Kichekesho%20Kipya Usikose πŸ“•Kitabu cha Vichekesho Vikuu Vikali 300+βœ” Kina kurasa 270 zenye pichaπŸ“· na vichekeshπŸ˜‚ zaidi ya 300πŸ’¨
πŸ‘‰Bofya hapa KuchukuaKizuri

.

πŸ‘‰ Mambo ya kufanya mwezi Disembaβœ…

✍🏽MAMBO YA KUFANYA MWEZI HUU WA DECEMBA

Habari: Hongera kuingia mwezi mpya!
Ikiwa leo ni tarehe *1/12/2016* huwezi amini kuwa hakuna tarehe 1 nyingine tutakayoiona ya mwaka huu hivyo sichelei kusema kuwa mwaka umeisha .Lakini mwaka unaishaje??? pengine hili ndilo swali gumu na la muhimu la kujiuliza .Je, Mwaka unaisha ukiwa umefanya nini cha kujipongeza??? .Je mwaka unakaribia kuisha maarifa yako yakiwa yameongozeka kwa kiasi gani???.Haya ni maswali muhimu sana unavyooanza kufikiria juu ya sherehe za mwisho wa mwaka.

Watu waliopiga hatua katika fikra (waliofanikiwa) huu ndio mwezi wao wa kurudi kwenye malengo waliyokuwa wameweka na kuona ni kwa njinsi gani wametembea na mambo waliyokuwa wameyapanga mwaka uliopita .

Leo nataka nikuekeze mambo muhimu ya kufanya mwezi huu pamoja na kuwa unawaza sikukuu na kusafiri kwenda kwenu .Mambo haya unaweza kuwa hujawahi kufanya lakini ni muhimu sana ukafanya mwaka huu ili mwakani tuone mabadiliko .Mambo hayo ni pamoja na ;

*1.Fanya Tathimini(Evaluation)*

Tathimini ni kipimo kinachoonesha kushindwa kwako na kufanikiwa kwako .Mwezi huu ni mwezi wa kukaa chini na kurejea kwenye malengo na mikakati uliyokuwa umejiwekea na kuona ni kwa jinsi gani umefanikiwa .Ainisha mambo uliyofanikiwa na ambayo hujafanikiwa .Kwa yale uliyofanikiwa jipongeze kwa kufanikiwa kwa yale ambayo hujafanikiwa jiulize kwanini hayajafanikiwa ili yakupe mbinu na hatua mpya 2017.

Andika kwa mtindo huu;

SEHEMU A:MAMBO NILIYOFANIKIWA 2016

-Mwaka 2016 nilifanikiwa kuwapata marafiki wazuri wanaounga mkono maono yangu
-Mwaka 2016 nilifanikiwa kuanzisha biashara ya genge
-Mwaka 2016 nilifanikiwa kusoma vitabu viwili

*Jitihidi sana kujipongeza kwa yale uliyofanikiwa na hii ni tabia ya watu waliofanikiwa .Usione umefanya madogo lahasha.*

SEHEMU B:MAMBO AMBAYO SIKUFANIKIWA 2016

-Sikufanikiwa kuhudhuria semina hata moja ya ujasiriamali
-Sikufanikiwa kuboresha ofisi

*Kwa yale ambayo hukufanikiwa jiulize kwanini hukufanikisha utagundua wewe ndiye sababu kubwa ya kutoyafanikisha .*

*2.Anza kuandaa malengo ya mwaka 2017(GOAL SETTING)*

_Pasipo maono, watu huacha kujizuia_
~(Biblia)

Ndiyo bila malengo hutafika na utafanya kila kitu bila mpangilio .Huu ndio mwezi kwako ambao unapaswa kuandaa malengo ya mwaka 2017 haijalishi hukuwahi kuweka malengo toka unazaliwa .Najua malengo yako yalikuwa yanakaa kichwani mwaka huu amua kuandika kwenye notebook Nzuri .Andika kwa ujasiri mkubwa sana .Malengo yako yafuate kanuni za malengo(yapimike,yawe na ukomo,yawe mahususi na yakufikika ).

Andika kwa mfano huu;

-Kufikia Mei 2017 nitakuwa nimefuga kuku watatu hata kama nyumba yangu ni ndogo .

-Kufikia Agosti 2017 nitakuwa nimehudhuria semina 2 za ujasiriamali

Ukiandika kwa mfumo huo itakusaidia kuyafikia malengo yako maana yamefuata kanuni za malengo.

