Updated at: 2024-05-25 10:23:10 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Unga - 1 Kikombe
Sukari ya kusaga - 3/4 Kikombe
Siagi - 125 gms
Yai - 1
Baking powder - 1/2 kijiko cha chai
Zabibu kavu - 1/2 kikombe
Cornflakes iliyovunjwa (crushed) - 2 Vikombe
Vanilla - 1 kijiko cha chai
MAANDALIZI
Tia kwenye mashine ya kusaga (blender) au mashine ya keki, siagi, yai na vanilla uchanganye hadi ichanganyike vizuri. Tia baking powder, zabibu na unga na changanya vizuri. Paka siagi sinia ya kupikia ya oveni. Tengeneza viduara vidogo vidogo. Weka cornflakes katika sahani ya chali (flat) na zungusha viduara humo kisha upange katika sinia ya oveni. Pika katika moto wa 350ΒΊF kwa muda wa dakika 20-25 hadi vigeuke rangi na viwive.
Updated at: 2024-05-25 10:34:45 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kupika tambi ni kama ifuatavyo
VIAMBA UPISHI
Tambi pakti moja
Sukari ΒΎ kikombe cha chai
Mafuta Β½ kikombe cha chai
Iliki kiasi
Maji 3 Vikombe vya chai
Vanilla / Arki rose 1-2 Tone
Zabibu Kiasi (Ukipenda)
JINSI YA KUPIKA TAMBI ZAKO
1. Zichambue tambi ziwe moja moja.
2. Mimina mafuta kwenye sufuria yakisha pata moto mimina tambi,zigeuzegeuze mpaka zibadilike rangi na kuwa brown.
3. Punguza mafuta kwa kuyachuja na zirudishe jikoni.
4. Nyunyizia iliki zilizosagwa koroga kidogo na mimina maji na tia arki na acha zichemke mpaka maji yakikaribia kukauka mimina sukari koroga kidogo na punguza moto. 5. Kisha tia zabibu ukipenda, zifunike ili zikaukie vizuri.
6. Zikishakauka pakua kwenye sahani tayari kwa kuliwa
Kidokezi: Itategemea na aina za Tambi unazopika kwa kukisia maji, kama utaona hazijaiva unaweza kuongeza maji kidogo.
Updated at: 2024-05-25 10:22:58 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Unga wa ngano (plain flour 1/2 of kilo) Siagi (butter vijiko 2 vya chakula) Yai (egg 1) Chumvi (1/2 ya kijiko cha chai) Hiliki (ground cardamon 1/4 ya kijiko cha chai) Maji ya uvuguvugu (warm water) Mafuta (vegetable oil)
Matayarisho
Weka unga wa ngano katika bakuli la kukandia, kisha tia chumvi na hiliki na uchanganye kwanza, baada ya hapo tia siagi na uichanganye vizuri na unga mpaka ipotee. Baada ya hapo tia tena yai na uchanganye vizuri. Mchanganyiko ukishachanganyika vizuri sasa unaweza kutia maji ya uvuguvugu kidogo, kidogo huku ukiwa unauchanganya ili kupata donge. Baada ya hapo anza kukanda hilo donge mpaka mabuje yote yapotee na unga uwe mlaini, ambapo itakuchukua kama dakika 15. Baada ya hapo tawanyisha unga katika madonge ya wastani (yasiwe makubwa sana au madogo sana) Ukimaliza hapo, andaa kibao cha kusukumia chapati kwa kukitia unga kidogo ili chapati isinatie kwenye kibao. Sukuma donge moja la chapati mpaka liwe flat na kisha weka kijiko kimoja cha mafuta na usambaze. ukisha maliza ikunje (roll). Fanya hivyo kwa madonge yote yaliyobakia. Baada ya hapo andaa chuma cha kuchomea (fry-pan) katika moto wa wastani. Kisha anza kusukuma chapati (ni vizuri ukaanza na zile ulizozikunja mwanzo ili kuzipa nafasi zile za mwisho ziweze kulainika) ukiwa unasukuma hakikisha zinakuwa flat (na zisiwe nene sana au nyembamba sana) Ukishamaliza hapo tia kwenye chuma cha kuchomea. Acha iive upande mmoja then igeuze upande wa pili. Tia mafuta ama kijiko kimoja kikubwa upande wa chini wa chapati na uanze kuukandamiza kwa juu uku ukiwa unaizungusha. fanya hivyo uku ukiwa unaigeuza kuiangalia kwa chini ili isiungue. ikishakuwa ya brown, geuza upande wa pili na urudie hivyohiyvo mpaka chapati iive. Rudia hii process kwa chapati zote zilizobakia.
