Siri ya mafanikio katika maisha: Usiangalie watu

Waziri mkuu wa zamani wa uingereza Sir Wiston Churchill aliwahi kusema
"huwezi kufika mwisho wa safari yako kama utakuwa unasimama kila mahali kumtupia jiwe kila mbwa anaye kubwekea"

โ–ชKauli hii ina maana kwamba kama una picha kichwani ya kule unakokwenda au umekusudia kufikia na kutimiza lengo fulani katika maisha, tambua kwamba unapokuwa njiani kutimiza lengo lako lazima utakutana na watu
โ–ช _watakaokuvunja moyo_ ,
โ–ช _watakaokusema vibaya_ ,
โ–ช _watakaokukatisha tamaa._
โ–ช _watakaokuchukia kwa sababu ya bidii yako_.

โ–ชMara nyingi sana unaweza kushawishika kutaka kumjibu kila mtu anayekusema vibaya , kukuchukia au kukukatisha tamaa (hapo ndo unakuwa sawa na yule anayesimama kumtupia jiwe kila mbwa anayebweka).

โ–ชWakati mwingine utashawishika kutaka kuona kila mtu anakukubali na kukuunga mkono, kitu ambacho hakiwezekani.
โ–ชmtu mmoja alisema "siri kubwa ya kufeli katika maisha ni kujaribu kumpendeza kila mtu".

โ–ชTambua kwambwa huwezi kumpendeza kila mtu hata ufanye jambo zuri kiasi gani "hata ukichezea maji utaambiwa unatimua vumbi", yaani ilimradi tu wakupinge.

โ–ชItazame hatima yako.

*MWAMBA*

Usipitwe na Nafasi za kazi kwa leo

<<Bofya HAPA kujua zaidi>>

.

KADI-PONGEZI-MZAZI.JPG
UJUMBE-WA-ZA-JIONI-KWA-NDUGU.JPG