Wachaga kweli kiboko: Mcheki huyu mchaga na mbuzi!!!
Updated at: 2024-05-25 18:12:25 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mchaga alinunua mbuzi akamwambia mpishi Nyama nusu ipike pilau na ingine itie kwenye friza. Kichwa fanya supu, miguu fanya mchuzi chukuchuku. Ngozi usitupe tutafanya mswala, utumbo pikia ndizi na mifupa tutawauzia wenye mbwa. Kinyesi kihifadhi kwa mbolea ya bustani.
Mpishi akamuuliza Hutaki na sauti ya mbuzi tufanye ring tone kwenye simu yako? Mchaga akajibu Yesuu! hivi inawezekana? bac fanya hivyo tuwauzie na wengine hiyo ringtone. ๐๐
Updated at: 2024-05-25 18:11:45 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
DOGO: Mama Jana Baba Alikuja Na Mwanamke Na Akaanza Kumtoa Nguo Huku Akimuita Beibโฆ BABA: Kwa Hasira Ebu Wacha Kuongea Na Chakula Mdomoni Wewe Mpumbavu Sana Khaa!!! MAMA: Eti Nini Hebu Endelea Mwanangu Alafu Wakafanya Nini Hawa Nguruweโฆ DOGO: Wakanza Kufanya Kama Vile Mlifanya Na Anko nassoro Wakati Baba Alikua Safari Za kikaziโฆ MAMA: Kwa Hasira Babako Amesema Uwache Kuongea Na Chakula Mdomoni We Kweli Mpumbavu sanaโฆ
Updated at: 2024-05-25 17:57:23 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kuna kijana alikua anajua kuwa mke wake
anatoka nje ya ndoa basi akamwuliza mke,
mkewe akakataa, akamwambia baba yake
akaambiwa na babaake tulia mwanangu ndoa
zina mengi! akawa kila siku analalamika kwa
babaake, mwisho babaake akamwambia basi
ntakusaidia. Itabidi ujifanye unaumwa sana hoi
hujiwez halafu nitakuonyesha jawabu!
Basi kijana akajifanya anaumwa mzee akaitisha
kikao cha ndugu wote pande 2,
Mzee akaanza kueleza jaman kijana wetu
anaumwa amepata ugonjwa wa utata hospital
zote umeshindikana hivyo tumeenda kwa mganga
wa jadi amenipa dawa na ina masharti, inatakiwa
atakaye iandaa hii dawa awe mwanamke mwenye
ndoa ambaye hajawah kutoka nje ya ndoa tangu
alipoolewa ndo kijana wetu atapona!
Kama ametoka nje ya ndoa asiandae dawa hii
kwa sababu tukimpa kjana wetu watakufa wote!
Je kina mama nani ataandaa? Walitoka nje
wamama mmoja mmoja hadi mkewe na mamake
mzazi wakatoka, akafata mama ake kijana,
mashangazi na dada zake, mwisho wakabakia
wanaume peke yao! Mzee akamwambia
mwanangu umeona hali za ndoa zilivyo?
Acha kujisumbua tulia na mkeo nadhani
umejionea hali halisi.
Cha zaidi omba Mungu sana juu ya ndoa yako!
Kijana akazimia!
SOMA TENA KISHA MTUMIE NA MWENZIO.
Alichojibu dalali baada ya kufumwa na mke wa mtu ndani ya nyumba ya kupanga
Dalali aliwatafutia jamaa chumba Buguruni karibu na reli, nyumba nzuri sana. Jamaa na mkewe wakahamia kwa furaha, lakini furaha yao iliisha walipokuja gudundua nyumba ile iko karibu mno na reli treni ikipita mpaka kitanda kinacheza.
Siku hiyo dalali akapita mke akamwita na kumwambia tatizo wakati treni inapita, wakaanza kubishana, yule mama akamwambia dalali kwa kuwa kuna treni itapita sasa hiviโฆ njoo ndani uone mwenyewe.
Updated at: 2024-05-25 18:05:28 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Dalali aliwatafutia jamaa chumba Buguruni karibu na reli, nyumba nzuri sana. Jamaa na mkewe wakahamia kwa furaha, lakini furaha yao iliisha walipokuja gudundua nyumba ile iko karibu mno na reli treni ikipita mpaka kitanda kinacheza.
Siku hiyo dalali akapita mke akamwita na kumwambia tatizo wakati treni inapita, wakaanza kubishana, yule mama akamwambia dalali kwa kuwa kuna treni itapita sasa hiviโฆ njoo ndani uone mwenyewe.
Bahati mbaya wakiwa wamejilaza kitandani ili dalali aone adhabu wanayopata, Mzee mwenye mali alirudi ghafla, akauliza,
'Nyie mnafanya nini hapa?'
Masikini dalali kwa woga mkubwa akajibu' Tunangoja treni'
Utoto raha..! Angalia hawa watoto wanachokifanya sasa
Updated at: 2024-05-25 18:10:48 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Leo nimepulizia Air Fresh yenye Harufu ya Pilau nyumbani kwangu sasa watoto wa Jirani wamehamia Mlangoni kwangu ndio wanacheza hapo. Kila nikitoka wananisalimia. Mama yao ndio kanimaliza kabisa nimetoka akaniambia
"Kumbe wewe ni Mpishi mzuri, Hongera"
Imebidi nisirudi nyumbani maana wale watoto wanaweza kuingia ndani kabisa na pilau hakuna.
Angalia alichojibu huyu mwanafunzi, Ungekua wewe ni mwalimu wake ungemfanyaje?
Updated at: 2024-05-25 17:55:55 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mwanafunz alikuwa kila siku anachelewa shule, na kila siku alikuwa anachapwa, basi siku moja mwalimu akaona ngoja amuulize.
Mwalimu: Mbona unachelewa kila siku? Mwanafunzi: Nakaa mbali mwalimu Mwalimu: (huku ana hasira akauliza)Mbali mbinguni? Mwanafunzi: Mbinguni kwa mbele๐๐๐๐๐
Updated at: 2024-05-25 17:09:46 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Leo nimechoka zangu alafu shangazi amekuja anataka nimuunganishe facebook. Imebidi nimwambie lazima awe na picha passport size 4 kwaajili ya kuweka profile picture, barua kutoka kwa afisa mtendaji na Atm card ya nmb bank. Alafu awe na marefa wanne ambao wamekuwa facebook for more than 3 years. Amesema hataki tena kujiunga fb!
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐ Saa ivi niko zangu nimelala naendelea kupunguza uchovu