Updated at: 2024-05-25 10:23:07 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Unga 2 ½ gilasi
Sukari ¾ gilasi
Samli 1 gilasi
Mayai 2
Baking powder 2 kijiko vya chai
Vanilla 1 ½ kijiko cha chai
Maganda ya chungwa 1
MAPISHI
Tia kwenye machine ya kusagia (blender) mayai, sukari, vanilla, samli na maganda ya chungwa, saga vizuri. Tia unga kwenye bakuli pamoja na baking powder, mimina vitu ulivyosaga kwenye bakuli, changanya. Punguza unga uliochanganya kidogo weka pembeni. Unga uliobakia tia kwenya tray ya kuchomeya, utandaze vizuri, tia jam juu yake. Chukua la kukwaruzia carrot (grater) ukwaruze unga uliuopunguza juu ya jam. Choma kwa muda dakika 20 moto wa 180 C.
Acha ipowe kidogo, zikate vipande vya mraba (square) Tayari kwa kula.
Updated at: 2024-05-25 10:34:47 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vitumbua ni aina ya vitafunwa vya chai ambavyo hutengenezwa kwa kutumia unga wa mchele. Kiasili vitumbua ni chakula ambacho hupendelewa sana na watu wa pwani. Na mara nyingi wamekuwa wakipika kwa kuchanganya na nazi ili kuvifanya view na ladha nzuri zaidi
Mahitaji:
Unga wa mchele ½ kg Sukari vijiko 4 vya mezani Tui bubu la nazi Mafuta ya kupikia Unga wa hiliki ½ kijiko cha chai Hamira kijiko 1 cha chai Chuma cha vitumbua
Maandalizi:
Chukua unga wa mchele na weka kwenye bakuli au sufuria ya kilo moja Weka hamira kisha weka sukari kisha miminia tui katika mchanganyiko wako Weka hiliki koroga hadi view uji mzito Acha uji huo kwa muda wa saa moja hadi uumuke, mara nyingi kuumuka kunategemea na hali ya hewa, Baada ya hapo weka mafuta kijiko kimoja cha chakula kila kishimo acha yapate moto Kisha kaanga virumbua vyako
Updated at: 2024-05-25 09:52:20 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Unga wa mchele ( Vikombe 2 vikubwa) Sukari (Nusu ya kikombe kikubwa) Hamira ( Nusu ya kijiko cha chai) Hiliki (Nusu ya kijiko cha chai) Tui la nazi ( Kikombe kimoja kikubwa) Unga wa ngano (Vijiko viwili vya chakula) Mafuta ya kuchomea (Vegetable oil)
Matayarisho
Unachanga unga, sukari, hamira, hiliki, unga wa ngano na tui la nazi pamoja katika bakuli la plastiki. Kisha unaukoroga mpaka mchanganyiko unakuwa kama uji mzito. Kava bakuli lililokuwa na mchanganyiko kisha hifadhi katika sehemu yenye joto kwa muda wa masaa matatu.
Jinsi ya kupika
Weka chuma cha kuchomea vitumbua katika moto wa wastani, kisha weka mafuta kwenye chuma cha kuchomea ( Kijiko kimoja cha chai) mafuta yakisha pata moto tia uji wako (upawa mmoja) katika kila shimo la chuma cha kuchomea. Acha mpaka kitumbua kikauke kisha geuza na tia mafuta. Acha upande wa pili wa kitumbua mpaka uwe rangi ya kahawia na hapo kitumbua kitakuwa kimeiva utakitoa. Rudia hatua hizo kwa vitumbua vyote vilivyobaki.
Chemsha nyama na chumvi na nusu ya limao mpaka iive kisha weka pembeni. Baada ya hapo andaa vitu vya pilau kwa kuloweka mchele kwenye maji kwa muda wa dakika 10.Menya na kukatakata vitunguu na viazi kisha weka pembeni na pia chemsha maji ya moto na uweke pembeni. Baada ya hapo weka sufuri jikoni na tia mafuta kiasi . Yakisha pata moto tia vitunguu na uvikaange mpaka viwe vya rangi ya kahawia na kisha uitie nyama na ikaange mpaka ipate rangi ya bown pia. Baada ya hapo tia kitunguu swaum na tangawizi na uikoroge vizuri kisha iache ikaangike kwa muda wa dakika 2 kisha tia spice ambazo ni Binzari nyembamba ya unga, hiliki,karafuu, amdalasini na pilipili mtama na viazi. Baada ya hapo unatakiwa ugeuze geuze mpaka mchanganyiko uchanganyike vizuri kisha tia mchele na ugeuzege mpaka uchanganyike na viungo. Baada ya hapo tia chumvi na maji ya kutosha na ukoroge vizuri kisha funika na uache uchemke katika moto wa wastani. Maji yakikaribia kukauka tia binzari nyembamba nzima na ufunike uache mpaka maji yakauke kabisa. maji yakisha kauka ugeuze na ufunike tena na uuache mpaka uive. Baada ya hapo andaa kachumbali kwa kukatakata vitunguu katika bakuli na kisha tia chumvi kwa ajili ya kuondoa ukali wa vitunguu. Baada ya hapo vioshe mpaka chumvi yote iishe. osha nyanya, Pilipili, hoho na kisha katakata slice nyembamba na uchanganye na vitunguu. Baada ya hapo tia chumvi, kamulia limao na uchanganye zote pamoja. Baada ya hapo chakula kitakuwa tayari kwa kuliwa.
