Je, Wewe unayesoma huu ujumbe una ndoto?

By, Melkisedeck Shine.

elimu-sayansi-na-tekinolojia.png

Je, Wewe unayesoma huu ujumbe una ndoto?

KILA mtu duniani ana ndoto ingawa haijalishi ni ndoto gani uliyonayo.
Ndoto uliyonayo ina thamani kubwa kuliko fedha wala kitu chochote kile. Ndoto uliyonayo ina nguvu kubwa ya kubadilisha maisha yako na kukufikisha sehemu ambayo ulitaka ufike ama zaidi ya pale ulipotarajia kufika.

Ndoto yako inaweza kukupeleka sehemu mbalimbali duniani ukazunguka kufanya mambo yako si kwa sababu una fedha sana, bali ni kwa sababu una ndoto. Ni vyema utambue nguvu ya ndoto uliyonayo ni kubwa kuliko fedha.

Ndoto inaweza kuzaa fedha kwa maana matunda yake yanaweza kuwa fedha, lakini katu fedha haiwezi kuzaa ndoto. Kwa hiyo bais, ndoto ni kubwa kuliko fedha.

Mtu mmoja aliwahi kusema kuwa, mtu maskini kuliko wote duniani ni yule asiyekuwa na ndoto!

Hivyo utakubaliana naye kuwa kila mwenye ndoto ni tajiri na si maskini, maana ana kitu cha thamani, cha pekee na cha tofauti ambacho hakuna mwenye nacho isipokua wewe mwenyewe.

Tatizo kubwa ni kwamba, watu wengi wameua ndoto zao kwa kisingizio cha kukosa fedha lakini wanashindwa kutambua kwamba hakuna fedha inayozidi ndoto isipokuwa ndoto inazidi fedha.

Tatizo lingine ni kwamba, watu wengi hawajui kuwa ndoto zao zina nguvu kubwa kufanikisha maisha yao kijamii, kiuchumi, kisiasa na kila nyanja.

Ndani ya ndoto zako kuna kila kitu unachokitaka ama unachokihitaji – iwe fedha, utajiri, umaarufu, familia nzuri, mume mzuri, mke mzuri, watoto wazuri, kazi nzuri, afya nzuri – hivyo ukiacha kutafuta fedha ukatafuta kutimiza ndoto zako utapata kila kitu ikiwemo utoshelevu na amani ya moyo.

Lakini tatizo lipo kwenye kufanya ndoto zako zitimie na zikuzalie mafanikio. Haijalishi una ndoto kubwa kiasi gani, kama hutaitimiza ikaja kwenye uhalisia tambua kwamba utakufa maskini ukiwa na utajiri wa ndoto, jambo ambalo linaumiza na linatesa maisha ya watu wengi wanaoishi maisha ya chini tofauti na walivyopaswa wawe.

Ndoto yako ndiyo imebeba kusudi la maisha yako. Kama hutaishi katika ndoto yako maana yake utakuwa hujaishi maisha yako ambayo kwa kiasi kikubwa yapo kwenye ndoto zako.

Mtu mmoja aliwahi kusema kuwa, watu wengi duniani hawaishi, bali wapo tu. Kuna tofauti kati ya kuishi na kuwepo. Kuishi ni kutimiza ndoto zako na ndani ya kusudi la maisha yako, lakini kama hutimizi ndoto hizo uko nje ya kusudi la maisha yako. Wewe utakuwa hauishi bali upo upo tu.

Anaamka asubuhi kwa sababu watu wanaamka. Ukimuuliza kwanini umeamka anasema ni kwa sababu watu wameamka! Hana sababu za msingi. Kataa kuishi bila agenda, bila kuwa na ndoto ambayo kila siku unapiga hatua kuifikia ama uko ndani yake sasa katika kuitimiza na kuifanikisha kwa kiwango cha juu.

Kila kitu kipo kwenye ndoto zako, tafuta kutimiza ndoto zako kuliko kutafuta fedha kwa sababu fedha ni moja kati ya bidhaa iliyomo ndani ya ndoto zako.

Sisemi watu wasitafute fedha, la hasha. Wazitafute, tena kwa bidi, ila wasisahau kutafuta kutimiza ndoto zao na kutumia fedha kama moja kati ya nyenzo za kuwawezesha kutimiza ndoto zao.

Ukweli ni kwamba, fedha daima huwa hazitoshi, hata kama ni nyingi kiasi gani. Kama unabisha waulize matajiri kama wamewahi kuridhika. Lakini katika kutimiza ndoto zako kuna utoshelevu kiasi na kuridhika kiasi fulani (satisfaction) hata kama si kwa asilimia 100.

Mwandishi mashuhuri wa vitabu, Myles Munroe, aliwahi kusema kuwa “Watu wenye kusumbuliwa na msongo mkubwa wa mawazo ni wale ambao ndoto zao hazijatokea kwenye uhalisia, zinawasumbua.”

Inawezekana unasumbuka sana kwenye maisha yako kwa sababu hujatimiza ndoto zako, maana ndoto huwa haimwachi mtu akatulia, inampa mahangaiko, mfadhaiko wa kutaifuta.

