a.gif Msimamizi wa ubatizo ana wajibu gani?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ ubatizo,
Msimamizi wa ubatizo ana wajibu gani?
Msimamizi wa ubatizo ana wajibu hizi;. read more...


a.gif Alama wazi ya Sakramenti ya Ubatizo ni nini?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ ubatizo,
Alama wazi ya Sakramenti ya Ubatizo ni nini?
Alama wazi ya Sakramenti ya Ubatizo ni kumwagia maji katika panda la uso na kutamka maneno "Fulani (jina lake linatajwa) nakubatiza kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu" (Mt 28:19). read more...


a.gif Anayebatizwa yampasa nini?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ ubatizo,
Anayebatizwa yampasa nini?
Yampasa kuungama imani yake ama mwenyewe akiwa mtu mzima ama kupitia wazazi kama akiwa mtoto mdogo. read more...


a.gif Je, Ubatizo ni lazima kwa wokovu?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ ubatizo,
Je, Ubatizo ni lazima kwa wokovu?
Ndiyo, nilazima kwa wokovu kwa wale ambao wametangaziwa injili na wanasifa ya kuomba Sakramenti hiyo. read more...


a.gif Kwa nini Kanisa linabatiza watoto wadogo?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ ubatizo,
Kwa nini Kanisa linabatiza watoto wadogo?
Kwa sababu wanazaliwa na dhambi ya asili hivyo wanahitaji kuwekwa huru kutoka mamlaka ya yule mwovu na kuingizwa katika ufalme wa uhuru wa wana wa Mungu. read more...


a.gif Nani aweza kubatiza?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ ubatizo,
Nani aweza kubatiza?
Mwenye mamlaka ya kubatiza kwa kawaida ni yule mwenye dataja takatifu katika Kanisa, lakini katika hatari ya kufa kila mtu anaweza kubatiza.. read more...


a.gif Kuna Ubatizo wa namna ngapi?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ ubatizo,
Kuna Ubatizo wa namna ngapi?
Kuna Ubatizo wa namna tatu;
1. Ubatizo wa maji - Ubatizo wa kawaida
2. Ubatizo wa tamaa - Mfano mtu akifa akiwa na nia ya kubatizwa au akitamani kubatizwa
3. Ubatizo wa Damu - Mtu akiifia Imani japo hajabatizwa. read more...


a.gif Sakramenti ya Ubatizo yatuletea nini?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ ubatizo,
Sakramenti ya Ubatizo yatuletea nini?
Sakramenti ya Ubatizo yatuletea;
1. Maondoleo ya dhambi ya asili
2. Maondoleo ya dhambi zote za binafsi na adhabu zake
3. Neema ya Utakaso kwa mara ya kwanza
4. Yatutia alama isiyofutika (1Kor 6:11, 12:13). read more...


a.gif Ubatizo ni nini?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ ubatizo,
Ubatizo ni nini?
Ubatizo ni Sakramenti inayotuwezesha kuzaliwa mara ya pili kwa Maji na Roho Mtakatifu, ni mlango (Kiingilio) kwa Sakramenti nyingine zote na ni ufunguo wa uzima wa milele. (Yoh 3:3, Mt28:19). read more...


a.gif Sakramenti ya ubatizo ni nini?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ ubatizo,
Sakramenti ya ubatizo ni nini?
Sakramenti ya Ubatizo ni Sakramenti yenye kuondoa dhambi ya asili pamoja na dhambi nyingine zote tulizotenda, kufufua roho zetu kwa kututia uzima wa Mungu, Kutuandika Wakristu Watoto wateule wa Mungu na wa Kanisa.. read more...


a.gif Sakramenti inayokamilisha ubatizo na kipaimara ni ipi?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ ekaristi kipaimara sakramenti ubatizo,
Sakramenti inayokamilisha ubatizo na kipaimara ni ipi?
Sakramenti inayokamilisha ubatizo na kipaimara ni ekaristi, iliyo kuu kuliko sakramenti zote kwa sababu ndiyo Yesu mzima, Mungu-mtu, katika maumbo ya mkate na divai.. read more...


