a.gif SALA YA KUMWOMBA MTAKATIFU TERESIA

Category 👉sala, Tags 👉 ahadi maombi mtakatifu nia watakatifu,
SALA YA KUMWOMBA MTAKATIFU TERESIA
Ee Mtakatifu Teresia wa mtoto Yesu, ulistahili kuitwa Msimamizi wa misioni katoliki za dunia yote. Kumbuka ile tamaa yako kuu uliyoonyesha huku duniani ya " kusimika Msalaba wa Yesu Kristu, katika nchi zote na kuhubiri Injili mpaka mwisho wa dunia" . Twakuomba kwa ajili ya maagano yako, wasaidie mapadre, wamisionari, na kanisa zima.. read more...


a.gif KUJIWEKA CHINI YA ULINZI WA MT. YOSEFU

Category 👉sala, Tags 👉 ahadi maombi nia watakatifu,
KUJIWEKA CHINI YA ULINZI WA MT. YOSEFU
Ee Mt. Yosefu, Baba Mlishi wa Mwokozi wangu, na mchumba safi wa Mama wa Mungu, leo ninakuchagua wewe, kama mwombezi wangu kwa Mungu Mwenyezi, na pia kama mfano wangu, na mlinzi wangu, na baba yangu, katika bonde hili la ugenini.
Ee Mt. Yosefu, ambaye Bwana alikufanya mlinzi wa Familia yake, ninakuomba uwe mlinzi wangu mwema katika mambo yangu yote. Uniwashie moyoni mwangu moto wa mapendo makuu kwa Yesu, na uniwezeshe kumtumikia kwa bidii na kwa uaminifu kwa mfano wako. Nisaidie katika udhaifu wangu katika kumheshimu Mama Maria kama Mwombezi wangu. Daima uwe kiongozi wangu katika njia ya fadhila na ibada, na unijalie, baada ya kukufuasa kwa uaminifu katika njia ya haki, nipate ulinzi wako wenye nguvu katika saa ya kufa kwangu.
Amina. read more...


a.gif SALA KWA MT. YOSEFU KWA AJILI YA KULIOMBEA KANISA LA MAHUJAJI

Category 👉sala, Tags 👉 maombi watakatifu,
SALA KWA MT. YOSEFU KWA AJILI YA KULIOMBEA KANISA LA MAHUJAJI
Ee Mtukufu Mt. Yosefu, ulichaguliwa na Mungu kuwa Baba Mlishi wa Yesu, mchumba safi kabisa wa Maria Bikira Milele, na mkubwa wa Familia Takatifu. Umechaguliwa na Mwakilishi wa Kristu kama Msimamizi wa kimbingu na mlinzi wa Kanisa alilolianzisha Kristu. Ndiyo maana ninakuomba kwa matumaini makuu usaidizi wako wenye nguvu kwa ajili ya Kanisa zima duniani. Mlinde kwa namna ya pekee, kwa upendo wa kikweli wa ki-baba, Baba Mtakatifu na Maaskofu wote na Mapadre wenye ushirika na Kiti cha Petro. Uwe mlinzi wao wote wanaotumikia wokovu wa wanadamu kati ya majaribu na mahangaiko ya maisha haya, na utujalie kwamba watu wote wa dunia hii wamfuate Kristu na Kanisa alilolianzisha.
Mpendwa Mtakatifu Yosefu, ukubali majitoleo ya nafsi yangu ambayo sasa ninafanya. Ninajiweka wakfu kwako kwa ajili ya utumishi wako, ili daima wewe uwe baba yangu, mlinzi wangu, na kiongozi wangu katika njia ya wokovu. Unijalie usafi mkuu wa moyo na matamanio makuu ya maisha ya kiroho. Unijalie ili matendo yangu yote, kwa mfano wako, yawe kwa ajili ya sifa na utukufu wa Mungu, pamoja na Moyo wa kimungu wa Yesu, moyo safi wa Maria, na moyo wako wa ki-baba. Uniombee, nami nishiriki kifo chako cha furaha na kitakatifu.
Amina.. read more...


a.gif SALA YA KUMWOMBA MT. YOSEFU MSAADA (SALA KUU KWA MTAKATIFU YOSEFU)