Siri ya chapati kuwa laini ni kutia siagi au mafuta ya kutosha kipindi unazikanda na pia kuzikanda mpaka unga uwe laini.
Jinsi ya kuandaa Biriani Na Sosi Ya Nyama Ya Mbuzi
Updated at: 2024-05-25 10:23:15 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Nyama Ya Mbuzi - 1 Kilo
Mchele - 4 Magi
Vitunguu - 3
Nyanya - 2
Nyanya kopo - 3 vijiko vya chai
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa - 2 vijiko vya supu
Pilipili mbichi iliyosagwa - 1 kijiko cha supu
Garam Masala (mchanganyiko wa bizari) - 2 vijiko vya supu
Hiliki - 1 kijiko cha chai
Chumvi - kiasi
Mafuta - Β½ kikombe
Zaafarani au rangi za biriani za kijani na manjano/orenji
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Sosi Ya Nyama
Changanya nyama na thomu, pilipili, chumvi na nusu ya garam masala. Tia katika treya ya oveni uipike nyama (Bake) hadi iwive. Au iwivishe kwa kuichemsha. Katika kisufuria kingine, tia mafuta (bakisha kidogo ya wali) kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi, kisha tia nyanya, nyanya kopo, bizari zote nyingine zilizobakia.
Namna Ya Kupika Wali
Mchele - 4 magi
Mdalasini - 1 kijiti
Hiliki - 3 chembe
Kidonge cha supu - 1
Chumvi
Osha na roweka mchele wa basmati. Tia maji katika sufuria uweke jikoni. Tia kidonge cha supu, mdalasini, hiliki na chumvi . Yakichemka maji tia mchele, funika upike hadi nusu kiini kisha uchuje kwa kumwaga maji. Tia mafuta kidogo katika mchele na zaafarani iliyorowekwa au rangi za biriani kisha rudisha mchele katika sufuria ufunike na upike hadi uwive. Pakua wali katika sahani kisha mwagia sosi ya nyama juu yake, pambia kwa kukatika nyanya, pilipili mboga na figili mwitu (Celery) au mboga yoyote upendayo.
Jinsi ya kutengeneza Bisikuti Za Kaukau Na Kahawa (Cocoa Coffee Biscuits)
Updated at: 2024-05-25 10:23:10 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Maji baridi β kikombe 1
Biskuti za kawaida β paketi 2
Kaukau (cocoa) β vijiko 3 vya kulia
Kahawa ya unga β kijiko 1 cha kulia
Njugu mchanganyiko zilokatwakatwa β kikombe 1
Sukari β kiasi upendavyo
MAANDALIZI
Changanya maji na kaukau na kofi na sukari Katakata biskuti kisha tia paketi moja na nusu uchanganye vizuri. Kisha nusu ya biskuti zilobakia katakata vipande vikubwa na weka juu ya mchanganyiko, kisha changanya kidogo tu. Weka katika foil paper na zungusha (roll) Kisha fungua umwagie njugu au mkassaraat zilosagwa Kisha roll katika foil paper na uweke katika freezer mpaka igande Kisha kata kata slices na iko tayari
Updated at: 2024-05-25 09:52:20 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Unga wa mchele ( Vikombe 2 vikubwa) Sukari (Nusu ya kikombe kikubwa) Hamira ( Nusu ya kijiko cha chai) Hiliki (Nusu ya kijiko cha chai) Tui la nazi ( Kikombe kimoja kikubwa) Unga wa ngano (Vijiko viwili vya chakula) Mafuta ya kuchomea (Vegetable oil)
Matayarisho
Unachanga unga, sukari, hamira, hiliki, unga wa ngano na tui la nazi pamoja katika bakuli la plastiki. Kisha unaukoroga mpaka mchanganyiko unakuwa kama uji mzito. Kava bakuli lililokuwa na mchanganyiko kisha hifadhi katika sehemu yenye joto kwa muda wa masaa matatu.