a.gif Sakramenti inayohusiana zaidi na ubatizo ni ipi?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ kipaimara sakramenti ubatizo,
Sakramenti inayohusiana zaidi na ubatizo ni ipi?
Sakramenti inayohusiana zaidi na ubatizo ni kipaimara, kinachoendeleza kazi yake.. read more...


a.gif Je, ubatizo tuu unatosha?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ madhehebu ubatizo,
Je, ubatizo tuu unatosha?
Hapana, ubatizo hautoshi, bali unahitaji kukamilishwa na kipaimara na ekaristi, kama vile baada ya kuzaliwa tunahitaji kukomaa na kudumisha uhai wetu kwa chakula.. read more...


a.gif Ubatizo wa watoto wachanga unafanyika tangu lini?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ madhehebu ubatizo,
Ubatizo wa watoto wachanga unafanyika tangu lini?
Ubatizo wa watoto wachanga unafanyika tangu mwanzo, usipingwe na yeyote kwa miaka elfu na zaidi. Ni kwamba Wayahudi walipokea watoto katika dini yao kwa kuwatahiri siku ya nane baada ya kuzaliwa.

β€œHata zilipotimia siku nane za kumtahiri, aliitwa jina lake Yesu” (Lk 2:21).. read more...


a.gif Je, imani ya watu wazima inaweza kufaidisha watoto?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ madhehebu ubatizo,
Je, imani ya watu wazima inaweza kufaidisha watoto?
Ndiyo, imani ya watu wazima inaweza kufaidisha watoto kama wengine pia.. read more...


a.gif Je, watu wazima wanaweza kuelewa sakramenti kwa dhati?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ sakramenti ubatizo,
Je, watu wazima wanaweza kuelewa sakramenti kwa dhati?
Hapana, watu wazima hawawezi kuelewa sakramenti kwa dhati, kwa kuwa zote ni mafumbo yanayotuzidi. Basi, kama Petro alipooshwa miguu, tumuachie Bwana atufanyie kazi anavyojua yeye.. read more...


a.gif Mbona watoto wachanga hawawezi kuelewa kinachofanyika wakati wa ubatizo halafu wanabatizwa?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ madhehebu ubatizo,
Mbona watoto wachanga hawawezi kuelewa kinachofanyika wakati wa ubatizo halafu wanabatizwa?
Ingawa watoto wachanga hawawezi kuelewa kinachofanyika, Mungu anaweza kuwamiminia rohoni mwanga wa imani.. read more...


a.gif Je, watoto wachanga wanaweza kubatizwa?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ madhehebu ubatizo,
Je, watoto wachanga wanaweza kubatizwa?
Ndiyo, watoto wachanga wanaweza kubatizwa kwa sababu hawakatai neema ya Mungu. Wanafunzi wa Yesu walipotaka kuwazuia wasiletwe kwake β€œalichukizwa sana, akawaambia, β€˜Waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie; kwa maana watoto kama hawa ufalme wa Mungu ni wao. Amin, nawaambieni: Yeyote asiyeukubali ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hatauingia kabisa” (Mk 10:14-15).
Yeremia aliambiwa,

β€œKabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa” (Yer 1:5).. read more...


a.gif Tofauti kubwa kati ya ubatizo wa Yohane na ule wa Yesu ni zipi?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ ubatizo,
Tofauti kubwa kati ya ubatizo wa Yohane na ule wa Yesu ni zipi?
Tofauti kubwa kati ya ubatizo wa Yohane na ule wa Yesu ni kwamba sakramenti inategemea imani kwa Kristo na kutushirikisha kifo na ufufuko wake.. read more...


a.gif Je, ubatizo uliotolewa na Yohane Mbatizaji ulikuwa sakramenti?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ sakramenti ubatizo,
Je, ubatizo uliotolewa na Yohane Mbatizaji ulikuwa sakramenti?
Hapana, ubatizo uliotolewa na Yohan Mbatizaji haukuwa sakramenti, kwa sababu yeye alikuwa mtangulizi tu wa Yesu, mwanzilishi wa sakramenti zote.. read more...


page 1 of 212next »