a.gif Hamu kuu ya binadamu ni ipi?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ mtu mungu,
Hamu kuu ya binadamu ni ipi?
Hamu kuu ya binadamu ni kumwona Mungu. read more...


a.gif Haki gani ya Binadamu ni ya msingi kupita zote?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ amri_ya_tano mtu,
Haki gani ya Binadamu ni ya msingi kupita zote?
Haki ya binadamu iliyo ya msingi kupita zote ni uhai wake ambao ni lazima uheshimiwe na kulindwa tangu siku ya kutungwa mimba. read more...


a.gif Je, mwili utakaofufuliwa ni huuhuu tulionao sasa?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ hukumu kifo marehemu mtu ufufuko,
Je, mwili utakaofufuliwa ni huuhuu tulionao sasa?
Ndiyo, mwili utakaofufuliwa ni huuhuu tulionao sasa, lakini katika hali tofauti: > β€œhupandwa katika uharibifu; hufufuliwa katika kutokuharibika” (1Kor 15:42).. read more...


a.gif Tutakapofariki dunia itatutokea nini?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ hukumu kifo madhehebu marehemu mtu ufufuo uzima_wa_milele,
Tutakapofariki dunia itatutokea nini?
Tutakapofariki dunia roho yetu isiyokufa, mbali na mwili unaooza, itapewa tuzo au adhabu tuliyostahili kwa maisha yetu. β€œIkawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa. Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake” (Lk 16:22-23). β€œKwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida… ninatamani kwenda zangu nikae na Kristo, maana ni vizuri zaidi sana” (Fil 1:21,23). β€œNasi tunaona ni afadhali kutokuwamo katika mwili na kukaa pamoja na Bwana” (2Kor 5:8). Kwa kuwa kifo ni β€œmavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa” (Mhu 12:7). Siku ya ufufuo roho na mwili vitaungana tena kwa ajili ya uzima au moto wa milele. β€œPumzi iliwaingia, wakaishi, wakasimama kwa miguu yao, jeshi kubwa mno” (Ez 37:10).. read more...


a.gif Kwa nini Yesu alishawishiwa/alijaribiwa na Shetani?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ dhambi mtu mungu uumbaji yesu,
Kwa nini Yesu alishawishiwa/alijaribiwa na Shetani?
Yesu alishawishiwa na Shetani kwa kuwa ni mtu kweli, akamshinda kwa niaba ya watu wote, akituonyesha namna ya kumtii Mungu moja kwa moja, β€œhata mauti, naam, mauti ya msalaba” (Fil 2:8).. read more...


a.gif Je, Mwana wa Mungu tangu atwae mwili ni mtu kamili mwenye akili na utashi wa kibinadamu?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ mtu mungu yesu,
Je, Mwana wa Mungu tangu atwae mwili ni mtu kamili mwenye akili na utashi wa kibinadamu?
Ndiyo, Mwana wa Mungu tangu atwae mwili ni mtu kamili mwenye akili na utashi wa kibinadamu. Katika umoja wa nafsi yake vipawa hivyo vinatenda kulingana na Umungu anaouchanga na Baba na Roho Mtakatifu milele.. read more...


a.gif Je, Umungu na utu wa Yesu vinachanganyikana?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ mtu mungu yesu,
Je, Umungu na utu wa Yesu vinachanganyikana?
Hapana, Umungu na utu wa Yesu vimeunganika katika nafsi moja visichanganyikane, kwa kuwa ndani yake hali hizo mbili zinatenda kila moja ya kwake.. read more...


a.gif Yesu ni Mungu au mtu?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ dhambi mtu mungu yesu,
Yesu ni Mungu au mtu?
1 Hapo mwanzo, kabla ya kuwapo kitu kingine cho chote, aliku wapo Neno. Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye alikuwa Mungu. 2 Tangu mwanzo Neno amekuwa na Mungu. 3 Vitu vyote viliumbwa na yeye, wala hakuna cho chote kilichoumbwa ambacho hakukiumba. 4 Uzima ulikuwa ndani yake na uzima huo ndio ulikuwa nuru ya watu. 5 Nuru hiyo huangaza gizani na giza haliwezi kamwe kuizima.. read more...


a.gif Katika unyonge wetu tutumainie nini?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ dhambi mtu,
Katika unyonge wetu tutumainie nini?
Katika unyonge wetu tutumainie huruma ya Mungu aliyetutumia Mkombozi hata β€œdhambi ilipozidi, neema ikawa kubwa zaidi” (Rom 5:20).. read more...


