a.gif Je Sakramenti ya Ekaristi hujulikana kwa majina yapi?

Category ๐Ÿ‘‰katekisimu, Tags ๐Ÿ‘‰ ekaristi misa,
Je Sakramenti ya Ekaristi hujulikana kwa majina yapi?
Majina haya;. read more...


a.gif Ni wakati gani katika Misa Mkate na Divai vinageuka Mwili na Damu yake Kristo?

Category ๐Ÿ‘‰katekisimu, Tags ๐Ÿ‘‰ ekaristi madhehebu misa,
Ni wakati gani katika Misa Mkate na Divai vinageuka Mwili na Damu yake Kristo?
Ni katikati ya Misa padri asemapo maneno Matakatifu aliyosema Yesu mwenyewe: "HUU NDIO MWILI WANGU; HII NDIO DAMU YANGU". read more...


a.gif Ni kwa nini ni Kweli Yesu Kristo yuko chini ya maumbo ya Mkate na Divai?

Category ๐Ÿ‘‰katekisimu, Tags ๐Ÿ‘‰ ekaristi,
Ni kwa nini ni Kweli Yesu Kristo yuko chini ya maumbo ya Mkate na Divai?
Nikweli Yesu Kristo yuko chini ya maumbo ya Mkate na Divai kwa sababu. read more...


a.gif Yesu Kristo alianzishaje Ekaristi Takatifu?

Category ๐Ÿ‘‰katekisimu, Tags ๐Ÿ‘‰ ekaristi,
Yesu Kristo alianzishaje Ekaristi Takatifu?
Yesu alitwaa mkate mikononi mwake, akashukuru, akaumega, akawapa mitume wake akisema: "TWAENI MLE WOTE: HUU NDIO MWILI WANGU UTAKAOTOLEWA KWA AJILI YENU". read more...


a.gif Yesu Kristo alianzisha lini Sakramenti ya Ekaristi?

Category ๐Ÿ‘‰katekisimu, Tags ๐Ÿ‘‰ ekaristi,
Yesu Kristo alianzisha lini Sakramenti ya Ekaristi?
Yesu Kristo alianzisha Sakramenti ya Ekaristi Takatifu jioni ya Alhamisi kuu yaani usiku ule kabla ya kukutwaliwa kwenye mateso na msalaba.. read more...


a.gif Sakramenti ya Ekaristi ni nini?

Category ๐Ÿ‘‰katekisimu, Tags ๐Ÿ‘‰ ekaristi maana misa sakramenti,
Sakramenti ya Ekaristi ni nini?
Sakramenti ya Ekaristi ni Sakramenti ya Mwili na Damu ya Yesu Kristo, aliye kweli katika Maumbo ya Mkate na Divai. (Yoh 6:1-17, Mt 26:26-28). read more...


a.gif Ekaristia ni chakula

Category ๐Ÿ‘‰katoliki-music, Tags ๐Ÿ‘‰ ekaristi,
Ekaristia ni chakula
audio: 'file:ekaristi-takatifu/EKARISTI-TAKATIFU.mp3'
maelezo: ''. read more...


a.gif Ekaristi inaadhimishwa kwa mpangilio gani?

Category ๐Ÿ‘‰katekisimu, Tags ๐Ÿ‘‰ ekaristi,
Ekaristi inaadhimishwa kwa mpangilio gani?
Ekaristi inaadhimishwa kwa mpangilio wa kupanda: tunalishwa Neno la Mungu katika mimbari, halafu Mwili na Damu ya Kristo katika altare. Vilevile sehemu ya kwanza (liturujia ya Neno) inatuletea masomo yakiwa na kilele katika Injili. Halafu katika sehemu ya pili (liturujia ya ekaristi) padri anafuata alichofanya Yesu katika karamu ya mwisho: anatwaa mkate na divai (kuandaa dhabihu zetu), anashukuru juu yake (sala kuu ya ekaristi inayogeuza dhabihu) na kuwapa waamini (komunyo, kilele cha yote, inayotugeuza ndani ya Kristo).. read more...


a.gif Kwa nini ekaristi inaitwa sakramenti ya upendo?

Category ๐Ÿ‘‰katekisimu, Tags ๐Ÿ‘‰ ekaristi,
Kwa nini ekaristi inaitwa sakramenti ya upendo?
Ekaristi inaitwa sakramenti ya upendo kwa sababu kila tunapofanya ukumbusho wa sadaka hiyo pekee tunazidi kujifunza na kupokea upendo ambao siku hiyo Yesu โ€œali amewapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapenda upeoโ€ (Yoh 13:1).. read more...


a.gif Je, ekaristi ni kafara (sadaka)?

Category ๐Ÿ‘‰katekisimu, Tags ๐Ÿ‘‰ ekaristi madhehebu,
Je, ekaristi ni kafara (sadaka)?
Ndiyo, ekaristi ni kafara ambayo Yesu alimtolea Baba msalabani na anaendelea kumtolea kwa wokovu wetu.. read more...


a.gif Baada ya mageuzo Yesu anabaki katika ekaristi mpaka lini?

