Updated at: 2024-05-25 10:37:48 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Makongoro (miguu ya ng'ombe) kiasi Limao 1 kubwa Kitunguu swaum Tangawizi Chumvi Pilipili
Matayarisho
Safisha makongoro kisha yatie kwenye pressure cooker. Kisha tia kitunguu swaum, tangawizi, chumvi,limao na maji kiasi. Baada ya hapo yachemshe mpake yaive na yawe malaini na pia ubakize supu kiasi inaweza kuchukua kama dk 45 au saa 1 hivi. Baada ya hapo yaipue na upakue supu yako kwenye bakuli katia pilipili kiasi kisha itakuwa tayari kwa kuliwa.
Note: Ukiwa unanunua makongoro hakikisha unachukuwa yale yasiyokuwa na manyoya na pia hakikisha usiyachemshe kupitiliza kwani yakiwa malaini sana utashindwa kuyaenjoy.
Updated at: 2024-05-25 10:37:57 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Unga 300gm
Siagi 225gm
Icing Sugar 60gm
Chokoleti iliyokoza (Dark Chocolate) - 225gm
Vanilla – Vijiko 2 vya chai
Yai -1
Baking Powder ½ kijiko cha chai
Njugu za vipande ½ kikombe cha chai
Njugu zilizosagwa ¼ kikombe cha chai
JINSI YA KUTAYARISHA
Piga sukari na siagi katika mashine ya keki mpaka iwe laini Kisha mimina yai na vanilla koroga vizuri Mwisho mimina unga na baking powder polepole mpaka ichanganyike. Kata kata umbo (shape) lolote unavyopenda (kama nyota, pembetatu,duara, kopa n.k) Panga kwenye treya na choma kwa moto wa 350°C , vikibadilika rangi kidogo tu vitoe Yayusha chokoleti tia kwenye bakuli ndogo. kisha paka kwa kijiko au chovyea upande mmoja mmoja wa biskuti kisha nyunyizia njugu za kipande na njugu ya unga. Panga kwenye sahani tiyari kunywewa na chai ya maziwa au kahawa.
Mapishi mazuri ya Wali Wa Kukaanga Kwa Kidari Cha Kuku
Updated at: 2024-05-25 10:23:11 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo vya Wali:
Mchele - 3 vikombe
*Maji ya kupikia - 5 vikombe
*Kidonge cha supu - 1
Samli - 2 vijiko vya supu
Chumvi kiasi
Hiliki - 3 chembe
Bay leaf - 1
Vipimo Vya Kuku
Kidari (chicken breast) - 1Kilo
Kitunguu - 1
Tangawizi mbichi - ½ kipande
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 7 chembe
Pilipili mbichi - 3
Ndimu - 2
Pilipilimanga - 1 kijiko cha chai
Mdalasini - ½ kijiko cha chai
Jira/Cummin ya unga - 1 kijiko cha chai
Maji - ¼ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Wali:
Osha na roweka mchele kisha weka sufuria katika moto tia samli ipashe moto. Tia hiliki, bay leaf, kaanga, kisha tia mchele ukaange kidogo. Tia maji, chumvi na kidonge cha supu, upike wali kama unavyopika pilau. *Maji kisia kwa kutegemea mchele ulivyo. *Unaweza kutumia supu yoyote badala ya kidonge.
