a.gif MASOMO YA MISA, IJUMAA, JULAI 19, 2019: JUMA LA 15 LA MWAKA

Category πŸ‘‰masomo-ya-misa, Tags πŸ‘‰ masomo_ya_misa,
MASOMO YA MISA, IJUMAA, JULAI 19, 2019: JUMA LA 15 LA MWAKA
Musa na Haruni walifanya ajabu hizo zote mbele ya Farao; Bwana akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, asiwape wana wa Israeli ruhusa watoke nchi yake.. read more...


a.gif MASOMO YA MISA, ALHAMISI, JULAI 18, 2019: JUMA LA 15 LA MWAKA

Category πŸ‘‰masomo-ya-misa, Tags πŸ‘‰ masomo_ya_misa,
MASOMO YA MISA, ALHAMISI, JULAI 18, 2019: JUMA LA 15 LA MWAKA
Musa alimwambia Mungu, Tazama, nitakapofika kwa wana wa Israeli, na kuwaambia, Mungu wa baba zenu amenituma kwenu; nao wakaniuliza. Jina lake n’nani? Niwaambie nini? Mungu akamwambia Musa, Mimi niko ambaye niko; akasema, Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli; Mimi niko amenituma kwenu.
Tena Mungu akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli maneno haya, Bwana, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenituma kwenu; hili ndilo jina langu hata milele, nalo ni kumbukumbu langu hata vizazi vyote.. read more...


a.gif MASOMO YA MISA, JUMATANO, JULAI 17, 2019: JUMA LA 15 LA MWAKA

Category πŸ‘‰masomo-ya-misa, Tags πŸ‘‰ masomo_ya_misa,
MASOMO YA MISA, JUMATANO, JULAI 17, 2019: JUMA LA 15 LA MWAKA
Musa alikuwa akilichunga kundi la Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani; akaliongoza kundi nyuma ya jangwa, akafika mpaka mlima wa Mungu, hata Horebu. Malaika wa Bwana akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kijiti; akatazama, na kumbe! Kile kijiti kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea. Musa akasema, Nitageuka sasa, niyaone maono haya makubwa, na sababu kijiti hiki hakiteketei. Bwana alipoona ya kuwa amegeuka ili atazame, Mungu akamwita kutoka katikati ya kile kijiti, akasema, Musa! Musa! Akasema, Mimi hapa. Naye akasema, Usikaribie hapa; vua viatu vyako miguuni mwako; maana mahali hapa unaposimama ni nchi takatifu. Tena akasema, Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. Musa akaficha uso wake; kwa maana aliogopa kumwangalia Mungu.. read more...


a.gif MASOMO YA MISA, JUMANNE, JULAI 16, 2019: JUMA LA 15 LA MWAKA

Category πŸ‘‰masomo-ya-misa, Tags πŸ‘‰ masomo_ya_misa,
MASOMO YA MISA, JUMANNE, JULAI 16, 2019: JUMA LA 15 LA MWAKA
Mtu mmoja wa nyumba ya Lawi aliondoka akaoa binti mmoja wa Lawi. Yule mwanamke akachukua mimba akazaa mwana, na alipoona ya kuwa ni mtoto mzuri akamficha miezi mitatu. Na alipokuwa hawezi kumficha tena, akampatia kisafina cha manyasi akakipaka sifa na lami, akamtia mtoto ndani yake, akakiweka katika majani kando ya mto. Umbu lake mtoto akasimama mbali ili ajue yatakayompata.. read more...


a.gif MASOMO YA MISA, JUMATATU, JULAI 15, 2019: JUMA LA 15 LA MWAKA

Category πŸ‘‰masomo-ya-misa, Tags πŸ‘‰ masomo_ya_misa,
MASOMO YA MISA, JUMATATU, JULAI 15, 2019: JUMA LA 15 LA MWAKA
Aliinuka mfalme mpya kutawala Misri, asiyemjua Yusufu. Akawaambia watu wake, Angalieni, watu wa wana wa Israeli ni wengi, tena wana nguvu kuliko sisi. Haya! na tuwatendee kwa akili, wasije wakaongezeka; tena, kukitokea vita, wao nao wasije wakashikamana na adui zetu na kupigana nasi, na kutoka katika nchi hii, Basi wakaweka wasimamizi juu yao wawatese kwa mizigo yao. Nao wakamjengea Farao miji ya kuwekea akiba, Pithomu na Ramesesi.. read more...


