Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
☰
AckyShine

Mapishi ya Ndizi Mbichi Za Nyama Ng'ombe

Featured Image

Vipimo

Ndizi mbichi - 10

Nyama - kilo 1

Nazi ya kopo - 1

Chumvi - 1 Kijiko cha chakula

Ndimu - 1

Bizari ya manjano - 1 Kijiko cha chai

Pili pili mbichi - 3

Nyanya (tomatoes) - 2

Kitunguu maji - 1

Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi iliyosagwa - 1 Kijiko cha chakula

Namna ya Kutayarisha Na Kupika

Kata nyama vipande vipande na uisafishe.
Chemsha nyama weka chumvi, thomu, tangawizi na ndimu. Iache iwive.
Kata kata nyanya na kitunguu, kisha mimina kwenye nyama inayochemka, weka na bizari nusu kijiko. Wacha supu iwive kisha weka pembeni. Ukumbusho: Hakikisha supu inakuwa kiasi na si nyingi.
Menya maganda ndizi na uzikate vipande vipande vya kiasi.
Zikoshe ndizi na uziweke ndani ya sufuria.
Weka maji ndani ya sufuria kisha zichemshe ndizi mpaka ziwe laini kidogo.
Zimwage maji ndizi kisha mimina supu na nyama ndani ya ndizi.
Mimina nazi pili pili na bizari nusu kijiko ndani ya ndizi na uziweke kwenye jiko zichemke mpaka zibakie na urojo kiasi. Onja chumvi na uongeze kadri utakavyopenda.
Weka pembeni zipoe.
Pakua ndizi kwenye sahani au bakuli tayari kwa kuliwa.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Jinsi ya kutengeneza Keki Ya Mbegu Za Mchicha

Jinsi ya kutengeneza Keki Ya Mbegu Za Mchicha

Viamba upishi

Unga ngano vikombc 3
Unga mbegu za mchicha kikombe 1
Baking powde... Read More

Jinsi ya kupika Mkate wa sinia

Jinsi ya kupika Mkate wa sinia

Mahitaji

Unga wa mchele (rice flour 2 vikombe vya chai)
Sukari (sugar 3/4 ya kikombe... Read More

Mapishi ya Chapati za maji za vitunguu

Mapishi ya Chapati za maji za vitunguu

Mahitaji

Unga wa ngano (plain flour) 1/4
Kitunguu kikubwa (chopped/slice onion) 1Read More

Jinsi ya Kujiandaa kwa Chakula cha Afya Ukiwa Safarini

Jinsi ya Kujiandaa kwa Chakula cha Afya Ukiwa Safarini

Jinsi ya Kujiandaa kwa Chakula cha Afya Ukiwa Safarini 🍏πŸ₯ͺπŸ›«

Kuwa na lishe bora ni ... Read More

Jinsi ya kupika Pilau Ya Samaki WaTuna Na Mboga

Jinsi ya kupika Pilau Ya Samaki WaTuna Na Mboga

Viambaupishi

Mchele 2 Mugs

Mboga mchanganyiko za barafu 1 Mug

(Frozen veg)Read More

Mapishi ya Pilau Ya Mchicha

Mapishi ya Pilau Ya Mchicha

VIPIMO

Mchele - 3 Vikombe

Mchicha

Mafuta - 1/2 kikombe

Vitunguu maji - ... Read More

Jinsi ya Kupika skonzi

Jinsi ya Kupika skonzi

Mahitaji

Unga wa ngano (self risen flour 2 vikombe vya chai)
Sukari (sugar 1/2 kijik... Read More

Mapishi ya Wali, mchicha wa nazi na nyama ya kukaanga

Mapishi ya Wali, mchicha wa nazi na nyama ya kukaanga

Mahitaji

Mchele (rice 1/2 kilo)
Mchicha uliokatwakatwa (spinach mafungu 2)
Nyam... Read More

Mapishi ya Pilau Ya Bilingani Na Kuku

Mapishi ya Pilau Ya Bilingani Na Kuku

Viambaupishi

Mchele wa basmati - 3 vikombe

Kuku - Β½

Bilingani - 2 ya kiasiRead More

Jinsi ya kuandaa Vileja Vya Tambi

Jinsi ya kuandaa Vileja Vya Tambi

MAHITAJI

Tambi (vermiceli Roasted) Mifuko 2

Siagi - 4 Vijiko vya supu

Maziwa ... Read More

Mapishi ya Biskuti Za Jam

Mapishi ya Biskuti Za Jam

VIAMBAUPISHI

Unga 2 Β½ gilasi

Sukari ΒΎ gilasi

Samli 1 gilasi

Mayai 2Read More

Upishi kwa Ajili ya Kusaidia Kinga: Kujenga Uimara

Upishi kwa Ajili ya Kusaidia Kinga: Kujenga Uimara

Upishi kwa Ajili ya Kusaidia Kinga: Kujenga Uimara 🍎πŸ₯¦πŸ‹οΈβ€β™€οΈ

Habari za leo ... Read More