Category 👉sala, Tags 👉 maombi nia watakatifu,
SALA YA KUMWOMBA MT. YOSEFU MSAADA (SALA KUU KWA MTAKATIFU YOSEFU)
Ee Mt. Yosefu mwenye heri, tunakimbilia kwako katika masumbuko yetu, na kisha omba shime ya Mchumba wako Mtakatifu, tunaomba pia kwa matumaini usimamizi wako. Kwa ajili ya mapendo uliyompenda Bikira Mtakatifu Mzazi wa Mungu, na kwa ajili ya kumtunza Mtoto Yesu, twakuomba sana, utuangalie kwa wema sie tuliokuwa fungu lake Yesu Kristu, tukakombolewa kwa damu yake. Tusimamie katika masumbuko yetu kwa enzi na shime yako.
Ee Mlinzi amini wa jamaa takatifu, uwakinge watoto wateule wa Yesu Kristu.
Ee Baba uliyetupenda mno tuepushe na kilema chochote cha madanganyo na upotevu. Ee kinga yetu mwezaji, utusimamie huko juu mbinguni ulipo, tunaposhindana na wenye nguvu wakaao gizani. Kama vile siku za kale ukamwopoa Mtoto Yesu katika hatari ya kuuawa, na leo hivi likinge Kanisa Takatifu la Mungu katika mitego ya adui, na katika shida yote; mtunze daima kila mmoja wetu, tufwate mfano wako, ili tupate na msaada wako, kukaa na utakatifu maisha, kufa kifo chema, na kupata mbinguni makao ya raha milele.
Amina.. read more...


a.gif SALA KWA MT. YOSEFU KWA WASIO NA AJIRA WAPATE AJIRA

Category 👉sala, Tags 👉 ahadi maombi nia watakatifu,
SALA KWA MT. YOSEFU KWA WASIO NA AJIRA WAPATE AJIRA
Ee Mt. Yosefu, tunakuomba kwa ajili ya wale asio na ajira, kwa ajili ya wale wanaotaka kujipatia kipato chao na kulisha familia zao.
Wewe u Msimamizi wa wafanyakazi, tujalie kwamba pasiwepo kati yetu mtu asiye na ajira, na kwamba wale wote ambao wako tayari kufanya kazi waweze kuelekeza nguvu zao na uwezo wao katika kuwatumikia wanadamu wenzao na kujipatia kipato halali.
Wewe u Msimamizi wa familia, usiwaache wale wenye watoto wa kuwatunza na kuwalea wakose namna ya kufanya hivyo. Uwahurumie ndugu zetu waliokosa ajira na kugubikwa na umasikini kwa sababu ya magonjwa au mipango mibaya ya kijamii. Wasaidie viongozi wetu wa kisiasa na walioshika usukani katika nyanja mbalimbali za kiuzalishaji wavumbue suluhu mpya na za haki za jambo hili. Utujalie ili kila mmoja wetu apate kujipatia kipato halali na kufurahia fursa ya kushiriki kadri ya uwezo wake, katika maisha bora zaidi kwa wote. Utujalie ili wote tushiriki pamoja katika raslimali alizotujalia Mungu, na pia utujalie tuwe tayari daima kuwasaidia wale walio wahitaji kuliko sisi.
Amina.. read more...


a.gif SALA KWA MT. YOSEFU KUOMBA KUFAHAMU WITO WAKO

Category 👉sala, Tags 👉 ahadi maombi nia watakatifu,
SALA KWA MT. YOSEFU KUOMBA KUFAHAMU WITO WAKO
Amina.. read more...


a.gif SALA YA UHAI KWA MT. YOSEFU

Category 👉sala, Tags 👉 ahadi maombi nia watakatifu,
SALA YA UHAI KWA MT. YOSEFU

(Sala hii inafaa sana kwa ajili ya kutetea uhai wa watoto wachanga wakiwa tumboni mwa mama zao, dhidi ya utoaji mimba au hatari nyingine dhidi ya uhai wa binadamu). read more...


