Je, wasichana wana viungo gani vya uzazi na kazi zake ni zipi?
Updated at: 2024-05-25 16:24:30 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viungo vya uzazi vya ndani vinaonekana katika michoro inayofuata:
Ukiangalia mchoro huu hapo juu, ambao unaonyesha via vya uzazi vya ndani, utaona uke, mfuko wa uzazi, kokwa za mayai na mirija ya kupitisha mayai. Uke ni mfereji ulio kati ya mfuko wa uzazi na sehemu ya nje ya via vya uzazi. Uke unatumiwa wakati wa kujamii ana, damu ya hedhi na mtoto hupita hapa. Urefu wa uke kwa wastani ni sentimita 7 hadi 8. Mfuko wa uzazi kwa kawaida huwa na ukubwa unaofikia embe ndogo. Yai moja lililorutubishwa hujishikilia kwenye kuta zake nazo huitunza mimba mpaka siku ya kuzaliwa mtoto. Wakati wa ujauzito mfuko wa uzazi hukua taratibu ukistahimili ukuaji wa mtoto. Kila upande wa mfuko wa uzazi i i ipo kokwa ya mayai, ambayo i ina ukubwa kama mbegu ya harage. Kila mwezi yai moja hukomaa kwa upande wa kulia au kwa upande wa kushoto na husafiri kwa kupitia katika mrija wa falopia. Kazi ya mirija ni kupitisha yai lililopevuka kila mwezi kutoka kwenye kokwa za mayai mpaka mfuko wa uzazi. Yai hutungishwa ndani ya mirija hii.
Ukiangalia mchoro huu unaoonyesha via vya uzazi vya nje, utaona midomo ya nje na midomo ya ndani, halafu kisimi, tundu la mkojo, sehemu ya haja kubwa na mlango wa uke. Midomo ya nje na ya ndani ni mii nuko ya ngozi na i iko hapo kuhifadhi sehemu za ndani za uke. Kisimi (au kinembe) ni sehemu ya juu kabisa ndani ya uke na ni sehemu ya uke ambayo humsaidia mwanamke awe na msisimko au asikie utamu wakati wa kujamii ana. Kama tulivyoona hapo juu, mlango wa uke ni tundu ambalo damu hutokea wakati wa hedhi. Pia ni sehemu unapoingia uume wakati wa kujamii ana na mtoto hutokea sehemu hii anapozaliwa. Tundu la mkojo ni juu ya mlango wa uke na ni tundu ambalo mkojo hutokea. Sehemu ya haja kubwa ni sehemu i inapopita haja kubwa (kinyesi).
Kama wewe ni msichana, unaweza kuamua kutumia kioo kujiangalia sehemu zako za via vya uzazi vya nje. Kwa njia hii unaweza kuyaelewa vizuri maumbile yako.
Je, nikila na mtu mwenye Virusi vya UKIMWI, nitaambukizwa na virusi vya UKIMWI na UKIMWI?
Updated at: 2024-05-25 16:22:28 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Hapana, ukila na mtu mwenyemaambukizi ya Virusi vya UKIMWI huwezi kuambukizwa Virusi vya UKIMWI wala UKIMWI, isipokuwa pale ambapo wote wawili mna vidonda mdomoni na mnachangia kijiko kimoja. Lakini uwezekano huu ni mdogo sana, kiasi tunachoweza kusema kwamba huwezi kuambukizwa Virusi vya UKIMWI na UKIMWI ukila sahani moja na mtu aliyeambukizwa na virusi. Lakini, kufuatana na kanuni za afya, ni vizuri zaidi kila mtu atumie vifaa vyake na baada ya kuvitumia avioshe kikamilifu.
Updated at: 2024-05-25 16:24:20 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Albino wana ngozi nyeupe, nywele nyeupe au nyekundu na macho ya kijivu au ya bluu. Ngozi yao ni nyeupe zaidi kuliko ndugu zao wa familia moja au watu wa jamii yake ambao hawana hali ya ualbino. Ngozi hii inaonekana zaidi kuwa nyeupe katika familia za watu weusi, ingawaje, ualbino hutokea kwa watu wa kila taifa, rangi, kabila na dini. Albino wako katika mabara yote ulimwenguni.
Nini kifanyike nini kwa mtu ambaye hafikii kilele au mshindo wakati anapofanya mapenzi?
Updated at: 2024-05-25 16:22:11 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kwa mwanaume, dalili ya kufikia mshindo ni uume kusimama halafu kumwaga manii . Manii kutotoka wakati wa kujamii ana inaweza kusababishwa na mambo mengi. Kutoa manii kunatumia nguvu nyingi za mwili.
Kwa hiyo chochote kile kinachompunguzia mwanaume nguvu za mwili kama vile maradhi mbalimbali, ulevi wa pombe au dawa za kulevya, njaa au lishe duni kunasababisha mwanaume ashindwe kutoa manii . Sababu nyingine muhimu ni kutokuwa tayari kimawazo au kutokuwa na huruma katika tendo la kujamii ana. Kama ulevi ni sababu ya shida yako, jitahidi kuyaacha mambo haya. Jaribu kutulia na kuongeza muda wa kutayarishana kimapenzi mpaka mtakapoona mko tayari.
Kwa mwanamke, kutofikia mshindo pia kuna sababu mbalimbali. Lakini mara nyingi i i inasababishwa na kutokuwa na subira katika maandalizi ya kujamii ana, kutokuwa tayari kimawazo au kuogopa matokeo ya kufanya mapenzi. Mwanamke akiwa tayari kimawazo kwa kujamii ana na mwanaume akijitahidi kumstarehesha vizuri, mwanamke atafikia mshindo bila shida. Pia kuwa wazi juu ya unachokipenda na usichokipenda i inasaidia sana katika kuwa na ngono ya kuridhisha kwenu wote wawili.
Je, nikiambukizwa virusi vya UKIMWI na UKIMWI nifanye nini?
Updated at: 2024-05-25 16:22:26 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jambo la msingi ni kutokukata tamaa na kuwa na matumaini. Mara nyingine i inasaidia kama utakuwa na mazungumzo na watu ambao tayari wanaishi na Virusi vya UKIMWI na UKIMWI au marafiki na ndugu unaowaamini. Jaribu kuongea na mwenzi wako i ili kumfahamisha juu ya hali yako ya maambukizi. Yeye pia anaweza kuwa ameambukizwa na angependa kupima. Ni muhimu kuzingatia kanuni muhimu za afya nzuri kama vile kula vyakula vyenye mlo kamili na kujiweka katika hali ya usafi. Kwa mantiki hiyo hiyo ni lazima kuharakisha kutibu maradhi mengine yatakayojitokeza. Watu wanaoishi na virusi i vya UKIMWI wanashauriwa wasitumie pombe wala kuvuta sigara, kwa sababu vyote hivyo huchangia katika kudhoofisha mwili. Kama watafanya ngono, ni lazima watumie kondomu i ili wasiambukize wengine. Aliyeambukizwa, baada ya miaka kinga ya mwili i wake i itaanza kupungua na atatakiwa kupata dawa za kupunguza makali ya UKIMWI (ARV). Kama mtu aliyeambukizwa na virusi vya UKIMWI atazingatia masharti haya, kuna uwezekano wa kuishi na kufurahia maisha kwa miaka mingi.