Mambo ya Kuzingatia ili uwe mrembo siku zote

By, Melkisedeck Shine.

Katika Jamii nyingi duniani, dhana ya urembo imekuwa na mitazamo tofauti kwa watu wengi. Kila mmoja anautafakari urembo kwa namna yake kulingana na malezi na tamaduni za mahali husika. Wako wanaoamini kuwa mrembo ni lazima awe na ngozi nyeupe, wengine hudhani kuwa ili kuonekana mrembo, lazima uwe na nywele ndefu, lakini pia wapo wanaodhani kwamba ili uwe mrembo ni lazima uwe na umbo namba nane na wapo wanaojua urembo ni kuwa mwembamba (kimbaumbau au Miss) au kuwa mrefu na wapo wanaoamini urembo ni kuwa mnene.

Hiyo yote ni mitazamo tu, lakini tafsiri halisi kutoka kwa wataalamu wa urembo ni kwamba; urembo ni hali ya kuwa na afya bora.

Je, Mpenzi msomaji ulikuwa unajua hili? Nakuomba Kabla hujafanya chochote kuhusu afya yako, unatakiwa kuamini kwamba wewe ni mrembo. Ikiwa utasimama katika hilo ni kweli utakuwa mrembo siku zote. Basi ili kubaki kuwa mrembo tujifunze haya machache leo ya kufanya:

1. SAFISHA NGOZI YAKO:

Hakikisha ngozi yako inakuwa safi muda wote. Unaweza kutumia njia mbalimbali kama vile kuondoa ngozi zilizokufa mara kwa mara. Kuondoa mafuta yaliyogandamana katika ngozi kwa kufanyia masaji ngozi yako ili kurahisisha mzunguko wa damu yako.
Ikiwa hili litafanyika kwa umakini ni wazi kuwa matatizo ya kuwa na chunusi au weusi katika ngozi yako havitakuwepo kwako.

2. SAFISHA NYWELE ZAKO:

Tumia bidhaa za nywele, ambazo zinaendana na nywele zako na hakikisha unazingatia mambo muhimu katika uboreshaji wa nywele zako.
Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na kutokutumia vifaa vinavyounguza vywele.

Epuka kuosha nywele kwa maji ya moto, pia kuchana nywele zikiwa na maji, kwani unaweza kusababisha kukatika kwa nywele zako.

3. USIPAKE VIPODOZI MARA KWA MARA:

Tumia vipodozi pale inapobidi, usipendelee kutumia vipodozi mara kwa mara kwani wakati mwingine matumizi ya mara kwa mara ya vipodozi, husababisha madhara katika ngozi yako, hasa unapotumia bila kufuata maelekezo ya wataalamu.

4. PATA USINGIZI WA KUTOSHA:

Hakikisha unapata usingizi wa kutosha kila siku. Kwa mujibu wa wataalamu, unatakiwa kulala si chini ya saa nane kila siku. Ikiwa utapata usingizi wa kutosha ni wazi kuwa macho yako yataonekana yenye nuru siku zote. Pia utazidi kuonekana kuwa mrembo zaidi.

5. FANYA MAZOEZI YA VIUNGO:

Hakikisha mazoezi yanakuwa sehemu ya maisha yako, hii itasaidia kukufanya uonekane siyo tu mrembo, bali pia mwenye kujiamini.

6. SAFISHA MENO YAKO:

Usafi wa meno pia ni miongoni mwa mambo ya kuzingatia unapoamua kuboresha urembo wako. Hakikisha unapiga mswaki walau mara mbili kwa siku kila siku au kila baada ya kula.