a.gif MASOMO YA MISA, JULAI 14, 2019: DOMINIKA YA 15 YA MWAKA C

Category πŸ‘‰masomo-ya-misa, Tags πŸ‘‰ masomo_ya_misa,
MASOMO YA MISA, JULAI 14, 2019: DOMINIKA YA 15 YA MWAKA C
Ukiwa utaifuata sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa kuyashika maagizo yake, na amri zake zilizoandikwa katika chuo hiki cha torati; ukimwelekea Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote. Kwa maana maagizo haya nikuagizayo leo, si mazito mno kwako, wala si mbali. Si mbinguni, hata useme, Ni nani atakayetupandia mbinguni akatuletee, aje atuambie tusikie, tupate kuyafanya? Wala si ng’ambo ya pili ya bahari, hata useme. Ni nani atakayetuvukia bahari, akatuletee, aje atuambie, tusikie, tupate kuyafanya? Lakini neno li karibu nawe sana, li katika kinywa chako na moyo wako, upate kulifanya.. read more...


a.gif MASOMO YA MISA, JUMAMOSI, JULAI 13, 2019: JUMA LA 14 LA MWAKA

Category πŸ‘‰masomo-ya-misa, Tags πŸ‘‰ masomo_ya_misa,
MASOMO YA MISA, JUMAMOSI, JULAI 13, 2019: JUMA LA 14 LA MWAKA
Yakobo aliwaamuru wanawe: Mimi ninakwenda kukusanywa pamoja na watu wangu; mnizike pamoja na baba zangu, katika pango iliyomo shambani mwa Efroni, Mhiti; katika ile pango iliyomo shambani mwa Makpela, iliyo mbele ya Mamre katika nchi ya Kanaani, aliyoinunua Ibrahimu pamoja na shamba kwa Efroni Mhiti, pawe milki yake pa kuzikia. Humo walimzika Ibrahimu, na Sara mkewe; humo wakamzika Isaka, na Rebeka mkewe; nami humo nikamzika Lea; shamba na pango iliyomo lililonunuliwa kwa bani Hethi.. read more...


a.gif MASOMO YA MISA, IJUMAA, JULAI 12, 2019 JUMA LA 14 LA MWAKA

Category πŸ‘‰masomo-ya-misa, Tags πŸ‘‰ masomo_ya_misa,
MASOMO YA MISA, IJUMAA, JULAI 12, 2019 JUMA LA 14 LA MWAKA
Israeli alisafiri pamoja na yote aliyokuwa nayo, akaja Beer-sheba, akamchinjia sadaka Mungu wa Isaka babaye. Mungu akanena na Israeli katika ndoto ya usiku, akasema, Yakobo, Yakobo. Akasema, Mimi hapa. Akasema, Mimi ni Mungu, Mungu wa baba yako, usiogope kushuka mpaka Misri; maana nitakufanya uwe taifa kubwa huko. Mimi nitashuka pamoja nawe mpaka Misri; nami nitakupandisha lena bila shaka; na Yusufu ataweka mkono wake juu ya macho yako. Yakobo akaondoka kutoka Beer-sheba; wana wa Israeli wakamchukua baba yao, na watoto wao wadogo, na wake zao katika magari aliyoyapeleka Farao ili kumchukua. Wakatwaa na wanyama wao, na mali zao walizokuwa wamezipata katika nchi ya Kanaani, wakaja Misri, Yakobo na uzao wake wote pamoja naye. Wanawe, na wana wa wanawe, pamoja naye, binti zake na binti za wanawe, na uzao wake wote, aliwaleta pamoja naye mpaka Misri. Yakobo akampeleka Yuda mbele yake kwa Yusufu, ili amwongoze njia mpaka Gosheni. Wakaja mpaka nchi ya Gosheni. Yusufu akatandika gari lake, akapanda kwenda kumlaki Israeli, babaye, huko Gosheni; akajionyesha kwake, akamwangukia shingoni, akalia shingoni mwake, kitambo kizima. Israeli akamwambia Yusufu, Na nife sasa, kwa kuwa nimekuona uso wako, ya kuwa ungali hai.. read more...


