a.gif Je, sanaa zinafaa kumuadhimishia Mungu?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ ibada,
Je, sanaa zinafaa kumuadhimishia Mungu?
Ndiyo, sanaa zinafaa kumuadhimishia Mungu kwa sababu tunapaswa kutumia kwa utukufu wake vipawa alivyotujalia, kama vile vya kujenga, kupamba, kuchonga, kuchora na kucheza. Kwa njia hizo tutokeze na kukoleza imani yetu na ya wenzetu.. read more...


a.gif Hekalu ndiyo nini?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ ibada maana,
Hekalu ndiyo nini?
Hekalu ndipo tunapomuendea Mungu kwa ibada. Vilevile sisi wenyewe ni Mahekalu.
Yesu aliheshimu na kutakasa hekalu pekee la taifa lake kama β€œnyumba ya Baba” yake (Yoh 2:16), lakini alitabiri kuwa litabomolewa moja kwa moja, na kuwa watu watapaswa kuabudu ndani yake aliye hekalu hai. β€œWayahudi walisema, β€˜Hekalu hili lilijengwa katika muda wa miaka arobaini na sita, nawe utalisimamisha katika siku tatu?’ Lakini yeye alinena habari za hekalu la mwili wake” (Yoh 2:20-21).. read more...


a.gif Je, kuna mahali pa lazima pa kumuadhimishia Mungu?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ ibada,
Je, kuna mahali pa lazima pa kumuadhimishia Mungu?
La! Hakuna mahali pa lazima pa kumuadhimishia Mungu, kwa kuwa yeye hafungwi na mahali.. read more...


a.gif Je, kuna nyakati za kufaa zaidi kumuadhimishia Mungu?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ ibada,
Je, kuna nyakati za kufaa zaidi kumuadhimishia Mungu?
Ndiyo, kuna nyakati za kufaa zaidi kumuadhimishia Mungu. Yesu aliyesema, β€œSikuja kutangua, bali kutimiliza” (Math 5:17), alifuata kalenda ya dini ya Kiyahudi, halafu kwa kufa na kufufuka amekuwa kiini cha ibada zetu zote. Hivyo Mitume waliadhimisha siku aliyofufuka kama β€œsiku ya Bwana” (Ufu 1:10) ambapo wakutane β€œili kumega mkate” (Mdo 20:7) wa ekaristi.. read more...


a.gif Je, tunapoadhimisha mafumbo hayo tuko peke yetu?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ ibada,
Je, tunapoadhimisha mafumbo hayo tuko peke yetu?
Hapana, tunapoadhimisha mafumbo hayo hatuko peke yetu, bali tunashiriki ibada ambayo Yesu anamtolea Baba milele.. read more...


a.gif Je, mafumbo yote yanaweza kuadhimishwa na yeyote?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ ibada,
Je, mafumbo yote yanaweza kuadhimishwa na yeyote?
Hapana, si mafumbo yote yanaweza kuadhimishwa na yeyote, bali mengine yanahitaji mhudumu wake awe amepewa daraja inayoshirikisha uwezo ambao Yesu aliwapa Mitume wake.

β€œIkawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu. Hata kulipokuwa mchana aliwaita wanafunzi wake; akachagua kumi na wawili miongoni mwao, ambao aliwaita Mitume” (Lk 6:12-13).. read more...


a.gif Tushiriki mafumbo hayo mara ngapi?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ ibada,
Tushiriki mafumbo hayo mara ngapi?
Tushiriki mafumbo hayo kadiri ya umbile la kila mojawapo. Kuna β€œubatizo mmoja” (Ef 4:5) kwa sababu ni kuzaliwa upya β€œkwa maji na kwa Roho” (Yoh 3:5), jambo lisiloweza kurudiwa.. read more...


a.gif Je, mafumbo yote saba yanazaa matunda yaleyale?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ ibada,
Je, mafumbo yote saba yanazaa matunda yaleyale?
Hapana, mafumbo yote saba hayazai matunda yaleyale, bali Yesu aliweka kila moja kwa lengo maalumu, litupatie Roho Mtakatifu kadiri ya nafasi na haja fulani ya maisha yetu.. read more...


a.gif Tunapoadhimisha mafumbo hayo, Mungu anatukuzwa vipi?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ ibada,
Tunapoadhimisha mafumbo hayo, Mungu anatukuzwa vipi?
Tunapoadhimisha mafumbo hayo, Mungu anatukuzwa kwa kuwa ndivyo anavyotufanya β€œtuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo… tupate kuwa sifa ya utukufu wake” (Ef 1:4,12).. read more...


a.gif Sisi tunahusika na mafumbo hayo kama nani?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ ibada,
Sisi tunahusika na mafumbo hayo kama nani?
Sisi tunahusika na mafumbo hayo kama walengwa ambao tuyatumie vema ili yazae matunda yote yaliyokusudiwa na Mungu.. read more...