Haya yameorodheshwa na wataalamu mbalimbali kuwa ni mambo yanayochangia urembo wa asili na mvuto wa ngozi na mwili.SALAMU-USIKU-23ND.JPG

Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Mambo ya Kuzingatia ili uwe mrembo siku zote;

a.gif Jinsi ya kufanya nywele zako ziwe na mvuto na kuvutia zaidi

Mwanamke unywele hasa ukiwa nao, hii ni kauli upya ambayo Muungwana blog inakupa siku ya leo. Miongoni mwa maswali ambavyo huwa tunaulizwa na wasamoaji wetu ni pamoja ni kwa jinsi gani naweza kutengeneza nywele zangu ili ziwe za kuvutia?.. endelea kusoma

a.gif Uvaaji wa Tai kulingana na Umbo lako

Kuna mambo mengi ya kufanya ili tuwe watu wa kuvutia kila wakati.Mpangilio wa mavazi hufanya mtu kuonekana maridadi. Kama wewe ni mvaaji wa tai unapovaa unazingatia mambo yapi? Na je unafunga tai yako kwa namna inayokubalika?.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya Kuvaa hereni kwa Mpangilio kuongeza Mvuto wako

HERENI ni pambo linavoliwa masikioni na kwa kiasi kikubwa linachangia kuongeza mvuto na muonekano mzuri. Kuna aina nyingi za hereni katika tamaduni mbalimbali. Zipo ambazo hutengenezwa kwa kutumia vito vya thamani kama vile Dhahabu, Almasi, Shaba au Kopa… endelea kusoma

a.gif Faida na namna ya kutumia mafuta ya Zaituni Olive Oil kwenye nywele

1. Yanasaidia kufanya mzunguko wa damu kufanya kazi vizuri kwenye ngozi ya kichwa na kupenyeza hadi kwenye shina ya nywele kisha kuifanya nywele inayoota kuwa imara.. endelea kusoma

[Kitendawili Kwako] 👉Bibi yako walipomzika hajaoza

[Fumbo Kwako] 👉Je, hawa walizikwa wapi?

[Chemsha Bongo Kwako] 👉Je, hii familia ina watoto wangapi?

UJUMBE-MSAMAHA-35JHF32.JPG

a.gif Jinsi ya kung'arisha sura yako kwa kutumia Asali, Sukari, Maziwa, na Limao

Usafi wa uso ni moja ya mambo muhimu sana kwa mwanamke au mwanaume yeyote yule ambaye anapenda kuwa nadhifu na mwenye mvuto. Kumbuka “reception ndio kila kitu “. Unapokutana na mtu sura yako na mwonekano wa sura yako ndio kitu cha kwanza kinachomtambulisha kwamba wewe ni nani na upo kwenye hali gani… endelea kusoma

a.gif Kampeni ya usafi na Utunzaji wa mazingira

Kampeni hii ilianzishwa na Melkisedeck Leon Shine mwaka 2018.
Lengo la kampeni Hii ni kuhamasisha watu kusafisha na kutunza mazingira yao kwa manufaa yao ya sasa na kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Kampeni hii inaamini kuwa mazingira yakisafishwa na kutunzwa vizuri yanaweza kuwa msaada kijamii, kiuchumi na kiafya kwa kizazi hiki na kizazi kijacho… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya Kutumia Bmia kuondoa chunusi Usoni

Wiki hii kwenye urembo tutaongelea mboga aina ya bamia jinsi inavyotibu chunusi na kuziondoa moja kwa moja. Mbali na chunusi, pia husababisha ngozi kuteleza na kuwa nyororo… endelea kusoma

a.gif Namna ya uvaaji wa mavazi mbalimbali kwa wanaume

Wanaume wanajali mavazi yao pia, sio wanawake tu. Ila, mwanaume anabidi aelewe kwamba badala ya kufuata mitindo, kupendeza kwenye tukio lolote kuna nguo ambayo utaihitaji. Nguo hizi ni kama:.. endelea kusoma

[Msemo wa Leo] 👉Hakuna uwezo Bila fursa.

FURSA.PNG

Fursa Ya Kazi Na Ajira Yenye Malipo Mazuri

Au soma zaidi hapa

.

KADI-SALAMU-MCHANA-JION.JPG
KADI-MSAMAHA-MZAZI.JPG

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.