Jinsi ya kupika
Weka chuma cha kuchomea vitumbua katika moto wa wastani, kisha weka mafuta kwenye chuma cha kuchomea ( Kijiko kimoja cha chai) mafuta yakisha pata moto tia uji wako (upawa mmoja) katika kila shimo la chuma cha kuchomea. Acha mpaka kitumbua kikauke kisha geuza na tia mafuta. Acha upande wa pili wa kitumbua mpaka uwe rangi ya kahawia na hapo kitumbua kitakuwa kimeiva utakitoa. Rudia hatua hizo kwa vitumbua vyote vilivyobaki.
β’ Chambua mgagani, oshana katakata. β’ Chemsha maji, weka chumvi kisha ongeza mgagani, funika zichemmke kwa β’ dakika 5-10. β’ Menye osha na katakata kitunguu. β’ Osha, menya na kwaruza karoti. β’ Kaanga karanga, ondoa maganda na saga. β’ Kaanga vitunguu na karoti mpaka zilainike ukikoroga. β’ Weka mgagani uliochemshwa koroga sawasa na funika kwa dakika 5 zilainike. β’ Changanya maziwa na karanga ongeza kwenye mgagani ukikoroga kasha punguza moto kwa dakika 5 ziive. β’ Onja chumvi na pakua kama kitoweo.
Updated at: 2024-05-25 10:37:35 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele - 3 vikombe
Samaki Nguru (king fish) - 5 vipande
Vitunguu - 2
Nyanya/tungule - 4
Mafuta - 3 vijiko vya supu
Tui la nazi zito - 2 vikombe
Pilipili mbichi - 5-7
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 7-9 chembe
Kotmiri - 1 msongo (bunch)
Bizari ya samaki - 1 kijiko cha chai
Ndimu - 2-3
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Osha samaki, kata vipande kiasi weka kando. Katakata kitunguu na nyanya vipande vidogo vidogo sana (crush) . Katakata kotmiri weka kando. Saga pamoja, pilipili mbichi, kitunguu thomu, ndimu na chumvi. Changanya pamoja na bizari ya samaki kisha paka katika vipande vya samaki acha kidogo vikolee. Weka mafuta katika sufuria au karai, kaanga vitunguu kidogo tu kisha tia nyanya/tungule endelea kukaanga hadi vilainike na kupondeka. Tia kikombe kimoja na nusu cha tui la nazi, kisha tia vipande vya samaki na masala yake, acha mchuzi uchemke samaki aive. Ongeza chumvi, ndimu, pilipili ikihitajika. Ongezea tui lilobakia acha motoni kwa daika chache tu. Epua mwagia kotmiri mchuzi ukiwa tayari.
Pika wali wa maji/mweupe kama kawaida utolee na mchuzi.
Updated at: 2024-05-25 10:22:17 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mawazo Rahisi na yenye Afya ya Kujiandaa kwa Chakula cha Kazi
Kwa mara nyingine tena, hapa ni AckySHINE nikikuletea mawazo bora na yenye afya ya kujiandaa kwa chakula cha kazi. Kama unavyojua, chakula ni nishati muhimu katika kuwezesha utendaji wetu wa kazi. Kwa hiyo, ni muhimu sana kuwa na chakula bora na kilicho na lishe ili kuboresha ubora wa kazi zetu. Hapa kuna orodha ya mawazo 15 rahisi na yenye afya ya kujiandaa kwa chakula cha kazi:
π Kula matunda na mboga safi kama tunda la kifungua kinywa. Matunda na mboga ni chanzo kikubwa cha vitamini na madini muhimu kwa afya yetu.
π Chagua protini nzuri kama kuku, samaki au maharagwe kama sehemu ya chakula cha mchana. Protini ni muhimu kwa ukuaji na ukarabati wa misuli yetu.
π₯¦ Ongeza mboga za majani kama spinach na kale kwenye sahani yako. Mboga hizi zina virutubisho muhimu kama chuma na vitamini C.
π₯ͺ Jenga sandwishi zenye afya kwa kutumia mkate wa ngano nzima, mboga mbalimbali na protini kama turkey au tofu. Hii itakupa nishati ya kutosha na kukusaidia kuhimili mawasiliano ya kazi yako.
π Tumia matunda kama vitafunio vya asili. Matunda yana virutubisho na sukari asili ambayo ni bora kuliko pipi au vitafunio vya sukari.
π Ongeza nyanya kwenye sahani zako. Nyanya zina lycophene, antioxidant ambayo inasaidia kulinda mwili dhidi ya magonjwa.