Mapishi ya Ugali Mchuzi Wa Samaki Nguru Wa Nazi Na Bamia Za Kukaanga
Updated at: 2024-05-25 10:37:38 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo Vya Ugali:
Unga wa mahindi/sembe - 4
Maji - 6 takriban
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Chota unga kidogo katika kibakuli uchanganye na maji kidogo . Weka maji mengineyo katika sufuria kwenye moto. Changanya na mchanganyiko mdogo ufanya kama uji. Kisha kidogo kidogo unaongeza sembe huku unakoroga na kuusonga ugali hadi uive.
Vipimo Vya Mchuzi Wa Samaki Wa Nazi
Samaki nguru - 5 vipande
Pilipili mbichi ilosagwa
Kitunguu maji kilosagwa - 1 kimoja
Nyanya ilosagwa - 2
Haldi/tumeric/bizari ya manjano - ¼ kijiko cha chai
Chumvi - kiasi
Ndimu - 2 kamua
Tui la nazi zito - 2 vikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Baada ya kumuosha samaki, weka katika sufuria. Tia chumvi, ndimu, pilipili mbichi ilosagwa. Tia vitunguu na nyanya zilosagwa Mkaushe kwa hivyo viungo, akianza kukauka tia tui la nazi. Acha kidogo tu katika moto tui liwive mchuzi ukiwa tayari.
Vipimo Vya Bamia
Bamia - ½ kilo takriban
Nyanya kopo - 1 kijiko cha chai
Methi/uwatu/fenugreek seeds ilosagwa - 1 kijiko cha chai
Dania/corriander ilosagwa - ½ kijiko cha chai
Chumvi - kiasi
Mafuta - 1 kikombe cha kahawa
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Katakata bamia kwa urefu. Weka mafuta katika karai, kisha tia bizari zote na nyanya kopo, kaanga kidogo. Tia bamia endelea kukaanga, kisha acha katika moto mdogomdogo ufunike. Kila baada ya muda funua karai ukaange bamia hadi ziwive zikiwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:34:53 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Unga 2 Vikombe
Samli au shortening ya mboga 2 Vijiko vya supu
Maziwa ¾ Kikombe
Iliki Kiasi
Mafuta ya kukarangia Kiasi
Shira
Sukari 1 Kikombe
Maji ¾ Kikombe
Vanila ½ Kijiko cha chai
Zafarani (ukipenda) Kiasi
Jinsi ya kupika na kuandaa
Katika kisufuria pasha moto maziwa na wakati huo huo chemsha Samli katika kisufuria kengine. Tia unga katika bakuli na iliki, kisha mimina samli iliyochemka na huku unachanganya, kisha tia maziwa na uwendele kuchanganya vizuri isiwe na madonge, ikiwa maziwa haitoshi ongeza maji kidogo. Kisha uwache unga ukae mahali pa joto kwa muda wa dakika 10 hivi. Halafu fanya viduara vidogo vidogo, kisha finyiza kwenye greta yenye vishimo vidogo ili upate umbo kama kwenye picha. Kisha karanga kwenye mafuta yaliyopata moto hadi vibadilike rangi ya dhahabu, kisha viepue vichuje mafuta. Chemsha shira, ikiwa tayari mimina visheti na upepete na kuzichanganya zipate shira kote. Weka kwenye sahani na zitakuwa tayari kwa kuliwa na kahawa.
Updated at: 2024-05-25 10:34:46 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji:
Unga sembe glass 1 Unga ngano glass 1 Sukari glass 1 (unaweza kupunguza kidogo) Maziwa glass 1 Mafuta 1/2 glass Mayai 4 Iliki iliosagwa 2tbs Bp 2tbs
Jinsi ya kupika:
Saga sukari yako uweke kwenye bakuli safi pamoja na mayai. Tumia mashine ya cake kusagia hadi ifure/ivimbe. Weka mafuta saga, weka maziwa saga, weka unga wa ngano na bp(bp imix kwenye unga kabla kumimina kwenye mchanganyiko) changanya vizuri halafu malizia kwa kuweka unga sembe na iliki usage vizuri.
Chukua trey au sufuria safi weka baking paper Mimina mchanganyiko wako na uoke.
Ukiwiva utoe na uwache upoe. Mkate wa sembe utakua tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:39 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Ndizi tamu (plantain) 3-4 Tui la nazi (coconut milk) kikombe 1 cha chai Sukari (sugar) 1/4 ya kikombe cha chai Hiliki (Ground cardamon) 1/4 ya kijiko cha chai Chumvi (salt) 1/4 ya kijiko cha chai
Matayarisho
Menya ndizi kisha zikwangue utomvu wote. Baada ya hapo zikate kati (kiurefu) na kisha kata tena kati katika kila ndizi vitoke vipande 4. baada ya hapo toa moyo wa katikai wa ndizi. Zioshe na kisha zikaushe maji na uziweke kwenye sufuria ya kupikia. Baada ya hapo tia tui la nazi, sukari, chumvi na hiliki. Ziinjike jikono na uziache zichemke uku ukiwa unalikoroga tui ili lisikatike. Baada ya dakika 10 tui la nazi litakuwa limepungua na kubaki kidogo na hapo ndizi zitakuwa zimeshaiva. Ziache zipoe na zitakuwa tayari kwa kuliwa. Zinaweza kuliwa kama mlo (main meal) au kitinda mlo (dissert) au mlo wa pembeni (side dish) haswa kwa futari.