Updated at: 2024-05-25 09:52:20 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Unga wa mchele ( Vikombe 2 vikubwa) Sukari (Nusu ya kikombe kikubwa) Hamira ( Nusu ya kijiko cha chai) Hiliki (Nusu ya kijiko cha chai) Tui la nazi ( Kikombe kimoja kikubwa) Unga wa ngano (Vijiko viwili vya chakula) Mafuta ya kuchomea (Vegetable oil)
Matayarisho
Unachanga unga, sukari, hamira, hiliki, unga wa ngano na tui la nazi pamoja katika bakuli la plastiki. Kisha unaukoroga mpaka mchanganyiko unakuwa kama uji mzito. Kava bakuli lililokuwa na mchanganyiko kisha hifadhi katika sehemu yenye joto kwa muda wa masaa matatu.
Jinsi ya kupika
Weka chuma cha kuchomea vitumbua katika moto wa wastani, kisha weka mafuta kwenye chuma cha kuchomea ( Kijiko kimoja cha chai) mafuta yakisha pata moto tia uji wako (upawa mmoja) katika kila shimo la chuma cha kuchomea. Acha mpaka kitumbua kikauke kisha geuza na tia mafuta. Acha upande wa pili wa kitumbua mpaka uwe rangi ya kahawia na hapo kitumbua kitakuwa kimeiva utakitoa. Rudia hatua hizo kwa vitumbua vyote vilivyobaki.
Updated at: 2024-05-25 10:37:55 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Nyanya 1 kg Maji Iita ½ Chumvi kijiko kidogo 1 Sukari
Hatua
• Osha nyanya, katakata na chemsha na maji mpaka zilainike. • Chuja juisi. • Pima juisi - vikombe 2 vya juisi kwa kikombe 1 cha sukari, weka kwenya sufuria safi . • Ongeza chumvi, chemsha ukikoroga mpaka ichemke. • Mara ikichemka epua, pozesha na weak kwenya chombo safi kwa kunywa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:43 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Salmon fillet 2 Potatao wedge kiasi Lettice kiasi Cherry tomato Limao 1 Swaum Chumvi Olive oil
Matayarisho
Mmarinate samaki na chumvi, swaum na nusu ya limao kisha muweke pembeni, baada ya hapo washa oven kisha tia potato wedge zikisha karibia kuiva anza kumpika samaki, tia mafuta kidogo sana kama kijiko kimoja cha chai hivi katika frypan isiyoshika chini yakisha pata moto kiasi muweke samaki wako (upande wenye ngozi chini kwanza) Mpike mpaka uone rangi ya kahawia kwa chini kisha mgeuze upande wa pili, uku samaki wako akiwa anaendelea kuiva, tayarisha salad yako kwa kusafisha lettice na nyanya kisha zichanganye pamoja kisha tengeneza salad dressing pembeni , kamua limao kisha tia olive oil na chumvi kidogo, Baada ya hapo samaki na potato wedge vitakuwa vimeiva, andaa mlo wako na utakuwa tayari kwa kuliwa.
Mapishi ya Chai ya maziwa, mandazi, uyoga na mayai
Updated at: 2024-05-25 10:22:58 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mandazi (angalia jinsi ya kupika katika recipe ya mandazi ya nyuma) Uyoga (mashroom kikombe 1 cha chai) Mayai (eggs 4) Hoho (greenpepper 1/4 ya hoho) Nyanya (fresh tomato 1) Kitunguu (onion 1/4 ya kitunguu) Chumvi (salt) Mafuta (vegetable oil) Hiliki nzima (cardamon 4) Masala ya chai (tea masala 1 kijiko cha chai) Pilipili mtama iliyosagwa (ground black pepper 1/4 ya kijiko cha chai) Maziwa (fresh milk 1 kikombe cha chai) Majani ya chai (tea leaves) Maji kiasi. Sukari (sugar)
Matayarisho
Jinsi ya kupika chai, weka maziwa, maji kiasi,hiliki, masala ya chai, pilipili mtama na majani katika sufuria. Chemsha kwa muda wa dakika 10 na chai itakuwa tayari. Jinsi ya kupika mayai, weka mafuta kiasi katika fry pan na utie vitunguu, vikaange kidogo kisha tia nyanya, chumvi na hoho. Pika kwa muda wa dakika 4 kisha tia mayai na uyaache yaive mpaka yakauke kisha geuza upande wa pili na uyapike mpaka ya ive kisha ipua. Jinsi ya kupika uyoga, weka mafuta kidogo katika fry pan kisha tia uyoga na chumvi na ukaange mpaka uive katika moto wa wastani. Ukisha iva breakfast yako itakuwa teyari kwa kuseviwa.