a.gif MASOMO YA MISA, ALHAMISI, JULAI 11, 2019 JUMA LA 14 LA MWAKA

Category πŸ‘‰masomo-ya-misa, Tags πŸ‘‰ masomo_ya_misa,
MASOMO YA MISA, ALHAMISI, JULAI 11, 2019 JUMA LA 14 LA MWAKA
Nchi yote ya Misri ilipoonnjaa, watu walilia Farao awape chakula. Farao akawaambia Wamisri wote, Enendeni kwa Yusufu; atakavyowaambia, fanyeni. Njaa ikawa katika dunia yote pia. Yusufu akazifungua ghala zote, akawauzia Wamisri. Njaa ikawa nzito katika nchi ya Misri. Watu wa nchi zote wakaja Misri kwa Yusufu; ili wanunue nafaka; kwa sababu njaa imekuwa nzito katika dunia yote. Wana wa Israeli wakaja wanunue chakula miongoni mwao waliokuja, kwa kuwa kulikuwa na njaa katika nchi ya Kanaani. Naye Yusufu alikuwa ni liwali juu ya nchi, ndiye aliyewauzia watu wote wa nchi. Nao ndugu zake Yusufu wakaja, wakainama kifudifudi mbele yake. Yusufu akawaona nduguze akawatambua, lakini alijifanya kama mgeni kwao. Akasema nao kwa maneno makali, akawaambia, Mmetoka wapi ninyi? Wakasema, Tumetoka nchi ya Kanaani, ili tununue chakula. Akawatia wote gerezani siku tatu. Yusufu akawaambia siku ya tatu, Fanyeni hivi, mkaishi, maana mimi namcha Mungu. Kama ni wa kweli ninyi, ndugu yenu mmoja na afungwe gerezani, nanyi nendeni mkachukue nafaka kwa njaa ya nyumba zenu, mkamlete ndugu yenu mdogo kwangu; hivyo maneno yenu yatahakikishwa, wala hamtakufa. Ndivyo walivyofanya. Wakaambiana, Kweli sisi tulimkosa ndugu yetu, kwa kuwa tuliona shida ya roho yake, alipotusihi, wala hatukusikia; kwa hiyo shida hii imetupata. Reubeni akajibu, akawaambia, Sikuwaambia, nikisema, msimkose kijana? Wala hamkusikia; kwa hiyo damu yake inatakwa tena. Wala hawakujua ya kwamba Yusufu anawasikia, kwa sababu alikuwapo mkalimani kati yao. Akajitenga nao akalia. Kisha akawarudia, na kusema nao, akamtwaa Simeoni miongoni mwao, akamfunga mbele ya macho yao.. read more...


a.gif MASOMO YA MISA, JUMATANO, JULAI 10, 2019 JUMA LA 14 LA MWAKA

Category πŸ‘‰masomo-ya-misa, Tags πŸ‘‰ masomo_ya_misa,
MASOMO YA MISA, JUMATANO, JULAI 10, 2019 JUMA LA 14 LA MWAKA
Nchi yote ya Misri ilipoona njaa, watu walilia Farao awape chakula. Farao akawaambia Wamisri wote, Enendeni kwa Yusufu; atakavyowaambia, fanyeni. Njaa ikawa katika dunia yote pia. Yusufu akazifungua ghala zote, akawauzia Wamisri. Njaa ikawa nzito katika nchi ya Misri. Watu wa nchi zote wakaja Misri kwa Yusufu; ili wanunue nafaka; kwa sababu njaa imekuwa nzito katika dunia yote.. read more...


a.gif MASOMO YA MISA, JUMANNE, JULAI 9, 2019: JUMA LA 14 LA MWAKA

Category πŸ‘‰masomo-ya-misa, Tags πŸ‘‰ masomo_ya_misa,
MASOMO YA MISA, JUMANNE, JULAI 9, 2019: JUMA LA 14 LA MWAKA
Yakobo aliondoka usiku ule akawatwaa wakeze wawili, na vijakazi wake wawili, na wanawe kumi na mmoja, akavuka kivuko cha Yaboki. Akawatwaa, akawavusha mto, akavusha na vyote alivyokuwa navyo.. read more...


