Madhara ya Kuvaa viatu virefu

By, Melkisedeck Shine.

elimu-sayansi-na-tekinolojia.png

Madhara ya Kuvaa viatu virefu

NI wazi kuwa viatu virefu huvutia sana vinapo kuwa vimevaliwa.Tulio wengi hasa mabinti au wanawake tunaokwenda na wakati hupenda kuvaa viatu virefu ilikuongeza muonekano wa umbile lako nikiwa na maana kuwa miguu huonekana yenye kuvutia zaidi unapo kuwa umevaa viatu virefu.

Kutokana na utafiti wa kitaalamu, mwanamke ana uwezo wa kutembea wastani wa hatua 10,000 kwa siku.Visigino virefu hufanya nguvu inayotumika kutembea hatua moja kuwa kubwa kuliko kawaida, huku vikikunyima raha ya kutembea kwa uhuru kiasi kwamba wengine hufikia hatua ya kuvua na kutembea peku.

Leo hii napenda kukujuza madhara ya uvaaji wa wa viatu virefu.Kwa kawaida, miguu ya binadamu hasa visigino, vimeumbwa ili kuuzuia uzito wa mwili juu ya ardhi.Uvaaji wa viatu virefu hufanya uzito wa mwili kubebwa na kisigino, hivyo uzito wa mwili kushindwa kuhimili uzito wote.

Matokeo yake husababisha misuli na mishipa ya miguu, kiuno, mgongo na shingo kufanya kazi kubwa ya kujaribu kusawazisha uzito.Kazi ambayo kwa kawaida hufanywa na visigino.Tatizo hilo hupelekea kiuno,Miguu na mgongo kuwa katika hatari ya matatizo ya kiafya pamoja na kuteguka na kuvunjika miguu.

Visigino virefu hubadili muundo wa mifupa ya miguu, hivyo hupelekea magoti na misuli ya mapaja kufanya kazi ya ziada ili kuupa mwili usawa.Kwa kuwa misuli inafanya kazi kubwa, uwezekano wa kupatwa na maumivu makali ya miguu na kushindwa kutembea katika siku za baadae huwa mkubwa zaidi. Visigino virefu husababisha maumivu ya visigino, damu kuvilia ndani ya miguu, mpangilio wa mifupa ya vidole kuvurugika, mishipa na misuli ya mapaja kuuma, neva za fahamu kufungana na kushindwa kufanya kazi yake.

Tatizo huendelea kwa vifundo vya miguu, magoti, na mifupa ya kwenye mapaja kushindwa kujivuta na kulegea na hivyo kusuguana wakati wa kutembea.

Jambo la kuzingatia kwa wale wanaopenda kuvaa viatu virefu,ni vema kama unapenda kuvaa viatu virefu hakikisha hutembei umbali mrefu kama una usafiri sio mbaya ukivaa viatu virefu,na kwa wale wanao kwenda ofisini jitahidi kuwa na viatu flati ndani ya mkoba wako ili unapokuwa umechoka unavua na kuvaa viatu vyako pia ukiwa ofisini waweza kuvua viatu virefu.

Mpenzi msomaji kama huwezi kutembelea viatu virefu nivema ukipitwa na wakati kuliko kujiabisha barabarani na kuonekana rimbukeni ikiwa wewe ni mjamzito epuka uvaaji wa viatu virefu.Usikose kujumuika nami katika safu hii ya urembo na mitindo.


USIKOSE HII๐Ÿ‘‰ Look for baseline survey expert?

Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Madhara ya Kuvaa viatu virefu;

a.gif Faida za kuogea maji ya Moto

Watu wengi hupendelea kutumia maji ya moto kuoga pale hali ya hewa inapobadilika na kuwa ya baridi au wakati mwingine mtu anaumwa hivyo anatumia maji ya moto.
Sehemu kama Dar es Salaam ni mara cheche utakuta wakazi wake wanaogea maji ya moto kutokana na hali ya joto katika jiji hilo… endelea kusoma

a.gif Madhara ya Kuvaa/ Kuweka Kope Za Bandia

Mapokeo ya urembo wa kisasa katika nchi zinazoendelea ni sehemu ya mchango wa urembo na mvuto tunaouona kwa baadhi ya wasichana na wanawake ambao kwa hakika unaleta hamasa ya kuangalia.
Hata hivyo, urembo huu huja na hatari zake ambazo wengi wanaweza kuzichukulia poa kwa kuwa hazitokei kwa haraka ama katika muda unaoweza kutolewa ushahidi kwa sasa… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kufanya ili uwe na umbo dogo la kuvutia

Unaweza kujiuliza, hivi inawezekanaje kuwa na umbo dogo la aina hii? Ukweli ni kwamba inawezekana, lakini inahitaji kazi ya ziada kufikia kwenye lengo hilo… endelea kusoma

a.gif Namna ya Kuifanya ngozi yako kuwa laini bila Madoa

Ili kufanya ngozi yako kuwa laini bila madoa zingatia mambo haya yafuatayo;.. endelea kusoma

a.gif Kampeni ya kutetea watoto

Kampeni hii ilianzishwa na Melkisedeck Leon Shine mwaka 2018.
Lengo la kampeni hii ni kuhamasisha watu wote kuwakuza watoto kwa maendeleo bora ya kimwili, kiroho na kijamii kwa manufaa ya watoto na kwa manufaa ya watu wote kwa sasa na kwa baadae.
Kampeni hii inaamini kuwa watoto ni kama mali ambayo inawekezwa sasa kwa matumizi na maendeleo ya baadae… endelea kusoma

a.gif Tiba mbadala ya chunusi na vipele usoni

Kuna idadi kubwa ya watu wanao kabiliwa na tatizo la vipele vya usoni ( Chunusi ). Kuwa na chunusi ni jambo lenye karaha sana, kwani linakufanya upoteze mvuto wako wa asili na hivyo kukukosesha raha… endelea kusoma

a.gif Mambo ya kuzingatia kama una ngozi yenye Mafuta

Ngozi yenye mafuta kwa kawaida huwa inang'ara, nene na yenye rangi iliyotitia. Mara nyingi ngozi yenye mafuta mengi sana huwa na chunusi nyingi na vipelepele na mara nyingine huwa na chunusi zenye vichwa vyeusi. Katika aina hizi za ngozi mafuta hutokana na tezi za sebaceous na kuzalisha mafuta zaidi ya kiwango kinachotakiwa. Mafuta hayo husambaa katika ngozi na kuifanya iwe na mafuta mafuta… endelea kusoma

a.gif Mambo ya msingi kwa mwanamke kuyajua unapojiremba

Kope nazo humpendezesha mwanamke kuna aina ya rangi za kupaka kwenye kope, lakini zinatofautiana. Ni vyema ukawasiliana na wataalamu wa mambo ya urembo kwa ushauri na siyo kukurupuka. Siyo umemuona fulani kapendeza na aina fulani ya rangi ya kwenye kope halafu na wewe ukakimbilia kupaka, utachekesha… endelea kusoma

afya-mapishi-na-lishe.png

.

uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png
KADI-MMISI-MZAZI.JPG
afya-mapishi-na-lishe.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.