Matumizi ya Papai Katika Urembo

By, Melkisedeck Shine.

elimu-sayansi-na-tekinolojia.png

Matumizi ya Papai Katika Urembo

Tunda la kitropiki la papai lina vitamini C na E likiwa na siri kubwa ya urembo na hutumika kutengeneza facial za aina mbalimbali.
Papai limekuwa likitumiwa kama njoia boya ya kutunza uso wako na kumfanya mtu kuwa na ngozi ya asili.

Bidhaa ambazo zimekuwa zikitengenezwa kwa kutumia tunda la papai ni pamoja na sabuni, lotion, tona, moisturiza, facial peels na nyingine nyingi.

Ukitumia facial mask ya papai utakuwa na sura nzuri ya asili na kukupa uonekanaji mzuri wa uso wako. Facial mask hii huweza hutumika kwa watu wa umri na aina yoyote ya ngozi.

Facial mask ya papai ina nguvu ya kung’arisha uso wako.
Pia inasaidia ngozi ambayo imeshaanza kupatwa na makunyanzi kutokana na umri kuonekana ya kuvutia kwani pia imekuwa ikiondoa chunusi na makunyanzi pia.

Ni rahisi kutengeneza facial mask ya papai na ukitumia itakusaidia katika kukabiliana na ngozi iliyoanza kuchoka, kung’arisha ngozi.

Kuna na njia nzuri za kuhakikisha kuwa, tunakuwa na nyuso nzuri zenye kupendeza na kuvutia ikiwemo kutumia vitu vya asili pamoja na matunda ya aina mbalim ambayo husaidia zaidi katika kuimarisha ngozi.

Mask ya mchanganyiko wa papai yai na yai ni nzuri katika kuhakikisha kuwa unakuwa na ngozi nzuri na nyororo.

Njia hii pia husaidia hata wale wenye nyuso za mafuta ambao wamekuwa wakisumbuliwa na chunusi mara kwa mara kwa kufanya ngozi kuwa kavu.

Unaweza kutengeneza aina hii ya mask kwa kufanya yafuatayo:-
Chukua papai likate kasha toa mbegu na kasha lisage kwa kutumia blenda ya kuondaponda kwenye kibakuli kwa kutumia kitukama mchi mdogo wa kinu.

Kisha weka mchanganyiko huo kwenye chombo ulichokichagua kama kikombe au bakuli.
Vunja yai na koroga kuhakikisha kuwa mchanganyiko huo umechanganyika vizuri.
Safisha uso wako kwa kutumia cleanser au maji ya vuguvugu na uondoeuchafu wote ulioganda usoni.

  • Kisha paka mask kuzunguka uso wako, na unapopaka hakikisha kuwa,
  • mchanganyiko huo haugusi macho yako.
  • Osha uso wako baada ya dakika 15 kwa kutumia maji ya vuguvugu.
  • Jifute kwa kutumia taulo safi
  • Unaweza kupaka losheni, tona au moisturiza.

Husaidia kutunza ngozi na kuondoa vipele na uchafu ulioganda usoni.
Hii ni njia rahisi ya kutengeneza uso isiyo na gharama.


elimu-sayansi-na-tekinolojia.png

Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Matumizi ya Papai Katika Urembo;

a.gif Jinsi ya Kujiremba Macho

Kuna urembo mbalimbali wa macho kulingana na taste ya mtu na mapendeleo yake . Leo nitazungumzia "smoky eyes" au macho yaliyapambwa kwa eye liner, mascara na eye shadows zenye rangi nyeusi, grey au za mng'aro… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kuchagua rangi sahihi wakati wa Kujipodoa

YAPO mambo mabalimbali katika tasnia ya urembo hasa katika vipodozi yanayopaswa kuzingatiwa katika kuboresha muonekano wa mtu.
Moja ya mambo hayo ni ujuzi na uelewa wa kutumia rangi katika kujipodoa kwani ni wanawake wachache wenye ujuzi huu.
Katika makala hii, nitakuelezea namna ya kuchanganya na kutofautisha rangi za vipodozi, lengo likiwa ni kuboresha muonekano wako… endelea kusoma

[Kitendawili Kwako] 👉Viwili vifananavyo

[Video Nzuri] 👉Mwanamme anavyozinguana na mwanamke

[Chemsha Bongo Kwako] 👉Ni herufi gani tatu zinafuata baada ya hizi?

vichekesho-bomba-vya-siku.png

a.gif Kampeni ya utunzaji wa wanyama pori

Kampeni hii ilianzishwa na Melkisedeck Leon Shine mwaka 2018.
Lengo la kampeni Hii ni kuhamasisha watu kutunza wanyama pori kwa manufaa yao ya sasa na kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Kampeni hii inaamini kuwa wanyama pori wakitunzwa vizuri wanaweza kuwa msaada kijamii, kiuchumi na kimazingira kwa kizazi hiki na kizazi kijacho… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kufanya ili uwe na umbo dogo la kuvutia

Unaweza kujiuliza, hivi inawezekanaje kuwa na umbo dogo la aina hii? Ukweli ni kwamba inawezekana, lakini inahitaji kazi ya ziada kufikia kwenye lengo hilo… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya Kuondoa Makovu Mwilini

Makovu sio kidonda naomba hili uelewe, ila makovu ni alama ya majeraha ambayo yamebaki kwenye ngozi baada ya kupona majeraha.
Kuna baadhi ya watu husumbuliwa na shida ya kuwa na makovu sehemu mbalimbali ya mwili.
Hivyo kama wewe ni miongoni mwao maandishi haya yanakuhusu sana… endelea kusoma

a.gif Madhara ya Kuvaa viatu virefu

NI wazi kuwa viatu virefu huvutia sana vinapo kuwa vimevaliwa.Tulio wengi hasa mabinti au wanawake tunaokwenda na wakati hupenda kuvaa viatu virefu ilikuongeza muonekano wa umbile lako nikiwa na maana kuwa miguu huonekana yenye kuvutia zaidi unapo kuwa umevaa viatu virefu… endelea kusoma

[Msemo wa Leo] 👉Kinga ya magonjwa na madhara yote

[Jarida la Bure] 👉Kijitabu cha Kilimo Bora cha Hoho

[Hadithi Nzuri] 👉Kisa cha mama na mwanae namkwe wake

uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png

.

uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png
KADI-PONGEZI-MZAZI.JPG
elimu-sayansi-na-tekinolojia.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.