a.gif MASOMO YA MISA, JUMATATU, JULAI 8, 2019: JUMA LA 14 LA MWAKA

Category πŸ‘‰masomo-ya-misa, Tags πŸ‘‰ masomo_ya_misa,
MASOMO YA MISA, JUMATATU, JULAI 8, 2019: JUMA LA 14 LA MWAKA
Yakobo alitoka Beer-sheba, kwenda Harani. Akafika mahali fulanl akakaa huko usiku kucha, maana jua lilikuwa limekuchwa; akatwaa jiwe moja la mahali pale akaliweka chini ya kichwa chake, akalala usingizi pale pale.. read more...


a.gif MASOMO YA MISA, JULAI 7, 2019 DOMINIKA YA 14 YA MWAKA C

Category πŸ‘‰masomo-ya-misa, Tags πŸ‘‰ masomo_ya_misa,
MASOMO YA MISA, JULAI 7, 2019 DOMINIKA YA 14 YA MWAKA C
Furahini pamoja na Yerusalemu, shangilieni kwa ajili yake, ninyi nyote mmpendao; furahini pamoja naye kwa furaha, ninyi nyote mliao kwa ajili yake; mpate kunyonya, na kushibishwa kwa maziwa ya faraja zake, mpate kukama, na kufurahiwa kwa wingi wa utukufu wake. Maana Bwana asema hivi, Tazama, nitamwelekezea Amani kama mto, na utukufu wa mataifa kama kijito kifurikacho, nanyi mtapata kunyonya; mtabebwa; na juu ya magoti mtabembelezwa. Mfano wa mtu ambaye mama yake amfariji, ndivyo nitakavyowafariji ninyi; nanyi mtafarijiwa katika Yerusalemu. Nanyi mtaona, na mioyo yenu itafurahi, na mifupa yenu itasitawi kama majani mabichi; na mkono wa Bwana utajulikana, uwaelekeao watumishi wake.. read more...


a.gif MASOMO YA MISA, JUMAMOSI, JULAI 6, 2019: JUMA LA 13 LA MWAKA

Category πŸ‘‰masomo-ya-misa, Tags πŸ‘‰ masomo_ya_misa,
MASOMO YA MISA, JUMAMOSI, JULAI 6, 2019: JUMA LA 13 LA MWAKA
Ikawa Isaka alipokuwa mzee, na macho yake yamepofuka asione, akamwita Esau, mwanawe mkubwa, akamwambia, Mwanangu. Nave akamwitikia, Mimi hapa. Akasema, Tazama, sasa mimi nimekuwa mzee, wala sijui siku ya kufa kwangu. Basi, nakuomba, chukua mata yako, podo lako na upinde wako, ukaende nyikani uniwindie mawindo; ukanifanyie chakula kitamu namna ile niipendayo, ukaniletee, ili nile; na roho yangu ikubariki, kabla sijafa.. read more...


a.gif MASOMO YA MISA, IJUMAA, JULAI 5, 2019 JUMA LA 13 LA MWAKA

Category πŸ‘‰masomo-ya-misa, Tags πŸ‘‰ masomo_ya_misa,
MASOMO YA MISA, IJUMAA, JULAI 5, 2019 JUMA LA 13 LA MWAKA
Umri wake Sara ulikuwa miaka mia na ishirini na saba, ndio umri wake Sara. Sara akafa katika Kiriath-arba, ndio Hebroni, katika nchi ya Kanaani. Ibrahimu akaja kumlilia Sara na kumwombolezea. Akaondoka Ibrahimu kutoka mbele ya maiti wake, akasema na bani Hethi, akinena, Mimi ni mgeni, ninatembea kwenu; nipeni mahali pa kuzikia kwenu, pawe pangu, nimzike maiti wangu atoke mbele yangu.. read more...


a.gif MASOMO YA MISA, ALHAMISI, JULAI 4, 2019 JUMA LA 13 LA MWAKA

Category πŸ‘‰masomo-ya-misa, Tags πŸ‘‰ masomo_ya_misa,
MASOMO YA MISA, ALHAMISI, JULAI 4, 2019 JUMA LA 13 LA MWAKA
Mungu alimjaribu Ibrahimu, akamwambia, Ee Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa. Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.. read more...


