Matumizi ya Asali kwenye Urembo wa ngozi na Nywele

By, Melkisedeck Shine.

picha-kali.png

Matumizi ya Asali kwenye Urembo wa ngozi na Nywele

Asali hutumika kulainisha Ngozi

Asali ina asili ya kuvuta unyevu kutoka kwenye hewa na kuipa ngozi uwezo wa kuhifadhi unyevu hivyo ni faida kwa mtu mwenye ngozi kavu.

Jinsi ya kuandaa
Chukua asali mbichi kijiko kimoja cha chai kisha paka usoni, kaa nayo kwa dakika 15 hadi 20 kisha safisha uso wako.

Asali katika kusafisha ngozi, kutibu na kuzuia chunusi

Kutokana na uwezo wa asali katika kuua bacteria na kuvuta uchafu katika matundu ya ngozi asali itakusaidia kutatua tatizo la chunusi.

Jinsi ya Kuandaa
Chukua asali mbichi Kijiko kimoja cha chakula changanya na mafuta ya nazi vijiko viwili changanya mchanganyiko uwe mlaini kisha paka usoni huku ukisugua taratibu kwa kufanya kama viduara huku ukiepuka kufikisha machoni. ukimaliza kusugua uso na mchanganyiko wako osha uso wako.

Jinsi ya kuandaa kama kisafisha ngozi, exfoliator
Changanya kijiko kimoja asali na kijiko kimoja baking soda. tumia mchanganyiko huu kusugua ngozi yako. Asali inaongeza lishe na chembe chembe kuzuia madhara yanayotokana na sumu za hewani zinazozeesha ngozi. Baking soda inasaidia kusafisha matundu ya ngozi.

Asali inasaidia ngozi iliyoungua na jua kujirudi na kung'aa.

Jinsi ya kutumia asali katika nywele
Asali inatibu nywele kavu zilizopauka, na kulainisha ngozi kavu ya kichwa na kutibu muwasho kichwani.

Jinsi ya kufanya
Changanya kijiko kikubwa cha asali na maji ya uvuguvugu kisha paka kichwani Acha kwa muda wa saa 1 iwe kama conditioner kisha safisha nywele zako.

Unaweza kuchanganya asali kiasi cha kijiko kimoja mpk viwili katika maji vikombe vitano kisha safishia nywele zako taratibu, yaani yapitishe tu hayo maji kwenye nywele zako ambazo ni safi.

Tahadhari: Asali kwa kiasi kikubwa hupausha weusi wa nywele kutokana na Hydrogen Peroxide inayopatikana ndani ya asali.

Ni vema ukatumia asali mbichi kujihakikishia faida za asali katika mwili wako.
Iwapo unavutiwa na matumizi ya kitu cha asili katika urembo wako unaweza kuongeza kitu hicho katika kitu kingine unachotumia mfano katika steaming yako au scrub unayotumia.


elimu-sayansi-na-tekinolojia.png

Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Matumizi ya Asali kwenye Urembo wa ngozi na Nywele;

a.gif Jinsi ya Kutumia Papai na Asali kuondoa Madoa Usoni

KUMEKUWA na sababu mbalimbali zinazofanya watu kutokuwa na ngozi zisizokubalika.Mbali na hali ya hewa pia matumizi ya pombe na sigara hata matumizi ya cream kali ambazo zimekuwa zikitumiwa na watu bila kujua madhara yake kumechangia kwa kiasi kikubwa tatizo hilo… endelea kusoma

a.gif Njia za kutunza nywele zako

Suala la kutunza nywele za asili wengi hutamani japokuwa ukweli kwamba kuna changamoto kadhaa, lakini kwa mtu aliye makini anao uwezo wa kupata kilicho bora katika nyewle zake. Leo tunaangazia vitu vya kufanya ili kukuza na kutunza nywele za asili… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kutunza kucha kujiepusha na maradhi shambulizi ya Kucha

Mikono, viganja na vidole ni kati ya sehemu muhimu katika mwili wa msichana. Mikono hutumika kufanya shughuli nyingi za nyumbani, shuleni na sehemu mbalimbali katika maisha kuanzia kutandika kitanda, kupika, kufanya usafi, kuandika, kujiremba pamoja na majukumu mengine mengi… endelea kusoma

a.gif Tiba mbadala ya chunusi na vipele usoni

Kuna idadi kubwa ya watu wanao kabiliwa na tatizo la vipele vya usoni ( Chunusi ). Kuwa na chunusi ni jambo lenye karaha sana, kwani linakufanya upoteze mvuto wako wa asili na hivyo kukukosesha raha… endelea kusoma

[Kitendawili Kwako] 👉Ng'ombe wa miguu minane

[Chemsha Bongo Kwako] 👉Je, hii familia ina watoto wangapi?

[Kichekesho Kwako] 👉Haya ndiyo madhara ya kulala kanisani

afya-mapishi-na-lishe.png

a.gif Kampeni ya Kudumisha Umoja Wa Imani na Amani kwa watu wote

Kampeni hii ilianzishwa Rasmi Tarehe 15/05/2012 na Melkisedeck Leon Shine.
Lengo la kampeni Hii ni kudumisha Amani na Umoja bila kuangalia tofauti za imani zetu za kidini… endelea kusoma

a.gif Uvaaji wa Tai kulingana na Umbo lako

Kuna mambo mengi ya kufanya ili tuwe watu wa kuvutia kila wakati.Mpangilio wa mavazi hufanya mtu kuonekana maridadi. Kama wewe ni mvaaji wa tai unapovaa unazingatia mambo yapi? Na je unafunga tai yako kwa namna inayokubalika?.. endelea kusoma

a.gif Kampeni ya kutetea watoto yatima

Kampeni hii ilianzishwa na Melkisedeck Leon Shine mwaka 2018.
Lengo la kampeni hii ni kuhamasisha watu wote kusaidia kulea na kuwakuza watoto yatima kwa maendeleo bora ya kimwili, kiroho na kijamii kwa manufaa ya watoto wenyewe na kwa manufaa ya watu wote kwa sasa na kwa baadae.
Kampeni hii inaamini kuwa watoto yatima kama walivyo watoto wengine nao ni kama mali ambayo inawekezwa sasa kwa matumizi na maendeleo ya baadae. Japokuwa hawana (wazazi) watu/mtu rasmi wa kuwatunza haimaanishi kuwa hawawezi kuwa watu wa maana baadae… endelea kusoma

a.gif Kampeni ya kusaidia na kutetea Wazee

Kampeni hii ilianzishwa na Melkisedeck Leon Shine mwaka 2018.
Lengo la kampeni hii ni kuhamasisha watu wote kusaidia na kutetea wazee kwenye mahitaji yao ya kimwili, kiroho na kijamii hasa wale wasioweza kujitegemea baada ya kuzeeka.
Kampeni hii inaamini kuwa wazee ni hazina katika jamii na bado wanaweza kuwa na mchango kwa jamii kutokana na uzoefu wa maisha. Uzee ni sawa na kurudi utotoni hivyo Wazee wanahitaji faraja na msaada hasa pale wanapokuwa hawawezi kujitegemea tena wenyewe… endelea kusoma

[Msemo wa Leo] 👉Maneno na matendo

[Jarida la Bure] 👉Biblia ya Kiswahili- Agano la Kale

uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png

.

afya-mapishi-na-lishe.png
Slide3-mabestimliopotezana.PNG
elimu-sayansi-na-tekinolojia.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.