Mambo 13 katika pesa ambayo unapaswa kuzingatia

By, Melkisedeck Shine.

1. Usikope pesa ya riba ili uanzishe biashara.
Usitegemee pesa ya mkopo kuianzishia biashara, upate faida kisha uirudishe pesa ya mkopo na riba yake.

2. Usitumie pesa ambayo bado haipo mikononi mwako.
Wala usije ukamuahidi mtu kumpa pesa ambayo umeahidiwa mahali fulani.

Kama kuna mtu kakwambia, Flan njoo kesho nikulipe deni lako- Basi ww usiende kukopa vitu dukani au kumuahidi mtu mwingine kumpa pesa ambayo na ww umeahidiwa

3. Kama unataka kuhifadhi/kutunza pesa, kila unapopata pesa usianze kuitumia kwanza kisha ukategemea kutunza kiasi kitakachosalia.

Hivyo basi, ukipata tu pesa, weka pembeni kiasi unachodhani kinafaa kutunzwa/kuhifadhiwa kisha tumia kiasi kilichobaki.

4. Ukipata nafasi ya kuonana na mtu tajiri, kamwe usiombe pesa.
Omba maarifa ya kutengeneza pesa kama yeye, tena kwa mtaji mdogo.

Maarifa ndio mtaji wa kwanza.
Unaweza kupewa/kusaidiwa pesa iwapo una mawazo mazuri ya kuzalisha pesa. Baadhi husema, "Omba ndoano, usiombe samaki"

5. Usitunze mbegu badala ya kuipanda.
Watu wengi hufurahia pesa wanayolipwa/kuipata kisha wanaiweka bank au nyumbani bila kuiwekeza.
Wekeza pesa ili uzalishe zaidi. Usiogope kuingia hasara, kila aliefanikiwa alipoteza kwanza kabla hajafanikiwa.Wengi walipoteza muda, pesa, afya na hata matumaini ya kufanikiwa, ila kwa uthubutu wao, mwisho wa siku walifanikiwa”

6. Kamwe usimkopeshe mtu pesa ambayo unahisi hatorudisha.

Unapomkopesha mtu huyo pesa, jiridhishe mwenyewe moyoni kuwa kama hatoweza kulipa basi deni lake-halitoathiri urafiki wenu. Ukihisi kwamba kushindwa kwake kulipa kunaweza kuathiri urafiki wenu, basi mshauri aende bank akakope”

7. Usikubali kumdamini mtu ambae huna uhakika kuwa atalipa kile unachomdhamini.
Kumbuka- dhamana maana yake utawajibika iwapo atashindwa kulipa

8. Epuka kutembea na pesa nyingi ambazo hata huna matumizi nazo wakati huo.
Unaweza kujikuta unafanya matumizi ambayo hayakuwa kwenye ratiba sababu ya ushawishi wa pesa ya mfukoni.
Ili kuepuka haya, tembea na pesa uliyopanga kuitumia katika safari yako.
Pesa nyingine itunze mahali pengine palipo salama”

9. Epuka kutunza pesa mahali pasipo sahihi.
Maeneo kama kwenye soksi, sidiria, chini ya mto wa kulalia, chini ya begi, kwenye kopo au hata kwenye begi la safari, si maeneo salama.
~Ni rahisi kusahau, kuibiwa au kupoteza pesa zako.

Ni bora ukatunza pesa kieletroniki; yaani bank au kwenye simu au kwenye pochi yenye kamba ngumu ya kuivaa mabegani au wallet ambayo inatosha kwenye mifuko imara na yenye vifungo kwenye nguo zako hasa uwapo safarini.

10. Usitumie pesa kwa kitu ambacho hakikuwa kwenye ratiba yako.

Jiulize kwanza kabla hujanunua,
"Bila kitu hiki, maisha yataenda au lah?”
Ukiona maisha yataenda bila kitu hicho, acha kukinunua. Tabasamu kisha ondoka.

12. Matumizi yako ya pesa yasizidi pato lako.

Unaweza kuwa una ndoto kubwa/matumizi makubwa ya pesa kuzidi pato lako.

Unapaswa kuwa bahili katika matumizi yako. Cheza na pato lako.
Fanya matumizi makubwa pale tu pato lako litakapoongezeka. Hii itakuepushia kushindwa kufanya baadhi ya mambo ya msingi na kisha ukajikuta unaishia kwenye madeni makubwa.
13. Una ndoto kubwa hapo baadae; labda kujenga nyumba, kununua gari, kununua kiwanja, simu nzuri hata pikipiki.