Kila mtu anapaswa azae, ndoto yako izae, uwezo ulionao uzae. Unaweza kukuzalia mafanikio makubwa, hivyo usikubali kufa na kitu cha thamani kilichoko ndani yako.

Hakuna ndoto kubwa wala ndogo. Fikiria mtu aliyegundua lipstick, leo hii wanawake dunia nzima wanapaka lipstick, si jambo dogo tena.

Hukuja duniani kuwa mtu wa kuhangaikia fedha, inatakiwa fedha ikuhangaikie wewe, ikupende na ikutamani na si wewe utamani fedha.

Tengeneza miundombinu ya fedha na hiyo miundombinu iko kwenye ndoto zako, maono yako, kipaji


Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Je, Wewe unayesoma huu ujumbe una ndoto?;

a.gif Ilinde ndoto yako

Ndoto ni nini?
Ndoto ambayo tunakwenda kuizungumzia sio ndoto unayoota ukiwa umelala ni ndoto ya mchana.
Ni kile kitu unachotamani kuja kukipata siku moja kabla hujaondoka duniani Ndoto inaweza kua katika makundi ya aina mbalimbali, unaweza kua na ndoto ya kuwa Rais, Mwimbaji bora, Mchezaji bora, Mwandishi Bora, Mfanyabiashara maarufu.
Vile vile unaweza kuwa na ndoto ya kumiliki vitu, nyumba nzuri ya kifahari sana labda ya milioni 300, Gari la kifahari sana, Unaweza kuwa na ndoto ya kumiliki utajiri au kuwa Bilionea,Kutembelea nchi fulani na kadhalika… endelea kusoma

a.gif Kukataliwa ni mtaji

Hakuna mtu duniani ambaye hajawahi kukutana na hali ya kukataliwa. Yaani kukataliwa katika hali yoyote ile. Waweza kuwa umekataliwa katika kupata ajira, umekataliwa katika mahusiano, umekataliwa kupata nafasi ya kusoma, umekataliwa kupata mtaji wa biashara, umekataliwa tuu..umekataliwa… endelea kusoma

a.gif Jiwekee Utaratibu utakaokuwezesha kuamua vizuri juu ya fedha utakazopata

Jiwekee utaratibu utakaokupa uzoefu wa kuamua vizuri juu ya fedha unazopata. Watu tumekuwa tukitumia fedha tunazopata bila kufikiria jinsi ya kugawa ktk matumiz badala yake baada ya kutumia ndio una/ninaanza kujuta Kwa nin nime/umetumia tofauti na mahitaji uliyonayo. Kiasi cha fedha ulichonacho chaweza kukufanya uwe maskini au tajir kutokana na maamuz unayofanya juu ya hiyo fedha. Ukitaka ufanikiwe na ukue kifedha jaribu kugawa fedha uliyopata Kwa mafungu yafuatayo:.. endelea kusoma

a.gif Mtu aliyefanya kazi ngumu zaidi afunguka

*SIMULIZI YA KUSISIMUA*
👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾🤔
*Mtu aliyefanya kazi ngumu zaidi afunguka*.. endelea kusoma

a.gif Jinsi ya kulima mahindi kitaalamu kama inavyotakiwa

Mahindi ni miongon mwa mazao makuu ya chakula hapa nchin Tanzania na ulimwa karibu kila mkoa. Ulimwa zaidi nyanda za juu kusini katika mikoa ya Mbeya, Iringa, Ruvuma, Njimbe na Katavi. Pia mikoa ya Morogoro Mwanza Dodoma Shinyanga Arusha Tanga na mikoa mingine. Kwakua ni zao la biashara hivyo karibu kila mkoa unalima zao hili… endelea kusoma

a.gif Kampeni Ya Wafanye Watabasamu

Let Them Smile Campaign au Kampeni ya Wafanye nao Watabasamu ni kampeni endelevu ya kuhamasisha ushirikiano, umoja na kusaidiana katika jamii kwa watu wa matabaka yote.
Kampeni hii ina lengo la kuamsha na kueneza furaha itokanayo na umoja na mshikamano kwenye jamii kwa njia ya kusaidiana na kushirikiana kimawazo, kwa matendo na kifedha. Ni kweli kwamba furaha ya kweli haiji kwa kujifurahisha mwenyewe bali kwa kufurahishwa… endelea kusoma

a.gif Usiyoyajua kuhusu pesa haya hapa

Habari za Leo Rafiki yangu wa Muhimu sana. Ni furaha yangu kujua unaendelea vyema sana na majukumu yako… endelea kusoma

a.gif Kampeni ya utunzaji wa wanyama pori

Kampeni hii ilianzishwa na Melkisedeck Leon Shine mwaka 2018.
Lengo la kampeni Hii ni kuhamasisha watu kutunza wanyama pori kwa manufaa yao ya sasa na kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Kampeni hii inaamini kuwa wanyama pori wakitunzwa vizuri wanaweza kuwa msaada kijamii, kiuchumi na kimazingira kwa kizazi hiki na kizazi kijacho… endelea kusoma

picha-kali.png

.

vichekesho-bomba-vya-siku.png
PONGEZI-MPENZI-24498UA8.JPG
picha-kali.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.