a.gif MASOMO YA MISA, JUMATANO, JULAI 3, 2019 JUMA LA 13 LA MWAKA

Category πŸ‘‰masomo-ya-misa, Tags πŸ‘‰ masomo_ya_misa,
MASOMO YA MISA, JUMATANO, JULAI 3, 2019 JUMA LA 13 LA MWAKA
Tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu. Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana. Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho.. read more...


a.gif MASOMO YA MISA, JUMANNE, JULAI 2, 2019: JUMA LA 13 LA MWAKA C

Category πŸ‘‰masomo-ya-misa, Tags πŸ‘‰ masomo_ya_misa,
MASOMO YA MISA, JUMANNE, JULAI 2, 2019: JUMA LA 13 LA MWAKA C
Hata alfajiri ndipo malaika walimhimiza Lutu, wakisema, Ondoka, mtwae mkeo na binti zako wawili waliopo hapa, usipotee katika maovu ya mji huu. Akakawia-kawia; nao wale watu wakamshika mkono, na mkono wa mkewe, mkono wa binti zake wawili, kwa jinsi Bwana alivyohurumia, wakamtoa wakamweka nje ya mji. Ikawa walipomtoa nje, mmoja alisema, Jiponye nafsi yako; usitazame nyuma, wala usisimame katika hilo bonde po pote; ujiponye mlimani, usije ukapotea. Lutu akawaambia, Sivyo, bwana wangu! tazama, mtumwa wako ameona kibali machoni pako, nawe umezidisha rehema zako ulizonifanyia kwa kuponya nafsi yangu, nami siwezi kukimbilia mlimani nisipatwe na yale mabaya, nikafa.. read more...


a.gif MASOMO YA MISA, JUMATATU, JULAI 1, 2019: JUMA LA 13 LA MWAKA C

Category πŸ‘‰masomo-ya-misa, Tags πŸ‘‰ masomo_ya_misa,
MASOMO YA MISA, JUMATATU, JULAI 1, 2019: JUMA LA 13 LA MWAKA C
Watu hao waliondoka huko wakaelekeza nyuso zao Sodoma. Ibrahimu akaenda pamoja nao awasindikize. Bwana akanena, Je! Nimfiche Ibrahimu jambo nilifanyalo, akiwa Ibrahimu atakuwa taifa kuu, hodari, na katika yeye mataifa yote ya dunia watabarikiwa? Kwa maana nimemjua ya kwamba atawaamuru wanawe, na nyumba yake baada yake waishike njia ya Bwana, wafanye haki na hukumu, ili kwamba Bwana naye akamtimizie Ibrahimu ahadi zake. Bwana akasema, Kwa kuwa kilio cha Sodoma na Gomora kimezidi, na dhambi zao zimeongezeka sana, basi, nitashuka sasa nione kama wanayotenda ni kiasi cha kilio kilichonijia; na kama sivyo, nitajua.. read more...


a.gif MASOMO YA MISA, JUNI 30, 2019 DOMINIKA YA 13 YA MWAKA C

Category πŸ‘‰masomo-ya-misa, Tags πŸ‘‰ masomo_ya_misa,
MASOMO YA MISA, JUNI 30, 2019 DOMINIKA YA 13 YA MWAKA C
Bwana alimwambia Eliya: Enenda, mtie mafuta Elisha mwana wa Shafati wa Abel-Mehola awe nabii mahali pako. Basi akaondoka huko, akamkuta Elisha mwana wa Shafati, aliyekuwa akilima, mwenye jozi za ng’ombe kumi na mbili mbele yake, na yeye mwenyewe alikuwa pamoja na lile la kumi na mbili. Eliya akapita karibu naye, akatupa vazi lake juu yake. Naye akawaacha ng’ombe, akamfuata Eliya mbio, akasema, Nipe ruhusa, nakuomba, nimbusu baba yangu na mama yangu, kisha mimi nitakufuata. Akamwambia, Enenda, urudi; ni nini niliyokutendea. Akarudi akiacha kumfuata, akatwaa lile jozi la ng’ombe, akawachinja, akatokosa nyama zao kwa ile miti ya ng’ombe, akawapa watu, wakala. Kisha akainuka, akamfuata Eliya, akamhudumia.. read more...


page 1 of 621123...620621next »