Angalia kilichojiri katika semina ya wanandoa kuhusu upendo
Updated at: 2024-05-25 18:00:09 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kulikuwa na semina ya wanawake kuhusu namna ya kuishi kwa upendo katika ndoa. Mwalimu aliwauliza ni wangapi wanawapenda waume zao? Wote wakanyoosha mikono kama ishara ya kuwa wanawapenda waume zao. Mwalimu akauliza tena, “Ni lini mara ya mwisho umemwambia mumeo “Nakupenda Mpenzi”?
Majibu yalikuwa kama ifuatavyo: Wengine wakisema Asubuhi ya leo, Wengine jana, Wengine wiki iliyopita Wengine mwezi uliopita Na wengine wakasema hawakumbuki! Mwalimu aliwapa kazi kila mwanasemina achukue simu yake na kumtumia mume wake meseji yenye neno “NAKUPENDA MPENZI” Baada ya meseji kwenda aliwaamuru kubadilishana simu kila mtu na jirani yake. Kila mwanasemina aliambiwa kusoma meseji za majibu kwenye simu aliyoshika
Simu ya 1 – “Samahani, nani mwenzangu”! Simu ya 2 – “Samahani, wrong number”! Simu ya 3 – “Si nimekuambia usinitumie messages kwenye namba hii”! Simu ya 4 – “Mh! leo mvua itanyesha”! Simu ya 5 – “Nikija tutaongea zaidi”! Simu ya 6 – “……Imedhibitishwa umepokea Tsh300,000 kutoka kwa ……”! Simu ya 7 – “Me too”! Simu ya 6 – “Huu ujumbe ndio ulikuwa unamtumia huyo hawara yako ee, leo utanikoma”!
Updated at: 2024-05-25 17:58:49 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ndio hizi sasa
1.Hicho ndicho chuo chako usiwe na chuo kingine ila hicho. 2.Usilitaje bure jna la chuo chako mana utawaumiza wengine. 3.Ikumbuke cku uliyochaguliwa na kuiheshimu. 4.Waheshimu tcu, bodi ya mkopo na uongoz wa chuo ili upate kuendelea kuwepo chuon. 5.Usisapu 6.Usidisko 7.Usitumie mkopo ovyo. 8.Usitaman chuo cha mwenzio 9.Usitamani fakat ya mwenzio 10. Usitaman bumu lake wala chochote alichonacho. hahaha chezea chuo weye!
Updated at: 2024-05-25 18:09:43 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
FUNDISHO : SAFARI NI SAFARI
Maisha ni ya ajabu sana, wakati mwingine maisha ni mazuri na mwingine ni mabaya, katika maisha yetu tumeshapitia safari nyingi sana na za aina mbalimbali kwa nyakati mbalimbali. Lakin kiukweli kila safari ni safari tuu.
Japokua kila safari ina changamoto zake lakini mwisho wake ni ule ule , kila safari ina uzuri na upekee wake.
Vile vile kila safari ina ubaya wake, kwa mfano kila safari ina gharama yake kulingana na upekee wake.
Usiwe na wasiwasi na mashaka na aina ya safari ulionayo, jipe moyo utaimaliza na kupata ulichokitarajia. Haya ndio maisha na wote tunatakiwa tuyafurahie.
Ingawa kila mtu ana safari yake bado wote tunatakiwa tufurahie pamoja kwa safari tuliyo nayo. Hata Uwe Na safar ya aina gani wewe furahi tuu. Hii ni kwa sababu safari mwisho wake ni mmoja kwa wote burudani ni ile ile
Safari🍺 ni safari 🍺hata kama ni ya chupa au ya kopo mwisho wake 💤💤
Updated at: 2024-05-25 18:11:56 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Nimekutana na dogo mmoja hivi hapa analia,namuliza analia nin??ananambia ''ALIPEWA MIA TANO ZIPO MBILI,MIA TANO MOJA YA NYANYA na MIA TANO NYINGINE YA VITUNGUU sasa KAKOSEA KAZICHANGANYA HAJUI TENA IPI NI YA NYANYA na IPI NI YA VITUNGUU!!!
Alichokisema mwizi baada ya kushinda bahati nasibu
Updated at: 2024-05-25 17:06:08 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Hapa mtaani kuna mwizi sugu ameshinda mil.10 za bahati nasibu ??. Alipoulizwa atafanya nini na hela nyingi hizo Akasema anataka kupanua shughuli zake. Mimi sijamuelewa na sasa hivi watu wameanza kuhama mtaa… 😂😂
Updated at: 2023-04-29 22:52:48 (3 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
HABARI MPASUKO..
jana katika taasisi ya wanyama pori ya Nat Geo ilitangazwa kuwa ametokea Nyoka hatar san Ambaye hajawah kutokea duniania.. wanadai kwamba nyoka huyo anaongezeka ulrefu wa 0.5sm kila akila chakula na huwa anakula chakula kuanzia sekunde 30 kurudi nyuma.. mpaka sasa hakuna siraha ya kuweza kumuua nyoka huyo isipokuwa akiji uma mwenye ndo anaweza kufa, wanasayansi hao walieleza japo uchunguz zaid bado unaendelea… huyu ni nyoka anayeua kuliko nyoka wote waliowah kutokea katika historia ya maisha ya mwanadam..
nyoka huyu hupatikana katika simu pekee za nokia toch katika sehem ya game inaitwa snake xenzia..
asanteni kwa kufurah na umakin mkubwa katika usomaji wa matini hii…
haya ni mambo ya wikiend jaman na iwe njema kwenu wote