Kaanga kitunguu kikishaiva tia nyanya na chumvi. kaanga mpaka nyanya ziive kisha tia nyanya chungu,curry powder na pilipili 1 nzima, baada ya hapo tia mchicha na uuchanganye vizuri kwa kuugeuzageuza. Mchicha ukishanywea tia tui la nazi na uache lichemke mpaka liive na hapo mchicha utakuwa tayari. Safisha nyama kisha iweke kwenye sufuria na utie chumvi, tangawizi, limao na kitunguu swaum. Ichemshe mpaka itakapoiva na kuwa laini. Baada ya hapo weka sufuria jikoni na mafuta kidogo yakisha pata moto tia vitunguu na nyama na uvikaange pamoja, kisha tia curry powder na ukaange mpaka nyama na viunguu vya brown. na hapo nyama itakuwa imeiva. Malizia kwa kupika wali kwa kuchemsha maji kisha tia mafuta, chumvi na mchele na upike mpaka uive. Baada ya hapo chakula kitakuwa tayari kwa kuseviwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:41 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Kabichi 1/2 kilo Nyanya ya kopo 1/2 Kitunguu 1 Curry powder 1/2 kijiko cha chai Chumvi Olive oil
Matayarisho
Kwanza kabisa bandua magada ya juu ya kabichi, kisha ioshe na uikaushe maji baaba ya hapo katakata kabichi (inapendeza zaidi kama ikikatwa nyembamba) kisha saga pamoja nyanya na kitunguu. Baada yahapo tia katika sufuria ya kupikia, ipike mpaka maji yote yatakapokauka kisha tia chumvi, curry powder na mafuta pika kwa muda kiasi kisha tia kabichi na upunguze moto. Pika mpaka kabishi itakapoiva kisha ipua na itakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuila kwa wali au ugali.
Mawazo Mazuri ya Kifungua Kinywa cha Haraka na Salama kuanza Siku Yako Vizuri
🌞 Karibu kwenye ulimwengu wa mawazo mazuri ya kifungua kinywa! 🍳 Unataka kuanza siku yako vizuri? Soma makala yetu na utajifunza mapishi rahisi na salama. Tazama ni kivipi unaweza kufurahia kiamsha kinywa kinachokufanya ukimbie siku yako na nguvu tele! 🔥 Sasa tafadhali fungua makala yetu na ujifunze zaidi! 👉🏽🤩 #kiamshakinywa #mapishi #sikuyakovizuri
Updated at: 2024-05-25 10:22:17 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mawazo Mazuri ya Kifungua Kinywa cha Haraka na Salama kuanza Siku Yako Vizuri 🌅
Hakuna jambo bora zaidi kuliko kuanza siku yako vizuri na kifungua kinywa kinachokupa nishati na furaha. Kwa kuwa AckySHINE, ninapenda kushiriki nawe mawazo mazuri ya kifungua kinywa cha haraka na salama ambacho kitakusaidia kuanza siku yako vizuri. Hapa kuna orodha ya mawazo 15 ambayo unaweza kuyajumuisha katika maisha yako ya kila siku:
🍳 Chagua kifungua kinywa kinachojumuisha protini, wanga na mafuta yenye afya. Kwa mfano, unaweza kula mayai yaliyopikwa kwa mafuta kidogo na mkate wa ngano nzima.
🥣 Jumuisha nafaka nzima kama oatmeal au millet katika kifungua kinywa chako. Nafaka hizi zina nyuzinyuzi nyingi na zitasaidia kudumisha afya ya utumbo wako.
🍌 Ongeza matunda kwenye kifungua kinywa chako. Matunda yana virutubisho vingi na yatakupa nishati ya kutosha kwa siku yako.
🥛 Kinywaji cha maziwa kitakusaidia kupata protini na madini ya kalsiamu. Unaweza kunywa glasi ya maziwa ya mbuzi au kula jogoo au jibini la Cottage.
🍵 Kunywa kikombe cha chai ya kijani. Chai ya kijani ina antioxidants ambazo zinasaidia kuboresha afya ya moyo wako.
🥜 Ongeza karanga au mbegu kwenye kifungua kinywa chako. Karanga na mbegu zina mafuta yenye afya na omega-3 ambayo ni muhimu kwa afya ya ubongo wako.
🥗 Chagua kifungua kinywa kinachojumuisha mboga mboga. Unaweza kuongeza mboga kwenye omeleti yako au kula sahani ya saladi yenye mboga mbalimbali.
