Jinsi ya kuondoa kitambi

By, Melkisedeck Shine.

elimu-sayansi-na-tekinolojia.png

Jinsi ya kuondoa kitambi

Hapo zamani kidogo tuliona na tulishuhudia watu wakisema ya kwamba mwanaume ambaye ana kitambi ndiye ambaye mwenye fedha, hiyo ni imani ambayo ilijengeka katika fikra na mitazamo yetu. Lakini katika karne hii mambo yamebadilika baada ya kuona baadhi ya madaktari wakieleza kwa kina ya kwamba kuwepo matumbo makubwa tanatokana na uwepo wa mafuta mengi katika kuta za tumbo.

Na mafuta hayo pindi ambao yanazidi huwa na athari sana kiafya, athari hizo za kiafya hupelekea mtu kuweza kupata magonjwa mbalimbali kama vile shinikizo la damu na magonjwa mengine mbalimbali.

Hivyo ili kuepukana na athari hizo zitokanazo na kitambi nakusihi ufanye yafuatayo:

2. Chakula

Huu ni msingi mwingine muhimu sana katika harakati za kupunguza unene na tumbo, kwa kifupi unahitaji kuzingatia yafuatayo:

  1. Kula mboga za majani kwa wingi kwani husaidia sana kiafya.
  2. Kunywa maji mengi sana
  3. Weka chakula cha kukutia hamu mbali na nyumba yako
  4. Kula vyakula ambavyo vitatumika kwa kiwango kikubwa katika kujenga mwili wako ila epuka kula vyakula vyenye mafuta kwa wingi.

2. Mazoezi ya viungo husaidia kupunguza tumbo.

Kwa kiwango kikubwa Unaweza kufanya mazoezi ya aina nyingi ili kupunguza tumbo. Mazoezi yoyote ya nguvu yatapunguza mafuta ya mwili wako pamoja na mafuta ya ndani (visceral fat).
Mazoezi ambayo nayazungumzia ni mazoezi ambayo yanasaidia kukata tumbo kwa kiwango cha juu sana. Mazoezi haya kwa karne hii ya teknolojia yapo wazi katika video mbalimbali.

Hivyo jaribu kutafuta video mbalimbali ambazo zitakusaidia kwa kiwango kikubwa katika kukata tumbo.

3. Hakikisha unapata usingizi Wlwa kutosha kwa siku.

Kupata usingizi kwa muda mzuri kumeonyesha kuwa na mchango katika kudhibiti kiwango cha mafuta katika mwili wa binadamu. Katika utafiti mmoja, watu waliopata usingizi kwa saa 5 hadi 7 kwa siku katika kipindi cha miaka 5, walionyesha kuwa na mafuta mwilini kidogo zaidi ukilinganisha na wale waliopata usingizi kwa pungufu ya saa 5 kwa siku.

Hivyo hakikisha unatenga muda wa kupumzika hasa pale unapokuwa una usingizi.


Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Jinsi ya kuondoa kitambi;

a.gif Jinsi ya kung'arisha sura yako kwa kutumia Asali, Sukari, Maziwa, na Limao

Usafi wa uso ni moja ya mambo muhimu sana kwa mwanamke au mwanaume yeyote yule ambaye anapenda kuwa nadhifu na mwenye mvuto. Kumbuka โ€œreception ndio kila kitu โ€œ. Unapokutana na mtu sura yako na mwonekano wa sura yako ndio kitu cha kwanza kinachomtambulisha kwamba wewe ni nani na upo kwenye hali gani… endelea kusoma

a.gif Mavazi ya Ofisini kwa Wadada

Wengi wetu tunashindwa kutofautisha mavazi ya sehemu husika mfano Ofisini, michezoni, na yale ya usiku na sehemu nyinginezo leo nitagusia vazi la ofisini kwa akina dada… endelea kusoma

a.gif Uvaaji wa Tai na Maana yake

Wachambuzi wa mambo ya saikolojia wanasema kwamba kwa kuchukua tai na kulivaa ile rangi ndiyo itakayoweza kupeleka ujumbe wa wewe unataka nini au unataka watu wakutambue kwa namna gani.
Wakati Joshua Blue, Makamu mkuu wa shule ya Kennedy mjini Hong Kong, anapoendesha baraza la wanafunzi anavaa tai lenye rangi ya light violet ili kumpa mamlaka… endelea kusoma

a.gif Vyakula vya Kukuza nywele na kuzifanya ziwe na Afya

Kuwa na nywele zenye afya nzuri ni muhimu kwa wote bila kujali jinsi, hali hii husababisha wengi kutumia madawa ya aina mbalimbali ya kuhakikisha nywele zao zinastawi na kuwa na muonekano mzuri.
Kwa bahati mbaya, wengi waliotumia madawa yanayotengenezwa kwa kemikali hujikuta katika wakati mgumu siku za usoni wakikabiliwa na matatizo ya nywele kukatika na hata kupata madhara katika ngozi ya kichwa… endelea kusoma

[Picha Nzuri] ๐Ÿ‘‰Huyu nyani ka mtu vile

[Msemo wa Leo] ๐Ÿ‘‰Kushindwa jambo kubwa

[Jarida la Bure] ๐Ÿ‘‰Biblia ya Kiswahili- Agano la Kale

[Hadithi Nzuri] ๐Ÿ‘‰Stori inayogusa!!

a.gif Jinsi ya kutunza kucha kujiepusha na maradhi shambulizi ya Kucha

Mikono, viganja na vidole ni kati ya sehemu muhimu katika mwili wa msichana. Mikono hutumika kufanya shughuli nyingi za nyumbani, shuleni na sehemu mbalimbali katika maisha kuanzia kutandika kitanda, kupika, kufanya usafi, kuandika, kujiremba pamoja na majukumu mengine mengi… endelea kusoma

a.gif Namna nzuri ya kuhudumia nywele zako za asili kirahisi

Kwa wale ambao tuna nywele asilia (natural hair), tayari tunafahamu changamoto kadhaa tunazokumbana nazo. Kwa wale mnaofikiria kuanza kuwa na nywele asilia, karibuni sana tuendelee kujuzana namna ya kutunza nywele zetu kama tulivyopewa na Mungu… endelea kusoma

a.gif Madhara ya kuchora tattoo mwilini

Tattoo ni nini?
Hii ni uwekaji wa wino kwenye ngozi ya ndani kitaalamu kama dermis kubadilisha rangi kabisa maisha yako yote au kwa muda tu, inateemea na uwekaji..
Kwa dunia ya sasa kujichora tatoo ni kama fasheni fulani kwenye jamii, ukienda kuchora tattoo kuna uwezekano mkubwa sana isitoke maisha yako yote hivyo kwa usalama wako ni vizuri ukamuona mtaalamu wa tattoo ambaye ni maarufu na ana sifa kubwa katika shughuli hizo, anaweza kua ana gharama kubwa lakini binafsi itakusaidia.kwa sasa nchi ya marekani inaongoza kwa kua na watu wengi wenye tattoo duniani… endelea kusoma

a.gif Faida za kuoga maji ya Baridi

Watu wengi hupenda kuogea maji ya moto, hii ni kutokana na kuogopa baridi au sababu za kimazoea tu. Ingawa mara nyingi umekuwa ukisisitiziwa kuwa maji moto yana manufaa mengi, lakini hata maji ya baridi nayo yana manufaa yake… endelea kusoma

picha-kali.png

.

vichekesho-bomba-vya-siku.png
Slide3-mliopoteana.GIF
afya-mapishi-na-lishe.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.