a.gif Dhambi zimetuathiri vipi tena?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ dhambi mtu,
Dhambi zimetuathiri vipi tena?
Dhambi zimetuathiri kwa ndani zaidi, zikitutia udhaifu katika mwili, ujinga katika akili na uovu katika utashi; madonda hayo yanatufanya tuzidi kushindwa.. read more...


a.gif Je, toka mwanzo sisi watu tunaasi mpango wa Mungu peke yetu?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ dhambi malaika mtu,
Je, toka mwanzo sisi watu tunaasi mpango wa Mungu peke yetu?
Hapana, toka mwanzo sisi watu tunaasi mpango wa Mungu kwa kuvutwa na mashetani, yaani malaika waliokataa moja kwa moja kumtumikia; baada ya dhambi ya asili hao wanatutumia sisi pia tuangushane na wenzetu.. read more...


a.gif Mungu angeweza kuzuia watu wasitende dhambi?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ dhambi mtu mungu,
Mungu angeweza kuzuia watu wasitende dhambi?
Ndiyo, Mungu angeweza kuzuia watu wasitende dhambi, lakini aliwaacha watende kwa hiari yao awaonyeshe ukuu wa huruma yake.. read more...


a.gif Je, Mungu aliumba watu wa kwanza katika hali ya mateso na mauti tuliyonayo sasa?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ mtu,
Je, Mungu aliumba watu wa kwanza katika hali ya mateso na mauti tuliyonayo sasa?
Hapana, Mungu aliumba watu wa kwanza katika hali ya heri, wakiwa na upendo wake, utakatifu na uadilifu.. read more...


a.gif Mungu aliwahi kujifunua kwa watu gani?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ mtu mungu,
Mungu aliwahi kujifunua kwa watu gani?
Mungu aliwahi kujifunua kwa wazazi wetu wa kwanza, akaendelea hasa kwa taifa la Israeli, hadi alipomtuma Mwanae ajifanye mtu wa taifa hilo teule.. read more...


a.gif Je, mwili wetu ni muhimu?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ mtu,
Je, mwili wetu ni muhimu?
Ndiyo, mwili wetu ni muhimu, kwa sababu umeumbwa na Mungu, umetwaliwa na Mwanae ili atuokoe, umehuishwa na Roho Mtakatifu atakayeutukuza siku ya ufufuo kwa mfano wa Yesu.. read more...


a.gif Sisi binadamu tukoje?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ mtu uumbaji,
Sisi binadamu tukoje?
Sisi binadamu ni umoja wa mambo mawili: roho iliyoumbwa na Mungu moja kwa moja, na mwili ulioumbwa naye kwa njia ya wazazi.. read more...


a.gif Malaika na watu wanaweza kuchagua hata nini?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ malaika mtu uumbaji,
Malaika na watu wanaweza kuchagua hata nini?
Malaika na watu wanaweza kuchagua hata wawe wema au wabaya milele.. read more...


a.gif Viumbe vyenye hiari ni vipi?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ malaika mtu uumbaji,
Viumbe vyenye hiari ni vipi?
Malaika na watu ndio viumbe pekee vyenye hiari ya kuchagua wenyewe wachangie mpango wa Mungu au la.. read more...


a.gif Mungu akiwa wema mkuu na mwenye uwezo wote, mbona katika viumbe vyake kuna ubaya? Kwa nini Mungu anaruhusu mabaya na maovu?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ dhambi mtu mungu,
Mungu akiwa wema mkuu na mwenye uwezo wote, mbona katika viumbe vyake kuna ubaya? Kwa nini Mungu anaruhusu mabaya na maovu?
Mungu akiwa wema mkuu na mwenye uwezo wote, hakuumba ubaya wowote. Tena kila anapovumilia ule uliosababishwa na viumbe vyenye hiari anaufanya uzae mema makubwa zaidi kwa njia tusizoweza kuzifahamu vizuri hapa duniani.. read more...


a.gif Mungu ametufunulia nini?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ mtu mungu,
Mungu ametufunulia nini?
Mungu ametufunulia pia ukweli juu yetu wenyewe akijibu kabisa maswali yanayotusumbua kuhusu maana na lengo la maisha yetu.. read more...


page 1 of 512345next »