Jinsi ya kulima mahindi kitaalamu kama inavyotakiwa

By, Melkisedeck Shine.

Mahindi ni miongon mwa mazao makuu ya chakula hapa nchin Tanzania na ulimwa karibu kila mkoa. Ulimwa zaidi nyanda za juu kusini katika mikoa ya Mbeya, Iringa, Ruvuma, Njimbe na Katavi. Pia mikoa ya Morogoro Mwanza Dodoma Shinyanga Arusha Tanga na mikoa mingine. Kwakua ni zao la biashara hivyo karibu kila mkoa unalima zao hili.

Matumizi.

Zao hili ulimwa na utumika kwa matumizi mbalimbali yakiwemo yafuatayo

★Chakula (stample food)
★Chakula kwa mifugo
★Nishati (biofuel)
☆Dawa za asiri(mbelewele zake)
☆kutengenezea mapambo.
☆mabaki utumika kama mbolea n.k.

Pia wapo wakulima waliojikita katika kulima zao hili kibiashara ambao uuza katika soko la ndani ya mkoa nje ya mkoa na nje ya nchi. Hapa itategemea uwekezaji wa mkulima husika.

MAZINGIRA NA HALI YA HEWA NZURI KWA MAHINDI

Mahindi uota vizuri katika jotoridi lenye wastani wa 20-30 nyuzi joto za centigradi. Pia linaitaji mvua hasa wakati wa uotaji na uotaji wa mbelewele.

MBEGU ZA MAHINDI

Kuna aina nyingi za mbegu. Zipo za Asili na pia zipo mbegu chotara (Hybrid F1 & F2) kutoka makampuni mbalimbali, za mda mfupi na za mda mrefu kulingana na kipindi/vipindi vya mvua kwa mwaka kwa mkoa usika.

Kwakua Tanzania ina kanda tofauti za hali ta hewa ikiwemo nyanda za juu kusini, nyanda za juu kaskazini, nyanda za kati na maeneo mengine ya pwani na pia ndani ya mkoa mmoja panaweza pakawa na matabaka tofauti yakijografia (geographical/ecological zone).

Hivyo mbegu za mahindi zinazofanya vizuri mikoa ya Pwani Morogoro Arusha Mwanza haziwezi kufanya viruzi katika mikoa ya Njombe Iringa n.k kwakua utofautiana katika ukanda.
Mbegu zinazofanya vizuri Njombe mjini ama wanging'ombe zinaweza zisifanye vizuri Ludewa ama Makete wilaya tofauti lakini mkoa mmoja.

Hivyo ni vema kujua kua mbegu upandao inafaa kwa ukanda upi?? Wa mvua za mda mrefu! Mda mfupi! Ama sehemu zenye ukame!!.

NAFASI

Hii itategemea aina ya mbegu na pia namna ya utunzaji ambao utegemea sana kusudi la ulimaji (chakula ama biashara).

UPANDAJI WA MAHINDI

Mche hadi mche ni sm 30-40. Mstar hadi mstari ni sm 70-75.
Yaani sm 75X30, pia waweza tumia sm 80X25 punje moja moja za mbegu chotara ya mahindi.

Ni vema ukapanda siku moja ambayo utaweka na mbolea. Anza na mbolea 5g kwa shimo fukia kidogo kisha weka mbegu ( mbegu moja kama ni Hybrid).
Mbolea nzuri zaidi yenye maboresho na lishe linganifu kwa mmea (balanced nutrition) ni YaraMila Cereal, Yara Vera Amidas na YaraBela Sulfan kutoka kampuni ya Yara Tanzania ltd. Mfuko mmoja mmoja, utapandia, utakuzia mkuzio wa kwanza na utamalizia mkuzio wa pili kama zilivyo orodheshwa hapo.

PALIZI YA MAHINDI

Kuna aina tatu za kupambana na magugu.

1. Palizi la mkono/jembe.

Hili lina gharama zaidi na linachukua mda mwingi na pia SIO SAHIHI kwakua halireti majibu mazuri katika kuzuia magugu.

2. Mbinu za Asiri.

Hapa utumika matandazo kama majana makavu, majani ya mgomba, pumba za mpunga n.k ( Mulching). Huitaji kujipanga zaidi na piaupatikanaji wa matandizo wakati wakilimo unaweza ukawa ni shida.

3. Palizi la Dawa.

Hapa ndio upatikana suluhisho sahihi kwa mkulima ingawa changamoto zipo katika ubora wa dawa wingi wa madawa uwepo wa dawa feki na gharama.
Ni vema ukatumia dawa zinazotumika kuzuia magugu mara baada yakupanda kabla ya magugu kuota (somo la magugu litafuata sio mda).
Tumia PRIMAGRAM GOLD kutoka Syngenta Tanzania Ltd epuka palizi la mkono okoa mda pata faida pata mda wakupumzika na kujishughurisha na mambo mengine na uongeze kipato.

WADUDU NA MAGONJWA KWENYE MAHINDI

WADUDU WA MAHINDI

Maize aphids, African armyworms, Bollworm, Stalk borer, leaf hoppers.

Dawa nzuri kuzuai hili ni Match 050EC na Karate 5EC/Karate 5CS(Originali kutoka Syngenta epuka dawa feki ilikopiwa nembo/lebo)

MAGONJWA YA MAHINDI

Magonjwa ya ardhini (soil born disease), kutu ya majani n.k.
Magonjwa ya kuvu sio tatizo sana ktk kilimo hiki ingawa maeneo ya nyanda za juu kaskazini yameoneka.
Tumia Artea na Amistar Kutoka kampuni ya Syngenta.

