mtoto anapozaliwa?

Je, ni kweli kuwa ulemavu unaweza kugundulika mara tu mtoto anapozaliwa?

Ni kweli kuwa daktari anaweza kufanya vipimo vya kugundua
kama mtoto aliye tumboni ni mwenye... Read More