a.gif SALA YA NOVENA YA SIKU TISA KWA MT. YOSEFU, YA ZAMANI, MIAKA 1900 ILIYOPITA

Category 👉sala, Tags 👉 ahadi maombi nia novena watakatifu yosefu,
SALA YA NOVENA YA SIKU TISA KWA MT. YOSEFU, YA ZAMANI, MIAKA 1900 ILIYOPITA
Ee Mt. Yosefu, ambaye ulinzi wako ni mkubwa, wenye nguvu na wa haraka mbele ya Kiti cha Enzi cha Mungu, ninakukabidhi nia na haja zangu zote. Ee Mt. Yosefu, unisaidie kwa maombezi yako yenye nguvu, na unipatie kutoka kwa Mwanao Mungu, baraka zote za kiroho, kwa njia ya Kristu Bwana wetu, ili nikishapata msaada wako wa mbinguni ningali bado hapa duniani, niweze nami kumsifu, kumwabudu na kumshukuru Mungu aliye Baba mwema kabisa kushinda wote. Ee Mt. Yosefu, sichoki kamwe kufikiri moyoni kwa upendo, jinsi Mtoto Yesu alivyokuwa amesinzia mikononi mwako. Akiwa amepumzika hivyo karibu na moyo wako, sithubutu kujongea, nisije nikamsumbua, bali nakuomba wewe umkumbatie na kumbusu kwa niaba yangu na kumwambia anipe busu lake nitakapovuta pumzi yangu ya mwisho.
Mtakatifu Yosefu Msimamizi wa wanaozimia roho; Utuombee.
Amina.. read more...


a.gif Mungu wangu

Category 👉katoliki-music, Tags 👉 kwaresma maombi,
Mungu wangu
audio: 'file:mungu-wangu-j-mgandu/Mungu-wangu-J-mgandu.mp3'
maelezo: ''. read more...


a.gif Kwa Ishara ya Msalaba

Category 👉katoliki-music, Tags 👉 kwaresma maombi,
Kwa Ishara ya Msalaba
audio: 'file:kwa-ishara-ya-msalaba-tradition/Kwa-ishara-ya-msalaba-Tradition.mp3'
maelezo: ''. read more...


a.gif Nyimbo na Sala za Ibada ya Njia ya Msalaba | Kwa siku za Ijumaa Kwaresma na Ijumaa Kuu

Category 👉sala, Tags 👉 ibada maombi maria mateso tafakari yesu,
Nyimbo na Sala za Ibada ya Njia ya Msalaba | Kwa siku za Ijumaa Kwaresma na Ijumaa Kuu
Picha na: ecatholic2000.com
--. read more...


a.gif Sala ya Kuombea Hali njema ya hewa na mvua

Category 👉sala, Tags 👉 ibada maombi,
Sala ya Kuombea Hali njema ya hewa na mvua
*SALA YA KUOMBEA HALI NJEMA YA HEWA NA MVUA*. read more...


a.gif Sala ya Usiku kabla ya kulala

Category 👉sala, Tags 👉 ibada maombi shukrani tafakari toba,
Sala ya Usiku kabla ya kulala
Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.. read more...


a.gif Novena ya Noeli

Category 👉sala, Tags 👉 ibada maombi novena yesu,
Novena ya Noeli
*Novena ya Noeli (maarufu kama novena ya Mt. Andrea)*. read more...


a.gif Haleluya

Category 👉katoliki-music, Tags 👉 maombi masifu shangwe toba,
Haleluya
audio: 'file:haleluya/HALELUYA.mp3'
maelezo: ''. read more...


a.gif Ee Mungu kwa wema wako

Category 👉katoliki-music, Tags 👉 maombi masifu shangwe tafakari utukufu,
Ee Mungu kwa wema wako
audio: 'file:ee-mungu-kwa-wema-wako/Ee-Mungu-Kwa-Wema-Wako.mp3'
maelezo: ''. read more...


a.gif Ee Bwana usikie kwa sauti yangu ninalia

Category 👉katoliki-music, Tags 👉 maombi,
Ee Bwana usikie kwa sauti yangu ninalia
audio: 'file:ee-bwana-utusikie/EE-BWANA-UTUSIKIE.mp3'
maelezo: ''. read more...


a.gif Ee Bwana fadhili zako zikae nasi

Category 👉katoliki-music, Tags 👉 maombi tafakari,
Ee Bwana fadhili zako zikae nasi
audio: 'file:ee-bwana-fadhili-zako/EE-BWANA-FADHILI-ZAKO.mp3'
maelezo: ''. read more...


a.gif Bwana ni kinga na ngome yangu

Category 👉katoliki-music, Tags 👉 maombi tafakari utukufu,
Bwana ni kinga na ngome yangu
audio: 'file:bwana-nikinga/Bwana-nikinga.mp3'
maelezo: ''. read more...


a.gif Bwana kama wewe

Category 👉katoliki-music, Tags 👉 kwaresma maombi tafakari toba,
Bwana kama wewe
audio: 'file:bwana-kama-wewe/Bwana-kama-wewe.mp3'
maelezo: 'Bwana kama wewe ungehesabu maovu yetu, nani angesimama….'. read more...


page 1 of 41234next »