Kundi la watu lilikwenda mahala wakakuta mawe yamezagaa. Ghafla wakasikia sauti ikisema: "Atakaeokota atajuta na asiyeokota atajuta," baadhi yao wakaokota na wengine hawakuokota. Wakarudi nyumbani. Asubuhi yale mawe yakageuka kuwa Dhahabu, waliookota wakajuta kwa nini wameokota machache, wasio okota wakajuta kwa nini hawakuokota. Hivyo ndivyo itakavyokuwa siku ya mwisho; "wapo watakaojuta kwa nini walitenda mema machache, na wapo watakaojuta kwa nini hawakutenda mema kabisa!!!". Nafasi ya kuokota ipo hapa duniani kabla Roho haijaachana na mwili.

πŸ™‰πŸ™‰πŸ™‰Usisahau kushare makala hii kuhusu Tafakari Kuhusu siku ya mwisho.πŸ‘ Share facebook, twitter n.k bila kusahau WhatsApp!πŸ’―βœ”


IMG_20180905_125537.jpg
Ujumbe wangu kwako kwa sasa

Mungu anasubiri sala zako kila siku. Anasubiri sala zako akujibu ili uone utukufu wake. Anasubiri sala zako ili akuze mahusiano yake na wewe. Sali daima kwani Mungu yupo milele kukusikiliza na kukuhudumia.

Mungu Akubariki sana… Tuombeane!

BIKIRA-MARIA-NI-MALKIA-WA-KIPEPEO.JPG

πŸ“š Endelea kusoma kuhusu;-πŸ‘‡

ufufuo-wa-wafu-upooo.JPG