JITAMBUE: Kipi hauna kati ya pesa na muda?

By, Melkisedeck Shine.

Soma kidogo hapa.. Kuna watu wa aina NNE tunapoongelea pesa na muda.

1. WANA MUDA MWINGI ILA HAWANA PESA

Watu ambao hawana pesa ila wana muda wa bwerere. Hawajui thamani ya muda. Hawa ndo wale ambao hawajui cha kufanya. Anaamka mpaka analala usiku hana specific timetable. Unaweza kumkuta anaenda dukani ukamwambia nisindikize saluni na akakubali. Yupo yupo tu. Unaweza kuta ameingia Facebook hajui hata kwa mini. Basi tu kwa sababu ana bando. Akiperuzi akaona mahali wanaongelea mpira yumo. Akiscroll post za chini akakuta kuna mtu kapost kuhusu UKAWA yumo. Akikuta kuna mtu kapost mtu ana uvimbe mkuuubwa watu wameambiwa wacomment AMEN na yeye huyo anacomment AMEN. Akikuta watu wanaongelea TRUMP na yeye anaingia kucomment. Kundi hili ni kundi lenye watu wengi mno. Watu wa aina hii kufanikiwa ni bahati nasibu. Labda kwa bahati tu akutane na post nzuri kama hii na post zingine nzuri huenda ikamsaidia. Otherwise hawa ndo hawaelewi maisha yanaenda wapi maana hawana kitu fulani specific wanachofanya. Wakisikia tu kuna kitu kiko kama dili hivi wanaenda. Wakikuta kumbe kinahitaji bidii na kujituma wanaondoka. Wanataka maisha mazuri yaje tu yenyewe.

2. WANA PESA ILA HAWANA MUDA

Hili ni kundi la watu wenye shughuli fulani ya kiuchumi. Labda ameajiriwa au amejiajiri. Wako busy kweli kweli. Na ukweli pesa inaonekana. Hawa huwezi kumwambia njoo tuonane akaja hapo hapo. Huyu lazima apange kwanza ratiba zake. Maana yupo busy. Au lazima aombe ruhusa kazini maana hana uhuru na muda wake. Muda wake kamuuzia mtu (mwajiri). Au labda atoroke ndo anaweza kupata muda wa kufanya mambo yake binafsi. Au asubiri weekend ambapo kila ratiba itategemea siku hizo mbili, kama ni ibada, usafi, kutembelea wagonjwa au ndugu kwenda mahali kuona labda kiwanja kinauzwa au kuona ujenzi au mradi wake unaendeleaje nk. Mara nyingi watu wa kundi hili hushindwa kufanya vitu vingi vinavyohusu maendeleo yako binafsi mfano kujisomea, kuhudhuria semina zinazofundisha mambo yanayoweza kuwa na manufaa kwake nk. Sababu ana ratiba iliyobana. Ukiwa na sherehe ukamwomba mchango hashindwi kukuchangia angalau chochote kile lakini muda wa kuja kujumuika na wewe ni vigumu akaupata.
Hili ni kundi ambalo kuna watu wanaitwa MIDDLE CLASS people. Watu wa maisha ya kati. Mambo yako si mabaya sana lakini si kwamba ni mazuri. Wasomi wengi na watafutaji wengi wapo hapa. Afu ndo wanahisi wanajua kila kitu. Na wengi wao huishia kupata changamoto za kifedha na kiafya ukubwani au uzeeni kama stress na maradhi mbali mbali nk. Sababu ya kutokuwa na muda hata wa kuangalia wa kuinvest na kujifunza biashara au ujasiriamali mapema wala kujishughulisha na afya zao, mazoezi, kupumzika vizuri nk kwa kuwa walikuwa busy siku zote. Maisha ya watu hawa middle class mwishoni huja kuwa magumu kwa kuwa hata kuwa na muda na majirani tu ilikuwa ishu. Kwa kuwa wengi wana magari (mengi ni mkopo. Wengine gari la kazini) na kwa kuwa wanaweza kulipa kodi ya nyumba au hata kupata kakiwanja na kuanza kujenga huko Malamba Mawili basi wanaridhika. Hawawezi kuota kumiliki nyumba Masaki au kununua kiwanja Upanga. Kama upo kundi hili lazima uanze kutafuta mbinu mbali mbali za kuyakabili maisha vizuri siku za usoni. Waangalie wastaafu ambao walikuwa busy zamani. Saivi utasikia mgongo, miguu, macho nk vinasumbua. Hawa middle class people ndo ukimkuta social media wengi wao wako critical kwa kila kitu. Maana haoni kama ana shida yoyote.

3. HAWANA MUDA WALA HAWANA PESA

Ulishasikia mtu anaambiwa "busy for nothing"? Ni kitu kama hicho. Yani mtu unakuta labda ni kibarua tu mahali anatumwa kazi asubuhi mpaka jioni. Labda ameajiriwa kazi ya ulinzi, au gereji, au kwenye mradi wa ujenzi anabeba zege au kupaka rangi. Hashindi njaa ni kweli lakini ukweli hana hela. Wala hatamani kuendelea kuwa hivyo. Kuamka alfajiri kulala saa tano usiku. Hela anayopata inatosha kula kwa mama ntilie tu na nauli. Basi. Hawezi kuota hata gari. Hata ya mkopo. Maana hata hakopesheki. Huyu hata muda wa Facebook ni nadra akiingia ni kupitisha macho afu anatoka. Au hata simu ya Facebook hana.

4. WANA MUDA NA WANA PESA

Hapa ndo utakuta wale ambao hana tena shida ya pesa. Pesa iko. Hana tena shida ya muda. Akihitaji kwenda mahali haombi ruhusa wala kuaga mtu labda kumuaga mwenza wake tu. Anaweza kusikia kuna shamba linauzwa mahali na hahitaji kutafuta hela tena ili akalinunue bali anaanza michakato ya kisheria pale pale kununua kama amelipenda. Kuna siku nilienda Morocco Square hapo Kinondoni jirani na Airtel kuna Apartments zinajengwa nikaonana na watu wa NHC waliokuwa wanakagua ujenzi unaendeleaje. Nikawauliza hizo apartments zinauzwaje wakasema kuna za milioni 600 na za milioni 800. Na unatakiwa kulipa cash 10% (yaani aidha milioni 60 au 80 cash) halafu inayobakia unaweza kuimalizia ndani ya miezi 12. Na kuna watanzania kadhaa wamenunua tena kwa hela halali. Hawa wako kundi hili hapa. Hela ipo. Muda upo. Kuna watu walienda kutembea Marekani kibiashara walipokuwa njiani kurudi wakapita mahalinchi nyingine wakakuta kuna mnada wa nyumba kwenye nchi hiyo. Hawakujiuliza mara mbili wakanunua. Kuna wazee fulani wana mtoto wao alikuwa akisoma Canada. Alipograduate wakamuuliza unataka kuishi wapi akasema huku huku Canada wakamnunulia nyumba Canada. Ukisikia hivyo unaanza kuwaza ni mafisadi. Mawazo yako ninkuwa bila ufisadi watu hawanunui nyumba Canada. Kwa taarifa yako Hawa siyo waajiriwa serikalini wala popote ni wafanya biashara.. Kundi la watu kwenye pesa. Na muda. Wanaweza kuamua kesho wakaenda kutembea visiwa vya Comoros. Watu wanaoishi kundi hili wana discipline kubwa ya maisha. Na watu wengi wanatamani kufika kundi hili. Lakini HAWANA discipline ya kujifunza tabia zinazoweza kukufikisha huko.

Swali muhimu tu la kujiuliza tu ni kuwa je, wewe upo kundi lipi.

Una muda mwingi lakini huna hela? = FUKARA

Una hela nyingi lakini huna muda? = MIDDLE CLASS

Huna muda wala huna hela.. Vijisenti unavyopata vinaishia nauli kula kodi ya nyumba nk? = MASKINI

Au una muda mwingi na hela siyo shida tena? = TAJIRI

[kitendawili kwako] πŸ‘‰Viwili vifananavyo

[fumbo kwako] πŸ‘‰Je Juma atatumia njia gani kuvuka?

Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, JITAMBUE: Kipi hauna kati ya pesa na muda?;

a.gif BADILIKA: Anza kupiga hatua ya maendeleo sasa

Ili kutoka hapo ULIPO uweze kwenda HATUA inayofuata kuna SWALI muhimu sana unahitaji kujiuliza.
Watu ambao huwa wanashindwa kupiga hatua katika maisha yao ni kwa sababu huwa wanajiuliza kinyume cha swali hili.
Swali hili ndilo wanalojiuliza watu wote waliofanikiwa:.. endelea kusoma

a.gif Kauli 10 za mtu ambaye unatakiwa umuepuke maishani

Kauli 10 za mtu asiye na malengo wala uthubutu
1)Sina mtaji
2)Sina Connection
3)Nitaanza rasmi kesho
4)Mimi ni wa hivihivi tu.. endelea kusoma

a.gif Angalia jinsi muda wako unavyopotea

Kila mtu ambaye ni hai amepewa muda Wa masaa 24 kila siku,168 kwa wiki,672 kwa mwezi,8064 kwa miezi 12 au kwa mwaka… endelea kusoma

tafuta-ndugu.gif

a.gif Mbinu 5 za kukunufaisha maishani

Mbinu 5 za kukufanikisha maishani Unaweza ukawa upo kwenye hali ya kulalamika maisha yako ni magumu na unashangaa kwa nini hufanikiwi katika maisha yako kama jinsi unavyotaka wewe. Hali hii inaweza ikawa inakuumiza pengine kila ukiangalia rafiki zako ama maisha ya wengine yanavyozidi kuwa mazuri, wakati wewe upo katika hali ngumu. Na pengine umekuwa ukijiuliza nini siri kubwa ya mafanikio yao ambayo wanaitumia ambayo wewe huna. Kutokana na hali hiyo umekuwa ukijilaumu kujilaumu na kujiuliza kwanini nyingi ambazo hazina majibu. Kitu usichokijua watu hawa huwa wanatumia mbinu fulani kufanikiwa. Kawaida, katika maisha kama ulivyomchezo wa miguu, au michezo mingine mara nyingi huwa zipo mbinu za kufanikisha kile tunachokifanya. Mbinu hizi huweza kutambulika kama sheria, kanuni, au siri lakini zote hulenga kukufanikisha kama unataka mafanikio ya kweli. Mbinu hizi zinapotumiwa kwa bahati mbaya au nzuri huwa hazifanyi ubaguzi zinamwendea yoyote na kuleta matunda unayoyataka. Hata kama ikitokea umezitumia mbinu hizi kwa bahati mbaya bila kujijua ni lazima utafanikiwa katika maisha yako. Mbinu hizi ndizo wanazozitumia wengi wenye mafanikio na kuwafanikisha, ingawa huwa sio kwao kuwa rahisi kukwambia mbinu hizo. Haijalishi unaishi kwa sasa maisha gani au upo kwenye matatizo mengi vipi, ukizitumia mbinu hizi, zitakufanikisha na kukupa maisha ya mafanikio unayoyataka. Acha kulalamika tena na kuishi bila amani. Sasa unaweza ukawa na mafanikio makubwa kama hao unaowaona wamefanikiwa, ikiwa utatumia mbinu hizi kukufanikisha. Unajua mbinu hizi ni mbinu zipi?.. endelea kusoma

a.gif Mafanikio ya maisha sio Elimu tuu

MAFANIKIO YA MAISHA SIO ELIMU TU, UTHUBUTU, KUJIAMINI NA UJASIRI WA MAAMUZI.. endelea kusoma

a.gif LISTI YA FURSA ZA BIASHARA NA MIRADI

LISTI YA FURSA ZA BIASHARA NA MIRADI
Karibuni;
1. Kununua Mashine za kukoroga zege na
kukodisha.
2. Kununua Mashine za kukata vyuma na
kuzikodisha.
3. Kutengeneza na kuuza tofali
4. Ufundi, Website updating/Database: Katika
Halmashauri, Manispaa, Mashule, Wizara, Wilaya
na Makampuni mbalimbali.
5. ** Kuanzisha kituo cha redio na televisheni.. endelea kusoma

a.gif Hii ndio sababu kwa nini huwezi kufanikiwa kibiashara

HUWEZI KUFANIKIWA KIBIASHARA KAMA UNAPENDA KUJIHURUMIA HURUMIA!
πŸ’₯Mama mmoja Mzungu alitembelea mlima Kilimanjaro miaka iliyopita. Alikuwa amepanga kupanda mlima Kilimanjaro mpaka kileleni, yaani Kibo na Mawenzi, ili hatimaye apewe cheti cha kupanda mlima mrefu Afrika… endelea kusoma

FURSA..! Kuna nafasi za kazi 100.

Au soma zaidi hapa

.

nn.gif
KADI-SHUKRANI-MZAZI.JPG

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.