Updated at: 2024-05-25 10:34:39 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Ngano nzima (shayiri) - 3 Vikombe
Kuku - ½ (3 LB takriban)
Thomu na tangawizi iliyosagwa - 1 kijko cha supu
Pilipili manga ya unga - ½ kijiko cha chai
Jiyrah (cumin/bizari ya pilau) - ½ kijiko cha chai
Chumvi - kiasi
Kidonge cha supu - 1
Samli ya moto - ½ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Roweka ngano (shayiri) tokea usiku au muda wa masaa. Katakata kuku mtie katika sufuria, tia maji kiasi viungo vyote. Mchemeshe awive na ibakie supu yake. Toa kuku, toa mifupa na umchambue chambue vipande vidogo vidogo. Chemisha ngano (shayiri) kwa kufunika sufuria hadi iwive na kukauka maji. Tia supu ya kuku katika ngano (shayiri), na kuku uliyemechambua. Tia kidonge cha supu. Tia samli nusu (bakisha nusu) kisha songa mchanganyiko uchanganye hadi ivurugike kuku na ngano (shayiri) vizuri. Mimina katika sahani, mwagia samli imoto ilyobakia likiwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:37:40 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Viazi ulaya 4 vya wastani Hoho jekundu 1/2 Hoho la njano 1/2 Hoho la kiajani 1/2 Njegere 1 kikombe cha chai Carrot 1 kubwa Broccoli kidogo Cauliflower kidogo Kitunguu 1 Nyanya 1/2 kopo Swaum/tangawizi 1 kijiko cha chakula Curry power 1 kijiko cha chakula Coriander powder 1 kijiko cha chai Tarmaric 1/2 kijiko cha chai Olive oil Chumvi 1/4 ya limao
Matayarisho
Katika sufuria isiyoshika chini kaanga vitunguu mpaka viwe vya brown kisha tia swaum/tangawizi na spice zote kaanga kwa muda mfupi kisha tia nyanya na chumvi. pika mpaka nyanya ziive kisha tia vegetable zote na vimaji kidogo sana na kisha kamulia limao, baada ya hapo punguza moto na kisha funika na zipike mpaka vegetable zote ziive na rojo ibakie kidogo. Baada ya hapo mboga yako itakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:48 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Tango 1/2 Kitunguu 1/2 Cherry tomato 8 Lettice kiasi Green olives kidogo Black olives kidogo Hoho jekundu 1 Carrot Giligilani kidogo
Salad dressing Yogurt 1/2 kikombe Swaum 1/2 kijiko cha chai Limao 1/2 Pilipili ya unga 1/4 kijiko cha chai Chumvi kidogo Olive oil kiasi
Matayarisho
Osha vitu vyote kisha vikaushe maji. Baada ya hapo ktk bakuli kubwa katakata, lettice, tango,hoho, kitunguu,giligilani na kisha ikwangue carrot na utie bila kusahau nyanya zote pamoja na olives.Baada ya hapo ichanganye vizuri, kisha tengeneza salad dressing kwa kuchanganya vitu vyote vilivyo (kwenye list ya salad dressing) kisha koroga vizuri.Baada ya hapo ichanganye na salad.Na hapo salad yako itakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuila na chochote upendacho kama vile chips, nyama choma au au chakula kikuu.
Updated at: 2024-05-25 10:37:55 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Nyanya 1 kg Maji Iita ½ Chumvi kijiko kidogo 1 Sukari
Hatua
• Osha nyanya, katakata na chemsha na maji mpaka zilainike. • Chuja juisi. • Pima juisi - vikombe 2 vya juisi kwa kikombe 1 cha sukari, weka kwenya sufuria safi . • Ongeza chumvi, chemsha ukikoroga mpaka ichemke. • Mara ikichemka epua, pozesha na weak kwenya chombo safi kwa kunywa.
Updated at: 2024-05-25 10:23:14 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele - 1 kilo
Kuku - 1
Vitunguu - 3
Viazi/mbatata - 5
Jira/bizari ya pilau nzima - 3 vijiko vya supu
Mdalasini - 1 kijiti
Pilipili manga - 1 kijiko cha supu
Hiliki - 3 chembe
Karafuu - 5 chembe
Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa - 3 vijiko vya supu
Tangawizi mbichi ilosagwa - 3 vijiko vya supu
Mafuta ya kupikia - ½ kikombe
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Baada ya kumsafisha kuku na kumkatakata, mchemshe kwa chumvi na ndimu, kijiko kimoja cha kitunguu thomu/somu na tangawizi yote.. Menya viazi, katakata vipande vya kiasi. Katakata vitunguu maji kisha kaanga kwa mafuta katika sufuria ya kupikia pilau. Tia bizari zote isipokuwa hiliki. Saga hiliki kisha tia pamoja na kitunguu thomu/somu ukaange kidogo. Mimina kuku na supu yake ikichemka kisha tia mchele na viazi. Koroga kisha acha katika moto mdogomdogo wali uwive kama kawaida ya kupika pilau.
