a.gif Sala ni kuongea na Mungu

Category πŸ‘‰katoliki-cotent, Tags πŸ‘‰ kusali sala,
Sala ni kuongea na Mungu
Jifunze na jijengea tabia ya kumsikiliza Mungu rohoni mwako unaposali. Sala ni mazungumzo ya Mungu na mwanadamu. Mazungumzo yanahusisha kuongea na kusikiliza.. read more...


a.gif Kuomba na Kushukuru

Category πŸ‘‰katoliki-cotent, Tags πŸ‘‰ sala,
Kuomba na Kushukuru
Unapo mwomba Mungu Usisahau Kushukuru. Kushukuru ni kuomba mara ya pili. Utazidishiwa kile ulichokiomba na kupewa hata usichokiomba kwa shukrani yako.. read more...


a.gif Uwe na subira Baada ya kuomba

Category πŸ‘‰katoliki-cotent, Tags πŸ‘‰ sala,
Uwe na subira Baada ya kuomba
Uwe na subira Baada ya kuomba kwa Mungu. Sio kila unachoomba kwa Mungu utakipata kwa wakati huo huo au kwa wakati unaofikiri. Mungu ni Mwaminifu Sana Kwenye kujibu maombi lakini vile vile ni mwenye Hekima Kwenye kukujibu, anajua wakati gani ni sahihi kukujibu maombi yako. Anaweza kukujibu saa hiyo hiyo, kesho, keshokutwa au hata mwakani kwa kuangalia wakati ufaao na kwa manufaa yako. Kwa hiyo unapoona hujajibiwa usife moyo, bali uwe na matumaini. Mungu anajua akujibu lini kwa kuwa anajua ni lini wakati ufaao na ni lini kitu kipi kina kufaa.. read more...


a.gif Namna Mungu anavyojibu Sala au Maombi

Category πŸ‘‰katoliki-cotent, Tags πŸ‘‰ sala,
Namna Mungu anavyojibu Sala au Maombi
Mungu ni mwenye Hekima, anajibu Sala zetu kwa kutupa kile tunachohitaji na chenye kutufaa na Sio kutupa kile tunachokitaka na kukitamani kwa kuwa anatupenda na kututakia mema.. read more...


a.gif Mnyororo wa Baraka za Mungu

Category πŸ‘‰katoliki-cotent, Tags πŸ‘‰ sala,
Mnyororo wa Baraka za Mungu
Usiache kusali na kutenda mema kwa kuwa huwezi jua ni watu wangapi wanategemea sala na matendo yako mema. Kumbuka Mungu alimwambia Abraham kama akikuta Wacha Mungu wengi hataiharibu Sodoma na Gomora. Vivyo hivyo Inawezekana wapo watu wengi wanaonufaika na Sala na matendo yako, hasa watu wako wa karibu uwapendao. Unapokuwa mtu wa Sala na mcha Mungu unabarikiwa wewe na wale wa karibu yako. KAMWE USIACHE KUMCHA MUNGU NA KUSALI. Ukiwa mregevu ni sawa na unakata Mnyororo wa Baraka za Mungu kwako na wenzako.. read more...


a.gif Mungu ni Mwaminifu

Category πŸ‘‰katoliki-cotent, Tags πŸ‘‰ sala,
Mungu ni Mwaminifu
Mungu ni Mwaminifu Sana na mwenye mipango na subira katika kila kitu hasa Sala na maombi yetu kwake. Tunaposali leo Mungu anatusikia na kujibu leo, kesho au hata miaka kumi ijayo. Inawezekana hata baraka zako za leo ni majibu ya Sala zako miaka kumi iliyopita. Sali bila kuchoka kwani hujui Sala zako zitakusaidia lini. Usitegemee majibu ya Sala zako wakati huo huo, amini katika uaminifu wa Mungu kwani anajua lini ni siku sahii ya kukujibu.. read more...


a.gif Tusali daima

Category πŸ‘‰katoliki-cotent, Tags πŸ‘‰ sala,
Tusali daima
Sala sio kitu cha muhimu kufanya wakati wa shida tuu. Sala ni kitu cha muhimu zaidi kila siku katika Maisha kuwe na shida au kusiwe na shida.. read more...


a.gif Njia ya sala

Category πŸ‘‰katoliki-cotent, Tags πŸ‘‰ sala,
Njia ya sala
Kwa njia ya sala Binadamu anampa Mungu Utukufu, Mungu anampa Binadamu Wokovu na Neema.. read more...


