Jinsi ya kulima vitunguu (vitunguu maji) kwa mbinu za kilimo bora na kwa faida

By, Melkisedeck Shine.

afya-mapishi-na-lishe.png

Jinsi ya kulima vitunguu (vitunguu maji) kwa mbinu za kilimo bora na kwa faida

Vitunguu ni zao la mbogamboga na hulimwa kwa ajili ya balbu zake ambazo hutumika kama kiungo cha chakula. Vitunguu vina matumizi mengi sana na vina madini joto, chuma, vitamin A, vitamin B, vitamin C na vitamin E.
Vitunguu hulimwa na hukubali zaidi nyanda za baridi. Nyanda zenye joto vitunguu hulimwa pia. Vitunguu vinaweza kulimwa mwaka mzima endapo maji yanapatikana.

Aina za vitunguu vinavyolimwa Tanzania

  • Red Creole
  • Bombay Red
  • Hybrid F1

Hali ya hewa

Joto linatakiwa sana kwa ajili ya ukuaji wa balbu ila joto likizidi vitunguu hukomaa mapema kabla balbu hazijafikia ukubwa unaostahili, hivyo mkulima anaweza kupata mazao kidogo.

Udongo

Vitunguu huweza kupandwa kwenye udongo wowote wenye rutuba, usiotuamisha maji na usionata sana. Hufanya vizuri kwenye udongo wenye asidi kidogo japo udongo wenye alkali kidogo sio mbaya sana. Kwenye udongo wenye mchanga mchanga umwagiliaji ni lazima. Udongo mzuri sana kwa ustawi wa vitunguu ni tifutifu-kichanga.

Mbolea

Epuka matumizi ya mbolea mbichi isioiva vizuri kwani husababisha vitunguu kuwa na shingo pana sana majani hukua sana badala ya balbu.

Umwagiliaji

Umwagiliaji ni muhimu sana hasa wakati wa kuanza kutengeneza balbu. Unyevu uliozidi ni hatari sana kipindi cha ukuaji.

Kitalu cha vitunguu

Ni muhimu kumwagilia maji ya kutosha siku kumi za mwanzo tangu kusia mbegu kitaluni. Vitunguu hukaa kitaluni kwa wiki 6-8 na miche ifikiapo upana wa penseli na urefu wa sm 15 ni tayari kwa kuhamishia shambani/bustanini.

Upandaji

Kabla ya kupanda udongo ni lazima utifuliwe vizuri na reki kuondoa mabaki ya mimea na mawe ama Vipande vikubwa vya udongo. Matuta yawe na upana wa mita moja. Vitunguu hupandwa kwa mstari mojakwamoja ama kutokea kitaluni. Pia huweza kupandwa kwa mstari pacha. Vitunguu hupandwa sm 10-15 kutoka mmea hadi mmea na sm 10-15 kutoka mstari hadi mstari, kama inavyoonekana kwenye mchoro hapa chini. Pia epuka kupanda vitunguu mahali palipopandwa mboga jamii ya vitunguu siku za nyuma. Mfano Vitunguu saumu na vitunguu majani.

Utunzaji wa shamba

Kutandazia shamba na majani yaliyooza vizuri ama mabua inashauriwa ili kuongeza ruba ya ardhi, zuia magonjwa yatokanayo na udongo na magugu. Kupanda vitunguu kwenye matuta yaliyoinuka ni muhimu sana kuzuiya utuamishaji wa maji na mlipuko wa magojwa ya miche. Kungoa magugu na uvunaji ufanywe kwa mkono.
Vitunguu hufanya vizuri kama shamba litawekewa mbolea ya samadi ama mboji ilioiva vizuri. Kiasi cha tani 25-40 kwa heka kinashauriwa. Hii ni sawa na kilo 7.5 -12 kwa tuta lenye urefu wa mita 3 na upana wa mita 1.

Uvunaji

Vitunguu huvunwa kuanzia siku 90-150 tangu kusia mbegu. Dalili za kukomaa ni kuanguka kwa majani. Vitunguu huvunwa kwa kuvuta kwa mkono na kuhifadhiwa siku kadhaa shambani vikiwa vimefunikwa na majani. Baada ya hapo majani hukatwa na balbu hupakiwa kwa ajili ya kuhifadhi kusubiria bei nzuri. Vitunguu huweza kuhifadhiwa hadi miezi 9 tangu vivunwe bila kuharibika. Vitunguu vihifadhiwe kwenye nyuzijoto chini ya 4.4 °C ama juu ya nyuzijoto 25°C ili visiharibike.


Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Jinsi ya kulima vitunguu (vitunguu maji) kwa mbinu za kilimo bora na kwa faida;

a.gif Jinsi ya kulima bamia inavyotakiwa

Bamia ni zao linalolimwa sana nchi za joto. Zipo aina nyingi za bamia, aina zile za kiasili nazo hutofautiana kulingana na eneo moja na lingine. Bamia huliwa kama matunda au hupikwa kama mboga pamoja na nyama, samaki au mboga nyingine… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kulima vizuri zao la kabichi

Kichwa cha kabichi kinapofunga vizuri, hutumika kama chakula na huvunwa baada ya kufunga na kukomaa vizuri. Kwa kawaida kabichi hupandwa kwa msimu mmoja, lakini iwapo itakuzwa kwa ajili ya kutoa mbegu hukuzwa zaidi ya msimu mmoja. Endapo inalimwa sehemu yenye maji ya kutosha, inaweza kulimwa msimu wote wa mwaka. Soko lake ni la uhakika katika kipindi chote na ni muhimu kwa afya. Pia, linaweza kutumika kama malisho ya mifugo
Mizizi: Mizizi ya kabichi hutawanyika ardhini vizuri. Kwa kawaida, huenda chini kiasi cha sentimita ishirini (20 sm), na hujitawanya kwa kiasi cha sentimita sabini na tano (75sm).
Shina: Shina la mmea wa kabichi huwa na rangi ya kijani au zambarau. Hii hutegemeana na aina ya kabichi, na kwa kawaida ni fupi… endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kulima vizuri vitunguu twaumu (swaumu)

Vitunguu twaumu viungo vinavyopendwa na watu wengi hasa kwa harufu yake nzuri Kwenye chakula na uwezo wake wa kuondoa harufu mbaya Kwenye chakula (shombo). Vile vile vitunguu twaumu vinatumika kama tiba mbadala ya maradhi mbalimbali… endelea kusoma

a.gif Kilimo kizuri cha pilipili hoho

Pilipili hoho ni zao la jamii ya pilipili isiyo kali, tunda lake ni nene kiasi la duara pia linaweza kuwa lililochongoka. Pilipili hoho hutumika katika kutengeneza rangi za asili za vyakula ambazo kwa sasa hupendwa zaidi kuliko zile zinazotokana na kemikali na pia huongeza ladha na harufu katika vyakula. Hivyo hutumika katika viwanda vya kusindika vyakula, kwa mapishi ya nyumbani na hata katika viwanda vya vipodozi kama rangi ya mdomo, uso n.k. Ina virutubisho muhimu vinavyohitajika mwilini kama madini ya chuma, vitamin A na C… endelea kusoma

a.gif UJASIRIAMALI NA CHANZO CHA MTAJI

Ni uthubutu au ujaribu wa ufanyaji wa
shughuli yoyote halali na kupitia shughuli
hiyo mtu watu huweza kupata kipato… endelea kusoma

a.gif Kampeni Ya Wafanye Watabasamu

Let Them Smile Campaign au Kampeni ya Wafanye nao Watabasamu ni kampeni endelevu ya kuhamasisha ushirikiano, umoja na kusaidiana katika jamii kwa watu wa matabaka yote.
Kampeni hii ina lengo la kuamsha na kueneza furaha itokanayo na umoja na mshikamano kwenye jamii kwa njia ya kusaidiana na kushirikiana kimawazo, kwa matendo na kifedha. Ni kweli kwamba furaha ya kweli haiji kwa kujifurahisha mwenyewe bali kwa kufurahishwa… endelea kusoma

a.gif Kuwa na kawaida ya kujiwekea Akiba ni njia na Siri ya kuwa tajiri

Watu wengi wanajiuliza, “Siri ya utajiri ni nini?”
Je ni mbinu gani zinaweza kumsaidia mtu kupata utajiri?
Siri kubwaya utajiri ni kujifunza elimu ya namna ya kutafuta mtaji, kuwekeza kwa busara kwa namna ambayo daima panakuwa naziada na faida… endelea kusoma

a.gif Elimu tuu haitoshi kukunufaisha maishani na kukupa mafanikio

EMBU SOMA HII KWA MAKINI SJUI NI KWELI? USIMAINDI LAKINI MAANA ITAKUGUSA TUU. MAFANIKIO YA MAISHA SIO ELIMU TU, UTHUBUTU, KUJIAMINI NA UJASIRI WA MAAMUZI
✍🏽Ukichunguza katika jamii, utabaini kuwa sehemu kubwa ya matajiri ni wale ambao wana elimu ndogo ama hawakusoma kabisa… endelea kusoma

uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png

.

uchumi-biashara-na-ujasiriamali.png
KADI-MSAMAHA-MZAZI.JPG
elimu-sayansi-na-tekinolojia.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.