a.gif Mhusika mkuu wa mafumbo hayo ni nani?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ ibada,
Mhusika mkuu wa mafumbo hayo ni nani?
Mhusika mkuu wa mafumbo hayo ni Mungu ambaye kwa njia hiyo anazidi kutufanyia maajabu alivyoyafanya Yesu alipokuwa duniani. Kama tunda la kutukomboa kwa kifo na ufufuko wake, Baba anatujaza humo Roho Mtakatifu kama advansi ya uzima wa milele.. read more...


a.gif Faida ya kupanga taratibu za ibada ni ipi?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ ibada,
Faida ya kupanga taratibu za ibada ni ipi?
Faida ya kupanga taratibu za ibada ni hasa kuhakikisha yote yafuate usahihi wa imani na maadili, yakidumisha umoja na upendo, badala ya kumuachia kiongozi au mwingine yeyote aseme na kufanya anavyotaka. Mitume wenyewe walianza kazi hiyo, wakidhibiti hata karama.. read more...


a.gif Maneno na ishara kwenye ibada vinaweza kubadilishwa na nani?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ ibada,
Maneno na ishara kwenye ibada vinaweza kubadilishwa na nani?
Maneno na ishara vinaweza kubadilishwa na waandamizi wa Mitume, waliokabidhiwa na Yesu mamlaka ya kuendeleza kazi yake katika mazingira mbalimbali hata mwisho wa dunia.. read more...


a.gif Ishara za mafumbo zimetokana na nini?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ ibada ishara,
Ishara za mafumbo zimetokana na nini?
Ishara za mafumbo zimetokana na viumbe (maji, mafuta, mkate, divai n.k.) na maisha ya jamii (kuosha, kupaka, kula na kunywa pamoja n.k.) na historia ya wokovu (kunyunyiza na kuzamisha, kuwekea mikono, kula Pasaka, n.k.),. read more...


a.gif Kwa nini maneno ndiyo muhimu zaidi kuadhimishia mafumbo?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ ibada,
Kwa nini maneno ndiyo muhimu zaidi kuadhimishia mafumbo?
Maneno ndiyo muhimu zaidi kuadhimishia mafumbo kwa sababu yanafafanua ishara nyingine na kuzitia nguvu ya kututakasa.. read more...


a.gif Je, hisi zetu zote zinaweza kutumika kuadhimishia mafumbo?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ ibada,
Je, hisi zetu zote zinaweza kutumika kuadhimishia mafumbo?
Ndiyo, hisi zetu zote zinaweza kutumika kuadhimishia mafumbo, kila moja kadiri ya uwezo wake: macho kwa kuona, pua kwa kunusa, kinywa kwa kuonja na kusema, mwili mzima kwa kugusa na kutenda, lakini hasa masikio kwa kupokea maneno yaletayo uzima wa Kimungu.. read more...


a.gif Mungu ametuagiza matendo maalumu ya ibada kwa sababu gani?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ ibada,
Mungu ametuagiza matendo maalumu ya ibada kwa sababu gani?
Mungu ametuagiza matendo maalumu ya ibada kwa kuzingatia umbile letu, kwamba binadamu ni umoja wa roho na mwili, hivyo anahitaji mwili na hisi zake ili kuingiza chochote rohoni na kutokeza yaliyomo katika roho yake isiyoonekana.. read more...


a.gif Matendo yetu yasipomtukuza Mungu, maana yake nini?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ ibada,
Matendo yetu yasipomtukuza Mungu, maana yake nini?
Matendo yetu yasipomtukuza Mungu, maana yake mafumbo hayakuadhimishwa vizuri.. read more...


a.gif Je, tuishie katika kusadiki na kuadhimisha mafumbo?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ ibada,
Je, tuishie katika kusadiki na kuadhimisha mafumbo?
Hapana, tusiishie katika kusadiki na kuadhimisha mafumbo, kwa kuwa imani na sakramenti zinadai kutekelezwa maishani.. read more...


a.gif Kanisa linaitaje ibada hizo tulizoagizwa na Yesu?

Category πŸ‘‰katekisimu, Tags πŸ‘‰ ibada,
Kanisa linaitaje ibada hizo tulizoagizwa na Yesu?
Kanisa linaita ibada hizo tulizoagizwa na Yesu sakramenti, yaani mafumbo. Ziko saba: Ubatizo, Kipaimara, Ekaristi, Kitubio, Mpako wa Wagonjwa, Daraja na Ndoa. Ndiyo β€œmafundisho ya mabatizo, na kuwekea mikono” (Eb 6:2) tuliyoyapata kupitia Mitume.. read more...