*3.Andaa Bajeti ya mwaka 2017(Budgeting)*

Hii ni sehemu ambayo inaleta shida sana .Na hii ni kwa sababu hata wazazi wetu wametulea bila kutufundisha bajeti.Masomo ya darasani wengi hatufundishwi kuishi kwa bajeti .Lakini Tusilaumu sana kutofundishwa maana lawama ni tabia ya kimaskini tuamue mwakani 2017 kuishi na kutembea na bajeti

Mara nyingi tukiulizwa hela zetu zinaenda wapi huwa hatuna majibu sahihi .Hii ni kwasababu hatuna bajeti .Kwanini bajeti??? .Bajeti hutusaidia kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na yaliyo nje ya bajeti .Bila bajeti sehemu ya kutembea kwa mguu utapanda bodaboda .Bila bajeti utanunua simu ya laki saba wakati unasema huna mtaji wa laki sita.Bajeti itaamua uchangie harusi na kitchen party ngapi kwa mwaka.

Ndiyo lazima tubadilike hata mimi nimeamua hivyo mwaka 2017.Kama una familia kaa na mke wako tengeneza bajeti ya mwaka.Kuna vitu vinaweza kujitokeza njiani na hivyo kumbuka kuweka dharura .

Bajeti itatoa picha ya nini kinahitajika 2017 na unahitaji kuwekeza nguvu kiasi gani za kwenda na bajeti hiyo.

πŸ™‰πŸ™‰πŸ™‰Usisahau kushare posti hii kuhusu; Mambo ya kufanya mwezi Disemba.πŸ’―βœ” Share facebook, twitter n.k bila kusahau WhatsApp, share wengine nao wafaidike!πŸ‘

Usisite kuniandikia maoni, mapendekezo au maswali kuhusu Mambo ya kufanya mwezi Disemba hapa

Jina
Mahali ulipo
Email
Itatumika kukujibu
Ujumbe wako
Usikubali kupitwa na πŸ“•Kitabu cha Mbinu za Kilimo Bora Cha MbogaπŸŒΏπŸ…. Kina kurasa 100 na utaalamu wa mazao zaidi ya 10. πŸ‘‰Bofya hapa KuchukuaπŸ‘ˆ

🐼 Endelea kusoma kuhusu;-πŸ™‰

.

Kichekesho%20Kipya Usikose Jarida la Picha Kali Lina picha Nzuri za kufurahisha πŸ‘‰Bofya hapa Kuchukua.Kizuri

.

Kichekesho%20Kipya Usikose πŸ“•Kitabu cha Mbinu za Kilimo Bora Cha MbogaπŸŒΏπŸ… Kina kurasa 100 na utaalamu wa mazao zaidi ya 10πŸ‘‰Bofya hapa Kuchukua.Kizuri

.

Kichekesho%20Kipya Usikose Jarida la Kilimo Bora cha Hoho Kilimo cha hoho kimeelezewa πŸ‘‰Bofya hapa Kuchukua.Kizuri

.

.

.

matikitijj.jpg
Kichekesho%20Kipya Usikose Jarida la Kilimo Bora cha Matikiti Linafundisha ulimaji wa matikiti .
πŸ‘‰Bofya hapa KuchukuaKizuri

.

vichekesho.jpg
Kichekesho%20Kipya Usikose πŸ“•Kitabu cha Vichekesho Vikuu Vikali 300+βœ” Kina kurasa 270 zenye pichaπŸ“· na vichekeshπŸ˜‚ zaidi ya 300πŸ’¨.
πŸ‘‰Bofya hapa KuchukuaKizuri

.

.

.

Melkisedeck

Habari msomaji wangu…?
Jina langu ni Melkisedeck Leon Shine Mwendeshaji wa blog hii.

Karibu Katika Blog yangu ya AckySHINE mahali pa kusoma makala kuhusu mada mbalimbali, vichekesho, picha, pamoja na videos

Unahakikishiwa kupata kitu kipya utakachopenda kila unapotembelea blog hii

Usisite kuniandikia maoni,mapendekezo au maswali hapa

Jina
Mahali ulipo
Email
Itatumika kukujibu
Ujumbe wako

Karibu tena kila wakati.

Nakutakia Pasaka njema

KUHUSU BLOG HII | MAWASILIANO | ABOUT AUTHOR | LEGAL GUIDELINES