Mungu alimpenda sana binadamu hata akauvaa Mwili wa Binadamu akashuka duniani na kuishi kama Binadamu ili amkomboe Mwanadamu na hata akaamua kufa kwa ajili ya Binadamu kwa malipizi ya dhambi za Binadamu na kwa maondoleo ya dhambi.

Je, ni Kitu gani ambacho Mungu angemfanyia mtu ambacho hajakifanya?

Kweli nakwambia hata kama Yesu angebaki duniani na kuwa hai mpaka leo bado watu wasinge mwamini na wapo ambao wangemchukia na kumfanya adui yao hata kumuwinda.

Ni watu wachache sana duniani wanaouona upendo huu mkuu wa Mungu, wengi hawaoni wala hawataki kuona. Wapo hata wacha Mungu lakini hawaelewi upendo huu.

πŸ™‰πŸ™‰πŸ™‰Usisahau kushare makala hii kuhusu Tafakari ya leo ya Katoliki kuhusu Upendo Mkuu wa Mungu.πŸ‘ Share facebook, twitter n.k bila kusahau WhatsApp!πŸ’―βœ”


images-14.jpeg
Ujumbe wangu kwako kwa sasa

Sala ndiyo chimbuko la fadhila. Kwa njia ya sala tunapata fadhila za Kimungu na Neema za Mungu. Asaliye daima hujazwa neema na fadhila.

Mungu Akubariki sana… Tuombeane!

ml.gif

πŸ“š Endelea kusoma kuhusu;-πŸ‘‡

SALAMU-MPENZI-MCHANA-33097HG34MX.JPG