TAFAKARI YA MAISHA: Vile unavyobariki, ndivyo unavyobarikiwa

Kiwango cha majukumu uliyonayo kinaamua kiwango cha baraka zinazofuatana na wewe.

LABDA NIKURAHISISHIE LUGHA UNIPATE VIZURI…

Huenda una ajira yako na unalalamika kwamba yasingalikua majukumu huenda ungekua mbali kimaendeleo. Labda unasomesha ndugu zako, labda unauguza kwa muda mrefu, labda wengi wanakutegemea wewe, labda mizigo mingi umerundikiwa wewe kiasi kwamba unaamini yasingalikua hayo ungekua mbali kimaendeleo.

KWA TAARIFA YAKO…

Kuna namna Mungu huenda alikupa hiyo ajira sio kwa ajili yako bali kwa ajili ya hao unaodhani wanakurudisha nyuma. Unaweza kukuta unapata urahisi wa kodi sio kwa ajili ya bidii zako bali Mungu anawaangalia aliowaweka mikononi mwako. Kuna watu mngekua mlishafukuzwa ama kupunguzwa kazini, ila Mungu akiangalia kuwa ni wewe unaetoa hela ya matibabu ya shangazi kule kijijini, basi anaendelea kuitunza hiyo ajira. Kuna wakati unalindwa na malaika usipate ajali sio kwa sababu gani, bali Mungu anajua wewe ukiumia kuna wengi wataumia.

KWA HIYO..

Kama una majukumu mengi sana ya kusaidia wengine, usilalamike hata kidogo. Wasaidie kwa kadiri uwezavyo ukiwa na furaha. Ukiacha, Mungu anaweza kukuachisha kazi! Ukiendelea kulalamika Mungu anaweza kuondoa ulinzi wa afya yako! Ukiwasema vibaya, majanga yanaweza kutokea kazini kwako!

NINACHOKUTHIBITISHIA….

Ni kwamba, baraka ulizonazo hadi sasa, Mungu hajakupa kwa ajili yako peke yako, bali amekubariki ili uwabariki wengine. Ukiona majukumu uliyonayo ni mzigo, maana yake unamwambia Mungu kwamba alipokubariki ni mzigo na wala asikupe baraka zaidi.
*Tuwe makini sana!*
🀝🀝🀝🀝🀝

.

.

IMG_20181021_134724.jpg

Kama Una mashaka na Imani na mafundisho ya Kanisa Katoliki soma hapa>>

Website hii inaletwa kwako na Melkisedeck Leon Shine.

Naomba utafakari kuhusu; Umuhimu wa kumsogelea Mungu. Mungu akubariki sana. Tuombeane…!