π Chagua mchele wa kahawia badala ya mchele mweupe. Mchele wa kahawia una nyuzi nyingi na unaweza kukusaidia kusimamia uzito wako na kuboresha digestion yako.
π₯ Kunywa maziwa ya jamii ya skim au maziwa ya mbuzi badala ya maziwa ya ng'ombe ya kawaida. Maziwa ya mbuzi na maziwa ya jamii ya skim yana mafuta kidogo na yanaweza kusaidia kudumisha uzito wako.
π½ Tumia nafaka nzima kama mkate wa ngano nzima, mchele wa kahawia au quinoa badala ya nafaka zilizopakuliwa. Nafaka hizi ni tajiri katika nyuzi na hutoa hisia ya kujazia kwa muda mrefu.
π₯ Ongeza karoti kwenye saladi yako. Karoti ni chanzo kikubwa cha vitamini A, ambayo inasaidia kuimarisha mfumo wetu wa kinga.
π Kula ndizi kama chakula cha baada ya mazoezi. Ndimu zina wanga na potasiamu, ambayo inasaidia kuimarisha misuli na kurejesha nishati baada ya mazoezi.
π Pika vyakula vyenye mafuta kidogo kama vile kukaanga kwa kutumia mafuta ya mizeituni. Mafuta ya mizeituni ni bora kwa afya ya moyo na yanaweza kusaidia kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo.
π₯€ Kunywa maji ya kutosha. Maji ni muhimu kwa afya na ustawi wetu. Unapaswa kunywa angalau glasi 8 za maji kwa siku.
π₯¦ Jaribu kuchemsha mboga zako badala ya kuzipika kwa muda mrefu. Kuchemsha mboga zitahifadhi virutubisho vyao na kuboresha ladha yao.
π₯ Jitahidi kula chakula kilichoandaliwa nyumbani na kuwa na udhibiti mkubwa juu ya viungo vyote unavyotumia. Hii inaweza kusaidia kuepuka vyakula vya haraka na kuongeza lishe kwenye chakula chako.
Hizi ni baadhi tu ya mawazo rahisi na yenye afya ambayo unaweza kuzingatia kujipatia chakula bora na kilicho na lishe wakati wa kukabiliana na changamoto za kazi. Kumbuka, chakula ni mafuta yetu ya ajabu ambayo inatuwezesha kufanya kazi vizuri na kwa ufanisi. Kwa hiyo, kula vizuri na ujaze nishati yako! Je, una mawazo mengine yoyote kwa chakula cha kazi? Tafadhali shiriki nasi katika sehemu ya maoni hapa chini!
Chemsha nyama na chumvi na nusu ya limao mpaka iive kisha weka pembeni. Baada ya hapo andaa vitu vya pilau kwa kuloweka mchele kwenye maji kwa muda wa dakika 10.Menya na kukatakata vitunguu na viazi kisha weka pembeni na pia chemsha maji ya moto na uweke pembeni. Baada ya hapo weka sufuri jikoni na tia mafuta kiasi . Yakisha pata moto tia vitunguu na uvikaange mpaka viwe vya rangi ya kahawia na kisha uitie nyama na ikaange mpaka ipate rangi ya bown pia. Baada ya hapo tia kitunguu swaum na tangawizi na uikoroge vizuri kisha iache ikaangike kwa muda wa dakika 2 kisha tia spice ambazo ni Binzari nyembamba ya unga, hiliki,karafuu, amdalasini na pilipili mtama na viazi. Baada ya hapo unatakiwa ugeuze geuze mpaka mchanganyiko uchanganyike vizuri kisha tia mchele na ugeuzege mpaka uchanganyike na viungo. Baada ya hapo tia chumvi na maji ya kutosha na ukoroge vizuri kisha funika na uache uchemke katika moto wa wastani. Maji yakikaribia kukauka tia binzari nyembamba nzima na ufunike uache mpaka maji yakauke kabisa. maji yakisha kauka ugeuze na ufunike tena na uuache mpaka uive. Baada ya hapo andaa kachumbali kwa kukatakata vitunguu katika bakuli na kisha tia chumvi kwa ajili ya kuondoa ukali wa vitunguu. Baada ya hapo vioshe mpaka chumvi yote iishe. osha nyanya, Pilipili, hoho na kisha katakata slice nyembamba na uchanganye na vitunguu. Baada ya hapo tia chumvi, kamulia limao na uchanganye zote pamoja. Baada ya hapo chakula kitakuwa tayari kwa kuliwa.