🍞 Ikiwa wewe ni mtu anayependa mkate, chagua mkate wa ngano nzima au mkate uliotengenezwa kwa unga mzima. Mkate huu una nyuzi nyingi na unakuweka kushiba kwa muda mrefu.
🍯 Ikiwa unataka kuongeza ladha tamu kwenye kifungua kinywa chako, tumia asali badala ya sukari. Asali ni afya na ina virutubisho vingi kuliko sukari iliyo na sukari nyingi.
🌿 Ongeza mdalasini kwenye kifungua kinywa chako. Mdalasini ina mali ya kupunguza sukari ya damu na inaweza kukusaidia kudhibiti hamu yako ya kula.
🥚 Ikiwa unapenda kula omeleti, hakikisha unatumia yai la kutosha na kuongeza mboga mboga zaidi. Hii itaongeza lishe na ladha ya chakula chako.
🥦 Jumuisha mboga kama broccoli kwenye kifungua kinywa chako. Broccoli ni tajiri na vitamini na madini na itasaidia kukuimarisha mfumo wako wa kinga.
🥤 Jaribu kinywaji cha smoothie kinachojumuisha matunda, mboga, na maziwa au maji. Smoothie itakupa nishati na virutubisho vingi.
🕙 Usikose mlo wa kifungua kinywa. Kula mlo wa kifungua kinywa ndani ya saa moja baada ya kuamka itasaidia kuamsha mwili wako na kuanza siku yako vizuri.
🍽️ Changanya vyakula tofauti katika kifungua kinywa chako ili uweze kufurahia ladha mbalimbali na kupata virutubisho vyote muhimu.
Kwa hivyo, kama AckySHINE, nakuomba ujaribu angalau moja ya mawazo haya ya kifungua kinywa. Utaona tofauti kubwa katika nishati yako na jinsi unavyohisi wakati wa siku. Kumbuka, kifungua kinywa ni muhimu sana na hakikisha unapata mlo kamili na lishe bora. Je, umeshajaribu njia yoyote ya kifungua kinywa ambayo imesaidia kuanza siku yako vizuri? Tuambie mawazo yako kwenye sehemu ya maoni hapa chini.
Updated at: 2024-05-25 10:37:56 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Ngogwe ½ kg Kitunguu 2 Bamia ¼ kg Karoti 2 Mafuta vijiko vikubwa 8 Maji vikombe 3 Mayai 2 Nyanya 2 Chumvi
Hatua
• Osha, menya na katakata nyanya na vitunguu. • Osha, menya na kata karoti virefu virefu. • Osha, kata ncha za bamia pande zote na kama ndefu sana kata vipande viwili. • Osha, kata vikonyo vya ngongwe, kama ni kubwa kata vipande viwili. • Kaanga vitunguu, ongeza nyanya, korogoa mpaka zilainike. • Ongeza ngogwe, karoti, bamia na chumvi, koroga mpaka zionekane kukolea rojo. • Ongeza maji vikombe 2 koroga na funikia kwa dakika 10-15 au mpaka ziive. Punguza moto. • Koroga mayai kwenye maji mpaka iwe kama maziwa, ongeza kwenye mboga na koroga polepole usiponde ngogwe wala bamia kwa dakika 5. • Onya chumvi, pakua za moto kama kitoweo.
Updated at: 2024-05-25 10:34:38 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Viazi - 3lb
Nyama - 1lb
Kitunguu - 1
Nyanya - 2
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 kijiko cha chai
Manjano - ½ kijiko cha chai
Curry powder - ½ kijiko chai
Nyanya kopo - 1 kijiko cha chai
Pilipili ya unga - kiasi upendavyo
Chumvi - kiasi
Kidonge cha supu - 1
Tui la nazi - 1 kopoau zaidi
Mtindi ukipenda - 3 vijiko vya supu
Kotmiri - kiasi ya kupambia
Nazi ya unga - 4 vijiko vya supu
Mafuta - 2 vijiko vya supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Kata nyama vipande vipande kisha chemsha na chumvi mpaka iive. Menya maganda viazi na ukate slice kubwa weka pembeni Kata kata kitunguu kisha kaanga na mafuta mpaka vibadilike rangi Tia thomu, bizari ya manjano, pilipili ya unga, nyanya kopo Kata kata nyanya nzima vipande vidogo tia na kidonge cha supu. Kisha tia viazi, nyama na tui la nazi finika mpaka viazi viwive lakini visiwe vikavu. Tia mtindi na nazi ya unga kama vijiko 4 vya supu iache motoni kidogo kisha pakua, tupia kotmiri juu na itakuwa tayari kuliwa.