UVUNAJI WA MAHINDI

Mda ambao mahindi uchukua kukaa shamban hadi kuvunwa inategemea na ukanda na pia na mbegu, mahindi ukaa wastan wa miezi mitano toka kupandwa shambani. Lakini ni tamaduni za wakulima wengi kuacha mahindi shambani kwa mda mrefu zaidi ili yakauke kwa matumizi ya biashara. Mahindi kwa ajiri ya gobo ukaa mda mfupi (sio kila mbegu ni ya gobo/mahind yakuchoma) zaidi uvunwa kabla yakukomaa.

Idadi ya gunia utazopata kwa ekari moja utegemea

→ utaratibu uliofuatwa wakitaalum (Agronomic practices)
→ aina ya mbegu
→mazingira (ukanda)-mvua ama umwagiliaji.
→mapambano dhidi ya wadudu magonjwa na magugu.
→ usimamizi/mbolea/rutuba ya udongo wako.
Kila mbegu hasa chotara zinakua na kiasi tajwa cha mavuno kwa ekari.
Mf. Gunia 30, 25-30, ama 40 n.k. (gunia tafsiri yake kitaalum ni 100kg.

SOKO LA MAHINDI

Soko utegemea sana wastani ama ungezeko la walimaji na uzalishaji. Soko lake utegemea sana watumiaji wa ndani.
Pia utokea soko katika mkampuni kama wanunuzi wadogo wadogo, kampuni ndogondogo za usagaji mahindi, taasis mbalimbali,Mohamed enterprise, Hifadhi ya taifa ya chakula, n.k na pia soko la nje ya nchi eg Kenya Uganda Sudani Ethiopia n.kUJUMBE-WA-MSAMAHA-KWA-NDUGU.JPG

Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Jinsi ya kulima mahindi kitaalamu kama inavyotakiwa;

a.gif Angalia jinsi muda wako unavyopotea

Kila mtu ambaye ni hai amepewa muda Wa masaa 24 kila siku,168 kwa wiki,672 kwa mwezi,8064 kwa miezi 12 au kwa mwaka… endelea kusoma

a.gif JITAMBUE: Kipi hauna kati ya pesa na muda?

Soma kidogo hapa.. Kuna watu wa aina NNE tunapoongelea pesa na muda… endelea kusoma

a.gif Uhusiano uliopo kati ya pesa na muda

Bila shaka upo uhusiano mkubwa kati ya pesa na muda…. endelea kusoma

a.gif Umasikini isiwe sababu wala utajiri isiwe sababu

Umasikini sio sababu ya kuwa mchafu wala utajiri Sio kuwa na kila kitu hata kama hukihitaji. Hebu angalia hapo nyumbani kwako!.. endelea kusoma

[Kitendawili Kwako] 👉Huenda nimepanda hurudi nimepanda

[Fumbo Kwako] 👉Je, hawa walizikwa wapi?

[Chemsha Bongo Kwako] 👉Je, hii familia ina watoto wangapi?

Slide3-mliopoteana.GIF

a.gif JINSI YA KUTENGENEZA BATIKI

Batiki

Batiki inatengenezwa kama ifuatavyo.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kulima vizuri zao la kabichi

Kichwa cha kabichi kinapofunga vizuri, hutumika kama chakula na huvunwa baada ya kufunga na kukomaa vizuri. Kwa kawaida kabichi hupandwa kwa msimu mmoja, lakini iwapo itakuzwa kwa ajili ya kutoa mbegu hukuzwa zaidi ya msimu mmoja. Endapo inalimwa sehemu yenye maji ya kutosha, inaweza kulimwa msimu wote wa mwaka. Soko lake ni la uhakika katika kipindi chote na ni muhimu kwa afya. Pia, linaweza kutumika kama malisho ya mifugo
Mizizi: Mizizi ya kabichi hutawanyika ardhini vizuri. Kwa kawaida, huenda chini kiasi cha sentimita ishirini (20 sm), na hujitawanya kwa kiasi cha sentimita sabini na tano (75sm).
Shina: Shina la mmea wa kabichi huwa na rangi ya kijani au zambarau. Hii hutegemeana na aina ya kabichi, na kwa kawaida ni fupi… endelea kusoma

a.gif Ufugaji wa nguruwe na faida zake

Patrick Tungu Sociologist.. endelea kusoma

a.gif Kampeni ya kutetea watu wenye ulemavu

Kampeni hii ilianzishwa na Melkisedeck Leon Shine mwaka 2018.
Lengo la kampeni hii ni kuhamasisha watu wote kusaidia na kutetea watu wenye ulemavu kwa maendeleo bora ya kimwili, kiroho na kijamii kwa manufaa ya walemavu wenyewe na kwa manufaa ya watu wote kwa sasa na kwa baadae.
Kampeni hii inaamini kuwa watu wenye ulemavu wanayo haki na nafasi sawa kama watu wengine katika jamii. Vile vile wanatamani kuishi kwa amani na furaha kwa hali ya kawaida kama watu wengine. Kwa hiyo kila mtu kwa nafasi yake anaweza akawawezesha kuishi kwa furaha na matumaini kama watu wengine… endelea kusoma

[Msemo wa Leo] 👉Ushauri kwa mtu

[Jarida la Bure] 👉Mapishi ya wali wa karoti na nyama

FURSA..! Kuna nafasi za kazi 100.

Au soma zaidi hapa

.

KADI-SALAMU-JIONI-MZAZI.JPG
KADI-MMISI-MZAZI.JPG

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.