a.gif Mungu ametufunulia nini?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ mtu mungu,
Mungu ametufunulia nini?
Mungu ametufunulia pia ukweli juu yetu wenyewe akijibu kabisa maswali yanayotusumbua kuhusu maana na lengo la maisha yetu.. read more...


a.gif Je, Mungu amejitambulisha pia kwa jina?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ mungu,
Je, Mungu amejitambulisha pia kwa jina?
Ndiyo, Mungu amejitambulisha pia kwa majina mbalimbali. Katika Agano la Kale jina muhimu kuliko yote liliandikwa β€œYHWH” yaani, β€œMimi Ndimi”. Tangu zamani Wayahudi hawalitamki, hivyo wakilifikia wanasoma kwa kutafsiri, β€œBwana”.. read more...


a.gif Hasa Mungu amejifunua kuwa nani?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ mungu,
Hasa Mungu amejifunua kuwa nani?
Hasa Mungu amejifunua kuwa upendo wenyewe.. read more...


a.gif Je, Mungu amewasiliana nasi?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ mtu mungu,
Je, Mungu amewasiliana nasi?
Ndiyo, Mungu amewasiliana nasi, akijitambulisha na kujitoa kwetu, tuweze kuishi katika urafiki naye na hatimaye tushiriki heri yake.. read more...


a.gif Mungu akiwa Roho, viungo ambavyo pengine anapewa vina maana gani?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ kuabudu mungu sanamu,
Mungu akiwa Roho, viungo ambavyo pengine anapewa vina maana gani?
Mungu akiwa Roho, viungo ambavyo pengine anapewa vinamaanisha tu sifa fulani: k.mf. macho ujuzi wake, mikono uwezo wake, mabawa ulinzi wake, n.k. β€œRoho haina mwili na mifupa” (Lk 24:39).. read more...


a.gif Mwenyezi Mungu yukoje basi?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ mungu,
Mwenyezi Mungu yukoje basi?
Mwenyezi Mungu ni ukamilifu mtupu usio na mipaka kwa milele yote.. read more...


a.gif Je, tunaweza kusema juu ya Mungu?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ mungu,
Je, tunaweza kusema juu ya Mungu?
Ndiyo, tunaweza kusema juu ya Mungu kuanzia wema, ukweli na uzuri wa viumbe vyake na kumsifu kiasi chetu kwamba ndiye wema, ukweli na uzuri wenyewe.. read more...


a.gif Tunaanzaje kumjua Mungu?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ mtu mungu uumbaji,
Tunaanzaje kumjua Mungu?
Tunaanza kumjua Mungu kwa kuzingatia viumbe vyake, hasa dhamiri yetu.. read more...


a.gif Nafasi ya Heshima kwa Bikira Maria ni ipi?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ bikira_maria kanisa mungu utatu_mtakatifu,
Nafasi ya Heshima kwa Bikira Maria ni ipi?
Nafasi ya Heshima kwa Bikira Maria inafuata baada ya Heshima kwa Utatu Mtakatifu. read more...


a.gif Kwa ajili gani Mwana wa Mungu (Yesu) alijifanya mtu?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ mungu yesu,
Kwa ajili gani Mwana wa Mungu (Yesu) alijifanya mtu?
Mwana wa Mungu (Yesu) alijifanya mtu kwa ajili yetu wanadamu na wokovu wetu ili atupatanishe na Mungu na kutushirikisha tabia ya umungu. (2Pet, 1:4). read more...


a.gif Neno hili kuwa nafsi tatu kwa Mungu mmoja laitwaje?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ fumbo mungu,
Neno hili kuwa nafsi tatu kwa Mungu mmoja laitwaje?
Laitwa fumbo la Utatu Mtakatifu. (Lk, 3:21-22). read more...


a.gif Katika Mungu mmoja kuna nafsi ngapi?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ mungu,
Katika Mungu mmoja kuna nafsi ngapi?
Katika Mungu mmoja kuna nafsi tatu nazo ni Baba, Mwana na Roho Mtakatifu; nafsi zote ni sawa.. read more...


a.gif Mungu wako wangapi?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ mungu,
Mungu wako wangapi?
Mungu yupo mmoja tuu Mkubwa wa wote na Baba wa wote. (Is: 44:6). read more...


a.gif Mungu ni mwenye subira maana yake ni nini?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ mungu,
Mungu ni mwenye subira maana yake ni nini?
Mungu ni mwenye subira maana yake mara nyingi akawia kuwaadhibu wakosefu maana ataka kuwapa nafasi ya kuongoka. (Eze, 33:11, Zb, 102;1-5). read more...


a.gif Mungu ni mwenye huruma maana yake nini?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ huruma mungu,
Mungu ni mwenye huruma maana yake nini?
Mungu ni mwenye huruma maana yake anawasamehe watu dhambi zao wakitubu.. read more...


a.gif Mungu ajua yote maana yake nini?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ mungu,
Mungu ajua yote maana yake nini?
Mungu ajua yote maana yake ajua ya sasa, ya zamani na ya wakati ujao hata mawazo yetu. read more...


a.gif Mungu aenea pote maaana yake ni nini?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ mungu,
Mungu aenea pote maaana yake ni nini?
Mungu aenea pote maaana yake yupo kila mahali mbinguni na duniani wala hakuna mahali asipokuwepo?. (Zab, 139:7-12). read more...


a.gif Mungu ni Mwenye haki maana yake ni nini?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ mungu,
Mungu ni Mwenye haki maana yake ni nini?
Mungu ni Mwenye haki maana yake kila mtu hupata kwa Mungu haki yake kadiri anavyostahili. read more...


a.gif Mungu ni mwema maana yake ni nini?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ mungu,
Mungu ni mwema maana yake ni nini?
Mungu ni mwema maana yake apenda na kuvitunza viumbe vyake vyote hasa wanadamu na anawatakia mema tu. (Zab, 25:8-10). read more...


a.gif Mungu ni wa Milele maana yake ni nini?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ mungu,
Mungu ni wa Milele maana yake ni nini?
Mungu ni wa Milele maana yake hana mwanzo wala mwisho, amekuwapo kabla ya nyakati, yupo na atakuwapo baada ya nyakati, yupo daima. (1Tim, 1:17). read more...