Kuku:
Katakata kidari cha kuku vipande vya kiasi, weka katika sufuria, tia ndimu, bizari zote, chumvi. Katakata kitunguu vipande vidogodogo, pilipili, na kitunguu thomu (chopped), tia katika kuku. Chuna tangawizi mbichi tia katika kuku. Changanya vitu vyote vizuri. Tia maji kiasi ¼ kikombe tu kiasi cha kumkaushia kuku. Weka katika moto mpike huku unageuzageuza. Anapokaribia kukauka epua akiwa tayari kuliwa na wali (na saladi upendayo)
Updated at: 2024-05-25 10:22:57 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Unga wa ngano (plain flour) ( 1/4 kilo) Yai (egg 1) Sukari (sugar 1/4 kikombe cha chai) Chumvi (salt 1/4 kijiko cha chai) Hiliki (ground cardamon 1/4 kijiko cha chai) Maji kiasi Mafuta (vegetable oil)
Matayarisho
Tia unga kwenye bakuli, kisha weka sukari, chumvi, hiliki na maji kiasi. Kisha koroga mpaka mchanganyiko wako uwe mzito. Baada ya hapo tia yai na ukoroge tena. hakikisha mchanganyiko hauwi mzito sana au mwepesi sana.Baada ya hapo onja kama kila kitu kimekolea. Injika chuma cha kupikia chapati (fry-pan) jikoni katika moto wa wastani. Baada ya hapo tia nusu kijiko cha chakula cha mafuta katika fry-pan na kisha yatandaze. Hakikisha chuma kinapata moto na weka upawa mmoja wa unga wa chapati na uutandaze mpaka uwe flat. Baada ya hapo subiri mpaka chapati ikauke juu na kisha igeuze upande wa pili tia mafuta kijiko 1 kikubwa cha chakula kwa upande wa chini na wa juu kisha uanze kuikandamiza kwa juu na kijiko ili iweze kuiva vizuri kwa chini. Ikisha kuwa ya rangi ya brown igeuze na upike upande wa pili kiasi kisha iipue na uiweke kwenye sahani yenye kitchen towel ili kukausha mafuta. Rudia hii process kwa unga wote uliobakia. Na chapati zitakuwa tayari
Updated at: 2024-05-25 10:23:07 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Unga 6 Vikombe
Sukari ya kusaga 2 vikombe
Siagi 500 gm
Baking powder 1 Kijiko cha chai
Kastadi ½kikombe
MAPISHI
Koroga siagi na sukari katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy). Mimina mchanganyiko uliopiga kwa mashine kwenye bakuli. Tia unga na baking powder na Kastadi. Kata usanifu (design) unaopenda halafu panga kwenye sahani ya kupikia (baking tray). Pika (bake) katika oven moto wa 350° F kama muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama.
Updated at: 2024-05-25 10:23:14 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Ndizi - 15 takriiban
Nayma ya ng’ombe - 1 kilo
Kitunguu maji - 1
Nyanya - 3
Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa - 1 kijiko cha supu
Tangawizi mbichi ilosagwa - 1 kijiko cha supu
Pilipili mbichi ilopondwa - 2
Jira/cummin/bizari ya pilau ilosagwa - 1 kijiko cha chai
Ndimu - 1
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Chemsha nyama kwa ndimu, chumvi na tangawizi mbichi na kitunguu thomu. Menya ndizi na zikatekate vipande kiasi, weka katika sufuria. Katakata kitunguu na nyanya utie katika ndizi. Tia jira na chumvi. Nyama ikiwiva mimina pamoja na supu yake ufunike ndizi ziwive na kuwa tayari kuliwa. Ukipenda tia pilipili mbuzi zichemke pamoja na ndizi.
Updated at: 2024-05-25 10:34:48 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Leo wapendwa nitaenda kuzungumzia mapishi ya mchuzi wa kuku (chicken curry).
Mahitaji
Kuku mzima Nyanya kubwa 3 Karoti mbili Pilipili hoho Kotmiri Tangawizi Kitunguu maji Kitunguu saumu kidogo Ndimu Mafuta ya kupikia Chumvi (pilipili ukipenda)
Matayarisho
1. Menya vitunguu saumu na tangawizi na uvitwange pamoja. 2. Katakata kuku vipande vidogo kisha ukamulie ndimu na kupaka mchanganyiko wa tangawizi na vitunguu saumu (kiasi tu). 3. Katakata vitunguu maji na pilipili hoho uweke pembeni. 4. Grind (Kwangua) kwenye grater nyanya na karoti pia uweke pembeni. 5.Katakata kotmiri vipande vidogo uweke pembeni. 6. Andaa kikaango na jiko.
Mapishi
1. Bandika kikaango jikoni na mafuta kiasi, yakishachemka weka vitunguu maji na kaanga hadi vimelainika na kuiva (hakikisha haviungui). 2. Weka pilipili hoho na karoti na endelea kukoroga hadi vyote viive na kulainika, Kisha weka chumvi. 3. Sasa weka vipande vya nyama koroga na funikia kwa dakika 3, kisha weka nyanya zako ulizo grind na koroga ili zichanganyike vizuri, vikishachanganyika weka kotmiri na pilipili kama utapenda. Acha vichemke kwa dakika 5. Hakikisha moto sio mkali sana. 4. Angalia kama nyama zimeiva vizuri kisha epua mchuzi wako. 5. Pakua kwenye bakuli na katakata kotmiri uweke kwa juu. Unaweza kula kwa ugali, wali, ndizi rost au chipsi.