Jinsi ya kusafisha na Kutunza Kucha zako

By, Melkisedeck Shine.

vichekesho-bomba-vya-siku.png

Jinsi ya kusafisha na Kutunza Kucha zako

Inashauriwa kwamba kabla ya kuchukuwa uamuzi wa kwenda kununua vifaa husika ambavyo utavitumia unapaswa kufahamu aina ya kucha ili uweze kununua vifaa vinavyoendana na kucha zako kwa lengo la kuzilinda badala ya kuvamia na kuziharibu.

Kwa kawaida kucha za mikononi na miguuni zinakabiliwa na mazingira magumu kutokana na majukumu ya kazi za kila siku hali inayochangia kuziweka katika mazingira magumu kiafya.

Mbali na kucha kukosa afya, pia kuharibu shepu yake ya awali kutokana na shughuli za kila siku katika maisha ya binadamu yeyote, hivyo ni vyema kuzikinga kucha zako na maradhi kwa kuzifanyia usafi kila siku au mara kadhaa kwa wiki ili kuzilinda zaidi.

Ili kuweza kugundua aina ya kucha zako katika kuzipangilia wakati wa kuzifanyia usafi, unapaswa kuwa makini wakati unachagua rangi ya kupaka, kuangalia muonekano wa kucha zako zilivyo ili uweze kupangalia rangi ziweze kuwa na mvuto zaidi.

Ni vyema kwa mtu anayejali afya ya kucha zake kuchukua muda mwingi kufuatilia kucha zake na kuelekeza nguvu zake katika kuhakikisha zinakuwa katika matunzo mazuri na kujitahidi kubuni mtindo ambao unaweza kuwa tofauti na wengine ambao wanapenda kuzifanya kawaida.

Hata hivyo katika kutunza kucha ziwe nzuri, vyakula ambavyo ni mlo kamili ni muhimu sana, vinginevyo utajikuta ukishauriwa na wataalamu kutumia vitamini mbalimbali kama vile vitamini A, vitamini C, Culcium, Folic Asidi, Protini na Vitamini B12.

JINSI YA KUSAFISHA KUCHA.

Wekeza vifaa vizuri vya kisasa vya kutunzia kucha.
Tumia brush ya kucha kwa kusugua chini ya kucha na kuutoa uchafu na kufikia sehemu ngumu ambapo uchafu unajilundika. Unaweza tumia mswaki ukiwa huna vifaa vya kisasa.
Tumia maji moto na sabuni ya kunawia mikono.
Anza kwa kusugua chini kabisa kwa kushikilia brush chini na sugua kuanzia nyuma kuja mbele pole pole, kisha juu ya kucha fanya hivyo kwa kuzunguka.

Toa rangi kwa kuloweka pamba kwenye polish remover na usugue kwa vidole vyenye hinna huna haja ya kuitoa. kwa vidole vya afya na nguvu vipumzishe kwa kutumia polish kila baada ya wiki kadhaa.

Loweka kucha na maji kwenye bakuli,au sinki,au kifaa cha uwezo wako hata dishi poa,kwa maji ya moto ya uvuguvugu na pitisha sabuni ya kunawia mikono.Na ni kucha tu usiloweke mkono mzima,kwa dakika tatu,sabuni kwenye maji hufanya mikono kuwa mikavu .

Suuza kwa maji ya bomba ya uvuguvugu,au yalokua kwenye chombo yaani jimwagie,kisha zifute na taulo laini.

Kisha tumia kikatio kucha kukata maana zitakua laini,au kifaa cha kuzipunguza kuweka sawa kama hauzikati.


Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Jinsi ya kusafisha na Kutunza Kucha zako;

a.gif Namna ya kuvaa vizuri kwa mwanamme upendeze na kuwa mtanashati

Nimeona leo nitoe darasa kidogo kuhusu mavazi sababu na mimi ni kipaumbele changu katika maisha… endelea kusoma

a.gif Mambo ya Msingi kujua kuhusu uvaaji wa Tai

Kuna mambo mengi ya kufanya ili tuwe watu wa kuvutia kila wakati.Mpangilio wa mavazi hufanya mtu kuonekana maridadi… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kuvaa viatu mbalimbali inavyotakiwa na ili upendeze

Viatu ni kinga kwa ajili ya kuhifadhi miguu. Vile vile viatu ni vazi ambalo linaongeza urembo na nakshi kwa mvaaji. Viatu vipo vya aina mbalimbali na vinavaliwa kulingana na mahali na mavazi yanayoambatana navyo. Tuangalie baadhi ya aina za viatu na wapi hasa na vipi vikitumika vinapendeza zaidi… endelea kusoma

a.gif Madhara ya kuchora tattoo mwilini

Tattoo ni nini?
Hii ni uwekaji wa wino kwenye ngozi ya ndani kitaalamu kama dermis kubadilisha rangi kabisa maisha yako yote au kwa muda tu, inateemea na uwekaji..
Kwa dunia ya sasa kujichora tatoo ni kama fasheni fulani kwenye jamii, ukienda kuchora tattoo kuna uwezekano mkubwa sana isitoke maisha yako yote hivyo kwa usalama wako ni vizuri ukamuona mtaalamu wa tattoo ambaye ni maarufu na ana sifa kubwa katika shughuli hizo, anaweza kua ana gharama kubwa lakini binafsi itakusaidia.kwa sasa nchi ya marekani inaongoza kwa kua na watu wengi wenye tattoo duniani… endelea kusoma

a.gif Mavazi ya Ofisini kwa Wadada

Wengi wetu tunashindwa kutofautisha mavazi ya sehemu husika mfano Ofisini, michezoni, na yale ya usiku na sehemu nyinginezo leo nitagusia vazi la ofisini kwa akina dada… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kutumia maziwa ya mtindi kufanya ngozi yako kuwa laini na soft

Ulisha wahi kukaa ukajiuliza mbona kuna baadhi ya watu wana ngozi nzuri laini na soft? lakini kwako ni tofauti?.. endelea kusoma

a.gif Namna nzuri ya kutunza Hips na Makalio

KUNA kitu ambacho wengi wetu huwa hawakifikirii nacho ni makalio. Makalio yetu ndiyo yanatoa shepu fulani kwa mwanamke katika vivazi na ukiyaachia ovyo yanaweza kukuletea mushkeli na kama ukiyatengeneza kama yale makalio yanayosifiwa sana na watu wa Televisheni ya Jeniffer Lopez hayawezi kufua dafu… endelea kusoma

a.gif Chanzo, dalili matibabu ya chunusi

Chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao hujit-okeza kama viuvimbe/vipele vidogo vidogo hasa sehemu za uso,kifuani na hata mgongoni.Vipele hivi hutokea wakati vishimo vya kupitisha jasho katika ngozi vinapozibwa kwa mafuta au seli za ngozi zilizokufa au wadudu yaani Bacteria… endelea kusoma

picha-kali.png

.

vichekesho-bomba-vya-siku.png
tafuta-rafiki.gif
uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.