Updated at: 2024-05-25 10:37:27 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Kupata takriban gilasi 6
Mabungo - 3
Maji - 6 au 7 Gilasi
Sukari - kiasi upendacho
Chumvi - kidogo sana
Namna Ya Kutayarisha:
Kata mabungo na toa nyama yake tia katika mashine ya kusagia. Tia maji, sukari na chumvi usage kidogo tu. Chuja kisha mimina katika jagi uweke katika friji. Mimina katika gilasi.
Updated at: 2024-05-25 10:23:12 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Mchele wa pishori (basmati) - 4
Nyama ya kuku bila mafupa - 1 Lb
Kamba saizi kubwa - 1Lb
Mchanganyiko wa mboga - njegere, karoti,
mahindi, maharage ya kijani (spring beans) - 2 vikombe
Figili mwitu (Cellery) - 2 mche
Vitunguu vya majani (spring onions) - 4-5 miche
Kebeji - 2 vikombe
Pilipili ya unga nyekundu - 1 kijiko cha chai
Pilipili manga ya unga - 1 kijiko cha chai
Sosi ya soya - 3 vijiko vya supu
Mafuta - 1/4 kikombe
Chumvi - kiasi
MAPISHI
Osha na roweka mchele. Tia kamba chumvi na pilipili nyekundu ya unga. Tia mafuta vijiko viwili katika kikaango (frying pan), kaanga kamba kidogo tu, weka kando. Katakata kuku vipande vidogo vidogo, tia chumvi na pilipili manga. Kaanga kaTika kikaango (ongeza mafuta kidogo) Weka kando. Katika karai, tia mafuta kidogo kama vijiko vitatu vya supu, tia kamba na kuku, tia mboga za mchanganyiko, sosi ya soya na chumvi, kaanga kidogo. (Kama mboga sio za barafu) itabidi uchemshe kidogo. Katakata kebeji, figili mwitu (cellery) na vitunguu vya majani (spring onions) utie katika mchaganyiko. acha kwa muda wa chini ya dakika moja katika moto. Chemsha mchele, tia mafuta kidogo au siagi, chumvi upikie uive nusu kiini, mwaga maji uchuje. Changanya vyote na wali rudisha katika sufuria au bakuli la oveni, funika na upike kwa moto wa kiasi kwa muda wa dakika 15-20 takriban. Epua na upakue katika sahani ukiwa tayari kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:49 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Miguu ya kuku (chicken legs) 10 Kitunguu swaum na tangawizi (ginger & garlic paste) 1 kijiko cha chakula Limao (lemon) 1 Pilipili iliyosagwa (ground scotch bonnet) 1/2 Giligilani iliyokatwakatwa (chopped coriander) kiasi Chumvi (salt) kiasi Mafuta ya kukaangia (veg oil)
Matayarisho
Safisha kuku kisha mtie kwenye sufuria na viungo vyote (kasoro mafuta na giligilani) kisha mchemshe mpaka aive na umkaushe supu yote. Baada ya hapo mkaange katika mafuta mpaka awe wa brown kisha mtoe na uweke katika kitchen towel ili kuchuja mafuta. Baada ya hapo weka katika sahani na umwagie giligilani kwa juu. Na hapo kuku wako atakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:56 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Ngogwe ½ kg Kitunguu 2 Bamia ¼ kg Karoti 2 Mafuta vijiko vikubwa 8 Maji vikombe 3 Mayai 2 Nyanya 2 Chumvi
Hatua
• Osha, menya na katakata nyanya na vitunguu. • Osha, menya na kata karoti virefu virefu. • Osha, kata ncha za bamia pande zote na kama ndefu sana kata vipande viwili. • Osha, kata vikonyo vya ngongwe, kama ni kubwa kata vipande viwili. • Kaanga vitunguu, ongeza nyanya, korogoa mpaka zilainike. • Ongeza ngogwe, karoti, bamia na chumvi, koroga mpaka zionekane kukolea rojo. • Ongeza maji vikombe 2 koroga na funikia kwa dakika 10-15 au mpaka ziive. Punguza moto. • Koroga mayai kwenye maji mpaka iwe kama maziwa, ongeza kwenye mboga na koroga polepole usiponde ngogwe wala bamia kwa dakika 5. • Onya chumvi, pakua za moto kama kitoweo.
Updated at: 2024-05-25 10:23:07 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Unga 6 Vikombe
Sukari ya kusaga 2 vikombe
Siagi 500 gm
Baking powder 1 Kijiko cha chai
Kastadi ½kikombe
MAPISHI
Koroga siagi na sukari katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy). Mimina mchanganyiko uliopiga kwa mashine kwenye bakuli. Tia unga na baking powder na Kastadi. Kata usanifu (design) unaopenda halafu panga kwenye sahani ya kupikia (baking tray). Pika (bake) katika oven moto wa 350° F kama muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama.