Jinsi ya kulima vizuri vitunguu twaumu (swaumu)

Mpendwa Msomaji, baada ya kukuandalia makala inayopendwa kuhusu; Angalia jinsi maamuzi yako ya jana na ya leo yanavyoweza kukuathiri, sasa nimekuandalia makala hii kuhusu;

Jinsi ya kulima vizuri vitunguu twaumu (swaumu).

Endelea kefurahia makala nzuri kila siku unapotembelea tovuti hii.

USIKOSE HIIπŸ‘‰ Look for Research Consultant?

Jinsi ya kulima vizuri vitunguu twaumu (swaumu)

By, Melkisedeck Shine.

Vitunguu twaumu viungo vinavyopendwa na watu wengi hasa kwa harufu yake nzuri Kwenye chakula na uwezo wake wa kuondoa harufu mbaya Kwenye chakula (shombo). Vile vile vitunguu twaumu vinatumika kama tiba mbadala ya maradhi mbalimbali.

Jinsi ya kulima vitunguu twaumu

Aina nyingi za vitunguu twaumu vitakuwa kama vinatoa mbegu kwenye mmea ingawa kuna nadharia nyingi lakini inashauriwa kukata hizi mbegu chini kabisa kwa kisu kikali na kisafi, usikate mapema mara baada ya kutokeza bali subiri mpaka mmea unapoanza kama kujikunja ndipo ukate. Mbegu hizi kwa kawaida zikipandwa kwa msimu wa kwanza zitazaa kitunguu kimoja tu cha duara lakini chenyewe ukikipanda tena kwenye mzunguko wa pili kitazaa vitunguu vingi kama kawaida.

Mahitaji ya udongo

Vitunguu twaumu vinahimili aina nyingi za udongo, ila vinastawi zaidi katika udongo usiotuamisha maji kabisa na wenye mbolea asili, kama mbolea si ya kutosha kwenye udongo, tumia samadi iliyokwisha oza vizuri usitoe samadi bandani na kuipeleka shambani moja kwa moja kwenye shamba la vitunguu thwaumu, labda kama utaliacha shamba bila kulimwa kwa zaidi ya miezi 6, pia unaweza kutumia mbolea za viwandani kama ammonium nitrate, ammonium sulphate, urea n.k wakati wa kupanda na kila baada ya wiki 4 – 6 mara mbili zaidi

Kupanda

Kipindi kizuri kwa upandaji ni kipindi ambacho hakuna joto. Uotaji mzuri hutegemea pia namna vitunguu thwaumu vilivyo hifadhiwa kabla ya kupandwa, kama vilihifadhiwa sehemu zenye joto na hewa finyu uotaji wake utakuwa duni na dhaifu. Unachukua kitunguu twaumu na kutenganisha vitunguu kimoja kimoja (bulbs) na kuchagua vile vikubwa maana hivi ndivyo vitakavyo kupa mazao mengi na bora, nafasi kati ya kitunguu na kitunguu ni sentimeta 10 na kati ya mistari ni sentimeta 30. Baada ya kupanda pandishia udongo na uukandamize kuhakikisha kwamba kimekaa vizuri na hakiwezi kuathiriwa na mvua au maji wakati wa kumwagilia ili kisikae upande au kungolewa kabisa.

Palizi

Ungoleaji wa magugu na majani ni muhimu muda wote ili kuondoa kugombea rutuba, hewa na maji shambani, kwa wenye mashamba makubwa wanaweza kutumia dawa za kemikali kama ROUNDUP na nyinginezo ili kudhibiti magugu.

Umwagiliaji

Kwa kipindi chenye upungufu wa mvua au ni kipindi cha kiangazi ni vizuri ukamwagilia vitunguu twaumu ni asubuhi na sio jioni au mchana, hii inasaidia vitunguu twaumu kujijengea uwezo wa kupambana na magonjwa, baada ya mizi miwili unaweza kupunguza umwagiliajai huku ukiangalia kwa kuchimba kidogo kama vitunguu twaumu vimezaliana vya kutosha na kuanza kukomaa, ukiona vimekomaa acha kabisa kumwagilia ili visioze

Magonjwa

Magonjwa kama botrytis (kuoza shingo) blue mould na fusarium (kuoza kwa vitunguu) husababisha hasara kubwa kama hayatadhibitiwa kwa kutumia viuatilifu mara unapoona dalili, pia magonjwa kama white rot huchukua zaidi ya miaka 20 kuondoka kama yatavamia shamba lako, inashauriwa kufanya mabadiliko ya zao kila baada ya miaka mitano kwa kupanda mazao mengine yasiyo jamii moja kama vitunguu maji, unaweza kupanda maharage, mahindi, karoti na kabichi katika mzunguko huo. Pia magonjwa kama kutu ya majani husababisha na unyevu mwingi hasa kama mimea itakuwa kwenye udongo unaotuamisha maji au mimea kumwagiliwa jioni au usiku,

Kudhibiti magonjwa

Tumia viuatilifu vinavyotakiwa kwa ugonjwa husika na pia kumbuka kumwagilia asubuhi tu Ili kudhibiti ugonjwa huu wa kutu mimea ingolewe na ichomwe au utumie viuatilifu vya kuulia fangasi wa mimea.

Usisahau kushare makala hii uliyoisoma kuhusu; Jinsi ya kulima vizuri vitunguu twaumu (swaumu). Share Facebook, Twitter bila kusahau WhatsApp.

Makala hii kuhusu, Jinsi ya kulima vizuri vitunguu twaumu (swaumu), imeonekana kupendwa na wasomaji wengi. Makala nyingine zinazopendwa ni kama hizi zifuatazo;

β€’ Jinsi ya kulima vitunguu (vitunguu maji) kwa mbinu za kilimo bora na kwa faida, endelea kusoma...

β€’ Unashangaa kwa nini hufanikiwi?, endelea kusoma...

β€’ Ushauri wangu kwa leo, endelea kusoma...

β€’ Jinsi ya kulima vitunguu (vitunguu maji) kwa mbinu za kilimo bora na kwa faida, endelea kusoma...

β€’ Jinsi ya kulima bamia inavyotakiwa, endelea kusoma...

β€’ Jinsi ya kulima vizuri zao la kabichi, endelea kusoma...

β€’ Mbinu kuu za Kilimo cha Mboga cha uhakika kwa mazao mazuri, endelea kusoma...

β€’ Ni vizuri kujua haya, endelea kusoma...

β€’ Mambo ya kufanya mwezi Disemba, endelea kusoma...

β€’ Wazo mbadala kuhusu ajira au kupata kazi, endelea kusoma...

Unaweza kusoma makala mpya nzuri kila unapotembelea website hii wakati wowote. Baada ya kusoma makala hii kuhusu; Jinsi ya kulima vizuri vitunguu twaumu (swaumu), sasa endelea kusoma makala hizi nyingine nzuri nilizokuandalia;

A Hichi ndicho unatakiwa uwe nacho kulingana na umri wako, soma zaidi...
A LISTI YA FURSA ZA BIASHARA NA MIRADI, soma zaidi...
A Jielewe, kipato chako kinakusaidia nini?, soma zaidi...
A Mizigo tuliyoibeba ambayo haina faida, soma zaidi...
A Jipe moyo kamwe usikate tamaa, soma zaidi...
A Mambo 13 katika pesa ambayo unapaswa kuzingatia, soma zaidi...
A Jifunze kupitia mfano huu Ili uishi kwa amani na watu, soma zaidi...

Usipitwe na Nafasi za kazi kwa leo

<<Bofya HAPA kujua zaidi>>

.

UJUMBE-ZA-USIKU-KWA-NDUGU.JPG
UJUMBE-KUOMNBA-KUKUTANA-NA-NDUGU.JPG