Usikurupuke, ukanunua kitu cha ndoto yako sasa eti tu sababu umekipata kwa bei ya punguzo.

Usichanganye kati ya mahitaji ya baadae na ya sasa.

Pesa unayotumia kutimizia ndoto sasa itumie kwa mahitaji ya sasa. Ndoto ibaki kuwa ndoto.

Hii itakuepushia kuingia katika madeni au kuishi kwa shida sababu ya tamaa.
Jipange taratibu kutimiza ndoto yako.

*Mwendo*nn.gif

Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Mambo 13 katika pesa ambayo unapaswa kuzingatia;

a.gif Jifunze kupitia mfano huu Ili uishi kwa amani na watu

Siku moja nilichukua taxi aina ya UBER nikiwa naelekea uwanja wa Ndege Mwl. Nyerere Dereva huku akiendesha kwa ustaarabu sana mara ghafla pasipo kutegemea gari ya taka ikajitokeza mbele yetu kutokea nje ya barabara. Dereva wa taxi kwa umakini na neema ya Mungu akalikwepa gari hilo na ilikuwa kidogo agonge gari zingine mbele yetu… endelea kusoma

a.gif Siri ya mafanikio katika maisha: Usiangalie watu

Waziri mkuu wa zamani wa uingereza Sir Wiston Churchill aliwahi kusema
"huwezi kufika mwisho wa safari yako kama utakuwa unasimama kila mahali kumtupia jiwe kila mbwa anaye kubwekea".. endelea kusoma

[Kitendawili Kwako] 👉Mchana Wablue usiku Mweusi

KUMSHUKURU-MPENZI-4559KJ438.JPG

a.gif Dunia haijali mazuri yako ila ubaya wako, jiamini songa mbele

Siku moja mwalimu wa shule aliandika ubaoni kama ifuatavyo:
9×1=7
9×2=18
9×3=27
9×4=36
9×5=45
9×6=54
9×7=63
9×8=72
9×9=81
9×10=90
Alipo maliza kuandika tu, akaona wanafunzi wote walikua wanamcheka, kwasababu alikua amekosea swali la kwanza… endelea kusoma

a.gif Sababu inayopelekea kushindwa kuishi maisha ya ndoto zako

1. Hauko Tayari kuthubutu na kujiunga
2. Kutokujiamini
3. Kutopata sehemu sahihi ya kupata ushauri
4. Kutokuwa na sababu za msingi au malengo ya msingi ya kupigania ndoto zetu
5. Kukaa katika shauli la wasio haki na barazani pa wenye mizaha.. endelea kusoma

a.gif Hii ndio sababu kwa nini huwezi kufanikiwa kibiashara

HUWEZI KUFANIKIWA KIBIASHARA KAMA UNAPENDA KUJIHURUMIA HURUMIA!
💥Mama mmoja Mzungu alitembelea mlima Kilimanjaro miaka iliyopita. Alikuwa amepanga kupanda mlima Kilimanjaro mpaka kileleni, yaani Kibo na Mawenzi, ili hatimaye apewe cheti cha kupanda mlima mrefu Afrika… endelea kusoma

a.gif Kwa nini watu wanapenda pesa

Watu wengi tunapenda sana Pesa lakini hatuko tayari kuzifanyia Pesa kazi nikiwa na maana kutumia njia sahihi kuzipata na tunapozipata hatuna Akili ya kuweza kuwa nazo muda mrefu zisiondoke.
Kama tujuavyo katika maisha yetu haya Pesa ndio kila kitu,tunahitaji Pesa ili tuweze kufanya mambo mengi mazuri na makubwa.Kitu kinachotukwamisha hatujui tufanye nini ili tuweze kuzipata hizi Pesa na tunapozipata tunakosea tena cha kuzifanyia ili zisipotee tena au zisiishe… endelea kusoma

[Msemo wa Leo] 👉Umakini

[Jarida la Bure] 👉Mapishi ya wali wa karoti na nyama

[Hadithi Nzuri] 👉Kisa cha kusisimua cha mama mjane

FURSA.PNG

Fursa Ya Kazi Na Ajira Yenye Malipo Mazuri

Au soma zaidi hapa

.

SALAMU-JIONI98HBS.JPG
MLO-MWEMA-KWA-NDUGU-UJUMBE.JPG

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.