a.gif Sifa za Sala yeyote

Category πŸ‘‰katoliki-cotent, Tags πŸ‘‰ sala,
Sifa za Sala yeyote
Sala yoyote ili iwe SALA lazima itolewe kwa Imani, Upendo, Unyenyekevu na kwa Matumaini. Sala kama hii ndiyo ipendezayo mbele ya Mungu.. read more...


a.gif Sala inayojibiwa

Category πŸ‘‰katoliki-cotent, Tags πŸ‘‰ sala,
Sala inayojibiwa
Hakuna sala yeyote itolewayo kwa unyenyekevu wa kweli katika imani, matumaini na mapendo inayopita bure mbele ya Mungu. Mungu hamtupi mwenye unyoofu wa moyo.. read more...


a.gif Sala ni ufunguo

Category πŸ‘‰katoliki-cotent, Tags πŸ‘‰ sala,
Sala ni ufunguo
Sala ni ufunguo wa kufungulia mema na kufungia Mabaya. Tusali ili tufungue mema katika maisha yetu na tufunge mabaya katika maisha yetu.. read more...


a.gif Sala ni Upendo

Category πŸ‘‰katoliki-cotent, Tags πŸ‘‰ sala,
Sala ni Upendo
Sala sio maneno mengi au maneno ya kurudiarudia. Sala ni maneno au hata neno moja la kimapendo litamkwalo kwa imani na kwa nia thabiti.. read more...


a.gif Sala sio maneno tuu

Category πŸ‘‰katoliki-cotent, Tags πŸ‘‰ sala,
Sala sio maneno tuu
Sala siyo maneno mazuri, bali sala ni NIA ya Upendo iliyobebwa na maneno mazuri. Tusali kwa kunuia kutoka moyoni na sio kwa kunena maneno tuu mdomoni.. read more...


a.gif Mambo muhimu katika sala

Category πŸ‘‰katoliki-cotent, Tags πŸ‘‰ sala,
Mambo muhimu katika sala
Sala pasipo Imani thabiti, ya nia ya kweli, upendo wa kweli, unyenyekevu wa ndani na tumaini la kweli katika Amani ya rohoni; Haijakamilika na haifai kitu.. read more...


a.gif Sala ni chimbuko la Fadhila

Category πŸ‘‰katoliki-cotent, Tags πŸ‘‰ sala,
Sala ni chimbuko la Fadhila
Sala ndiyo chimbuko la fadhila. Kwa njia ya sala tunapata fadhila za Kimungu na Neema za Mungu. Asaliye daima hujazwa neema na fadhila.. read more...


a.gif Sala ni chakula cha roho

Category πŸ‘‰katoliki-cotent, Tags πŸ‘‰ sala,
Sala ni chakula cha roho
Sala ni kama chakula cha Roho, Bila sala roho inakufa. Tusali daima ili roho zetu ziwe hai siku zote.. read more...


a.gif Sala za kila siku

Category πŸ‘‰katoliki-cotent, Tags πŸ‘‰ sala,
Sala za kila siku
Sala za kila siku katika maisha ndiyo hazina kubwa na msaada hasa wakati wa kufa. Adumuye katika sala Mungu hatomwacha saa ya mwisho. Tusali, tusali, tusali daima…. read more...


a.gif Sali daima

Category πŸ‘‰katoliki-cotent, Tags πŸ‘‰ sala,
Sali daima
Kama mtu anasali kila siku katika maisha yake hakuna kitu kitakachokuwa kigumu. Sala ni njia ya kujipatia neema za kuendesha maisha yetu. Usiache kusali kila siku hata kama upo katika hali gani.. read more...


a.gif Mungu anasubiri sala zako

Category πŸ‘‰katoliki-cotent, Tags πŸ‘‰ sala,
Mungu anasubiri sala zako
Mungu anasubiri sala zako kila siku. Anasubiri sala zako akujibu ili uone utukufu wake. Anasubiri sala zako ili akuze mahusiano yake na wewe. Sali daima kwani Mungu yupo milele kukusikiliza na kukuhudumia.. read more...


a.gif Maisha ya Kikristo ni sala

Category πŸ‘‰katoliki-cotent, Tags πŸ‘‰ sala,
Maisha ya Kikristo ni sala
Hakuna Maisha ya Kikristo bila Kusali. Kama kuna Mkristo anaishi bila kusali huyo siyo Mkristo bali Mkristo mfu. Sala ndiyo uhai wa Mkristo. Hakuna Njia nyingine yoyote ya kumfikia Mungu isipokua sala.. read more...


page 1 of 41234next »