Category ๐Ÿ‘‰katekisimu, Tags ๐Ÿ‘‰ ekaristi,
Baada ya mageuzo Yesu anabaki katika ekaristi mpaka lini?
Baada ya mageuzo Yesu anabaki katika ekaristi moja kwa moja. Maumbo ya mkate na divai yanazidi kudokeza uwepo wake kama chakula na kinywaji chetu, hata kwa faida ya wagonjwa na wengineo wasiohudhuria.
Ndiyo sababu tunazidi kumuabudu katika ekaristi, ingawa hatumuoni.. read more...


a.gif Katika karamu ya Bwana tunakula na kunywa nini?

Category ๐Ÿ‘‰katekisimu, Tags ๐Ÿ‘‰ ekaristi,
Katika karamu ya Bwana tunakula na kunywa nini?
Katika karamu ya Bwana tunakula na kunywa Mwili wa Damu ya Kristo. Katika sala kuu ya ekaristi padri anaporudia maneno ya Yesu juu ya mkate na divai, Roho Mtakatifu anavigeuza kwa dhati: mkate si tena mkate, wala divai si tena divai, ingawa maumbo yanabaki yaleyale kwa hisi zetu.. read more...


a.gif Hatimaye Yesu alitumia divai kufanyia nini?

Category ๐Ÿ‘‰katekisimu, Tags ๐Ÿ‘‰ ekaristi madhehebu,
Hatimaye Yesu alitumia divai kufanyia nini?
Kama alivyofanya Melkizedeck anayefananishwa na Yesu. โ€œMelkizedeki mfalme wa Salemu alileta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu aliye juu sanaโ€ (Mwa 14:18), โ€œamefananishwa na Mwana wa Munguโ€ (Eb 3:7). Alimtolea Mungu kama sadaka. read more...


a.gif Je, divai (pombe) ni halali?

Category ๐Ÿ‘‰katekisimu, Tags ๐Ÿ‘‰ ekaristi madhehebu,
Je, divai (pombe) ni halali?
Ndiyo, divai ni halali, mradi itumike kwa kiasi isije ikaleta madhara.. read more...


a.gif Mara nyingi waamini wanapokea umbo la mkate tu kwa lengo gani?, Kwa nini hatupokei mwili na damu, tunapokea mwili tuu?

Category ๐Ÿ‘‰katekisimu, Tags ๐Ÿ‘‰ ekaristi,
Mara nyingi waamini wanapokea umbo la mkate tu kwa lengo gani?, Kwa nini hatupokei mwili na damu, tunapokea mwili tuu?
Mara nyingi waamini wanapokea umbo la mkate tu kwa lengo la kukwepa umwagaji wa Damu ya Kristo na kurahisisha ibada, hasa kama washiriki ni umati (hata milioni 4 katika misa moja).. read more...


a.gif Yesu alitumia mkate na divai kwa sababu gani?

Category ๐Ÿ‘‰katekisimu, Tags ๐Ÿ‘‰ ekaristi,
Yesu alitumia mkate na divai kwa sababu gani?
Yesu alitumia mkate na divai kwa sababu vilikuwa vya maana sana katika utamaduni wake na katika Agano la Kale.. read more...


a.gif Ekaristi maana yake nini? Je ni kweli Yesu yupo katika Maumbo ya Mkate na Divai?

Category ๐Ÿ‘‰katekisimu, Tags ๐Ÿ‘‰ ekaristi kanisa madhehebu yesu,
Ekaristi maana yake nini? Je ni kweli Yesu yupo katika Maumbo ya Mkate na Divai?
Ekaristi maana yake ni shukrani, iliyokuwa msimamo wa msingi wa Yesu kwa Baba maisha yake yote, hasa alipofikia wakati wa kutolewa awe kafara ya wokovu wetu.

23Maana mimi nilipokea kwa Bwana yale maagizo niliyowaachieni: Kwamba, usiku ule Bwana Yesu alipotolewa, alitwaa mkate, 24akamshukuru Mungu, akaumega, akasema: โ€œHuu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa kunikumbuka.โ€ 25Vivyo hivyo, baada ya kula, akatwaa kikombe cha divai, akasema: โ€œHiki ni kikombe cha agano jipya linalothibitishwa kwa damu yangu. Fanyeni hivi, kila mnapokunywa, kwa kunikumbuka.โ€
26Maana kila mnapokula mkate huu na kukinywa kikombe hiki, mwatangaza kifo cha Bwana, mpaka atakapokuja. 27Kwa hiyo, kila aulaye mkate huo au kunywa kikombe cha Bwana bila kustahili, atakuwa na hatia dhidi ya mwili na damu ya Bwana. (1Kor 11:23-27).. read more...


a.gif Sakramenti inayokamilisha ubatizo na kipaimara ni ipi?

Category ๐Ÿ‘‰katekisimu, Tags ๐Ÿ‘‰ ekaristi kipaimara sakramenti ubatizo,
Sakramenti inayokamilisha ubatizo na kipaimara ni ipi?
Sakramenti inayokamilisha ubatizo na kipaimara ni ekaristi, iliyo kuu kuliko sakramenti zote kwa sababu ndiyo Yesu mzima, Mungu-mtu, katika maumbo ya mkate na divai.. read more...


page 2 of 2« previous12